ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 19, 2015

KIZIMBANI KWA KUPELEKA WANAWAKE KENYA KUFANYA BIASHARA YA NGONO.

Picha kutoka maktaba.
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
WANAWAKE wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kusafirisha mabinti kutoka Tanzania kwenda Kenya kwa ajili ya kuwafanyisha ngono.
Washtakiwa hao Jackline Milinga (23) na Mary Amukowa (29) ambaye ni Mkenya walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka ya kuwasafirisha mabinti 10.
Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Waliarwande Lema na Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori na Selestine Makoba walidaiwa kutenda makosa hayo Septemba 4 mwaka huu.
Nyantori alidai washtakiwa kwa pamoja, Septemba 4 mwaka huu maeneo ya Magomeni na Makumbusho waliwaajiri mabinti hao kumi na kuwasafirisha.
Inadaiwa waliwaajiri Najma Suleiman, Leah Mussa, Zulfa Ally, Rahma Mohammed, Salima Komba, Angelina Banzi, Leila Chorobi, Elizabeth Nalimu, Amina Abdi na Sada Hussein.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuwasafirisha mabinti hao kutoka Tanzania kwenda Kenya kwa shughuli za ngono huku wakijidai kuwa waliwapeleka kufanya kazi.
Inadaiwa mabinti waliokuwa wakipelekwa Kenya ni wenye umri kuanzia miaka 18 mpaka 22.
Washtakiwa waliposomewa mashtaka hayo walikana kuhusika lakini walirudishwa rumande kwa sababu mashtaka hayo hayana dhamana.
Hakimu lema aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 30 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
CHANZO: MTANZANIA

JE WAANDISHI WA HABARI WANAITENDEA HAKI TASNIA YA HABARI KIPINDI HIKI CHA KAMPENI?


Kutana na meneja wa maadili kutoka baraza la habari MCT akielezea mwenendo wa vyombo vya habari kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Friday, September 18, 2015

NAVY KENZO KUKAMUA LEO NDANI YA CLUB ROCK BOTTOM MWANZA.

Leo Ijumaa ndani ya Club Rock Bottom kutakuwa na Special Game Party ambapo kundi la Navy Kenzo linaloundwa na wakali wawiliAika na Nahreel. Pichani Aika akizungumza katika mahojiano ndani ya kipindi cha DRIVE MIXX ya Jembe Fm Mwanza.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHIJIRI.
Leo Ijumaa ndani ya Club Rock Bottom kutakuwa na Special Game Party ambapo kundi la Navy Kenzo linaloundwa na wakali wawiliAika na Nahreel. Pichani Nahreel akizungumza katika mahojiano ndani ya kipindi cha DRIVE MIXX ya Jembe Fm Mwanza.
Mpango mzima soma bango.

SERIKALI YAAGIZA SHULE ZIFUNGWE KENYA

Mwalimu shuleni
Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia Jumatatu huku mgomo wa walimu ukiendelea.

Walimu wamekuwa wakiishinikiza serikali kuwalipa nyongeza ya mishahara ya asilimia 50 hadi 60.
Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia Jumatatu huku mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.
Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT ameambia BBC kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.
Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule “zamani”.
Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali au la.
CHANZO: BBC SWAHILI.

TEMEKE WATINGA NUSU FAINALI

Mchezaji wa timu ya Ilala Rukia Annaph (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1
Mchezaji wa timu ya Ilala Tumaini Michael (Kulia) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17). Temeke iliibukana na ushindi wa magoli 2-1.
Mchezaji wa timu ya Ilala Jackline Albert (Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1.

Temeke watinga fainali ARS.
Temeke girls jana walifanikiwa kutinga hatua ya fainali, baada ya kuwagaragaza majirani zao wa Ilala kwa kuwafunga mabao 2-1 katika muendelezo wa michuano ya U-17 ya Airtel Rising Stars, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Ilala ambao walionekana kuumiliki mpira kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi cha kwanza walifanikiwa kuandika bao lao mnamo dakika ya 1 baada ya Tumaini Michael kuachiashuti na kutinga wavuni huku kipa wa Temeke akiwahana la kufanya.

Alamanusra Ilala wapate bao la pili manmo dakika ya 20 baada ya Tumaini Michael tena kupiga mpira wa kichwa ambao ulipaa kidogo langoni mwa Temeke.

Katika kipindi cha pili, Temeke walionekana kucharuka huku wakicheza kwa kasi kubwa, na ndipo mshambuliaji wa timu hiyo, Shamimu Hamisi mnamo dakika ya 40, alipomalizia kwa umaridadi mpira uliotemwa na kipa wa Ilala na kuukwamisha moja kwa mojawavuni na kusawazisha goli.

Temeke waliofanikiwa kuandika goli la pili mnamo dakika ya 61 kupitia kwa Asia Juma na kudidimiza matumaini ya Ilala kutinga hatua ya fainali.

Baada ya mchezo huo kocha wa Ilala Omari Bwezi alisema: “Tumekubali matokeo, wachezaji wangu walicheza vizuri kipindi cha kwanza lakini walionekana kuchoka sana kipindi cha pili na kuwapa nafasi ya kutawala wenzetu na ndio maana tukafungwa”.


Naye kocha wa Temeke Daudi Siang’a alisema: “Vijana wangu walifuata niliyowalekeza wakati wa mapumziko na waliporudi uwanjani walifanya nilicho waeleza na hatimaye tukapata matokeo”.

MKUTANO WA KAMPENI YA MGOMBEA WA URAIS CCM DR. ALI MOHAMED SHEIN JIMBO LA MKOANI PEMBA

Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai alipowasili katika viwanja vya mkutano vya Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba kwa ajili ya kampeni yake kwa wananchi wa Jimbo hilo la Mkoani.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Siasa jukwaa kuu baada ya kuwasili katikac viwanja hivyo kwa ajili ya mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya mpira Black Wizard Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Mkutano wake wa Kampeni Jimbo la Mkoani Pemba.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM katika viwanja vya Mpira Black Wizard Chokocho Pemba ,
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, akizungumza na Wananchi wa Wilaya Mkoani Jimbo la Mkoani Pemba akiwatambulisha Viongozi waliofuatana na Dk Shein wakati wa Mkutano wake wa Kampeni Pemba.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Pemba Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Mberwa Hamad Mberwa akizungumza wakati wa Mkutano huo wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
WanaCCM wakishangilia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM uliofanyika katika viwanja vya mpira Black Wizard Chokocho Pemba Wilaya ya Mkoani.
 Mhe Zainab Omar akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mkoanni wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Chokocho, kumuombea Kura Rais wa Zanzibar Dk Shein kwa Wananchi wa Pemba ili kuendelea kupata maendeleo kupitia CCM.
Mhe Pandu Ameir Kificho akiwasalimia Wananchi wa Pemba Wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanbja vya Chokocho Mkoani Pemba.
Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia Wana CCM katika mkutano wa kampeni wa CCM katika viwanja vya Black Wizard Chokocho Mkoani Pemba na kuwataka wananchi kumchagua Mgombea wa CCM Dk Shein.
Viongozi wa Jukwaa kuu wakiinua mikono wakati wa mkutano huo kuashiria kumpigia kura Mgombea wa Urais wa Zanzibar mgombea wa CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni.
Mhe Mohammed Aboud Mohammed akiwahutubia WanaCCM Kisiwani Pemba wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi kuelezea Sera za CCM na mafanikio yaliopatika katika Uongozi wa Rais Dk. Shein, na kuwataka kumchagua kwa mara ya Pili Dk. Shein kuendelea kuleta maendeleo kwa Wananchi wake katika sekta mbalimbali za Jamii Zanzibar
Viongozi wa Jukwaa kuu wakisimama wakati Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akipanda jukwaani kuwahutubia Wana CCM katika mkutano wake wa kampeni kisiwanin Pemba uliofanyika katika viwanja vya mpira vya black wizard mkoani Pemba.

Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mkoani kisiwani Pemba wakati wa mkutano wake wa Pili kisimwani Pemba kuomba ridhaa za kuchaguliwa tena kwa mara ya pili kuongoza Zanzibar kwa maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali za kijamii.
Baadhi ya Wanachama wa CCM Pemba wakimshangilia Mgombea wa CCM Dk Shein wakati akiwahutubia katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba, wakati wa mkutano wake wa kampeni kisiwi humo.  
Mwanachama wa CCM akiwa katika viwanja vya kampeni akimsikiliza Mgombea wa CCM Dk Shein akiwa na picha ya mgombea Urais wa Zanzibar wakifuatilia mkutano huo.
Viongozi wa meza kuu wakifuatlia hutuba ya Mgombea wa Urais wa CCM Dk Shein wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya black wizard chokocho Mkoani Pemba.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mgombea wao wa CCM wakati akiwahutubia katika mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba katika viwanja vya black wizard chokocho Mkoani Pemba.
Viongozi wa Jukwaa kuu wakifuatilia mkutano wa kampeni wakati akihutubia Wananchi wa kisiwani Pemba katika mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, akiwahutubia Wananchi wa Pemba katika mkutano wake wa Kampeni kisiwani huo uliofanyika katika viwanja vya mpira black wizard Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mkoani Pemba Profesa Makame Mbarawa,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya mpira black wizard mkoani Pemba. 
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Mtambile CCM Ndg Khamis Salum Khamis wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kiwani CCM Ndg.Rashid Abdalla,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Chambani Pemba Ndg. Mohammed Abdrahaman. Mwinyi,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mkoani Pemba. CCM Ndg Mmanga Mgengo,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mtambile Pemba. CCM Ndg. Mgaza Mohammed,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Chambani Pemba. CCM Bi.Bahati Khamis Kombo,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiwani Pemba. CCM Ndg Mussa Fumu Mussa,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Udiwani katika Wilaya ya Mkoani Pemba kupitia CCM, kwa Wananchi na kuwataka kuwapigia kura ya Ndio wakati wa uchaguzi Mkuu mwezom Oktoba 2015. wakati wa  mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mwanachama wa CCM akiwa na vyazi lake la kitenge la jengo la ASP wakati huo kwa sasa ni CCM akifuatlia mkutano huo, vitenge hivi vimetoka wakati wa miaka ya 70 kisiwani Zanzibar. 

Shekh akisoma dua baada ya kumalizikia kwa mkutano wa mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya black wizard chokocho
Viongozi wa jukwaa kuu wakiitikia dua baada ya kumalizikika kwa mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Wananchi wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa kampeni ya Urais kisiwani Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM akisalimiana na Vijana waliohidhuria mkutano huo wa kampeni yake katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Kijiji cha Chokocho kisiwani Pemba baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni ya Urais katika Jimbo la Mkoani Pemba.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot. zanzinews.com

MSAFARA WA SUGU WASHAMBULIWA KWA MAWE AKIELEKEA KATIKA KAMPENI ZAKE ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA

Gari la Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Sugu likiwa kituo cha Polisi kati jijini Mbeya mara baada ya kushambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Sugu akiwa kituo cha Polisi na wafuasi wake.Picha Kenneth Ngelesi Mbeya .
(JAMIIMOJABLOG MBEYA )


Na Emanuel Kahema ,Mbeya

MGOMBEA ubunge  kupitia chadema jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi leo  amejikuta katika wakati mgumu baada ya msafara wake kushambuliwa na mawe na wafuasi wanaosadikiwa kuwa ni wa chama   cha mapinduzi CCM na kwamba katika tukio hilo watu wawili wamejeruhiwa akiwemo dereva aliyekuwa akimuendesha mgombea huyo  .


Tukio hilo la kushambuliwa kwa msafara huo, limetokea majira ya saa 11 za jioni katika eneo  la barabarani lililopo katika Kata ya Ghana mtaa wa Mbata jijini hapa  ambapo inasemekana mgombea huyo alikuwa  katika harakati za kampeni kuomba kura kwa wananchi wa Iziwa  ambapo mgombea huyo alikuwa ndani ya gari yake yenye namba za usajili T161 CPP Toyota  Land Cruser VX .


Awali, wafuasi wa chama cha mapinduzi CCM, walikuwa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wao ngazi ya Udiwani katika kata ya Ghana iliyopo ndani ya Jiji la Mbeya, hivyo wakiwa kwenye harakati hizo inasemekana walishangaa kuona msafara wa sugu ukipita katikati ya mkutano huo hivyo kushindwa kuvumilia na kuanza kurusha mawe huku wengine wakishikana mithili ya kutaka kupigana.



Katika vurugu hizo gari aliyokuwa amepanda mgombea huyo  lilipasuliwa kioo cha mbele na gari ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mbeya, ikipasuliwa kioo cha mbele .

Aidha Vurugu hizo zimesababisha   majeruhi wawili ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya akiwemo dereva wa mbunge huyo na mfuasi mmoja wa chadema.


Kutokana na hali hiyo  mgombea huyo wa ubunge mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema alilazimika kuikatisha zoezi lake la kuongea na wakazi wa Kata ya Iziwa iliyopo Jijini Mbeya kwa muda, kutokana na kulazimika kuripoti katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.


Mgombea huyo ilimlazimu kufika kituoni na kuchukuliwa maelezo na baada ya hapo aliruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kisiasa lakini gari yake yenye namba za usajili T161 CPP aliyokuwa akiitumia katika kampeni zake ikibaki polisi.


Hata hivyo, mgombea huyo alipomaliza kutoa maelezo  katika kituo cha polisi cha kati cha Wilaya ya Mbeya, aligoma kuzungumza na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa kwenye eneo la tukio na kuwataka wafike katika mkutano kwani ndipo atakapotolea ufafanuzi wa suala hilo hilo.

MWALIMU HOSEA DANIEL KUTOKA FOLUMA TUITION CENTRE AELEZA UMUHIMU WA MASOMO YA ZIADA

Pichani ni Mwalimu Hosea Daniel kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.
Na:Binagi Media Group
Mwl.Daniel anasema kuwa Masomo ya ziada ni mhimu kwa mwanafunzi kwa kuwa husaidia katika kukuza uelewa na ufahamu kwa mwanafunzi na hivyo kuongeza ufaulu kwa mwanafunzi.
Pichani ni Mwalimu Hosea Daniel kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.
Kushoto ni Madam Elizabeth Daniel akiwa pamoja na Mwalimu Hosea Daniel. Wote ni kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.
Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) Foluma Tuition Centre kilichopo Bomani-Tarime Mkoani Mara ni mkombozi kwa wanafunzi wa darasa la awali pamoja na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wakati wa likizo.
Kutana na Mwl.Hosea Daniel, Madam Elizabeth Daniel, Mwl.Evance Malaba pamoja na Mwl.Malima Mjinja kwa maendeleo ya mwanao kielimu.
0755 77 82 47