Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa iliyopo katika tarafa ya kibengu alipotembelea kujua changamoto za shule hiyo.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akisalimiana na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akifurahia jambo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisusa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MBUNGE wa jimbo la Mufindi
Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametumia zaidi ya shilingi 81,667,221 katika ukarabati
na ujenzi wa shule za msingi za tarafa ya kibengu iliyopo wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu.
Akizungumza mara baada ya
kumaliza ziara katika tarafa hiyo Mgimwa alisema kuwa katika kata ya Mapanda
amesaidia ukarabati na ujenzi wa Madarasa mawili shule ya msingi Mtwivila
Saruji 90 na fedha kiasi cha shilingi jumla ya shilingi laki sita na nusu,shule
ya msingi ukami saruji 70 na rangi kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule
hiyo.
“Saruji mifuko 220 imetumika
katika ukarabati na ujenzi wa madarasa katika shule za msingi ya Chogo,Ihimbo
na Uhafiwa pamoja na fedha kiasi cha
shilingi laki tano kwa ajili ya uingizaji wa umeme katika shule ya msingi
Uhafiwa zote hizo ni juhudi zangu” alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa katika kata
ya Kibengu amechangia jumla ya mifuko 210 ya saruji,bati 280,madawati 10 na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki
tano kwa ajili ya kuboresha elimu katika shule ya msingi Kibengu,Igomtwa,Kipanga,Igeleke,Usokami
na Ilogombe.
Aidha Mgimwa alisema kuwa kata
ya Ihalimba inajumla ya shule za msingi nne ambazo ni Vikula,Ugesa,Nundwe na Ihalimba
ambapo ametoa saruji mifuko 50 bati 310 na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni
44,932,221 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo shule ya msingi Ihalimba pamoja na
utengenezaji wa madawati 60 kwa ajili ya shule zote za kata hiyo.
“Hizi zote ni juhudi zangu
binafsi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi tub ado hapo
sijaelezea kuhusu shule za sekondari
lakini unakuta watu wamekaa tu vijiweni wanasema mbunge hajafanya kitu
sasa hivi wewe mwandishi umejine kwa macho na umewasikia wananchi wenyewe
kwenye mikutano ya hadhara” alisema Mgimwa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.