ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 17, 2024

MAMIA YA WANANCHI WAJITOKEZA VISIGA KUMZIKA MPENDWA WAO MHE.DIWANI DORICE


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani pamoja na maeneo mengine ya jirani  leo wamejitokeza kwa wingi kwa ajili kutoa heshima zao za mwisho pamoja na   kumzika katika nyumba yake ya milele aliyekuwa Diwani wa viti maalumu wa chama cha mapinduzi (CCM) katika halmashauri ya mji Kibaha mhe.Dorice Michael.


Mazishi  hayo ambayo yamefanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu  huyo eneo la Visiga Madafu Wilaya ya Kibaha  yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo viongozi wa chama,serikali,viongozi wa dini pamoja na wananchi.

Viongozi ambao  wamehudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha mji Mwalimu Mwajuma Nyamka, pamoja na viongozi mbali mbali wa jumuiya  zote za chama kuanzia ngazi chini ikiwemo  za Wilaya na Mkoa.
Pia katika msiba huo viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon pamoja viongozi wengine wakiwemo wakuu wa idara na viongozi mbali mbali.
Akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha Katibu Method Mselewa amewapa pole wafiwa wote familia ya marehemu pamoja na ndugu jamaa na marafiki ambao wameondokewa na mpendwa wao.

Mselewa alisema kwamba Mhe.Mbunge alipaswa kujumuika katika mazishi hayo lakini ameshindwa kuhudhuria kutokana na kupata dharura ambazo zipo nje ya uwezo ikiwemo kuuguliwa na mzee wake.
Naye Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka alisema amesikitishwa sana kifo cha diwani huyo ambaye alikuwa ni mchapa kazi hodari hivyo ameacha pengo kubwa katika chama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha mji Mwajuma Nyamka alisema chama kimepoteza mtu muhimu sa na kutokana na diwani huyo alikuwa mcheshi na anashirikiana na viongozi mbali mbali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Mussa Ndomba ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha mji alisema kwamba katika baraza la madiwani wamepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuyafanyia kazi yale ambayo amekuwa akijifunza.

Diwani wa kata ya Visiga Kambi Legeza wakati akitoa salamu zake za rambi rambi  alimuelezea marehemu Dorice alikuwa ni kiungo kikubwa  sana katika kusaidia jamii na kutatua changamoto zao mbali mbali zinazowakabili.

Nao baadhi ya viongozi wa dini hawakusita kumwelezea marehemu Dorisi kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele katika kumcha Mungu ikiwa sambamba na kushirikiana na viongozi wa dini katika ngazi mbali mbali.
Kuhusiana na taasisi  mbali mbali ambazo marehemu alishafanya nazo kazi kwa pamoja walisema wameguswa na msiba huo kutokana na marehemu aliweza kuwapambania kwa hali na mali kuweza kupata fedha ambazo zinatolewa na halmashauri.

Katika msiba huo  ambao umeweza kugusa na kuumiza mioyo ya mamia ya wansnchi na viongozi  kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya Kibaha mkoani Pwani na maeneo ya jirani ya Jiji la Dar es Salaam.

Marehemu Dorice ambaye alizaliwa mwaka 1980 mpaka kifo chake ameacha watoto wawili na alikuwa ni diwani wa viti maalumu kupitia tiketi ya CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mjini ambapo ameacha alama kubwa kutokana na uchapakazi wake.

Wednesday, May 15, 2024

POLISI PWANI YAONYA BODABODA WANAOVAMIA MISAFARA YA VIONGOZI.

IMEANDALIWA NA VICTOR MASANGU/PWANI NA KUSOMWA NA ALBERT G. SENGO

JESHI la Polisi Mkoa wa  Pwani limewaonya  vikali baadhi ya  madereva wa Bodaboda kuacha kabisa tabia kuingilia misafara ya viongozi waandamizi na badala yake wanapaswa kuiheshumu pindi inapopita ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaweza kupelekea watu kujeruhiwa vibaya na kupoteza maisha.


Onyo hilo  limetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani  wakati Jeshi la Polisi  kwa kushirikiana na Kampuni ya Pyriamid Oil walipotoa Elimu ya usalama barabarani sambamba na  uzinduzi rasmi  wa kituo ha mafuta  kilichopo eneo la kwa Mbonde  mkoani Pwani

UGOMVI WA FAMILIA KUKOSA MALEZI YA KIROHO MATUNZO AFYA YA MWILI SABABU ZA ONGEZEKO LA WATOTO MITAANI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Ni jambo lililowazi kwamba hakuna jamii hasa ile inayojielewa, inayoweza kufurahia kuona watoto wakitenganishwa na familia zao. Ugomvi wa baba na mama, malezi ya mzazi mmoja yanayopelekea kushindwa kumudu mahitaji, kukosa malezi ya kiroho, elimu, matunzo ya afya ya mwili ni moja kati ya sababu alizozitoa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angeline mabula zinazochangia ongezeko la watoto wa mitaani. Mabula ameyasema hao katika hafla maalum ya maadhimisho ya siku ya mama duniani iliyofanyika mwishoni mwa juma, siku hiyo ikiambatana na kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake ambapo mbunge huyo aliamua kuitumia kwa kutoa misaaada kwa kituo cha watoto wenye uhitaji cha Fonerisco kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza. #samiasuluhuhassan #mwanza #ILEMELA #Angelina_Mabula

RPC PWANI AZINDUA KITUO CHA PYRAMID OIL KIBAHA AWAPA SOMO BODA BODA KUTII SHERIA

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

JESHI la Polisi Mkoa  Pwani limewaonya  vikali baadhi ya  madereva wa Bodaboda kuacha kabisa na kuingilia misafara ya viongozi waandamizi na badala yake wanapaswa kuiheshumu pindi inapopita ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinaweza kupelekea watu kujeruhiwa vibaya na kupoteza maisha yao.

Onyo hilo  limetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani  Pius Lutumo wakati Jeshi la Polisi  kwa kushirikiana na Kampuni ya Priamid oil walipotoa Elimu ya usalama barabarani sambamba na  uzinduzi rasmi  wa kituo ha mafuta  kilichopo eneo la kwa Mbonde  mkoani Pwani


Kamanda Lutumo alisema kwamba madereva wa boda boda wanapaswa kuweka misingi ya kuheshimu misafara ya viongozi waandamizi ikiwa sambamba na kuzingatia sheria mbali mbali za barabarani.

Aidha Kamanda Lutumo aliwapongeza wawekezaji wa kiwanda hicho cha Pyramid Oil kwa kuamua kukijenga katika eneo la Kibaha ambalo kwa sasa lina viwanda mbali mbali ni moja ya hatua ya kuleta chachu ya maendeleo.


Kwa upande Kaimu Mkuu wa kikosi cha  Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani Miraj Mkojera amewataka bodaboda hao kuachana kabisa  na tabia ya kubeba mishikaki na kuwahimiza kuvaa kofia  ngumu ili kujilinda pindi ajali inapotokea.

Naye mmoja wa wawekezaji ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo hicho cha mafuta cha Piramid Victor  Betram amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba uwezezaji huo wa kituo cha mafuta umeweza kuwapa fursa mbali mbali za ajira kwa wakazi kutoka Wilaya ya  Kibaha kwa kiwango cha asilimia mia moja.

Pia Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba kituo hicho ambacho kimefunguliwa rasmi kimeshatoa fursa za ajira zaidi ya 15 na kwamba kitaendelea kutoa ajira kadiri ya mahitaji.

Nao baadhi ya madereva wa  bodaboda ambao wamehudhuria katika halfa hiyo wameahidi kutekeleza maagizo na maelekezo yote ambayo yametolewa na jeshi la Polisi.

Kadhalika walisema ujio wa mradi huo wa kituo cha mafuta utaweza kuwasaidia kuondokana na kwenda kutafuta huduma ya mafuta katika eneo la mbali na kudai  kwao ni mkombozi mkubwa.

Katika halfa ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho cha mafuta pia kulitolewa mafunzo mbali mbali kwa madereva wa boda boda kutoka kwa jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuzingatia sheria za barabarani bila kushurutishwa.

Monday, May 13, 2024

YANGA BINGWA TENA. SASA NI MARA 30.

  


LIGI Kuu ya NBC Tanzania bara ikiendelea tena leo Mei 13, 2024 huku macho na masikio yakielekezwa katika dimba la Manungu Complex, Turiani Morogoro ambapo Wananchi wametawazwa  kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya 30 kihistoria baada ya  ushindi wa goli 3-1 wakizoa pointi dhidi ya Wakata Miwa.


Yanga Sc wamefikisha alama 71 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote kwa mechi zilizosalia kabla ya kufungwa kwa pazia la Ligi.

Azam Fc waliopo nafasi ya pili wakishinda mechi tatu zilizosalia watafikisha pointi 69 sawa na Simba Sc ambao watafikisha pointi 69 wakishinda michezo yao minne iliyobaki.

MSIMAMO 🔝3️⃣
🥇Yanga Sc — mechi 27 — pointi 71
🥈 Azam Fc — mechi 27 — pointi 60
🥉 Simba Sc — mechi 26 — pointi 57

MBUNGE ILEMELA ATOA MIFUKO MIA MOJA UJENZI WA MSIKITI WA AL HIKMA KITANGIRI

 


MBUNGE
wa Jimbo la Ilemela MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula ametoa mifuko mia moja ya saruji kwaajili ya ujenzi wa msikiti wa Al Hikma uliopo kata ya Kitangiri wilaya ya Ilemela 

Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mifuko hiyo ya saruji Dkt Angeline Mabula amesema kuwa aliona uhitaji wa msikiti huo kupitia kituo cha Luninga cha kiislam cha Mahaasin Tv kuwa waumini wa msikiti huo Wana zoezi la ujenzi na wanahitaji wadau kuwaunga mkono hivyo kuweka adhma ya kuwasaidia kwa kile ambacho amejaaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiwataka wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono ujenzi wa msikiti huo

‘.. Namshukuru Mungu nimeweza kufanya jambo hili, Maana niliona kwenye Tv wakihitaji kuungwa mkono nami nikaweka nadhiri ya kuwasaidia bila kumshirikisha mtu yeyote na leo nmeweza kukabidhi mifuko hii wakakamilishe ujenzi ..’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Mabula amewapongeza waumini wa msikiti huo kwa kuanza kujichangisha hao wenyewe kufikia hatua iliyopo sasa ya ujenzi wa msikiti huo na kwamba ataendelea kuungana na jamii katika kutatua  mbalimbali zinazowakabili 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi ya msikiti huo Shekh Athumani Issa Hamis mbali na kumshukuru Mbunge huyo kwa msaada wake huo ameongeza kuwa ipo haja kwa viongozi wengine kuiga mfano wa Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa kuwa amekuwa akisaidia sana dini mbalimbali hata ambazo si za imani yake ikiwemo uislam licha ya yeye kuwa mkristo

Zakaria Yakubu ni muumini wa msikiti huo ambapo amemuombea Dua Mbunge huyo kufuatia msaada alioutoa huku akimuomba Mwenyezi Mungu kumbariki na kuendelea kuwa mwema kwani ujenzi wa msikiti wao ulikuwa ukisuasua kutoka na ukosefu wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji.

NILIVYO LEO.

 


Habari ya Uzima Ndugu Yangu wa Karibu ni Mimi Rafiki Yako Mpendwa Putteny Anthony Muimbaji wa Nyimbo za Injili, Nipo apa kukuomba Support Yako Kwa Kuchangia Huduma Kwa KUCHUKUA FLASH YENYE JUMLA YA NYIMBO 13- ZA AUDIO NA VIDEO-6 KWA 20000/= Tsh 

Kwa Unyenyekevu Mkubwa Nakutegemea Sana Rafiki Angu Mwema  Unishike Mkono Kwenye  Hili Na Mungu Atakubariki  Katika Sehemu  Uliyoguswa Kusupport Kazi Ya Mungu Flash Ziko Tayari  Zitakufikia Mkoa Wowote Ulipo 

KWA MAWASILIANO ZAIDI +255713618153

AHSANTE SANA MUNGU AKUBARIKI

JAMAA ALIYEPANDIKIZWA FIGO YA KWANZA YA NGURUWE AFARIKI DUNIA

 


Mwanamume wa kwanza kupandikizwa figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba amefariki miezi miwili baada ya upasuaji huo, hospitali iliyotekeleza utaratibu huo imesema.

Richard "Rick" Slayman, 62, alikuwa akiugua ugonjwa wa figo hatua ya mwisho kabla ya kufanyiwa upasuaji huo mnamo mwezi Machi.

Hospitali kuu ya Massachusetts (MGH) ilisema Jumapili hakuna dalili kwamba kifo chake kilikuwa matokeo ya upandikizaji.

Upandikizaji wa viungo vingine kutoka kwa nguruwe waliobadilishwa vinasaba haukufaulu hapo awali, lakini operesheni dhidi ya Bw Slayman ilisifiwa kuwa hatua muhimu ya kihistoria.

Mbali na ugonjwa wa figo, Bw Slayman pia aliugua kisukari cha Aina ya 2 na shinikizo la damu. Mnamo 2018, alipandikizwa figo ya binadamu, lakini ilianza kushindwa kufanya kazi baada ya miaka mitano.

Kufuatia upandikizaji wa figo yake ya nguruwe mnamo Machi 16, madaktari wake walithibitisha kuwa hahitaji tena dayalisisi baada ya kiungo hicho kipya kusemekana kufanya kazi vizuri.

"Bw Slayman ataonekana milele kama mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wengi wa upandikizaji duniani kote na tunamshukuru sana kwa imani yake na nia yake ya kuendeleza uwanja wa upandikizaji wa xeno," ilisema taarifa ya MGH.

Xenotransplantation ni kupandikiza seli hai, tishu au viungo kutoka kwa spishi moja hadi nyingine.

MGH ilisema "imehuzunishwa sana" na kifo chake cha ghafla na kutoa rambirambi kwa familia yake.

Jamaa wa Bw Slayman walisema simulizi yake ilikuwa ya kutia moyo.

“Rick alisema kuwa moja ya sababu zilizomfanya afanyiwe utaratibu huu ni kutoa matumaini kwa maelfu ya watu wanaohitaji upandikizaji kuishi,” walisema.

"Rick alitimiza lengo hilo na matumaini yake yatadumu milele.

"Kwetu sisi, Rick alikuwa mtu mwenye moyo mkunjufu na mcheshi ambaye alijitolea sana kwa familia yake, marafiki, na wafanyikazi wenzake," waliongeza.

Ingawa Bw Slayman alipokea figo ya kwanza ya nguruwe kupandikizwa kwa binadamu, sio kiungo

Wagonjwa wengine wawili wamepandikizwa moyo wa nguruwe, lakini taratibu hizo hazikufua dafu kwani waliopokea huduma hiyo na kufariki wiki chache baadaye.

Katika kesi moja, kulikuwa na ishara kwamba mfumo wa kinga ya mgonjwa ulikuwa umekataa kiungo, ambayo ni hatari ya kawaida katika upandikizaji.

CHANZO:- BBC SWAHILI

RUNALI WAGAWA VIROBA 800,000VITABU NA KAMBA KWA WAKULIMA WA NACHINGWEA, RUANGWA NA LIWALE

 

Meneja wa RUNALI Jahida Hassan akiongea na wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa AMCOS kutoka wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale wakati wa mafunzo kwa viongozi hao
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Nachingwea Adinan Mpyagila akiongoza zoezi la ugawaji wa vifungashio vya mazaoBaadhi ya washiriki wa mafunzo yanayotolewa na RUNALI 
CHAMA kikuu cha ushirika (RUNALI) kimegawa jumla ya viroba laki 800,000, vitabu pamoja na kamba kwa wakulima wa wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale kuelekea msimu wa mauzo ya mazao ya ufuta, Mbazi na Korosho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vifungashio hivyo, meneja wa RUNALI Jahida Hassan alisema kuwa wamegawa vifungashio hivyo kwa lengo la kuwawezesha wakulima kuhifadhi mazao kwenye ubora unaotakiwa sokoni.

Hassan alisema kuwa RUNALI wamekuwa wanatoa elimu mara kwa mara kwa wakulima ili waweze kulima kilimo kilicho bora na kufanikiwa kupeleka mazao yaliyo bora sokoni.

Alisema wapo tayari kwa kuanza msimu mpya wa Mbaazi na ufuta na lengo la mafunzo haya ni kuwajengea utayari wa kwenda kwenye msimu mpya pia wametoka kifahamishana umuhimu wa kufanya ukaguzi.

Licha ya kutoa vifungashio hivyo lakini RUNALI walitoa mafunzo kwa wenyeviti na makatibu 212 ambapo mgeni rasmi alikuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila kuwataka viongozi waliopata mafunzo kwenda kutoa elimu kwa wajumbe wa bodi na makalani katika vyama vyao.

Mpyagila amewasihi wakulima kutouza mazao kiholela na kuweka vituo kwenye mipaka ya wilaya ili mazao yasiuzwe nje ya wilaya kwa kuwa itapelekea kupoteza mapato ya Halmashauri kwenye mazao ya mbaazi na ufuta.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha ushirika (RUNALI) Odas Mpunga amewapongeza vyama vya Ushirika kwa kazi kubwa waliyofanya na kuingiza mapato makubwa. Pia, amewataka kuyatumia vema mafunzo haya kwa vitendo ili kuleta Matokeo chaya.

TAASISI YA BINTI LINDI INITIATIVE YAGAWA MIZINGA 50 NACHINGWEA

 

Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Lindi initiative Kijakazi Yunus akiongea na wananchi na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea wakati akikabidhi mizinga 50 ya kufugia nyuki kwa lengo la kuwainua kiuchumi na utunzaji wa mazingira 
Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Lindi initiative Kijakazi Yunus akikabidhi mizinga 50 ya kufugia nyuki wananchi na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwa lengo la kuwainua kiuchumi na utunzaji wa mazingira Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Lindi initiative Kijakazi Yunus akikabidhi mizinga 50 ya kufugia nyuki wananchi na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwa lengo la kuwainua kiuchumi na utunzaji wa mazingira


Na Fredy Mgunda, Lindi.

TAASISI ya Binti Lindi Initiative imegawa mizinga 50 ya kufugia nyuki kwa vikundi vitano ya Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi vyenye watu zaidi ya 50.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mizinga hiyo 50 ya kufugia nyuki, mkurungenzi wa taasisi ya Binti Lindi initiative Kijakazi Yunus alisema kuwa amekabidhi mizinga hiyo kwa lengo la kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya ya Nachingwea na Lindi kwa ujumla.

Yunus alisema kuwa anaunga mkono juhudi za Rais Dr Samia Suluhu Hassan katika kuhifadhi mazingira na kukuza uchumi wa wananchi kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Aidha Yunus alisema kwamba taasisi hiyo inajihusisha kusaidia mabinti na wanawake kwenye sekta ya elimu na uchumi kwa sababu kumekuwa na mmong'onyoko wa maadili unaopelekea kutokea mimba nyingi za utotoni ambazo mara nyingi kukatisha ndoto za mabinti wengi.

Yunus alisema kwamba wanawake wakiwa na uchumi mzuri unasaidia maendeleo ya taifa lakini kwa sasa maadili ya watanzania yameporomoka kwa kiasi kikubwa hivyo taasisi ya Binti Lindi initiative inatoa elimu ya umuhimu wa kuwa na maadili mazuri.


Kwa upande wake afisa tarafa ya Nambambo Christopher Mkuchika alimpongeza mkurugenzi wa taasisi ya Binti Lindi initiative Kijakazi Yunus kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kutoa elimu ya malezi na uchumi kwa mabinti na wanawake.