ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 20, 2023

WAANDISHI PWANI WAFUNDWA KUINGIA KATIKA UWEKEZAJI NA AJASILIAMALI ILI PAMBANA NA UMASIKINI.

VICTOR MASANGU,PWANI Waandishi wa habari wametakiwa kuwa wazalendo na kuhakikisha wanaweka misingi imara ya kuanzisha miradi mbali mbali kama lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi ilikuondokana wimbi la umasikini. Kauli hiyo hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Pwani Ally Hengo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Kibaha.


Friday, May 19, 2023

MAUMIVU MAKALI YA KIUNO & MGONGO KWA BODABODA NA MAMALISHE BUGANDO YAENDESHA KLINIKI BURE & MATIBABU

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Katika kuhakikisha inaiunga mkono Serikalini kwenye utoaji huduma bora ya afya kwa kila Mtanzania Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imeendesha zoezi la upimaji wa afya bure kwa magonjwa mbalimbali haswa yasiyoambukizwa. Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhadhiri wa Chuo cha Afya Bugando(CUHAS) Samson Apolinary amesema kuwa zoezi wanalofanya linalenga haswa magonjwa yasiyoambukizwa huku akiongeza kuwa katika zoezi hilo wamewalenga haswa waendesha boda boda na bajaji kwani ni moja kati ya kundi lililosahaulika. Aidha Apolinary ametoa wito kwa wakazi wa Mwanza kujitokeza kwenda kupima afya zao sambamba na kupatiwa ushauri wa kitaalamu pamoja na matibabu pale inapobidi.

BENKI YA NMB KANDA YA KASKAZINI YAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA MKOANI TANGA

 

 



Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Praygod Godwin akizungumza na wafanyabiashara mkoani Tanga jana kuhusu namna walivyojipanga kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wafanyabiashara pamoja na ,kuwaelezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye benki hiyo kushoto n i Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga



Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth  Chawinga akizungumza wakati wa Halfa hiyo

Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa Halfa hiyo


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho


Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe akizungumza wakati wa kikao hicho

Sehemu ya Washiriki wa Kikao wakifuatilia kikao hicho



Na Oscar Assenga,Tanga

BENKI ya NMB Kanda ya Kaskazini leo wamefanya kikao na wafanyabiashara mkoani Tanga (NMB Business Club) huku wakieleza kwamba wamekuwa wakitoa zaidi ya Bilioni 60 kila mwezi kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo hapa nchini

Hatua hiyo inatajwa kama juhudi za benki hiyo kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu kuwawezesha wajasiriamali wadogo wasogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji maendeleo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho na wafanyabiashara ambao wanawahuduma na Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe ambapo alisema kwamba walianza kutoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali tokea mwaka 2000.

Mashaga alisema kwamba hatua hiyo imewajengea uzoefu mkubwa namna ya kuwahudumia wajasiriamali hao na kwamba kutokana na utoaji wa mikopo hiyo umewawezesha kuongeza nguvu kwenye mitaji yao na hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Leo hapa Tanga tulikutana na wateja kuwaambia kitu gani wamekianzisha na wakifanye ili kuweza kuboresha huduma zao kwa sasa wana huduma waliyoanzisha kwa ajili ya wateja wanaofanya huduma kwenye masoko yanayosimamiwa vizuri na serikali yana vizimba na wateja wameandikishwa”Alisema

Alisema kwamba ili kuhakikisha nao wananufaika na mikopo hiyo wameanza kutoa mikopo kuanzia 100,000 mpaka 1000000 bila dhamana na baadae milioni 1 hadi 2 mteja anaweka dhamana na wana mikopo mengine zaidi ya hapo inakwenda mpaka Milioni 5 kwa wateja wao.

“Lakini pia tumeanzisha mikopo kwa ajili ya vijana wanaojihusisha na bodaboda ambapo kitu ambacho kinahitajika ni kujiandikisha kwenye vyama vyao ambavyo vinatambulika na serikali na yeye ni kutafuta asilimia 20 ya chombo anachokitaka akishapata benki inaongzekja kiasi kilichobaki ili kumpatia”Alisema Meneja huyo Mwandamizi wa mikopo NMB Makao Makuu.

Hata hivyo alisema kwamba baadae wanafanya biashara na kufanya marejesho kila wiki kumaliza deni kwa kipindi cha miezi sita hadi 12 mpaka watakapoikamilisha ili kuwezesha na wengine kunufaina nayo.

Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya NMB-Playgod Godwin alisema kwamba leo wamekutana na wafanyabiashara kuweza kutengeneza mtandao na kubadilishana uzoefu ikiwemo kuwapa mafunzo ya vitu mbalimbali na mwaka huu wamewafundisha vitu vitatu.

Alisema kikao hicho kilikuwa ni mahususi kuwakutanisha wafanyabiashara (Bussness Club) kuwakutanisha ili kuwaeleza kwamba mteja anatakiwa kuaangalia mfano anafanyabiashara ya usafirishaji anatumia petrol lakini dunia inabadilika magari mengi yanabadilika kwenye matumizi ya gesi na mama lishe anatumia mkaa lakini dunia ya leo wanatoka kwenye mkaa kwenda kwente gesi hivyo watawafundisha mbinu mbalimbali na mambo ya kurekodi taarifa za mapato na matumizi na umuhimu wake na wapo wataalamu wazuri.

Hata hivyo alisema pia wataalamu hao watawafundisha jinsi mfanyabiashara kuangaa ikitokea amepata changamoto za kiafya,uzee nani atasimamia biashara zake pia wataangalia namna ya kuwafudnisha katika mambo hayo muhimu.

Katika kikao hicho kiliwakutanisha wafanyabiashara 150 wa mkoa wa Tanga wenye matawi 12 kwa mkoa ambapo inaelezwa kwamba kitakuwa na tija kwa siku zijazo katika kuendeleza biashara zao na hatimaye kukuza mtaji wao.

Naye kwa upande wake Mfanyaabiashara Celina Ndumbaro alisema kwamba alichojifunza katika mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kuweza kuona namna ya kufanya biashara zao kwa tija na kuweza kupata mafanikio.

Thursday, May 18, 2023

 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, ameibeba tena klabu ya Yanga, akisema kuwa katika mechi za fainali ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa Mei 28 na marudiano ni Juni 3, kila bao la ushindi atalipa Sh Milioni 20, sambamba na kutoa ndege ya serikali kuipeleka timu hiyo nchini Algeria kwa ajili ya kumenyana na wapinzani wao USM Alger.

 

Timu mbili hizo zinatarajiwa kukwaana katika mechi mbili za fainali ya Kombe la Shirikisho, mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga na Watanzania kwa ujumla kuishuhudia ikiweka historia ya kutwaa taji hilo linaloratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

 

Akizungumza katika tukio la uzinduzi wa Mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam, Rais Samia alisema uamuzi huo unatokana na matamanio yake ya kuona timu ya Tanzania inafanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

 

“Nilianza kwa kutoa sh Milioni 5 kila goli kwa timu ya Simba na Yanga kwenye michuano hii, lakini pia nikatoa Sh Milioni 10 kila goli moja ambapo bahati mbaya Simba wao wameishia njiani na kuwaacha wenzao Yanga.

 

“Kwa maana hiyo sasa natoa Sh Milioni 20 kwa kila goli la ushindi la mechi ya Yanga, bila kusahau kuwapa ndege ya kuwapeleka na kuwarudisha nje ya nchi kwenda kucheza na wapinzani wao nikiamini kuwa itakuwa ni motisha kwa timu yetu,” Alisema.

 

Uamuzi wa Rais Samia kutoa mamilioni kwa timu za Simba na Yanga umechangia kwa kiasi kikubwa kuzipaisha timu hizo sambamba na kutangaza soka la Tanzania, ambapo Yanga kwa mara ya kwanza ikifanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho.

MBIO ZA MWENGE ZARIDHISHWA NA MIRADI YOTE 12 YA HALMASHAURI YA KIBAHA MJINI.



Na Victor Masangu,Kibaha 


Halmashauri ya mji Kibaha mkoani Pwani imetumia kiasi cha shilingi bilioni 3.9 katika kutekeleza miradi 12 ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya,elimu,miundombinu ya barabara,pamoja na mambo mengine ya huduma za kijamii.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon wakati alipokuwa akitoa taarifa ya miradi ambayo itatembelewa katika mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka wa 2023.

Mkuu huyo aliongeza kuwa alisema kwamba Mwenge huyo utaweza kupita katika katika miradi mbali mbali ambapo baadhi yao itawekewa mawe ya msingi,kutembelewa pamoja na kuzinduliwa.

"Katika halmashauri ya Kibaha mji tumetembelea miradi yapatayo 12 ya maendeleo ambayo jumla yake imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.9 ambapo fedha nyingine kati ya hizo zimetoka kwa wadau wengine wa maendeleo,"alisema Nikson.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Kibaha mji Mshamu Munde alisema kwamba miradi ambayo wameianzisha watahakikisha kwamba wanailinda na kuitunza kwa hali na mali kwa lengo la kuwasaidia wananchi.


Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalah Kaim ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuweza kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo ambayo imegusa maslahi ya wananchi kwa ujumla.
Pia ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kuulaki Mwenge wa Uhuru Mwaka huu kwani unakuja kuangazia Maendeleo yanayoendelea kutamalaki kwenye Halmashauri za Mkoa wa Pwani  ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Mbio za Mwenge wa Uhuru umeweza kukimbizwa katika halmashauri ya mji Kibaha katika sekta mbali mbali ikiwemo,afya,elimu,miundombinu ya barabara,maji,mapambano dhidi ya madawa ya kulevya pamoja na marelia.

AJUZA WA MIAKA 77 AJIOA BOMANI MWAKE MIAKA 50 BAADA YA KUTALIKIANA NA MUME


Akiwa na umri wa miaka 77, Dorothy Fideli amefanya sherehe ya kipekee ya harusi kusherehekea penzi lake kwa nafsi yake mwenyewe.

Fideli alijifungisha  ndoa katika sherehe ya harusi katika karamu ya kusisimua iliyojaa mbwembwe na mahanjam ya aina yake.

hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Wastaafu wa O'Bannon Terrace huko Goshen, Ohio.

 Akiwa amezingirwa na wapendwa wake, bibi aliyejawa furaha alikubali utimilifu wa hamu yake ya ndani: yaani kujioa mwenyewe.

Baada ya kufunga ndoa mnamo 1965, alitalikiana na mumewe baada ya miaka tisa.

Fideli alijikwaa na wazo hilo lisilo la kawaida wakati wa ziara ya kanisa na bila kupoteza muda akamwendea Rob Geiger, meneja wa mali katika nyumba hiyo ya wastaafu, ili kuongoza sherehe hiyo ya aina yake.

Alisema:"Wazo fulani lilinijia siku moja kanisani kwamba unapaswa kujifanyia jambo fulani maalum. Nikasema, unajua nini? Nimefanya kila kitu kingine maishani. Mbona basi nisijaribu hili? Nitajioa mimi mwenyewe."

Bintiye Fideli, Donna Pennington, alikubali wazo hilo kwa shauku na kuchukua jukumu la kuanza kuandaa hafla hiyo.

Familia ilipanga kwa uangalifu mavazi maridadi, upishi, na mapambo ili kuhakikisha sherehe  hiyo inafana kwa kiasi chake.

Fideli alikiri kukumbana na hisia za woga na msisimko kwa wakati mmoja, kama vile bibi harusi yeyote yule.

"Hili ni jambo jipya kwangu. Sijawahi kuolewa namna hii hapo awali. Ni hisia mseto kwangu kwa sababu hili ni jambo ambalo nimekuwa nikitamani kwa muda mrefu."

JAMAA AVUNJIKA MOYO BAADA YA MPENZIWE ALIYEDHANIA KUWA NA MIMBA YAKE KUZAA MTOTO WA KIHINDI


Mwanamume mmoja Mkenya ameelezea uchungu wake baada ya mpenzi wake aliyedai kuwa na mimba yake kujifungua mtoto mwenye asili ya Kihindi.

Akisimulia masaibu yake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, mwanamume huyo alikuwa amejawa na machungu  akisimulia jinsi mpenzi wake alimdanganya kuwa ana uja uzito wake

Alisikitika kuwa licha ya kuwa mpenzi alimyejali sana katika kipindi chote cha ujauzito wake na kukidhi mahitaji yake yote alimzalia mtoto mwenye asili ya Kihindi

Akisimulia masaibu yake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, mwanamume huyo alikuwa amejawa na machungu.

alisema aliumia sana moyoni mpenziwe aliyedhania kabeba uja uzito wake alijifungua mtoto wa kiume wa Kihindi hospitalini dhahiri kwamba alikuwa akimdanganya.

Huku mmoja wa wafuasi wake kwenye Twitter akimuuliza iwapo katika familia yake kuna watu wenye asili ya Kihindi, alisema mpenzi wake alikuwa mhudumu katika mkahawa mmoja wa Kihindi na kumfanya afikiri kwamba ndipo alipomlaghai na kupata motto.

Alisikitika kuwa licha ya kuwa mpenzi alimyejali sana katika kipindi chote cha ujauzito wake na kukidhi mahitaji yake, baadaye aligundua kuwa mtoto huyo hakuwa wake.

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA BENKI YA CRDB KWA KUTOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI KUIMARISHA USALAMA KWA WATALII JIJINI ARUSHA

 

 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa (wa pili kushoto) akiwa katika pikipiki zilizokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha kwa ajili ya kusaidia katika doria na kuimarisha ulinzi na usalama kwa watalii. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya Arusha, Felician Mtahengerwa (wa kwanza kulia), na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.
 
========   ========   =========

Arusha Tarehe 18 Mei 2023 - Serikali imeipongeza Benki ya CRDB kwa kutoa msaada wa pikipiki 15 kwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha ili kuimarisha doria zitakazoongeza usalama kwa watalii wanaokuja nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Utalii na Maliasili, Mohamed Mchengerwa alipopokea pikipiki hizo zenye thamani ya TZS 40 milioni kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia kilichopo jijini hapa.
Waziri amesema sekta ya utalii ina umuhimu mkubwa katika uchumi na maendeleo ya wananchi nchini kwani ndiyo inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni, ikiwa ya pili kwa kuchangia kwenye Pato la Taifa (GDP), na ya tatu kwa kutoa ajira.

“Ripoti za Benki Kuu Tanzania (BOT) zinaonyesha sekta ya utalii inaendelea kuimarika baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO-19. Mapato yatokanayo na utalii kwa Machi yalifikia Dola za Marekani bilioni 2.787 ikilinganishwa na dola milioni 885 kipindi kama hicho mwaka 2021. Katika mwezi huo, jumla ya watalii 1,574,630 waliingia nchini,” amesema Mchengerwa na kuongeza huku akipongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Samia katika kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Royal Tour.

“Kipeeke kabisa naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa msaada huu wa pikipiki 15 ambao Benki yetu ya CRDB imeutoa kwa kituo chetu hichi. Pikipiki hizi zitawawezesha askari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Askari watakabiliana haraka na dharula jambo litakalosaidia kuimarisha usalama kwa watalii na kuifanya nchi yetu kuwa kivutio kikubwa hivyo wageni wengi kuja kuitembelea.” 
Mwaka 2020, sekta ya utalii ilichangia asilimia 10.6 kwenye pato la taifa ila kiasi hichi kilishuka hadi asilimia 5.7 mwaka 2021 kutokana na athari za UVIKO-19 hivyo kuilazimu Serikali kuchuku ahatua za makusudi kuifufua kwa kufuata taratibu za Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanya matangazo kimataifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe kurekodi filamu ya ‘The Royal Tour.’

Ili kuhakikisha usalama wa watalii wanaokuja nchini, Serikali ilianzisha kitengo maalum cha utalii na diplomasia kwa ajili ya kuwahudumia watalii na wanadiplomasia wanaofika nchini kutalii ama kuwekeza kwa haraka.

Kwa kuwa jiji la Arusha ndio kitovu cha utalii nchini, kituo hicho kimejengwa huko na askari wake walipewa mafunzo ya ziada ndani na nje ya nchi juu ya namna bora ya kuhudumia watalii. Vituo vingine vidogo vimefunguliwa katika wilaya za Arumeru, Karatu, Monduli na Longido.
Akikabidhi pikipiki hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa amani, utulivu na usalama katika maendeleo ya nchi kiuchumi, kijamii na kisiasa hivyo ni jukumu la jamii nzima kushiriki kuuimarisha.

“Pamoja na kuwepo hali ya amani na utulivu nchini, bado baadhi ya matukio ya uhalifu hujitokeza kama vile vile uporaji wanaofanyiwa raia hata watalii wanaokuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini. Ili Jeshi la Polisi litekeleze majukumu yake kwa ufanisi linahitaji vitendea kazi vya kutosha,” amesema Nsekela.

Mkurugenzi huyo amesema wanayo furaha kubwa kukabidhi pikipiki hizo ili kuwasaidia askari kukimbizana na wahalifu wanaowapora watalii au kusafirisha mihadarati hivyo kuharibu sifa njema za jiji hili la kitalii.
“Tunaamini matumizi sahihi ya pikipiki hizi yatasaidia kudhibiti uhalifu jijini hapa na tunaahidi tutaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kupunguza baadhi ya changamoto zinazokwamisha ufanisi wake ili nchi yetu iendelee kuwa salama kwa biashara na uwekezaji,” amesema Nsekela.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Edith Swebe, amesema jitihada zinazoendelea kuutanga utalii wa Tanzania umelifanya Jiji la Arusha kupokea wageni wengi wanaoongeza haja ya askari polisi kuwapo katika kila eneo.
“Tunachokifanya sasa hivi ni kusimamia mradi wa utalii salama ambao unahitaji askari kuwapo kila walipo wageni. Pikipiki hizi tunazozipokea zitasaidia kuwafikisha askari kwenye maeneo ambako magari hayawezi kufika kwa urahisi zikiwamo barabara nyembamba. Jeshi la Polisi linaaminimazingira salama ni kivutio cha utalii,” amesema Edith ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu.

Hata hivyo, ameiomba Serikali na wadau wengine wa utalii kuliwezesha jeshi hilo kupata pikipiki nyingine 10 zitakazofanya kata zote 25 za Jiji la Arusha kuwa na pikipiki moja ya doria itakayosaidia utekelezaji wa mradi wa utalii salama. 









KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AMFAGILIA KOKA KWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KWA WANANACHI.

 


Na Victor Masangu,Kibaha 


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Abdalah Shaib amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuweza  kuchochea maendeleo ya wananchi katika nyanja mbali mbali ikiwemo elimu pamoja na afya.

Pongezi hizo amezitoa mara baada ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ikiwemo kuweka jiwe la msingi katika maktaba na jengo la utawala katika shule ya sekondari Mwambisi forest.

Kiongozi huyo alibainisha kwamba ameridhishwa na mradi huo na kudai kumetokana na juhudi mbali mbali zinazofanya na Baraza la madiwani,kwa kushirikiana na Mbunge wao kwa lengo la kuweza kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo
Aidha kiongozi huyo wa mbio za Mwenge alimpongeza mkuu wa Wilaya ya Kibaha pamoja na jopo lake lote kwa kuanzisha miradi ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia wananchi.

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akitoa salamu zake kwa kiongozi wa mbio za Mwenge alisema kuwa katika shule hjyo ya Mwambisi alishachangia kufanikisha mradi wa ujenzi wa darasa moja ili Wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki.

Kadhalika Mbunge huyo aliongeza kwamba ataendelea kusaidia na kuchagiza kasi ya maendeleo kwa wananchi wa Jimbo lake katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu,afya,maji,miundombinu ya barabara na huduma nyingine za kimaendeleo.

Nao baadhi ya wananchi wamepongeza ujio wa Mwenge wa Uhuru ambapo wamesema unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuzindua miradi na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbali mbali ya maendeleo na mingine imepata fursa ya kuetembelewa.


Mbio za Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya Kibaha mji zimeweza kukagua na kupitia miradi 12 ya maendeleo katika nyanja tofauti zikiwemo,afya,elimu,maendeleo ya jamii,barabara sambamba na mapambank dhidi ya madawa ya kulevya,ukimwi,rushwa,na malaria.

TIRA YAIKABIDHI BENKI YA CRDB LESENI YA KUANZISHA KAMPUNI TANZU YA BIMA CRDB INSURANCE COMPANY LTD

 

 Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware (wapili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela leseni ya kuanzisha kampuni tanzu ya huduma za bima CRDB Insurance Company Ltd katika hafla iliyofanyika leo katika hoteli ya Gran Melia jijini Arusha. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Insurance Company, Gerald Kasato (wakwanza kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Insurance Company, Wilson Mnzava.
 
=============   ===========    ============
 
Arusha 17 Mei 2023 - Katika kutanua huduma za bima nchini, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeipa Benki ya CRDB leseni kuanzisha kampuni tanzu ya kampuni ya bima ijulikanayo kama CRDB Insurance Company (CIC) Ltd hivyo kuwa benki ya kwanza nchini kumiliki kampuni kamili ya bima.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi leseni hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha, Dkt Baghayo Saqware, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kukua katika utoaji wa huduma za bima kutoka kuwa wakala mpaka kampuni kamili ya bima.

“CRDB Insurance ni mtoto mpya kwenye soko la bima na mtoto mwingine kwa Benki ya CRDB kwenye soko la fedha nchini. Inafurahisha kuona mnakua kutoka hatua moja kwenda nyingine. Naamini ndani ya miaka mitano ijayo mtaenda kwenye hatua nyingine kubwa zaidi ya hii. Kuna fursa kubwa kwenu kukua katika soko letu,” amesema Dkt. Saqware.

Dkt. Saqware alisema kwa uzoefu ambao Benki ya CRDB inao katika sekta ya bima, TIRA ina imani CRDB Insurance Company (CIC) Ltd itakwenda kusaidia utekelezaji wa lengo la Serikali la kuchochea ujumuishi wa wananchi kwenye huduma za bima ili Watanzania wanaotumia bidhaa zake wawe walau asilimia 50 ifikapo mwaka 2030 kutoka asilimia 18 ya sasa.

“Katika kuchochea ujumuishi wa kibima Serikali imepitisha sheria ya kufanya baadhi ya bima kuwa za lazima ikiwamo bima ya majengo, makandarasi, afya, na za vyombo vya usafiri. Mkiweza kuja na mkakati madhubuti wa kuchangamkia vizuri maeneo haya na kuhudumia kwa walau asilimia 30 niwahakakikishie ndani ya kipindi kifupi mtatoka kuwa kampuni changa na kuwa moja ya kampuni kubwa za bima nchini,” amesema Dkt Saqware.
Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema ni furaha kubwa kwao kupata leseni ya huduma za bima za jumla yaani ‘general insurance’ ukiwa ni muda mfupi tangu walipopata leseni ya kutoa huduma za benki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Benki ya CRDB inayo historia kubwa ya kufanya biashara ya bima kwani takriban miaka 15 iliyopita imekuwa ikiifanya kwa namna tofauti ikianza kama wakala na sasa ni kampuni kamili ya bima. Mafanikio haya yanadhihirisha mazingira rafiki ya kufanya biashara nchini,” amesema Nsekela.

Nsekela amesema kampuni ya CRDB Insurance Company itajikita katika ubunifu wa bidhaa na huduma za bima za jumla “general insurance” kwa kuzingatia viwango vilivyo bora na kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wananchi walio wengi ili kuchcohea maendeleo ya uchumi wa nchi. 

“Malengo yetu ni kuwa kiongozi katika sekta ya bima nchini kama ilivyo kwa Benki yetu na kampuni zetu tanzu nyengine. Lakini ili kuwa kiongozi ni lazima tuweze kutoa huduma zilizo bora na za mfano katika soko, lazima tuweze kuwekeza katika miundombinu ya usambazaji na uuzaji wa bima ikiwamo kuwatumia mawakala, madalali, banc assurance, na majukwaa ya kidijiti kuuza bima. Naomba nikuhakikishie Kamishna tumejipanga kutekeleza hayo yote,” amesema Nsekela.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Insurance Company Ltd, Wilson Mnzava amesema wamejipanga kikamilifu kuanza kutoa huduma za bima kwa wananchi kuanzia bima zote za jumla huku akielezea kuwa tayari kampuni hiyo imeshaanza mchakato wa kuleta huduma bunifu za bima katika sekta za kimakati nchini ikiwamo sekta ya kilimo.

“Napenda kuwakaribisha Watanzania wote binafsi, taasisi, na kampuni kupata huduma katika kampuni yao ya CRDB Insurance Company Ltd. Niwahakikishie wananchi kwamba CRDB Insurance Company Ltd ndio chaguo sahihi kwao. Tumejiandaa kikamilifu kuwahudumia. Nikuahidi Kamishna kuwa kampuni yetu itashirikiana kwa karibu na TIRA kuboresha huduma na kuyafikia matarajio ya sekta ya bima kwa ujumla,” amesema Mnzava.

Taarifa za TIRA zinaonyesha mpaka Desemba 2022, kulikuwa na kampuni 32 za bima nchini hivyo CRDB Insurance Compaany Ltd inakuwa kampuni ya 33. Katika kipindi hicho, pia kulikuwa na mawakala wa bima 1,500, benki 32 zinazotoa huduma za bima na kampuni tano zinazotoa huduma za bima kidijitali.

Kwa sasa sekta ndogo ya bima inachangia asilimia 1.68 kwenye pato la taifa, malengo yaliyopo ni kufikisha asilimia tatu hadi mwaka 2030 na dalili za kufanikisha hilo zinaonekana kwani mwaka 2022 tozo za bima zilizolipwa (premiums) zilikuwa na thamani ya TZS 1.154 trilioni kutoka TZS 913 bilioni mwaka 2021.

 



Wednesday, May 17, 2023

YANGA WALEEE FAINALI SHIRIKISHO AFRIKA YAIFUMUA MARUMO NYUMBANI KWAO 1-2

 NA ALBERT G.SENGO/SPORTS RIPOTI

NGOMA imesoma Gallants Marumo 1-2 Yanga ukiwa ni mchezo wa hatua ya nusu fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika. Kazi kubwa imefanywa na wachezaji wote wa Yanga wakiongozwa na Nasreddine Nabi ambaye ni Kocha Mkuu. Ni Fiston Mayele alianza kupachika bao la kuongoza kwa Yanga dakika ya 44 kisha ngoma ikapachikwa na Kenned Musonda dakika ya 67. Musonda alimalizia kazi ya Mayele na kufanya Yanga kuwa mbele kwa jumla ya mabao 4-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa Yanga ilishinda mabao 2-1. Bao pekee la Marumo iliyokuwa nyumbani limefungwa na Chivaviro dakika ya 90 lakini ni la kufutia machozi tu. Yanga wanatinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni kazi kubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi. Historia imeandikwa, hongereni Yanga, HONGERA TANZANIA

Tilioni 3.1 zatumika katika miradi 14 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru kibaha vijijini



Na Victor Masangu,Kibaha 

MWENGE wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi katika mradi wa Maji wa Ruvu Stesheni ambao uliibuliwa na wananchi baada ya mradi wa awali kutokidhi mahitaji ya sasa.


Mradi huo ambao unatarajia kukamilika June mwaka huu unatekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)  Wilaya ya Kibaha kwa gharama ya sh.Miln 328.7.
 
Akitoa taarifa wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika katika mradi huo kuweka jiwe la Msingi Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kibaha Mhandis Debora Kanyika amesema mradi huo umehusisha ujenzi wa tenki la maji la lita 50,000 juu ya mnara wa mita 12.

Aidha amesema mradi huo unaendana na kampeni ya Kitaifa ya kusogeza huduma karibu na wananchi ili kumtua mama ndoo kichwani na kwamba kila ndoo ya lita 20 itauzwa kwa sh. 40.


Amesema awali mradi huo ulikuwa unahudumia na unaunganishia wananchi maji nyumbani na kwenye Taasisi  na sasa mradi huo umeongeza wanufaika wapya  waliokuwa mbali na huduma ya maji.


"Ndugu kiongozi wa Mbio za Mwenge mradi huu ukikamilika utahudumia wananchi kwa miaka 20 ambapo utatoa huduma kwa wananchi hadi kufikia kaya 520 kwa mwaka 2042" amesema.


Mhandisi Debora amesema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa vituo sita vya kuchotea maji, nyumba ya mtambo na utandazaji wa mabomba umbali wa km 3.7


Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru  umezindua vyumba vitano vya Madarasa ambavyo vinalwenda kutatua tatizo la.msongamano uliotokana na ongezeko la wanafunzi kutokana na sera ya elimu bila Malipo

Mwenge wa Uhuru umepitia miradi 14 yenye thamani ya sh. Trillion 3.1kati ya fedha hizo sh. Miln 193.5 mchango wa Halmashauri, sh. Biln 5.9 kutoka Serikali kuu  na Trilion 3.1 nguvu za wananchi na michango ya mwenge ni sh. Miln 3.1.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2023 Abdallah Shaib amepongeza miradi ya utunzaji wa mazingira inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo ikiwemo upandaji miti unaoendelea kwenye Taasisi na maeneo mbalimbali.

Tuesday, May 16, 2023

MAMA ALIYENASWA KWENYE VIDEO AKIMLISHA MTOTO WA KAMBI KINYESI AKAMATWA

 


Mwanamke mwenye umri wa miaka 26, ambaye alinaswa kwenye video akimlisha mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 4, kinyesi amekamatwa

 

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na polisi nchini Uganda Jumatatu, Mei 15, mwanamke huyo anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Jinja ambapo kesi ya kuteswa na unyanyasaji wa watoto ilifunguliwa dhidi yake.

 

Video hiyo ambayo tarehe yake ya kurekodiwa haijulikani, inamuonyesha mwanamke huyo ambaye polisi wamemtambua kwa jina la Esther Nabirye, akimlazimisha mtoto huyo kula kinyesi chake baada ya kudaiwa kujisaidia haja kubwa kwenye sebule.

 

Msemaji wa polisi, Fred Enanga alitaja vitendo vya Nabirye kuwa vya kinyama na visivyo vya kibinadamu.

 

Polisi walisema mvulana huyo atapelekwa kwenye makazi ya dharura ya watoto

MWENYEKITI UVCCM TANGA ATEMBELEA MRADI WA BBT KATIKA CHUO CHA MLINGANO MATI MUHEZA ATOA NENO

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM) Ramadhan Omary kulia akiwa na jembe akishiriki kulima na vijana kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mohammed Kawaida wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM) Ramadhan Omary kushoto akiangalia namba vitalu vya miche vilivyopandwa na vijana kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mohammed Kawaida wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).

Na Oscar Assenga, MUHEZA


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM) Ramadhan Omary leo amefanya ziara ya kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Tanga kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mohammed Kawaida kutembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).


Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Mwenyekiti huyo aliwataka vijana kuitumia fursa hiyo ya uwepo wa chuo hicho kwa manufaa yao binafsi na jamii inayowazunguka kwasababu serikali imetumia gharama kubwa kujenga kwaajili ajili ya kuwanufaisha na kuwaajiri Vijana kwenye sekta ya Kilimo,


Alisema kwamba mradi huo wa BBT ni moja kati ya miradi iliyotupa heshima kubwa vijana hivyo watahikishe wanaufanye kwa ustadi na uaminifu mkubwa ili uweze kuleta tija


Mwenyekiti hiyo alitumia fursa hiyo kushauri uongozi wa chuo kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wakulima wa maeneo ya hayo na maeneo ya karibu kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima wa Maeneo hayo na kuweza kukuza kilimo bora kwa jamii inayokuzunguka,


"Mkoa wetu unafursa nyingi za kilimo kaimu mkuu wa chuo angalieni namna chuo hiki kitaweza kuwanufaisha vijana/ jamii inayo wazunguka ili tuwe na kilimo chenye tija"Alisisitiza Omary


Aidha katika hatua nyengine Omary aliwataka Makada wa CCM na Vijana wa Chuo cha Mati Mlingano kwa niaba ya vijana wote wa Tanga kuwa namna pekee ya Kumlipa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia kuyasema mazuri anayoyafanya na kuyatangaza mema anayoyafanya kwa Watanzania wote kiujumla kwani ameyafanya mengi kwa ajili ya Watanzania.

"Kwa kweli sisi kama vijana katika mkoa wa Tanga tunapongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu hivyo kama vijana lazima tuzitangaze kazi hizo tusiishie kusema mama anaupiga mwingi "Alisema Mwenyekiti huyo

"Lakini pia tumuombe Mungu atujalie viongozi wengi mithili ya Bashe kwa sababu unamuona kabisa anaguswa na changamoto za vijana na jamii ya Kitanzania"Alisema