NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo pamoja na kutaja vipaumbele 12 vya chama chake iwapo kitapewa ridhaa ya kuunda Serikali baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, huku akiahidi mageuzi makubwa katika sekta za afya, elimu, ajira na maslahi ya wafanyakazi. Pamoja na hayo amejibu maswali ya waandishi wa Habari kuhusu kwanini wao kama chama kikongwe nchini Tanzania, hawakuungana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA) ambao uliunda UKAWA kusimama kwenye msimamo wa "No Reforms No Elections"..... Gombo amesema CUF imeamua kuanzia Mwanza kwa sababu ni mkoa wa kimkakati kisiasa na kwamba yeye mwenyewe ni mzawa wa eneo hilo. #uchaguzimkuu2025Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment