MBUNGE wa Jimbo la Ilemela MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula ametoa mifuko mia moja ya saruji kwaajili ya ujenzi wa msikiti wa Al Hikma uliopo kata ya Kitangiri wilaya ya Ilemela
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mifuko hiyo ya saruji Dkt Angeline Mabula amesema kuwa aliona uhitaji wa msikiti huo kupitia kituo cha Luninga cha kiislam cha Mahaasin Tv kuwa waumini wa msikiti huo Wana zoezi la ujenzi na wanahitaji wadau kuwaunga mkono hivyo kuweka adhma ya kuwasaidia kwa kile ambacho amejaaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiwataka wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono ujenzi wa msikiti huo
‘.. Namshukuru Mungu nimeweza kufanya jambo hili, Maana niliona kwenye Tv wakihitaji kuungwa mkono nami nikaweka nadhiri ya kuwasaidia bila kumshirikisha mtu yeyote na leo nmeweza kukabidhi mifuko hii wakakamilishe ujenzi ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula amewapongeza waumini wa msikiti huo kwa kuanza kujichangisha hao wenyewe kufikia hatua iliyopo sasa ya ujenzi wa msikiti huo na kwamba ataendelea kuungana na jamii katika kutatua mbalimbali zinazowakabili
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi ya msikiti huo Shekh Athumani Issa Hamis mbali na kumshukuru Mbunge huyo kwa msaada wake huo ameongeza kuwa ipo haja kwa viongozi wengine kuiga mfano wa Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa kuwa amekuwa akisaidia sana dini mbalimbali hata ambazo si za imani yake ikiwemo uislam licha ya yeye kuwa mkristo
Zakaria Yakubu ni muumini wa msikiti huo ambapo amemuombea Dua Mbunge huyo kufuatia msaada alioutoa huku akimuomba Mwenyezi Mungu kumbariki na kuendelea kuwa mwema kwani ujenzi wa msikiti wao ulikuwa ukisuasua kutoka na ukosefu wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.