Akiwa na umri wa miaka 77, Dorothy Fideli amefanya sherehe ya kipekee ya harusi kusherehekea penzi lake kwa nafsi yake mwenyewe.
Fideli alijifungisha ndoa katika sherehe ya harusi katika karamu ya
kusisimua iliyojaa mbwembwe na mahanjam ya aina yake.
hafla hiyo ilifanyika katika
Ukumbi wa Wastaafu wa O'Bannon Terrace huko Goshen, Ohio.
Akiwa amezingirwa na wapendwa wake, bibi
aliyejawa furaha alikubali utimilifu wa hamu yake ya ndani: yaani kujioa
mwenyewe.
Baada ya kufunga ndoa mnamo
1965, alitalikiana na mumewe baada ya miaka tisa.
Fideli alijikwaa na wazo
hilo lisilo la kawaida wakati wa ziara ya kanisa na bila kupoteza muda
akamwendea Rob Geiger, meneja wa mali katika nyumba hiyo ya wastaafu, ili
kuongoza sherehe hiyo ya aina yake.
Alisema:"Wazo fulani
lilinijia siku moja kanisani kwamba unapaswa kujifanyia jambo fulani maalum.
Nikasema, unajua nini? Nimefanya kila kitu kingine maishani. Mbona basi
nisijaribu hili? Nitajioa mimi mwenyewe."
Bintiye Fideli, Donna
Pennington, alikubali wazo hilo kwa shauku na kuchukua jukumu la kuanza kuandaa
hafla hiyo.
Familia ilipanga kwa
uangalifu mavazi maridadi, upishi, na mapambo ili kuhakikisha sherehe hiyo inafana kwa kiasi chake.
Fideli alikiri kukumbana na
hisia za woga na msisimko kwa wakati mmoja, kama vile bibi harusi yeyote yule.
"Hili ni jambo jipya
kwangu. Sijawahi kuolewa namna hii hapo awali. Ni hisia mseto kwangu kwa sababu
hili ni jambo ambalo nimekuwa nikitamani kwa muda mrefu."
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.