ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 30, 2025

CHADEMA WAMEKOMAA NA NO REFORMS NO ELECTIONS KWANINI NINYI MSIUNGANE NAO MMEBAKI KWENYE UCHAGUZI

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo pamoja na kutaja vipaumbele 12 vya chama chake iwapo kitapewa ridhaa ya kuunda Serikali baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, huku akiahidi mageuzi makubwa katika sekta za afya, elimu, ajira na maslahi ya wafanyakazi. Pamoja na hayo amejibu maswali ya waandishi wa Habari kuhusu kwanini wao kama chama kikongwe nchini Tanzania, hawakuungana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA) ambao uliunda UKAWA kusimama kwenye msimamo wa "No Reforms No Elections"..... Gombo amesema CUF imeamua kuanzia Mwanza kwa sababu ni mkoa wa kimkakati kisiasa na kwamba yeye mwenyewe ni mzawa wa eneo hilo. #uchaguzimkuu2025

Friday, August 29, 2025

MBARONI MADAI YA KUWAREKODI MAUDHUI YASIYOFAA WAHADZABE

 


RAIA wa kigeni na baadhi ya waongoza watalii, ambao ni wazawa wa Tanzania, wanahojiwa na mamlaka za serikali wakituhumiwa kuwarekodi maudhui yasiyofaa kuhusu wananchi wanaotoka jamii ya waokota matunda na warina asali wa Kabila la Hadzabe, wanaoishi katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Jana, Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Lameck Karanga, alisema serikali kupitia mamlaka husika, imeanza kuchukua hatua dhidi ya watu hao.

Kwa mujibu wa Dk. Karanga, ofisi yake kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji, baada ya kuwakamata na kuwahoji raia hao wa kigeni, wamebaini kuwa hawaishi kihalali nchini kutokana na vibali vyao kuisha muda huku akisema hatua stahiki dhidi yao zitachukuliwa.

Aidha, alisema waongoza watalii walioshiriki katika tukio hilo, wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufungiwa kupeleka watalii katika eneo la Wahadzabe.

'Ni kweli jambo hili limetokea na sisi kama serikali tumeanza kuchukua hatua kali. Kwa sababu si jambo jema na si kitendo kizuri kinachofanyika na hawa wenzetu. Kikubwa ni kwamba kimefanyika na watu ambao sio Watanzania.

"Ni watu wa mataifa mengine wanakuja wanachukua picha, halafu wanawanywesha watoto wa Wahadzabe pombe na wakati mwingine wanachukua tena nyama kutoka wanakojua na hata wakati mwingine hatujui zina nini wanawalisha zikiwa mbichi, “ alisema. 

" Kwa kweli tutachukua hatua kali sana na hivi leo tunavyoongea tumewakamata tuko nao na tunawahoji. Na hao watu kiukweli wamekuwa wakifanya vitendo hivi vinavyodhalilisha jamii ya Wahadzabe. Kama unavyofahamu ni jamii adimu ambayo inatupa kipato kupitia utalii hapa Karatu," aliongeza. 

Mkuu huyo wa wilaya, alisema watu hao wanawafanyia hivyo kwa sababu pengine hali waliyonayo au wakiwa na makusudi yao ya kuiharibia nchi yetu suala la utalii.

"Walikuwa na Watanzania ambao wakati mwingine tunawaita tour guides au ni waongoza watalii na ni wazawa wa Tanzania, ambao nao wanakiuka taratibu.Kwa mfano, hao wenzetu waliofanya haya matukio wameenda bila kibali cha filamu, lakini vilevile wameenda kukaa kule muda mrefu kufanya haya matukio.

"Wako na wenzetu wanaowaongoza kwenye yale maboma ya Wahadzabe. Kwa sababu wao hawajui na wakati mwingine wanatumia hata pikipiki. Kwa hiyo sisi kama serikali tumejikita hadi sasa kuongeza upana wa kuweka vyombo vyetu vya ulinzi katika maeneo hayo ili kuweza kibaini. Tumeenda kuangalia pasport zao (hati za kusafiria) zime-expire (zimeisha muda wake). Wakati mwingine wamekuja hapo kutembea lakini wanajifanya kama watalii," alisema. 

Kutokana na tukio hilo, Mkuu huyo wa wilaya alisema Idara ya Uhamiaji imefanya kazi yake vizuri kwa kuwa ilifanya operesheni hiyo na kuwabaini walikuwa wamejificha kwenye nyumba za waendesha utalii. Alisema baada ya uhamiaji kuwakamata, walizuia hati zao za kusafiria ili kuwahoji.

"Kauli ya serikali ni kwamba huu utaratibu haukubaliki wa kwenda kupiga picha kwenye jamii hii ya Wahadzabe bila kuwa na utaratibu. Hatutavumilia, tutachukua hatua kali, "alisema.

Jamii ya Wahadzabe ni moja ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza shughuli za uwindaji, ikiishi eneo pekee la kaskazini mwa Tanzania, ikila matunda na mizizi na aina mbalimbali za wanyama.

CHUO CHA FURAHIKA KUNOGILE KUWAPATIA MAFUNZO STADI VIJANA WAPATAO 300 MWEZI OCTOBA


 NA VICTOR MASANGU

Katika kuunga mkono juhudi mbali mbali zinazofanywa na  Rais wa  awamu ya sita. Dkt. Samia Suluhu Hassan hususan katika kundi la vijana uongozi wa chuo cha Furahika education College (FEC) kilichopo Jijini Dar es Salaam inatarajia kuwapatia  mafunzo ya fani mbali mbali kwa vijana wapatao 300 ambapo watapataa fursa ya kusoma masomo tifauti kwa kipindi cha mwaka mmoja bure bila malipo yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mkuu wa chuo hicho cha  Furahika Dkt. David Msuya amesema kwamba lengo kubwa  la mafunzo  hayo ni kwa aajili ya kuweza  kuwasaidiaa vijana kuondokana na wimbi la matumizi yaa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika maakundi mabaya.

Msuya amebaainisha kwamba  chuo chao  kimeamua  kushirikian bega kwa bega na serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia,  wanawake na makundi maalum  katika kuweka mipango madhubuti ya kutoa mafunzo hayo bure kwa lengo la kuwasaidi vijana kupat ujuzi n maharifa mbali mbali bila malipo yoyote.

"Chuo chetu cha Fuhahika kwa sasa tumeamu kuung mkono juhudi za serikali y wamu y sit n kwamba tunshirikiana na Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia, wanawake na makundi maalum na hii yote ni kwa ajili  ya kuwasaidia vijana wetu kupata mafunzo na ujuzi wa fani mbali mbali  ili wasiweze  kujingize katika makundi mabaya ikiwemo kujihusisha na madawa ya kulevyaa pamoja ngono,"amebaainish Dkt Msuya.

Kaimu mkurugenzi huyo amebainisha kwamba vijana hao  300 aambaao wanatarajia  kuanza rasmi mafunzo hayo mwezi 0ctoba mwaka huu  na kubainisha kwamba  zoezzi la usahili kwa wanafunzi  hao unatarajiwa  kuanza kufanyika  tarehe 2 mwezi wa tisa kupitia tovuti ya chuo au kwenda  katika ofisi zao zilizopo maeneo ya  Buguruni malapa.

Aidha Msuya amezitaaja badhi ya kozi ambazo watafundishwa vijana hao ni pamoja na ufundi selemala,mapishi,kompyuta (ICT) ,upigaji wa picha,masuala ya bandari,kozi na ususi,kozi ya udereva, biashara  na masoko, kozi ya utalii pamoja na fani nyingine mbali mbali za uongozi katika mambo ya kibiashara.

"Pia amewahimiza wazazi, walezi pamoja viongozi wa chama wakiwemo wale wa jumuiya kuhaakikisha wanawahimiza vijanaa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kupta ujuzi mbali mbali naa hatimaye kuweza kujiajiri na kuondokana na kuwa tegemezi,"amebinisha Msuya.

Katika hatua nyingine Msuya amebainisha kwamba watapatiwa mafunzo hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo gharama zake zote zitagharimu kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zimetolewa  na wafadhili kutoka nchini Ujerumani kwa lengo la kuweza kuwakomboa vijana kutoka Tanzania bara na visiwani ambao wameshindwa kujiendeleza na wengine hawana ujuzi wowote.

MGOMBEA MWENZA CCM, Dk. NCHIMBI ATUA MWANZA, KUANZA KAMPENI.


Mgombea mwenza CCM, Dk. Nchimbiatua Mwanza, kuanza kampeniMgombea mwenza wa urais CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi amewasili mkoani Mwanza leo Agosti, 29 tayari kwa kuanza ziara ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu.

Dk. Nchimbi amewasiri katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza majira ya saa 2 asubuhi na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi ( INEC) Dk. Nchimbi leo atafanya mkutano mdogo Kwimba na baadaye mkutano mkubwa Ilemela na Nyamagama.

Akizungumza baada ya kuwasili mkoani Mwanza, Dk. Nchimbi amesema: "Tupo tayari na timamu kuanza kampeni za kuipeperusha bendera ya chama. 

Amesema pia, timu yake ipo tayari kuitangaza na kuitekeleza Ilani ya CCM.

................. ..................

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, kupitia kwa Mwenyekiti wake Comrade Peter John Begga, @begamotabiluteteia kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya, kinapenda kuwataarifu na kuwaalika wanachama na wananchi wote kuwa ijumaa hii ya tarehe 29 Agosti 2025 kuanzia saa 4:00 asubuhi Mgombea Mwenza wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Mheshimiwa Dkt. Emmanuel John Nchimbi atawasili jijini Mwanza. Mapokezi rasmi yatafanyika Kata ya Buhongwa, na baadaye kufuatiwa na Mkutano Mkubwa wa Hadara wa Uzinduzi wa Kampeni za Mkoa utakaofanyika katika Uwanja wa Furahisha. Tunawakaribisha: - Mabalozi na wajumbe wao - Viongozi wa CCM wa Matawi yote 105 - Viongozi wa Kata zote 18 - Jumuiya za CCM (UWT, Wazazi, na Vijana) - Wananchi wote wa Jiji la Mwanza na maeneo ya jirani - Makundi mbalimbali: bodaboda, machinga, mama/baba lishe, wakulima, wafanyakazi, wajasiriamali na makundi maalumu. Njoo usikilize sera za maendeleo – si kelele. #Kazi_iendelee ............................................ KAMA UNAHITAJI KUTENGENEZEWA TANGAZO PIGA SIMU NAMBA 0754074152 JINA ALBERT GEORGE SENGO

Thursday, August 28, 2025

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) TAIFA NDUGU SAMIA AKIZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU 2025

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM )Taifa Ndg Dkt. Samia Suluhu Hassan Akizindua Kampeni ya Uchaguzi Mkuu Tanzania 2025 Kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Katika Viwanja vya Tanganyika Peckers Kawe Dar es Salaam, leo tarehe 28 Agosti 2025.

Wednesday, August 27, 2025

KOKA-NIKICHAGULIWA KUWA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJINI NITALETA CHACHU YA MAENDELEO

 


Victor Masangu, Kibaha

Mbunge mteule  wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) amerejesha leo fomu rasmi  kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge Jimbo hilo na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na madiwani wote ambao wameteuliwa katika kuleta mabadilko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali.

Akizungumza  na wanachama wa CCM pamoja na wananchi pamoja na viongozi mbali mbali ambao wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumsindikiza katika zoezi hilo la urudishaji wa fomu amebainisha kwamba endapo atapata fursa ya kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo ataendeleza  kusikiliza kero na chanagmoto za wananchi na kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Aidha Koka amesema kwamba kwa sasa wanachama wote wa CCM wanapaswa kumpa ushirikiano wa kutosha kwa lengo la kuweza vunja makundi na kushikamana kwa pamoja lengo ikiwa ni kuweza kumpa kura nyingi za kishindo kwa nafasi ya  Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge pamoja na nafasi ya udiwani.

"Nawashukuru sana wana ccm wote  wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kuweza kuniamini na kunipa kura nyingi katika mchakato wa kura za maoni na leo hii nimeweza kupata fursa y kuweza kurejesha fomu  kwa ajili ya kuweza kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kbaha mjini naa kwamba taratibu zote zimekwenda vizuri na fomu zote ambazo zinastahili tayari nimeshazirejesha,"amebaisha Koka.

Aidha amebainisha kwamba kwa sasa hivi kitu kikubwa ni kuhakikisha wanawekaa misingi imara ambayo itaweza kuleta maabadiliko makubwa katika suala zima la kuweza kupata kura nyingi za kishindo katika kuelekea  uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu wa 2025.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Nyamka amesema kwa sasa zoezi la mchakato wa kura za maoni tayari umeshamlizika hivyo wagombea walioshindwa pamoja na wanachama wote kuvunja makundi yote  na kuwa kitu kimoja lengo kubwa ni kuwa na  nguvu ya pamoja ambayo itasaidia kuweza kushinda  kwa kishindo katika uchaguzi mkuu.

Tuesday, August 26, 2025

"SASA NI WAKATI WAKUACHANA NA MATUMIZI YA MKAA NA KUNI" PIKA PIKA KWA NISHATI SAFI.

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

“Kiongozi wa Ubia na Uhusiano wa Mradi wa Masuala ya Nishati Safi kutoka Modern Cooking Energy Services (MECS), Bw. Charles Barnaba, amefafanua umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya umeme kwa ajili ya kupikia, wakati wa mahojiano maalum mapema hii leo ndani ya kipindi cha Mchaka Mchaka, kupitia Jembe FM. . Ametoa elimu hiyo akisisitiza usalama, ufanisi na faida za kiafya zitokanazo na kuachana na nishati chafu majumbani kama vile kuni na mkaa. .
Kiongozi wa Ubia na Uhusiano wa Mradi wa Masuala ya Nishati Safi kutoka Modern Cooking Energy Services (MECS), Bw. Charles Barnaba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Jembe Fm ya jijini Mwanza, Bi. Florencia Peter (katikati) na Dj Eazy (kushoto)

Kiongozi wa Ubia na Uhusiano wa Mradi wa Masuala ya Nishati Safi kutoka Modern Cooking Energy Services (MECS), Bw. Charles Barnaba akizungumza na Jembe Fm.

Bango linajieleza Kiongozi wa Ubia na Uhusiano wa Mradi wa Masuala ya Nishati Safi kutoka Modern Cooking Energy Services (MECS), Bw. Charles Barnaba akimkabidhi zawadi ya Tshirt Dj Eazy wa Kipindi cha Mchakamchaka

@ukintanzania @wizara_ya_nishati_tanzania

MWENEZI MRAMBA ATEMA CHECHE KWA WANA CCM PWANI KUELEKEA KWENYE TUKIO LA UZINDUZI WA KAMPENI ZA KITAIFA

 


Na Victor Masangu,Kibaha

Katibu wa siasa na uenezi na mafunzo  wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani David Mramba amewahimiza viongozi na  wanachama wote kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi tukio kubwa la kihistoria la uzinduzi rasmi wa kampeni ambao unatarajiwa kufanyika Agosti 28 katika viwanja vya Tanganyika Peckars jijini Dar es Salaam.

Mramba ameyabainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho  kuhusiana na uzinduzi huo ambapo amesema kwamba wanachama wanapaswa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuweza kumsapoti Rais Dkt. Samia kwani ameweza  kufanya mambo makubwa  katika suala zima la kutenga fedha kwa ajil ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

" Kwa kweli sisi kama chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani tumejipanga kushiriki kikamilifu katika tukio kubwa la uzinduzi wa kampeni kitaifa ambazo zitafanyika Jijini Dar es Salaam na kwamba kitu kikubwa ninachowaomba  viongozi  na  wanachama wote kujitokeza kwa wingi ikiwa  ni  pamoja na kusikiliza utekelezaji wa Ilani,"amebainisha Mramba.

Aidha Mramba amebainisha kwamba hatowavumilia baadhi ya wanachama ambao wamekuwa na tabia ya kukisaliti chama na kwamba akijatumamwanachama yoyote yule kwenda  kuhamia katika chama kingine cha upinzani.
"Kumekuwepo  na baadhi ya wanachama ambao ni kivuli   na kuamua kukisaliti chama kwa hivyo mimi nawaomba ni lazima kuhakikisha kwamba wanazingatia kanuni na taratibu za chama.

Aidha Mwenezi Mramba wamewahimiza madiwani na wabunge wote katikaMkoa wa Pwani ambao wamepata fursa ya  kuteuliwa ya kuwania nafasi zao kuhakikisha kwamba wanaweka misingi  ya kupeperusha vyema bendera ya chama cha mapinduzi na kumpa kura nyingi za kishindo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.

Monday, August 25, 2025

MWANAMKE ASHIKILIWA KWA TUHUMA KUUA MPENZI WAKE KWA WEMBE.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi

MWANAMKE aitwaye Pendo Medusela (37), mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake, Timithoy Magesa (35), kwa kumkata kwa wembe sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amebainisha hayo leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23, mwaka huu, saa tatu usiku katika nyumba ya wageni ya Bwashee, iliyopo Ndala Manispaa ya Shinyanga.

Amesema kabla ya mauaji hayo, Pendo alipigiwa simu na mwanamke mwingine kwa kutumia simu ya marehemu, akimuonya aachane naye kwa madai kwamba ndiye anayempenda. na baada ya muda Timothy alimtafuta Pendo na kumtaka wakutane katika nyumba ya wageni hiyo, ili wazungumze.

“Hata hivyo, walipokutana walianza kugombana kuhusu mwanamke aliyempigia simu, hali iliyosababisha Pendo kutumia wembe aliokuwa nao na kumkata Timothy sehemu mbalimbali za mwili na kuvuja damu nyingi,” amesema Kamanda Magomi.

Ameongeza kuwa, Timothy amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Kamanda Magomi amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na kueleza kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani, mara baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha, amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi na badala yake kutumia njia za amani kutafuta suluhu pindi wanapokumbwa na migogoro ya kimahusiano.


KAUSHA DAMU IMEWAFILISI WAFANYABIASHARA WENGI JIJINI MWANZA

 ALBERT G.SENGO/MWANZA

WAFANYABIASHARA mkoani Mwanza wamesema kinacho wakwamisha kuendelea kiuchumi, kukuza biashara zao ni kukithiri kwa mikopo yenye riba kubwa ‘mikopo kausha damu’. Wamesema mikopo hiyo huwafanya kushindwa kutekeleza vyema kazi zao hali inayowafanya wengi wao kufilisika na kuwa maskini. Walisema hayo juzi wakati wakizungumza na viongozi na maofisa wa benki ya Equity Bank waliofika jijini hapa kutoa mafunzo ya kuendesha biashara, kukuza mitaji kwa wanawake na wafanyabiashara. Biashara ni Maendeleo! Equity Bank Mwanza inashirikiana na wafanyabiashara kuleta suluhisho za kifedha Equity Biashara Forum, mahali pa mabadiliko. #samiasuluhuhassan #biashara #EquityBankTanzania #EquityBiasharaForum #EquiyInMwanza

ASKOFU MARTIN SHAO AFARIKI DUNIA

Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Martin Shao Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Martin Shao, amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Mhandisi Zebadia Moshi, kupitia taarifa yake aliyoitoa leo (Agosti 25,2025), imeeleza kuwa Askofu Dk. Shao, amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rufani ya Kanda ya KCMC, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dk. Martin Shao, alikuwa Askofu wa awamu ya tatu wa Dayosisi hiyo ya Kaskazini, tangu mwaka 2004 alipochaguliwa kumrithi mtangulizi wake, Askofu Dk. Erasto Kweka (sasa marehemu).

Alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa (PhD), na Chuo Kikuu cha Midland Lutheran College of Nebraska, USA kutokana na uongozi wake uliotukuka na utumishi wa muda mrefu katika huduma za dini.    


GGML WATOA UFADHILI WA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA 932 WA BAJAJI NA PIKIPIKI GEITA

 


KAMPUNI ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) imetoa ufadhili wa programu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa maofisa usafirishaji 932 kitengo cha bajaji na pikipiki ili kupunguza ajali za barabarani wilayani Geita.


Programu hiyo ilizinduliwa Agosti 21, 2025 kwa kuhusisha mafunzo ya awamu ya kwanza kwa washiriki 491 ambao ni maofisa usafirishaji kutoka halmashauri ya manispaa ya Geita.

Mwakilishi wa Meneja Mwandamizi wa Mahusiano GGML, Elibariki Jambau alisema mbali na maofisa usafirishaji, elimu hiyo pia itafikishwa kwenye shule ambazo zitapatiwa mafunzo ya usalama barabarani.

Alisema Kauli mbiu ya programu hiyo ni Uendeshaji Salama Barabarani Unaanza na Wewe ambapo pia itaambatana na utoaji wa viaksi mwanga (reflectors) kwa waendesha bodaboda. 

"Usalama barabarani siyo jukumu la serikali peke yake bali ni la kila mmoja, hii ni zaidi ya kampeni, ni jukumu letu kuchukua hatua kujifunza na kuongeza uelewa kwa changamoto inayotugusa wote.

“Kila ajali barabarani siyo hasara bali ni pigo kwa mstakabari wa Geita na Tanzania kwa ujumla. Hii ndio sababu kubwa ya GGML kushirikiana na halmashauri na jamii katika kutoa, alisema na kuongeza; 

"Tunaamini kwa dhati kabisa kwamba uelewa, nidhamu na uwajibikaji barabarani unaweza kuokoa maisha ya watu, huu ni utamaduni tunaopaswa kuujenga pamoja na kuuishi.

Ofisa Mkuu wa Polisi wilaya ya Geita, Renatus Katembo alikiri kuwa program hiyo itaimarisha usalama barabarani kwani ni wazi kwamba waendesha bodaboda na bajaji wamekuwa chanzo kikubwa cha ajali.

“Hili kundi ni muhimu sana likapata elimu ya matumizi bora ya barabara, takwimu zinaonyesha kwamba bajaji na bodaboda wanapata sana ajali, inawezekana na kujisababishia au za kusababishwa.

Katembo alitaja changamoto kubwa ya bajaji na bodaboda ni kuvunja sheria za barabarani kwa kusimama bila utaratibu, kutembea kwa mwendo mkubwa pamoja na kubeba abiria zaidi ya uwezo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Bodaboda mkoa wa Geita, Fred Fidel aliishukuru GGML kwa program hiyo na kueleza kuwa ni njia sahihi kuwaongezea bodaboda uelewa ili wawe mabalozi wa usalama barabarani.

Fidel aliiomba GGML kupanua uwigo wa mafunzo hayo kwenye wilaya zote mkoani Geita ili kuwafikia waendesha bodaboda wtakribani 30,000 ndani ya mkoa mzima wa Geita.

Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Bajaji mkoa wa Geita, Mussa Kisoke aliiomba serikali kupitia Wakala wa Barabara Nchini(TANROADS) kuboresha alama za barabarani na maeneo ya maegesho ili kuweka mazingira rafiki kwa wasafirishaji.

Sunday, August 24, 2025

YANGA SC YAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-1 MECHI YA KIRAFIKI MWENGE

 

TIMU ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo na beki Aziz Andambwile Mwambalaswa ambaye pia alijifunga kuwapatia bao la kufutia machozi Fountain Gate.

Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima kwa Yanga katika maandalizi ya msimu mpya chini ya benchi jipya la Ufundi, baada ya awali kuifunga Rayon Sports ya Rwanda 3-1 wiki iliyopita Jijini Kigali Kigali – mbali na ule ambao walishinda 4-0 dhidi ya wadogo zao, U20 hapo hapo KMC Complex.

Yanga SC inatarajiwa kuuanza msimu kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Simba SC Septemba 16 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Lakini Yanga inaweza kuwa na mchezo mwingine mkubwa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi Septemba 12 hapo hapo Uwanja wa Mkapa.
Benchi jipya la Ufundi Yanga lipo chini ya Kocha Mkuu, Mfaransa Romain Folz na Msaidizi wake, Mspaniola Alejandro Manu Rodríguez Lázaro na Kocha wa Makipa, Majdi Mnasria.
Wengine ni Mtaalamu wa Viungo (Physiotherapist), Youssef Ammar wote kutoka Tunisia, Kocha wa Physic, Tshephang ‘Chyna’ Mokaila kutoka Botswana, Mchambuzi wa Video, Thula Bantu na Mkurugenzi wa Ufundi, Paul Matthews wote raia wa Afrika Kusini.

MUHEZA YAIGARAGAZA BUMBULI MAGOLI 3-2 MICHEZO SHIMISEMITA




Na Oscar Assenga,TANGA

TIMU ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri  ya Wilaya ya Muheza imebamiza Halmashauri ya wilaya ya Bumbuli mabao 3-2 katika michuano ya Shirikisho la Michezo la Mamlaka za Serikali za Mitaa kaika mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya Shule ya Ufundi Tanga.

Shirikisho hili la Michezo linahusisha watumishi waliopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ( Halmashauri) waliopo kwenye idara na vitengo mbalimbali.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu kutaka kupata ushindi lakini Halmashauri ya wilaya ya Muheza iliweza kuhimili na kuutawala vyema mchezo huo na hatimaye kuweza kuibuka na kidedea
Mashindano ya Shirikisho la Serikali za Mitaa Tanzania ( SHIMISEMITA) yalianza rasmi Agosti 15, 2025 na yanatarajiwa kukamilika Agosti 29, 2025 huku yakilenga kuwakutanisha watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kushirikiana pamoja, kufahamiana, kubadilishana mawazo, kujenga Afya za watumishi ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo kisukari na shinikizo la damu.
Michezo hii inaendelea katika Viwanja mbalimbali vya Michezo vilivyopo Jijini Tanga huku yakiwa yamebeba Kauli mbiu ya SHIMISEMITA 2025  " Jitokeze kupiga Kura kwa maendeleo ya Michezo".

MAONESHO YA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI KUANZA AGOSTI 29, 2025 MWANZA

Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kuanza Ijumaa Agosti 29,2025 hadi Jumapili Septemba 07, 2025 katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Maonesho hayo huandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) ambapo kwa mwaka huu ni ya 20 tangu kuanzishwa.

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene amesema maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene akitoa taarifa kuelekea Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu 2025.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene akitoa taarifa kuelekea Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu 2025.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene akitoa taarifa kwa wanahabari Ijumaa Agosti 22, 2025 kuelekea Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu 2025 yanayotarajiwa kuanza Ijumaa Agosti 29, 2025 uwanja wa Nyamagana.