
Meneja wa Real Madrid Jose Mourinho amekanusha kwamba timu yake ilifedheheshwa na Barcelona baada ya kushindiliwa mabao 5-0 katika uwanja wa Camp Nou. Mabingwa wa Hispania Barca walicheza katika kiwango cha juu walipoisambaratisha Madrid katika mchezo wa kwanza wa El Clasico kwa Mourinho tangu aanze kuifundisha Madrid.

Alisema:"Timu moja ilicheza katika kiwango chake na nyingine haikucheza vizuri. "Kupoteza sawa tumepoteza, lakini kufedheheshwa hapana. Ilikuwa sahihi kupoteza mchezo ule, kwa sababu hatukucheza vizuri. "Nimezungumza na wachezaji wangu na nimewaambia msimu haujamalizika. Aliuliza: "Nani ajuaye kitakachotokea mwaka huu?"


Kwa upande wa Pep Guardiola, ambaye ameshinda kwa mara ya tano El Clasico tangu awe meneja wa Barcelona, amesema amefurahishwa sana kuona namna timu yake ilivyocheza katika kiwango cha juu na kuangaliwa na mamilioni ya wapenda soka duniani kupitia televisheni zao wanaokisiwa kufikia milioni 400. Alijigamba: "Ningependa kuzoa pointi nyingi zaidi dhidi ya Madrid lakini hilo haliwezekani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.