ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 18, 2023

MBIO ZA MWENGE ZARIDHISHWA NA MIRADI YOTE 12 YA HALMASHAURI YA KIBAHA MJINI.



Na Victor Masangu,Kibaha 


Halmashauri ya mji Kibaha mkoani Pwani imetumia kiasi cha shilingi bilioni 3.9 katika kutekeleza miradi 12 ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya,elimu,miundombinu ya barabara,pamoja na mambo mengine ya huduma za kijamii.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon wakati alipokuwa akitoa taarifa ya miradi ambayo itatembelewa katika mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka wa 2023.

Mkuu huyo aliongeza kuwa alisema kwamba Mwenge huyo utaweza kupita katika katika miradi mbali mbali ambapo baadhi yao itawekewa mawe ya msingi,kutembelewa pamoja na kuzinduliwa.

"Katika halmashauri ya Kibaha mji tumetembelea miradi yapatayo 12 ya maendeleo ambayo jumla yake imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.9 ambapo fedha nyingine kati ya hizo zimetoka kwa wadau wengine wa maendeleo,"alisema Nikson.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Kibaha mji Mshamu Munde alisema kwamba miradi ambayo wameianzisha watahakikisha kwamba wanailinda na kuitunza kwa hali na mali kwa lengo la kuwasaidia wananchi.


Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalah Kaim ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuweza kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo ambayo imegusa maslahi ya wananchi kwa ujumla.
Pia ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kuulaki Mwenge wa Uhuru Mwaka huu kwani unakuja kuangazia Maendeleo yanayoendelea kutamalaki kwenye Halmashauri za Mkoa wa Pwani  ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Mbio za Mwenge wa Uhuru umeweza kukimbizwa katika halmashauri ya mji Kibaha katika sekta mbali mbali ikiwemo,afya,elimu,miundombinu ya barabara,maji,mapambano dhidi ya madawa ya kulevya pamoja na marelia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.