Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan akiongea na waandishi wa habari baada ya kutelea mabanda kadhaa katika maonyesho ya nanenane mkoani Lindi
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wanawake wa Mkoa wa Lindi wilaya ya Nachingwea
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan amesema amejipanga kuandaa mpango kabambe wa kuwakomboa wanawake wa huo kiuchumi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wiki ya nane nane Mikoa ya nyanda za kusini, mbunge huyo alisema kuwa amewaona wanawake wengi wakishughulisha na shughuli mbalimbali za kujikomboa kiuchumi alipotembelea mabanda ya moenyesho hayo.
Mbunge Pathan alisema kuwa amefarijika kuona wanawake wengi wamejikita kwenye shughuli za kukuza uchumi hivyo ameamua kuandaa mpango kabambe wa kuwaongezea ujuzi wanawake wa Mkoa wa Lindi.
Alisema kuwa mkoa wa Lindi unafursa nyingi za kiuchumi hivyo ni lazima kuwapatia elimu ya uchumi na ujasiliamali wanawake wa Mkoa huo.
Alimazia kwa kuwataka wanawake kuendelea kujikita kufanya shughuli za kimaendeleo bila uoga wowote ule.