ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 23, 2019

ZAIDI MILIONI THEMANINI NA MOJA ZATUMIKA KUBORESHA ELIMU YA MSINGI TARAFA YA KIBENGU

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa iliyopo katika tarafa ya kibengu alipotembelea kujua changamoto za shule hiyo. 
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akisalimiana na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akifurahia jambo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisusa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


MBUNGE wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametumia zaidi ya shilingi 81,667,221 katika ukarabati na ujenzi wa shule za msingi za tarafa ya kibengu iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara katika tarafa hiyo Mgimwa alisema kuwa katika kata ya Mapanda amesaidia ukarabati na ujenzi wa Madarasa mawili shule ya msingi Mtwivila Saruji 90 na fedha kiasi cha shilingi jumla ya shilingi laki sita na nusu,shule ya msingi ukami saruji 70 na rangi kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo.

“Saruji mifuko 220 imetumika katika ukarabati na ujenzi wa madarasa katika shule za msingi ya Chogo,Ihimbo na Uhafiwa  pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya uingizaji wa umeme katika shule ya msingi Uhafiwa zote hizo ni juhudi zangu” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa katika kata ya Kibengu amechangia jumla ya mifuko 210 ya saruji,bati 280,madawati  10 na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kuboresha elimu katika shule ya msingi Kibengu,Igomtwa,Kipanga,Igeleke,Usokami na Ilogombe.

Aidha Mgimwa alisema kuwa kata ya Ihalimba inajumla ya shule za msingi nne ambazo ni Vikula,Ugesa,Nundwe na Ihalimba ambapo ametoa saruji mifuko 50 bati 310 na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 44,932,221 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo shule ya msingi Ihalimba pamoja na utengenezaji wa madawati 60 kwa ajili ya shule zote za kata hiyo.

“Hizi zote ni juhudi zangu binafsi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi tub ado hapo sijaelezea kuhusu shule za sekondari  lakini unakuta watu wamekaa tu vijiweni wanasema mbunge hajafanya kitu sasa hivi wewe mwandishi umejine kwa macho na umewasikia wananchi wenyewe kwenye mikutano ya hadhara” alisema Mgimwa

WAFANYAKAZI TBL WATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSITIRI WASICHANA WAKATI WA HEDHI MASHULENI

Meneja Ugavi wa TBL, Poul Canute akikabidhi vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi kwa Afisa Mwandamizi kutoka taasisi ya Her Africa, Asnath Ndosi Wakati wa hafla hiyo,wengine pichani ni wafanyakazi wa TBL
 Meneja wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi (wa tatu kushoto) Akiongea Wakati wa hafla hiyo.
 Maofisa wa taasisi ya Her Africa wakifurahia msaada huo wa kusaidia wasichana kukabiliana na changamoto ya hedhi wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo. Na Cathbert kajuna - Kajunason/MMG. Wafanyakazi wa kampuni yak Bia Tanzania (TBL Group), chini ya kampuni mama ya kimataifa ya AB InBev, wametoa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya kuwasitiri wasichana wanafunzi wanaosoma shule za sekondari kupitia mradi wa kukabiliana na changamoto za hedhi unaoendeshwa na taasisi ya Her Africa. 

 Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika ofisi za makao makuu ya TBL zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi maofisa kutoka taasisi ya Her Africa na wafanyakazi wa TBL. 

 Akiongea wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, alisema kuwa msaada huo umetolewa kutokana na michango ya wafanyakazi baada ya kuguswa na changamoto ya vifaa vya hedhi mashuleni kwa wasichana, hususani wanaotoka kwenye familia zenye vipato vidogo na kuwapunguzia uwezo wao wa kufaulu vizuri kutokana na wengine kutohudhuria masomo wanapokuwa kwenye vipindi hivyo.

 “TBL tunayo sera ya kujenga ulimwengu maridhawa ambayo inatekelezwa pia na wafanyakazi, ambapo mara nyingi wamekuwa wakijitoa kukabiliana na changamoto za kijamii na sio kwa kutoa pesa tu bali pia wamekuwa wakitoa hata muda wao kushiriki katika kazi za kijamii kama ambavyo wamefanikisha kutoa mchango huu” alisema Mutiganzi.

 Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa taasisi ya Her Africa nchini, Salha Kibwana, alishukuru wafanyakazi wa TBL kwa kulipa kuipa umuhimu changamoto ya vifaa vya Watoto wa kike wa sekondari kujisitiri wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi mashuleni, kwa kutoa msaada huo na amewahakikishia kuwa utawafikia walengwa “Nawashukuru kwa kujitoa na nina imani tukizidi kuunganisha nguvu tutafanikiwa kusaidia wanafunzi wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini” alisema.

Wednesday, August 21, 2019

UBAKAJI NDANI YA NDOA, NDOA ZA JINSIA MOJA NA FALAGHA:- HAKI ZA BINADAMU ZINAZUNGUMZAJE.. JAMII zetu zinaendelea kugubikwa na matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za binadamu  jambo linalotajwa kuchochea ongezeko la madhara na athari za kisaikolojia, kiuchumi na kadhalika.

WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO MOROGORO WAFIKIA 100


Idadi ya waliofariki kutokana na ajali ya moto wa lori la mafuta mkoani Morogoro, Agosti 10, 2019 imefikia 100.

Hii inatokana na majeruhi mwingine mmoja kufariki jana usiku Jumanne wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini  Dar es Salaam.

Kifo hicho kimekuwa cha tatu kwa siku ya jana Jumanne ambapo hadi saa 10 jioni ya jana Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kabwe alisema majeruhi wawili kati ya 18 walikuwa wamefariki.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa MNH, Aminiel Aligaesha amewataja waliofariki ni Mazoya Sahani, Khasim Marjani na Ramadhani Magwila.

Amesema majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo waliolazwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) ni 13 na wawili wametolewa ICU na kulazwa wodi ya Sewahaji.

MAONESHO YA 14 YA AFRIKA MASHARIKI YAJA MWANZA.

Mwenyekiti wa TCCIA Dk Elibariki Mmari akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.

Wanunuzi zaidi ya laki tatu(300,000) na wafanyabiashara zaidi ya 300 kukutana jijini Mwanza kuanzia tarehe 30Agosti hadi tarehe 8 Septemba, katika maonesho ya bidhaa mbalimbali ya 14 ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo Mwenekiti wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) Dk Elibariki Mmari amesema maonesho hayo yana malengo ya kutoa fursa kwa makampuni ya Tanzania na Afrika Mashariki kujitangaza.
‘’Kikubwa ni kutoa fursa kwa makampuni ya Tanzania kujifunza na kukuza wigo wa biashara za nje kati yetu nan chi nyingine kwenye masoko ya Agoa,Eba,Sadc na Jumuiya ya Afrika Mashariki’’ alisema Dk Mmari
Maonesho hayo yatakyofanyika kwenye viwanja vya Rock City mall yana kaulimbiu ya ‘’Kuongeza ubunifu katika uzalishaji na biashara katika kukuza uchumi’’ ambapo bidhaa za nguo,ngozi,ICT,ujenzi, umeme,pembejeo za kilimo bidhaa nyingine ni huduma za kiuhandisi,mbao,bidhaa za kazi za mikono na zawadi.
Ambapo katika maonesho hayo bidhaa zilizopigwa marufuku ni siraha za moto na milipuko,masuala ya kisiasa na mambo ya kidini ambapo hayataruhusiwa kupata nafasi kwenye viwanja hivyo.
Dk Mmari amechukua fursa hiyo kuwakaribisha waoneshaji wa kutoka nje ya Tanzani na kuwakumbusha kulipia vibali vyao kwa wakati kabla ya kusafirisha bidhaa ili kuondokana na usumbufu utakao wakuta.

TBL YATOA MSAADA YA VIPURI VYA MAGARI KWA JESHI LA POLISI KITUO CHA ILALA JIJINI DAR

 Meneja wa kiwanda cha TBL ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin, akiwa na wafanyanyakazi wa kiwanda hicho wakikabidhi masada wa vipuri kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma,kwa ajili ya kuboresha usafiri wa Jeshi hilo.
 Meneja wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi na Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma, wakisaini nyaraka za makabidhiano ya vipuri hivyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala, wakishuhudia makabidhiano hayo katika hafla iliyofanyika katika kiwandani.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma, akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala jijini Dar es Salaam Wakati wa hafla hiyo

Kampuni ya TBL chini ya kampuni ya Kimataifa ya ABInBev,imekabidhi masada wa vipuri vya kukarabati magari ya kituo cha polisi cha Ilala akiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuimarisha usalama kupitia kuboresha usafiri katika Jeshi hilo.

Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala, Calvin Martin na ulipokelewa naMkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam,  ASP Nyararo Otuma,ambaye alishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia taasisi za Serikali sambamba na kufanya nazo kazi kwa kariibu katika  kufanikisha kampeni mbalimbali zenye kunufaisha jamii.

Meneja wa kiwanda cha Ilala,Calvin Martin, alisema kuwa TBL, itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali  kama ambavyo imetoa vipuri (Shock Absorber) kwa ajili ya kufanikisha kutengeneza magari ya kituo cha Polisi cha Ilala, kwa ajili ya kuboresha usafiri wa askari wakati wa kutekeleza majukumu yake ya ulinzi na huduma mbalimbali katika jamii.

Aliongeza kusema kwa muda mrefu kampuni ya TBL imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisi katika kufanikisha kampeni zake mbalimbali za kijamii hususani zinazohusu usalama barabarani,kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia na kampeni ya kuhamasisha matumizi yenye vinywaji vyenye kilevi kistaarabu.

Tuesday, August 20, 2019

UHALIFU WAPUNGUA NCHINI

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisoma taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani),wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo leo jijini Dodoma.Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,akitoa ufafanuzi unaohusu utendaji wa Taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo leo jijini Dodoma.Kulia  ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizunguma wakati wa uwasilishaji waTaarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo leo jijini Dodoma. .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Uhalifu wapungua nchini
Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu nchi imeendelea kuwa katika amani na utulivu huku uhalifu ukipungua kwa asilimia 2.2 kwa makosa makubwa ya jinai ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita hali inayopelekea wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi kwa amani na usalama.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akisoma taarifa ya Serikali mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliyohusu Hali ya Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa Kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu ikiwemo utekelezaji wa dhana ya Ulinzi Shirikishi.
“Kuanzia Januari hadi Juni ndani ya mwaka huu jumla ya makosa makubwa ya jinai yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi nchi nzima yalikuwa 28,252 tofauti na kipindi kama hiki mwaka uliopita ambapo makosa 28,889 yaliripotiwa vituoni, tukiangalia vizuri hesabu zetu ndani ya mwaka huu tumepunguza makosa 637 hii yote inatokana na juhudi za askari wetu na utekelezaji wa dhana ya ulinzi shirikishi” alisema Masauni
Naibu Waziri Masauni ameyataja makosa hayo makubwa ya jinai kuwa ni Makosa dhidi ya binadamu, Makosa dhidi ya Maadili ya Jamii, Makosa ya kuwania mali na Makosa ya Uhalifu wa Kifedha
Akizungumzia makosa ya usalama barabarani Naibu Waziri Masauni amesema kumekuwepo na mafanikio katika kupunguza makosa ya usalama barabarani hali inayochagizwa na usimamiaji wa sheria na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu..
“Takwimu za makosa ya ajali za barabarani katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu zinaonesha kuwepo kwa jumla ya makosa 1,610 yaliyoripotiwa ikilinganishwa na makosa 2,200 mwaka uliopita huku takwimu zikiweka wazi makosa 590 kupungua katika vipindi hivyo viwili” alisema Masauni
Alisema kutokana na kupungua kwa makosa ya barabarani hata idadi ya ajali zilipungua hali iliyopelekea kupungua kwa vifo kwani mwaka jana watu 1,051 walifariki tofauti na mwaka huu ambapo kuanzia mwezi Januari mpaka Juni watu 781 walipoteza maisha.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alisema mafanikio hayo ya kupungua kwa uhalifu nchini yamechangiwa pia na matumizi ya teknolojia katika kupambana na uhalifu huku akiwaonya wahalifu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya.
“Tunatumia vifaa maalumu ikiwepo drones katika kudhibiti uhalifu japo kwasababu za kiintelijinsia hatuwezi kusema ziko ngapi na maeneo gani muhimu tunawaasa wahalifu kuacha mipango yao ya kuvuruga amani ya nchi hii nawahakikishia hawatabaki salama,tunataka wananchi wafanye shughuli zao za kiuchumi” alisema IGP Sirro
Vikao vya Kamati za Bunge zinaendelea jijini Dodoma huku wizara mbalimbali zikiwasilisha taarifa zao kwa kamati hizo huku vikao vya Bunge vikitarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.

HOSPITALI YA SEKOU TOURE YAMTUNUKU CHETI MWENYEKIT THE DESK & CHAIR

 Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Alhaji Sibatin Meghjee (kulia) akimkabidhi hati ya kamabidhiano ya vyoo nane kati ya 20, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) jana.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) jana akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Alhaji Sibatin Meghjee (kulia).Cheti hicho ametunukiwa na uongozi wa hospitali hiyo kutokana na kutambua mchango wake kwenye jamii na hospitali yenyewe.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kulia) akifungua mlango wa moja ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Nyuma ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) akifungua bomba na kwenye sinki la maji nje ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.
.Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki akiflash maji kwenye moja ya vyoo walivyojengwa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Picha zote na Baltazar Mashaka 

NA BALTAZAR MASHAKA

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure imemtunuku na kumkabidhi cheti Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Cair Foundation (TD &CF), Alhaji Sibtain Meghjeekwa a kutambua mchango wake wa kusaidia jamii.

Alhaji Meghjee alikabidhiwa cheti hicho jana na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Bahati Msaki muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi matundu nane ya vyoo kwenye hospitali hiyo yaliyotolewa na The Desk & Chair Foundation na kugharimu  sh. zaidi ya sh. milioni 20.3.


Akimkabidhi cheti hicho Dk Bahati alisema, Alhaji Meghjee kupitia taasisi hiyo amejitoa na kufanya mambo mengi kwenye  jamii na kujenga miundombinu ya jengo la kupumzikia pamoja na vyoo matundu saba kwa ajili wananchi wanaokuja kuona wagonjwa kwenye hospitali hiyo.

Pia amejenga vyoo matundu manne kwenye jengo la kuhifadhia maiti ikiwa ni pamoja na kutoa msaada waa manteki ya kuhifadhia maji, madawa na vifaa tiba pamoja na mgodoro kwa ajili ya wagonjwa.

“Tutakuwa ni wezi wa wafadhila tusipoenzi na kutambua mchango wa Alhaji Meghjee na taasisi yake katika kusaidia jamii ikiwemo hospitali hii na wapokea huduma wake.Hivyo tunamkabidhi cheti hiki ikiwa ni kumbukumbu yake kwa mazuri aliyotufanyia hospitali ya Sekou Toure,”alisema Dk.

Kwa upande wa alhaji Meghjee alishukuru kwa cheti hicho na kuahidi kitakuwa chachu ya kuendelea kusaidia jamii.

“Najisikia faraja kwa kupata zawadi hii ambayo itakuwa chachu ya kuendelea kusaidia jamii katika sekta mbalimbali kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wananchi wanatimiza ndoto zao,”alisema.  

WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGS & ONLINE TV' WAPIGWA MSASA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media -  Blogs/ Online TV) nchini wametakiwa kujitafakari na kutimiza wajibu wao katika utetezi wa haki za binadamu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 20,2019 na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu Jijini Dodoma yanayoratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu mjini Dodoma yaliyoshirikisha waandishi wa habari mtandaoni (Blogs/Online Tv ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media)
 Gwandu alisema ni vyema waandishi wa habari wa vyombo vya habari wakatumia mafunzo wanayopewa na kuonesha kwa vitendo namna gani mafunzo ambayo wamekuwa wakipewa yanawasaidia katika kazi zao.

"Washiriki wa Work Group Three inayohusisha waandishi wa habari mtandaoni tutimize wajibu wetu kwa yaliyo ndani ya uwezo wetu, bado hatujaona habari za haki za binadamu na demokrasia kama ambavyo tunatakiwa kufanya",alisema.

"Tunaendelea kufuatilia kwa makini namna gani tutapunguza washiriki katika kundi hili, wafadhili wetu wameendelea kujiuliza na kuhoji kuhusu mafunzo tunayopewa na wajibu wetu",

"Nyinyi ni watu wazima mjitathimini mmesafiri kutoka kwenu kuja kushiriki mafunzo yanayogharamiwa kwa fedha nyingi,halafu hatuoni mabadiliko makubwa,hatutasita kupunguza washiriki ili tubaki na wale wanaozingatia kinachofundishwa",aliongeza Gwandu.
 Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Wakili Froldius Mutungi akizungumzia kuhusu haki alisema, haki za binadamu hazirithiwi wala kutolewa na mtu hivyo ni wajibu wa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kulinda haki za binadamu na kupaza sauti pale haki zinapovunjwa.

Mafunzo hayo ya Haki za Binadamu ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).
WAZIRI UMMY MWALIMU KUZINDUA CHAMA CHA UREMBO NA VIPODOZI TANZANIA (TCA) AGOSTI 26,2019

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) Agosti 26 mwaka 2019.

Akizungumza leo Agosti 19,2019 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Shekha Nasser amesema sekta ya urembo na vipodozi inakua kwa kasi na kutoa ajira nyingi kwa watanzania walio wengi.

"Tukio hilo la kihistoria la kuzindua chombo hiki muhimu ndani ya nchi yetu litafanyika Agosti 26, 2019 katika jengo la PSSSF –KISENGA, Kijitonyama . Mgeni rasmi ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,"amesema.

Amefafanua wamekuwa wakishuhudia ongezeko la warembaji, wenye salons, watengeneza kucha, watengenezaji na wanaoingiza bidhaa za urembo na vipodozi,hivyo ni wakati muafaka kuwa na chama chao ambacho kitaaunganisha wadau wote.

Amesisitiza TCA ni chama kinachoanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuhudumia na kuunganisha wadau wote katika sekta ya urembo na vipodozi nchini."Chama hiki kitahusisha wadau wote kuanzia waelimishaji, wajasiriamali wakubwa na wadogo, wazalishaji wa viwanda vidogo na vikubwa.

"Pia watengenezaji wa bidhaa asilia, watoa huduma, wasambazaji na watabibu wa ngozi katika sekta nzima hii ya urembo na vipodozi,"amesema.
Amesema kupitia ndani ya ya TCA kutakua na mafanikio ya kukuza sekta ya urembo na vipodozi baada ya kuona changamoto nyingi wanazozipitia washikadau.

Ametoa mfano pamoja na Wizara ya Elimu kupitia NACTE kupitisha mtaala wa kwanza wa elimu ya Stashahada hivi karibuni, lakini vyuo vya kutoa NTA Level 4, 5 na 6 bado havipo. 

Ameongeza pamoja na VETA kuwa na mtaaala wa kozi ya cheti cha Cosmetology lakini changamoto kubwa ni walimu wenye sifa ya Diploma wa kufundisha wanafunzi ili wafanye mtihani wa Taifa na kupata walimu wenye Weledi na sifa nchini. 

Amesema kuwa ukosefu huo wa walimu wa Cosmetology nchini unasababishwa na mambo mengi yakiwemo ya sekta hiyo kutotambulika rasmi na kujengewa heshima yake inayostahili kama ilivyo katika nchi za jirani Kenya, Uganda na South Afrika.

"Watanzania wengi huenda kwenye nchi hizo kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu ya Cosmetology ngazi ya Stashahada,"amesema Nasser na kuongeza kutokana na muamko huo wameona ni wakati muafaka wa kuanzisha chombo kitakachowaunganisha wadau wote wa sekta hiyo.

Mwenyekiti huyo wa TCA ametumia fyrsa hiyo kuwakaribisha wadau wote wa sekta ya urembo nchini Tanzania kufika ili kushuhudia tukio hilo la kipekee kwa mara ya kwanza Tanzania lenye kauli mbiu " Urembo na vipodozi katika uchumi wa Viwanda". 

 Mwenyekiti wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) ,Shekha Nasser  akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar kuhusu  uzinduzi  wa chama hicho, Agosti 26,mwaka 2019, ambapo Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Kulia ni Katibu wa TCA Braison Makena na kushoto ni Meneja Utawala TCA,Judy Charles  
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.

TEDx OYSTERBAY YAKUTANISHA WADAU KUJADILI MAENDELEO NA CHANGAMOTO MBALI MBALI


Kongamano la kuongeza maarifa la TEDx Oysterbay, liilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau kutoka nyanja mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. ambapo walipata fursa ya kusikiliza mada na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na masuala ya ubunifu, mapinduzi ya teknolojia,michezo na mada nyinginezo nyingi zenye kuelimisha zilizotolewa na wataalamu.Kampuni ya bia Tanzania (TBL) ilikuwa mmoja wa wadhamini wa kongamano hilo.

 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa kongamano la TEDx Oysterbay lililofanyika katika ukumbi wa The Little Theatre jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakibadilishana mawazo wakati wa kongamano hilo
Baadhi ya washiriki wakifurahi katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kongamano hilo

Monday, August 19, 2019

LAKAIRO INVESTMENT CO. LTD FUNGA FUNGUA MWAKA 2019


KATIKA kuchochea ari ya uchapakazi kwa maksudi ya kufikia Uchumi wa Viwanda wenye tija Wafanyakazi wa Lakairo Investment Company Limited, kutoka katika viwanda wazalishaji wa bidhaa mbalimbali jijini hapa wamefanya sherehe za funga & fungua mwaka zilizofanyika katika hotel ya ufukweni mwa ziwa Victoria ijulikanayo kama Bugando Beach, Nyanguge wilayani Magu.

Sherehe hizo zilizofana zimeambatana na kongamano la kujadili na kutathimini shughuli za utendaji sanjari na changamoto za wafanyakazi na viongozi.

 Akizungumza wakati wa sherehe hizo Mkurugenzi Mkuu wa Lakairo Investment Company Limited, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rorya  Lameck Airo amewapongeza wafanyakazi wote kwa ubunifu na uchapakazi waliouonyesha katika kampuni hiyo kiasi cha kuwa moja ya chachu ya mafanikio na maendeleo yanayoonekana sasa na kuwasihi kuzingatia maadili ili waweze kufikia malengo ya kampuni na wao kunufaika.