ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 25, 2016

KESSY ATACHEZA DHIDI YA MAZEMBE? TFF IMETOA UFAFANUZI

Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia msemaji wake, Alfred Lucas limesema kuwa, linashughulikia sakata la uhamisho wa mchezaji Hassan Kessy Ramadhani kutoka Simba kwenda Yanga ili aweze kucheza kwenye mchezo wa kimataifa kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumanne June 28 kwenye uwanja wa taifa.

“Tayari Yanga wameshaandika barua imekuja TFF wakiomba suala la Kessy liweze kumalizwa haraka ili waweze kumtumia kwenye mchezo wao wa Jumanne dhidi ya TP Mazembe,”amesema Alfred Lucas afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania.

“Niwahakikishie mashabiki wa Yanga kwamba TFF weekend yote hii kwa maana ya leo Jumamosi na Jumapili tutalifanyia kazi hilo na tayari mawasiliano yameshafanyika ili Yanga waanze kumtumia mchezaji huyu mara baada ya mkataba wake kuisha.”

“Lakini kama kuna kikwazo chochote tunajaribu kufikiria ili Yanga wawe huru kusiwe na dosari yeyote kwenye michuano hii halafu sababu ikawa ni kuwakosa wachezaji wake wote iliyowasajili kwa ajili ya michuano hiyo.”

“Naamini kwa uungwana waliokuwa nao Simba kama kuna kikwazo watakiondoa ili mchezaji huyo aendelee kipaji chake na maisha mengine yaendelee.”

Kessy hakuruhusiwa kucheza kwenye mchezo wa kimataifa kati ya Yanga dhidi ya MO Bejaia kwasababu kibali chake kutoka Simba kwenda Yanga kilikuwa hakijathibishwa.

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA HUENDA IKASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UTENGENEZAJI MADAWATI

Na EmanuelMadafa,Jamiimojablog


Halimashauri ya jiji la Mbeya huenda ikashindwa kutekeleza  agizo la Rais John Pombe Magufuri, lililozitaka halmashauri  kuhakikisha zinamaliza tatizo la uhaba wa madawati shuleni ifikapo Juni 31, mwaka huu kutokanana kutokuwepo kwa msukumo wa kutosha katika  utekelezaji wa agizo hilo.



Halmashauri ya Jiji la Mbeya, imeweza kutengeneza na kukamilisha madawati 1500, wakati uhitaji ni madawati 10,000.

Katika upungufu huo, shule za msingi zinauhitaji wa madawati 9894, wakati sekondari zikihitaji madawati 605.



Akizungumza wakati wa hafla ya   uzinduzi  wa mradi wa utengenezaji wa madawati katika chuo cha ufundi VETA jijini Mbeya , Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Mussa Mapunda, alisema katika madawati hayo 1500 ambayo tayari yamekamilika, madawati 798 ni ya shule za msingi huku madawati 477.



Alisema, kupatikana kwa madawati hayo 477 kwa shule za sekondari halmashauri itakuwa imemaliza deni kwa upande huo na kubaki na deni la madwati 9096 kwa shule za msingi ambao nayo yapo katika mchakato wa kukamilika.



Akizungumza na baadhi ya wananchi wakiwemo wanafunzi, madiwani na watumishi wa serikali, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi, alisema madawati 9096 ambayo yanahitajika katika shule za msingi yapo katika mchakato wa kukamilika.



Aidha, Meya huyo alisema, licha ya halmashauri hiyo kukabiliwa na changamoto ya rasilimali fedha lakini imeweza kufanya kazi hiyo kwa haraka hasa ukiangali ni kipindi kifupi tu, tangu kuungua moto kwa mabweni zaidi ya mawili ya shule ya sekondari ya iyunga na kuteketeza vitanda 150 na magodoro yake.



“Ninawashukuru wadau kwa kujitolea kwani wakati wakichangia shule ya Iyunga, suala la madawati nalo likaingia hivyo ninaamini kwamba halmashauri itaweza kukamilisha tatizo la madawati na wanafunzi wote kuondokana na tatizo la kukaa chini,”alisema.


Friday, June 24, 2016

UNAWEZA KUSTUKA KUSIKIA PAUL POGBA NA MESUT OZIL WAGUSWA NA MTOTO WA KITANZANIA


Paul Pogba na Mesut Ozil wanafanya zaidi ya shughuli mbili katika msimu huu wa michuano ya Euro mwaka 2016 huku Tanzania ikitajwa.
Kama nyongeza katika kung'arisha Nyota zao msimu huu wa kiangazi mmoja akiwakilisha Ufaransa huku mwingine Ujerumani kwenye michuano ya European Championship, wachezaji wote wawili wanarejesha kwa jamii yenye uhitaji duniani na wote kila mmoja akigharamia Afya ya upasuaji kwa watoto 11, katika Bara la Afrika.

Mungu ni mkubwa Oparesheni hiyo imemwaga neema kwa mtoto wa Tanzania who have suffered from serious burns or a club foot. The players are sponsoring the surgeries in league with charity BigShoe11, who are on the lookout for 11 international players to work with them during Euro 2016.

Sikiliza LIVE sasa @jembefm #SPORTSRIPOTI ina mzigo kamili ukiwa na @elikanamathias @jumaayoo featuring sports lady @nattyebrandy nami @gsengo kwa mbaaali 📻ijumaa ni saa 2 3 CC:-@jembenijembe @dvjfrank @deejaykflip


The surgeries are for children with burn injuries and club foot – prevalent issues in developing and newly industrialised countries.

BigShoe began at World Cup 2006, when the Togo national team got together to fund a young Togolese girl’s operation.

HIZI HAPA SABABU ZA TANZANIA KUFUNGUA UBALOZI NCHINI ISLAEL BAADA YA KUKATA MAHUSIANO YAKE HAPO NYUMA.

Hizi hapa sababu zilichangia ubalozi wa Tanzania kufungua ubalozi wake nchini Israel baada ya kukata mahusiano yake hapo nyuma. 

KAMPUNI YA BIA SERENGETI YAZINDUA MRADI WA MAJI WA m/- Katesh, Hanang


Mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha akizungumza na wananchi wa katesh wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wenye uwezo wa kuhudumia wakazi wapatao 12000 katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang ,mkoa wa Manyara.

Diwani wa Kata ya Gidahababieg,Hassan Hilbagiroy akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata hiyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Gidahababieg,Katesh akifurahia maji mara baada ya ufunguzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Thobias Mwilapwa akiwa na picha ya pamoja na wananchi mara ya baada ya ufunguzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang mkoa wa Manyara.



Hanang, Juni 22, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang’ ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.

Mradi huo wenye uwezo wa kuwahudumia watu 12,000 unajumuisha kisima kilichochimbwa pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ukiwa na uwezo wa kuzalisha  lita 45,000 za maji kila baada ya saa sita.

Akizungumza latika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha,  alisema kuwa kisima hicho ni mkakati wa kampuni hiyo ya bia wa kuisaidia jamii chini ya mpango uitwao Maji ya Maisha na kuongeza kuwa SBL imeshatekeleza  miradi kama hiyo katika mikoa ya   Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma  ambayo imenufaisha watu zaidi ya milioni moja kwa kuwapatia maji safi na salama.

Wanyancha alisema kuwa mradi wa Katesh  sio tu kwamba utaboresha afya za wenyeji wa eneo husika bali pia utaongeza uzalishaji  kiuchumi “hususani miongoni mwa wanawake na watoto wa kike  ambao hawatalazimika kutumia saa nyingi   kutafuta maji sehemu nyingine. Hii inatoa fursa kwa watoto wa kike kuhudhuria masomo shuleni.”

“Kampuni ya Bia ya Serengeti ina sera iliyojikita katika kuleta ustawi wa jamii ambapo Maji ya Uhai ni mojawapo ya maeneo manne iliyoyapa kipaumbele. Maeneo mengine utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuhimiza Unywaji wa pombe Kistaarabu.

Mkurugenzi huyo wa mahusiano aliongeza kuwa SBL  ina programu ya kilimo  ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imewasaidia  wakulima zaidi ya 100  hapa nchini kwa kuwapatia misaada ya kitaalamu na kifedha ambapo imewasaidia  kuboresha maisha yao pamoja na maisha ya jamii zao.

Aidha Wanyancha aliongeza: “Kupitia mpango huu wa kusaidia SBL imeweza kuongeza upatikanaji wa shayiri inayotumika kama malighafi katika utengenezaji wa bia kutoka tani sifuri 10,000 jambo ambalo limechochea ukuaji wa kasi wa kampuni yetu.”

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Tobias Mwilapwa  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameipongeza kampuni ya SBL kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidi miradi ya kijamii nchini jambo ambalo amesema ni chachu katika kuiletea jamii maendeleo.

“Licha ya  kuchangia katika  kukua kwa uchumi wa taifa  kupitia malipo ya kodi kwa wakati, kampuni ya Serengeti  imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa  hususani katika uzinduzi wa huduma za miradi ya maji safi na salama  nchini,” alisema.

HUU NI UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO JUNE 24, 2016


Huu ni uchambuzi wa habari za magazeti ya leo June 24, 2016.

SIMU.tv: Atakayempa mwanafunzi mimba jela miaka 30, NMB yajitoa malipo wastaafu hewa, Mafuriko ya kisiasa marufuku hadi 2020. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa

Magufuli awajibu Jenerali na Gwajima, Millya amjia juu Tulia, JPM asema Nitawalinda marais wastaafu, UKIMWI kupimwa nyumba kwa nyuma. Pata undani wa magazeti ya leo hapa 


Wanaokosoa marais wastaafu ni wapuuzi, Zitto amjibu rais Magufuli, Risasi zarindima Zanzibar watatu wajeruhiwa. Pata undani wa dondoo hizi hapa. 

MKUU WA MKOA WA MWANZA ALIPOPATA FURSA KUKARIBISHA WAGENI WALIOHUDHURIA MKUTANO MKUBWA WA INJILI WA REINHARD BONNKE LIKIHUBIRIWA NA DANIEL KOLENDA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela Alhamisi ya tarehe 23 mwezi juni katika uwanja wa Furahisha Kirumba jijini Mwanza amewakaribisha wageni wote na wenyeji kuzitumia vyema fursa zipatikanazo ndani ya mkoa wake, huku akiwahimiza wananchi hao kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kuilinda amani ya familia na nchi kwa ujumla.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akizungumza na kusanyiko la Mkutano wa Injili la Reinhard Bonnke linaloratibiwa na Umoja wa Makanisa Mwanza na kuhubiriwa na mhubiri wa Kimataifa toka nchini Ujerumani Daniel Kolenda.
Ummati uliofurika katika viwanja vya Furahisha kirumba jijini Hapa kwaajili ya kulishwa neno.
Kamati ya maandalizi iliyoundwa na wachungaji na maaskofu kutoka Umoja wa Makanisa mkoa wa Mwanza ikiwa jukwaa kuu na Muhubiri wa Kimataifa Daniel Kolenda wa tano kutoka kushoto.
Sehemu waliyoketi waratibu wa mkutano.
Kusanyiko katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akipongezwa na mtumishi wa Mungu mara baada ya kuzindua kusanyiko.
Kuna salamu iliyoendelea toka jukwaa kuu ambayo iliwavutia wengi...ambayo iliambatana na kushangaa juu ya ukuu wa Mungu, ni Muhubiri Daniel Kolenda na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela!!
Kusanyiko lilipunga mkono kuashiria kushangilia.
Kona na kona viwanja vya Furahisha kusanyiko la Mkutano mkubwa wa Injili wa Reinhard Bonnke unaohubiriwa na Daniel Kolenda kutoka nchini Ujerumani.
Amen
Usikivu ni kwa asilimia 100.
Injili inapenya ndani ya kusanyiko hili litakalodumu kwa uda wa siku tatu mfululizo kiliele kikiwa siku ya jumapili ya tarehe 26 June 2016.

Thursday, June 23, 2016

KAMPUNI YA TOMONI FARMS LIMITED YAFUNGUA DUKA NA MGAHAWA WA KISASA WA MAZAO YA KILIMO DAR

DSC_8013
Willybroad Alphonce.
Muonekano wa nje unavyoonekana katika duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani.
Kampuni ya Tomoni Farms Limited, inayomilikiwa na wazawa, wakijishughulisha na Kilimo cha umwagiliaji cha mazao ya Matunda na Mbogamboga, wamefungua duka na Mgahawa wa Kisasa kwa ajili ya uuzaji wa mazao yao katika hali ya usafi na usalama wa hali ya juu uliopo eneo la jirani na Victoria, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Jijini Dar Es Salaam, wakati wa utambulisho wa duka hilo na shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ya Tomoni Farms Limited, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni hiyo Bwana Franklin Bagalla ameeleza kuwa, wameamua kuwasogezea watanzania bidhaa bora za kilimo ambazo watazipata moja kwa moja kupitia duka lao hilo na watajiona kama wapo shambani ama bustanini kwa namna ya uwekezaji wao walivyoweza kuuandaa ikiwemo mazingira safi na utunzaji wa kisasa kutoka shambani hadi kumfikia mlaji.
“Baada ya kuwekeza kwa miaka mine katika kilimo cha Matunda na Mboga mboga kwa kutumia teknolojia ya umwagiliaji, huku tukiwa na uhakika wa kutoa mazao Mwaka mzima, sasa tumewekeza katika miundo mbinu ya kuhakikisha mazao yetu yanawafikia walaji yakiwa katika hali ya usafi na usalama. Hivyo kupitia katika duka letu hili la kisasa hapa Dar es Salaam linatoa fursa kwa wananchi kujipatia bidhaa za kila aina na watazipata kwa hali ile ile kama zipo shambani na tunawakaribisha sana” alieleza Bwana Bagalla.
Aliongeza kuwa, Mazao yote yanavunwa na kusafirishwa katika magari maalumu kutegemea na uhitaji wa mazao hayo, na hupokelewa, kuchambuliwa na hatimaye kuhifadhiwa katika jokofu kubwa la baridi kuhakikisha kwamba ubora wa bidhaa unabakia kama ule wa shambani na baada ya hapo bidhaa hizo huuzwa kupitia duka hilo la kisasa na zingine hutumika katika mgahawa wao ambao pia unatengeneza aina mbali mbali za Juice nzito na nyepesi ambazo mara nyingi wataalam wa Afya wanashauri watu kutumia.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo ya Tomoni Farms Limited, Bwana Willybroad Alphonce amesema kuwa katika kufikia malengo na uendeshaji wameweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha cha Zaidi ya Bilioni moja.
Na kuongeza kuwa, wakiwa miongoni mwa Watanzania wazawa, wamewaomba watanzania kuwaunga mkono kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia mkulima aliyoko kijijini ambaye bidhaa zake zinaharibika huku mijini zikihitajika kwa wingi, kwani licha ya wao kuendesha shughuli za kilimo pia wamekuwa wakinunua baadhi ya mazai kutoka kwa wakulima wengine ikiwa tu na lengo la kusaidia soko hasa la ndani.
“ Wateja watakao fika dukani kwetu watajipatia vitu mbalimbali. Ni wakati muafaka sasa kuchangamkia fursa hii ya bidhaa za mashambani ambazo zinatoka kwenye ardhi yetu ya nyumbani yenye rutuba za kutosha na uhifadhi wa hali ya usafi na usalama kwa mlaji.
Tunawakaribisha wote wanaotambua umuhimu wa kupata lishe bora kupitia matunda na mboga mboga huku tukiwasisitiza wale wote wenye watoto kuhakikisha wanawaleta pale Farm Fresh Bar waanze kuzoea toka mapema kuchangamana katika Bar zenye manufaa Kiafya” alimalizia
Tomoni Farms Limited inaendesha duka hilo la kisasa la mazao ya shambani, pia ina mgahawa na Bar maalum ambayo inahudumia bidhaa za matunda pekee ikiwemo juice za kila aina pamoja na masuala yote ya vyakula vya mboga mboga ambavyo ni vya asili.
DSC_8003 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani wakati wa utambulisho wa tukio hilo mapema leo Juni 23.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana 
DSC_8045
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akifafanua jambo ndani ya duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani
DSC_8047
Baadhi ya bidhaa zinavyoonekana ndani ya duka hilo.
DSC_8049 DSC_8057Baadhi ya mbogamboga za aina mbalimbali zikiwa zimehifadhiwa katika vifaa maalum
DSC_8059
DSC_8071
Sehemu ya mchele na bidhaa zingine za nafaka zinazopatikana katika duka hilo.
DSC_8065sehemu ya matunda
DSC_8077 DSC_8089
Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya maboga bidhaa zinazopatikana dukani hapo.
DSC_8081
Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha mboga mboga za aina mbalimbali zinazopatikana dukani hapo.
DSC_8097Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha bidhaa maharage ya aina tofauti dukani hapo.
DSC_8099
DSC_8096Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za kalanga dukani hapo.
DSC_8085 DSC_8093 DSC_8094 DSC_8117baadhi ya bidhaa zikiwa kwenye jokofu maalum zinapohifadhiwa.
DSC_8121Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akionyesha wanahabari (Hawapo pichani) bidhaa mahala zinapohifadhiwa katika jokofu maalum la matunda na mboga mboga.
DSC_8136Baadhi ya wanahabari na wadau wakijadiliana jambo nje ya kamouni hiyo ta Tomoni Farms Limited.
DSC_8148 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akiwa nje ya Bar maalum ya masuala ya matunda halisi pamoja na mbogamboga
MatataG_4336Nje ya duka hilo la kisasa linavyoonekana lililopo katika jengo la Green House, eneo la jirani na Victoria, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).