ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 4, 2010

MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI YAFANA.

Fainali za mashindano ya mitumbwi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager zimefanyika leo katika fukwe za mwaloni jijini Mwanza, washindi kupatikana na kukabidhiwa vitita vya zawadi.

,Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Fimbo Butallah amesema, Ni zaidi ya miaka mitano sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki mafanikio yameonekana, licha ya kutoa burudani washiriki wameweza kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa matarajio ya baadaye kuyafanya mashindano yawe sehemu ya utalii.

Mashindano hayo ya kupiga kasia ambayo leo yamefikia tamati, yameshirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe, huku yakiendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Washindi vinara kwa upande wa wanaume ni kutoka mkoa wa kagera hapa ni pale walipofika ukingoni.

SUGUA KISIGINO!!! Bendi maarufu ya muziki wa Dansi ya African Stars (Twanga Pepeta) wakitoa burudani ya aina yake kwa mashabiki katika fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi jijini Mwanza.

AAaaah! Balimi inashuka safi ukipiga ndizi na nyama choma.

Mabadiliko ya hali ya hewa yakiambatana na mvua kali katikati ya mashindano hayakubadili chochote ngoma ilisongeshwa, ile hali kwa mashabiki ilikuwa hakuna kutoka mtu.

"Hii mvua ni ya mtu!!" Mr. Msangi akiteta na wadau wenzake wa TBL katikati ni Editha Mushi meneja wa mawasiliano na mahusiano wa kampuni hiyo.

Kikundi cha ngoma asili toka ukerewe nacho kilialikwa kutia nakshi mashindano, Wanakatika haoOOO!!

Palikuwa hapatoshi kwani watu walimiminika haswaa.

Kapteni wa Washindi wa kwanza wanaume Thobias Kaichum Toka bukoba akichukua zawadi sh milioni mbili na nusu.

Kapteni wa Washindi wa kwanza wanawake Salome Ernest toka bukoba akichukua zawadi sh milioni mbili, nafasi ya pili Mwanza ikachukuwa milioni mbili, nafasi ya tatu ikaenda Ukerewe nao wakakamata kitita cha milioni moja na nusu.

Kapteni wa Washindi wa pili wanawake Yunus Lewis toka Ukerewe akikabidhiwa kitita cha sh milioni moja na nusu, nafasi ya 3 ilichukuliwa na washiriki toka Mwanza laki saba na nusu, nafasi ya 4 ilikwenda Ukerewe laki tano,huku nafasi ya 5 ikienda tena Bukoba laki mbili.

Dj Ommy jr akinogesha Shughuli ndani ya Mashindano hayo yaliyoanza saa 3 asubuhi na kumalizika majira ya jioni, yalishirikisha timu tano toka kila kituo kilichoshiriki ngazi ya awali toka mikoa ya yote mitano ya kanda ya ziwa.

Friday, December 3, 2010

"MENU YA STONE CLUB WIKI NI NOUMAa!!!"

MWEZI BADO MBICHI NA NAJUA BADO MNAZO.
IJUMAA NA JUMAMOSI KANBAAAaa!
ONCE AGAIN THA SAGA CONTINUE TONIGHT PALE CHIMBO LA KATI NAZUNGUMZIA 'STONE CLUB'
ITALETA MAANA ZAIDI UKIJUMUIKA NASI!!!!!!
GATE PASS NI 5,000tsh.

URUSI KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2018

Shirikisho la soka duniani, Fifa, limetangaza Urusi kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2018, baada ya kuzishinda nchi za England, Ureno na Uhispania, na Uholanzi na Ubelgiji.

Aidha Qatar nayo imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Nchi nyingine zilizokuwa zikiwania nafasi hiyo ni Australia, Marekani, Japan na Korea Kusini.

Kwa mara ya kwanza katika historia, mashindano hayo ya kombe la dunia yanakwenda kufanyika nchini Urusi, Captain wa timu ya taifa hilo Andrey Arshavin ambaye pia hukiputa katika timu ya Arsenal, huku akishangilia, aliruka kwa furaha toka katika kiti alichokuwa amekaa akimpa mkono kila aliyekutana naye kuonyesha furaha yake ambayo ilikuja kama zali la mentali.

"Nina furaha kubwa, kwasababu hili ni tukio kubwa kwetu. Hakuna anayeelewa tukio hili lina maana gani kwa nchi yangu. Lakini ninaamini mara baada ya 2018 watu watatuelewa nini tunamaanisha." Kauli yake Arshavin.

CECAFA TUSKER CHALLANGE CUP ETHIOPIA YAINYUKA KENYA 2-1.

Mchezaji Timu ya Kenya akijitahidi kwa udi na uvumba kuwatoka mabeki wa Ethiopia lakini wapi, Kenya ikabamizwa goli 2-1 hadi kipyenga kinalia.

Wadau kulia Adam Mossi pamoja na mkurugenzi wa Zizzou Fashion, Othman Tippo wakifuatilia kwa makini kandanda safi iliyokuwa ikichezwa kati ya Kenya na Ethiopia.
HABARI KAMILI TEMBELEA MICHUZI JR.

Thursday, December 2, 2010

TAFAKARI YA LEO, NAMALIZIA HIVI.......

NAITWA 'NYANI MZEE'- NAJUA NDANI YA MSIMU HUU WA MWISHO NCHANI MWA 'NOVEMBA NOMA' UMEMMISI MAMBO YA NYANI MWEZANGU B(...)E, BASI KAMATA HII!

'AFRIKA YAWEZA KUJILISHA'

AFRIKA INA UWEZO WA KUJILISHA YENYEWE NA PIA IKAZALISHA CHAKULA CHA KUTOSHA KUUZA NJE.KILIMO.
Hayo ni kwa mujibu wa kitabu kipya kilichozinduliwa hii leo na professa wa chuo kikuu cha Havard Calestous Juma. Kitabu hicho 'The New Harvest' kinatoa wito kwa viongozi wa Afrika kutilia mkazo upanuzi wa kilimo kupitia sera na mikakati yao ya kitaifa.

Kuafikia hilo, viongozi wa Afrika watahitaji kuboresha miundo mbinu, kutumia teknologia ya kisasa pamoja na kuhimiza kilimo cha mazao ya kufyatua kisayansi, yaani GM.

Ripoti hiyo itawasilishwa kwa viongozi wa Afrika siku ya Ijumaa mjini Arusha katika mkutano unaofanyika ndani ya hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge nchini Tanzania, ambapo Marais wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanafanya kikao kuzungumzia usalama wa chakula pamoja na suala la mabadiliko ya hali ya anga.

Professa Juma alisema viongozi wa Afrika hawana budi kutambua uhusiano wa kilimo na uchumi wa Afrika. ''Ni jukumu la viongozi wa Afrika kuuboresha uchumi wao na hiyo inamaanisha kuanza kutumia teknonologia ya kisasa katika kilimo''.

Kwa mujibu wa Professa Juma, uzalishaji wa chakula duniani unaendelea kuongezeka lakini katika maeneo mengi ya Afrika hali ni tete licha ya kuwepo na ardhi ya kutosha ya kilimo.

PIGA KURA SASA FILAMUCENTRAL BORA ZA 2010.

Muda umewadia kwa wapenzi wa filamu kuweza kuthibitisha BORA ZA 2010. PIGA KURA kuchagua wale Bora wa 2010 kupitia www.filamucentral.co.tz

MAKUNDI YA FILAMUCENTRAL BORA ZA 2010.

Msanii chipukizi wa mwaka
Muigizaji bora wa kike
Muigizaji bora wa kiume
Mwandishi bora wa Mswaada
Mchekeshaji Bora
Filamu Yenye Kava bora
Mtayarishaji bora wa filamu
Kampuni bora ya utengenezaji filamu
Msambazaji Bora
Muongozaji Bora

ILI UWEZE KUCHAGUA TEMBELEA
http://www.filamucentral.co.tz/bora-za-2010/

WE-WE-CHINI YA ULINZI......!!!

Vuta nikuvute hii ilitokea jumamosi iliyopita pale mtanzania huyu mwenye asili ya Asia mwenye (pikipiki no hizo....) alipotoa lugha chafu na kejeli kwa walinda usalama wa moja ya benki hapa Mwanza, kisa na mkasa - kuzuiwa kuingia ndani ya benki kupata huduma kwani muda ulikuwa umekwisha wa kutoa huduma.
Wakati akielezwa kuondoka eneo hilo raia huyo alimsukuma mmoja wa askali polisi, kiasi cha askari huyo kupoteza balansi na kuangusha silaha aliyokuwa kaitundika begani. Wewee!.. mbona kikamgeukia, ikawa seleka..... Mara baada ya hapo jamaa akaarestiwa kwenye chumba maalum kwa mahojiano ..... na sikujuwa kilichoendelea.

MEMORIAL TREE.

MEMORIAL TREE WHICH IS FOUND IN MWANZA TANZANIA.

MEMORIAL TREE.
Used by Germany colonial rulers to hang criminals during the period of 1890 - 1918.

Wednesday, December 1, 2010

GADNA AJIENGUA CLOUDS FM!!

MTANGAZAJI MAHIRI WA KIPINDI CHA JAHAZI KINACHO RUSHWA KILA SIKU JIONI SAA YA 10 HADI 12 KAMILI KUPITIA REDIO YA WATU CLOUDS FM AMEAMUA KUJIENGUA KWA SABABU AMBAZO AMESEMA NI ZA KUTAKA KUJARIBU UJASIRIAMALI BINAFSI.Uongozi wa CLOUDS FM umethibitisha habari hizo na kwamba kesho tarehe 2DEC.2010 utatoa tamko rasmi siyo tu kwa kuondoka GADNA ambaye alijulikana kama KEPTEEEEEIN!!na kumechi vilivyo na mtangazaji mwenzie KIBONDE katika kipindi pendwa cha jioni ambacho huwapa kampani sana watanzania kote inapofika redio hiyo.

Awali kabla ya hatua hiyo ya Gadna mtangazaji wa kike SOPHIA KESSY nae alitangaza kuvunja ndoa baina yake na kipindi cha Afrika Bambataa na kusema kuwa ameamua kujitosa kwenye majukumu mengine bila kufafanua kama ilivyo kwa Gadna ambaye pia hajafafanua juu ya ujasiliamali anaokwenda kudil nao.

"Habari za Gadna ni za kweli, ameondoka, hayo mengine tutayaweka bayana kesho tutakapotoa tamko rasmi wa jinsi tunavyo jiandaa na mambo mapya ya mabadiliko". Alisema mmoja wa wakurugenzi wa CLOUDS MEDIA, bwana RUGE MUTAHABA.

DUH NOVEMBER NI NOMA!!!

MAAFALI YA MADAKTARI WETU YAJA.......!!!!

KUTOKA KUSHOTO MR.R.TIBAIJUKA, MKUU WA CHUO PROF. J.P MTABAJI NA PROF. W.MAHALU.
Chuo kikuu kishiriki cha sayansi za afya Weill Bugando cha chuo kikuu cha mtakatifu Agustino Tanzania jumamosi ya tarehe 4Desemba2010 kinataraji kufanya maafali yake ya tatu kutunukisha stashahada na shahada.
UONGOZI WA CHUO NA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI.
Maafali hayo yatatanguliwa na kongamano la wafanyakazi na wanafunzi wote linalofanyika leo trh 1 Nyumbani hotel ambapo mada mbalimbali zitatolewa. Na tarehe 3 pambano la soka baina ya Wafanyakazi na Wanafunzi.

WAANDISHI WA HABARI NA KIFUNGUA KINYWA.
Tatizo la uhaba wa madaktari NCHINI limekuwa sugu kwa muda mrefu kutokana na wazazi wengi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama kubwa kuwasomesha vijana wao masomo hayo amabyo yanakadiriwa kufikia kiasi cha SHILLINGI MILLIONI 25 HADI 50 ILI KUWA DAKTARI KAMILI.

Mgeni rasmi wa maafali hayo atakuwa Mhashamu askofu mteule JUDE THADEUS RUWA'AINCHI. Chuo cha Bugando kimejitenga toka SAUTI kutokana na kuwa na uwezo wa kujilea, na kimeingia katika mchakato huo ili kujikita zaidi ktk fani ya tiba. Mwaka 2010 utakuwa wa kipekee kwa chuo hicho kwani vimeongezeka vitivo toka kimoja na kuwa vitano.

BAADA YA REAL MADRID KULIZWA RUNGU 5 NA BARCELONA, MOURINHO AKATAA TIMU YAKE KUFEDHEHESHWA.

USHABIKI KAZI.
Meneja wa Real Madrid Jose Mourinho amekanusha kwamba timu yake ilifedheheshwa na Barcelona baada ya kushindiliwa mabao 5-0 katika uwanja wa Camp Nou. Mabingwa wa Hispania Barca walicheza katika kiwango cha juu walipoisambaratisha Madrid katika mchezo wa kwanza wa El Clasico kwa Mourinho tangu aanze kuifundisha Madrid.

"HABARI YAKE BHANA!!"
Alisema:"Timu moja ilicheza katika kiwango chake na nyingine haikucheza vizuri. "Kupoteza sawa tumepoteza, lakini kufedheheshwa hapana. Ilikuwa sahihi kupoteza mchezo ule, kwa sababu hatukucheza vizuri. "Nimezungumza na wachezaji wangu na nimewaambia msimu haujamalizika. Aliuliza: "Nani ajuaye kitakachotokea mwaka huu?"

Mourinho, ambaye katika ufundishaji wake wa soka ya kulipwa hajawahi kuongoza timu iliyowahi kufungwa hata mabao manne kwa bila, amesema dakika 90 za mchezo na Barcelona hazikuonesha makali ya kweli ya Madrid. Aliongeza:"Sidhani kama matokeo ya mechi ile yanaonesha tofauti ya wazi baina ya timu hizi mbili. "Na pia mbio za ubingwa hazijamalizika leo.

PEP GUARDIOLA.
Kwa upande wa Pep Guardiola, ambaye ameshinda kwa mara ya tano El Clasico tangu awe meneja wa Barcelona, amesema amefurahishwa sana kuona namna timu yake ilivyocheza katika kiwango cha juu na kuangaliwa na mamilioni ya wapenda soka duniani kupitia televisheni zao wanaokisiwa kufikia milioni 400. Alijigamba: "Ningependa kuzoa pointi nyingi zaidi dhidi ya Madrid lakini hilo haliwezekani.

Tuesday, November 30, 2010

MAMA HASHEEM THABEET AKABIDHI MSAADA KWA TIMU ZA BASKETBALL MWANZA.

ERNEST RICHARD WA BUGANDO WORRIOUS AKIPOKEA MSAADA WA JEZI TOKA KWA MAMA HASHEEM, KWA NIABA YA TIMU YAKE.
Mama Hasheem Thabeet (Rukia Thabeet) leo amefanya ziara yake jijini Mwanza kwania ya kutoa msaada wa jezi kwa timu tatu za mpira wa kikapu jijini Mwanza nia na lengo ikiwa ni kuuendeleza mchezo huo nchini.


SHAMSA KAZOBA, MCHEZAJI MUWAKILISHI WA BUTIMBA DAY SEC SCHOOL AKIPOKEA MSAADA HUO, TIMU NYINGINE ILIYOPATA MSAADA HUO NI PAMBA SEC SCHOOL YA JIJINI MWANZA, AMBAPO KILA TIMU IMEPATA MOJA YA JEZI.

KAMISHNA WA WATOTO VIJANA NA MAENDELEO YA SHULE WA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU MWANZA, BRAZA SOSHO KIZITO AKITOA SHUKURANI ZAKE KWA MAMA.

Msaada huo toka kwa Hasheem Thabeet anayekiputa huko marekani kwenye ligi ya NBA umekuja kwa nia ya kuutukuza mchezo huo, kuinua uthaminike hatimaye kuwa ajira rasmi kama ilivyo kwa nchi ya Marekani.

Mama Thabeet pia alipata fursa ya kukabidhi tuzo kwa mlezi na mdhamini mkuu wa mpira wa kikapu Mansoor DOGO kwa ushiriki wake katika kuchangia maendeleo ya mchezo huo MWANZA.
MANSOOR AKA DOGO AKIRINGIA TUZO YAKE.

PICHA YA PAMOJA KWA WADAU BAADA YA MAKABIDHIANO HAYO YALIYOFANYIKA NYUMBANI HOTEL JIJINI MWANZA (MOJA KATI YA WADHAMINI).

BEI MPYA YA SODA ZA COCA COLA KANDA YA ZIWA YATAMBULISHWA SAMBAMBA NA MOTISHA.

Kampuni ya Coca cola Nyanza Bottling company limited (NBCL) leo imetangaza rasmi bei mpya za soda zake, akitangaza bei hizo Mkuu wa mauzo na masoko wa kampuni hiyo bw. Bhubhinder Singh amezitaja bei hizo ni kama ifuatavyo...
Bei ya soda za kampuni hiyo zimepanda kutoka shilingi 400 kwa ujazo wa chupa ya ml350 hadi shilingi 500 kwa ujazo huo huo. Coca cola inawasihi wateja wake wote kutolipa zaidi ya shilingi 500 katika ununuzi wa soda kama ilivyoainishwa kwenye jedwali hapo juu.
Bei hiyo halali itatambulishwa kwa nguvu zote kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mabango, vipeperushi kwenye sehemu za mauzo, kwenye friji za mauzo, kalenda zitakazotoka za mwaka 2011, t-shirts, kofia na promosheni za mitaani ili kutusaidia hata pale tunapokwenda sehemu za vijijini tusibamizwe na wauzaji, kwani kwa vijijini bei ni hiyo ya 500 hata kabla haijapanda kihalali.
Bei ya kreti moja inapanda kutoka 8,100 hadi 9,600 huku faida ya muuzaji ikipanda kutoka asilimia 18 na kuwa asilimia 25.
Kampuni hiyo imetoa changamoto kwa wadau wake kwa kuwazawadia chupa 3 za vinywaji bure kwa kila kreti moja watakalonunua kuanzia tarehe 1 hadi 10 december 2010 na kuanzia december 11 hadi 20.2010 Nunua kreti moja upate chupa mbili za vinywaji.