Temeke
girls jana walifanikiwa kutinga hatua ya fainali, baada ya kuwagaragaza majirani
zao wa Ilala kwa kuwafunga mabao 2-1 katika muendelezo wa michuano ya U-17 ya
Airtel Rising Stars, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam.
Ilala ambao walionekana kuumiliki mpira kwa kiasi kikubwa
sana katika kipindi cha kwanza walifanikiwa kuandika bao lao mnamo dakika ya 1
baada ya Tumaini Michael kuachiashuti na kutinga wavuni huku kipa wa
Temeke akiwahana la kufanya.
Alamanusra Ilala wapate bao la
pili manmo dakika ya 20 baada ya Tumaini Michael
tena kupiga mpira wa kichwa ambao ulipaa kidogo langoni mwa Temeke.
Katika
kipindi cha pili, Temeke walionekana kucharuka huku wakicheza kwa kasi kubwa, na
ndipo mshambuliaji wa timu hiyo, Shamimu Hamisi mnamo dakika ya 40, alipomalizia
kwa umaridadi mpira uliotemwa na kipa wa Ilala na kuukwamisha moja kwa mojawavuni
na kusawazisha goli.
Temeke waliofanikiwa
kuandika goli la pili mnamo dakika ya 61 kupitia kwa Asia Juma na
kudidimiza matumaini ya Ilala kutinga hatua ya fainali.
Baada
ya mchezo huo kocha wa Ilala Omari Bwezi alisema:
“Tumekubali matokeo, wachezaji wangu walicheza vizuri kipindi cha kwanza
lakini walionekana kuchoka sana kipindi cha pili na kuwapa nafasi ya
kutawala wenzetu na ndio maana tukafungwa”.
Naye kocha wa Temeke Daudi Siang’a
alisema: “Vijana wangu walifuata niliyowalekeza wakati wa mapumziko na
waliporudi uwanjani walifanya nilicho waeleza na hatimaye tukapata matokeo”.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.