ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 3, 2023

BUGANDO WANAUMIZA VICHWA KUBAIN CHANZO KANDA YA ZIWA KUWA NA IDADI KUBWA YA WATOTO WENYE UTUMBO NJE

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Bugando inapokea watoto si chini ya 290 kwa mwaka wanazaliwa wakiwa na utumbo nje na wengi wao huko nyuma walikuwa wanapoteza maisha. Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Watoto Wanaozaliwa na Utumbo Nje Duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dk. Fabian Massaga amesema kwa dunia takwimu zimeeleza kati ya watoto 4000 wanaozaliwa mmoja anakuwa na changamoto hiyo.

"Hapa Bugando kama hospitali ya kanda kwa mwaka mzima tunapokea wastani wa watoto 290 wenye changamoto ya utumbo nje" "Kwa mwezi siyo chini hya watoto 10, kwa wili watoto wa 3 hadi wa 5, sasa unaweza kuona jinsigani tatizo ni kubwa" amesema Dkt Massaga. Daktari Mkuu kitengo cha Upasuaji wa Watoto Dkt Langa Michael ametoa ushauri kwa akina mama wanapokuwa wajawazito kufanya kipimo cha Ulta Sound ili kugundua tatizo hilo mapema kwa watoto wao kabla ya kujifungua. Dkt. Neema Neema Kayanga ni Mkuu wa Idara ya watoto "Tusiishie tu kupunguza madhara tata kwa kuwaasa akinamama wajawazito kuchukuwa vipimo mapema kabla ya kujifungua, bali pia kama madaktari kupitia takwimu tulizonazo tunalo jukumu na wajibu la kujikita katika kufanya tafiti ili kubaini kwa nini idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na tatizo la utumbo nje nchini wanatokea Kanda ya Ziwa!?" "Tufanyeje, mbona Kanda nyingine tatizo hili ni dogo?"


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.