Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma, Dominic Dhanah (watatu kushoto) na Mrajisi wa Jumuiya sisizo za Kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdullah (watatu kulia) wakikabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni Nne kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Mkunazini baada ya mwanafunzi Raya Zubeir Hemed(kulia), kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani kwenye hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimpa zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkunazini, Saidat Jumbe zawadi baada ya kujibu swali lililohusiana na Kanuni za Uvukaji wa Barabara ili kuepuka ajali.Hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimkabidhi kikombe mshindi wa kwanza wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani mwanafunzi wa Shuke ya Msingi Mkunazini Rayah Zubeir Hemed.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma,Dominic Dhanah.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma,Dominic Dhanah, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Pili Salum Ali Khatib baada ya kushika nafasi hiyo katika Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani lililodhaminiwa na kampuni hiyo.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.