Friday, January 28, 2011
HABARI
Mwanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wa Uganda ambaye mwaka jana alilishtaki gazeti lililomtoa kwa jinsia yake hiyo amepigwa mpaka kufa. Polisi wamethibitisha kifo cha David Kato (pichani kulia) na kusema wamemkamata mshukiwa mmoja.
Gazeti la Uganda la Rolling Stone lilichapisha picha za watu kadhaa ambao walisema ni wapenzi wa jinsia moja na huku pembeni kukiwa na kichwa cha habari "WANYONGENI"
Kumekuwa na wimbi la matukio ya "mauaji kutumia chuma" huko Mukono, alipokuwa akiishi Bw Kato, ambapo watu wamekuwa wakiuliwa na vipande vya chuma. Walioshuhudia wanasema kwamba mtu mmoja aliingia nyumbani kwa Bw Kato karibu na Kampala, na kumpiga mpaka kumwuua kabla hakuondoka. Polisi wamesema licha ya kumkamata mshukiwa mmoja, mshukiwa mkuu- ambapo wanasema alikuwa akiishi naye amekimbia.
GAZETI LILILO MWAGA DATA:-Kundi lake liitwalo (Smug) limesema Bw Kato alikuwa akipata vitisho tangu jina, picha na anwani yake kuchapishwa na Rolling Stone mwaka jana. Nae Frank Mugisha, mkurugenzi mtendaji wa kundo hilo, amesema kuwa "ameshtushwa" kupata habari hizo kutoka New York. "Marehemu alikuwa na wasiwasi na vitisho alivyokuwa akivipata hivi karibuni".
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria Uganda, na adhabu ya miaka 14 jela. Hivi karibuni mbunge mmoja alijaribu kuongeza adhabu kwa kuwepo kwa hukumu ya kifo kwa baadhi ya makosa.
Shirika la kutetea haki za binadamu (HRW) lilitoa wito wa kufanyiwa uchunguzi kwa kifo chake.
Thursday, January 27, 2011
BANGO
Umeona eeeh... don'Miss this @ The place.
SOUND INACHAPA KISAWASAWA KILA KONA, PLACE INARUHUSU, WATU WANAPENDEZA, WANANUKIA, NYUSO ZA RAHA WACHA ZITAWALE, YAAAaaaNI NI UTAMU TU!
'PRAKATATUMBA' Ijumaa na Jumamosi hii!
SIMTAKUJA EEEeeH!
SEMA SAWaaaaaa!!..!!
KITU KINAPATIKANA ENEO LA CAPRIPOINT KARIBU NA UWANJA WA TENIS MWANZA CLUB, UKIFIKA UTAONA MAZINGIRA MAZuuuuRI.!! KWA MASUALA YA MISOSI, BITES, VINYWAJI AINA ZOTE, MAPOCHOPOCHO, TAKE AWAYS, 'BASI HAPA UMEFIKA'
FOR MORE INFO. CHEKI BANGO HAPO JUU.
Thursday, January 27, 2011
HABARI
Idhaa ya BBC ya World Service imetangaza mipango yake ya kufunga idhaa tano zinazotangaza kwa lugha mbali mbali- Kiserbia, Albania, Macedonia, Kireno kwa Afrika pamoja na idhaa inayotangaza kwa lugha ya Kiingereza huko Caribbean. Inakadiriwa idadi ya wasikilizaji itapungua kwa zaidi ya milioni 30 kutoka wasikilizaji milioni 180 wa sasa.Mkurugenzi mkuu wa BBC World Service, Peter Horrocks, amesema hatua hii inafuatia mpango wa serikali wa kupunguza ufadhili wake. Hata hivyo ameongezea kuwa bado atahakikisha BBC World Service itabakia kwenye nafasi ya juu katika kutoa habari.
Hatua hii ya BBC imeshutumiwa na Muungano wa Kitaifa wa waandishi wa habari (NUJ).
Akizungumza katika idhaa ya BBC Radio 4 hii leo, katibu mkuu wa NUJ, amesema idhaa ya World Service ni muhimu sana na inapaswa kulindwa ipasavyo.
CHARLES HILARY & SALIM KIKEKE. PICHANI KULIA--->
BBC World Service itasitisha matangazo yake kupitia ShortWave katika idhaa zingine sita ifikapo mwezi Machi, 2011 zikiwemo - Hindi, Indonesian, Kyrgyz, Nepali, Kiswahili pamoja na Maziwa Makuu.
Ingawa matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC kupitia Shot Wave yatasitishwa, tayari kuna ushirikiano wa idhaa hiyo na mashirika mengine ya utangazaji kupitia vipimo vya FM. Mipango ya sasa ni kuangazia zaidi ushirikiano kama huu pamoja na kupeperusha matangazo yake kupitia kwa mtandao na simu. Pia kuna mipango ya kuanza kushirikiana na vituo vya televisheni kupeperusha matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
HISANI YA BBC SWAHILI.
Bei ya vyakula inazidi kupanda kila kukicha huku wafanyabiashara na wananchi wakilalamikia hali hiyo inaongeza ukakasi wa maisha kwa watu wengi.
MFUMUKO WA BEI
-Mafuta ya kula :kwa lita, vibaba au chupa ya Orange
-Sukari
-Ngano
Kama mfumuko utaendelea ile hali kipato cha mwananchi katika usakaji wa ngawira au pengine mshahara unabaki pale pale, hakika wengi watashindwa kumudu maisha.
Wako.
'Mjini pachungu, kijijini pagumu'
Wednesday, January 26, 2011
CHEREKO
Ni siku ya jumapili ya tarehe 9 mwezi january 2011, katika kanisa katoliki Kawekamo jijini Mwanza, ndipo shughuli rasmi ya kumsimika Askofu Mkuu mpya jimbo la Mwanza, mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa'Ichi ilipochukuwa nafasi.
KADINARY PENGO (KUSHOTO) NA RUWA'INCHI.
Tukio hili la usimikwaji limekuja mara baada ya Taarifa zilizotoka mwishoni mwa mwaka jana kutolewa kutoka Ubalozi wa Vatican nchini kwenda kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ikielezea uteuzi huo na kufafanua kuwa Askofu Mkuu Ruwa’ichi anapaswa kwenda kuziba nafasi ya aliyekuwa Askofu wa jimbo hilo, Anthony Mayalla aliyefariki dunia Agosti 19, mwaka juzi.
Askofu Ruwa’ichi ambaye pia ndiye Rais wa TEC amekuwa mwanashirika wa watawa wa Mtakatifu Fransisco kwa kipindi kirefu.
Wageni waalikwa na wadau wa kanisa.
Wageni mbalimbali toka serikalini nao walipata mwaliko kuhudhuria sherehe hizo. Kutoka kulia Waziri Stephen Wasira, mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro, mama, mtoto, Mbunge wa Ilemela Mh.Hainnes Samson na Mh.Wenje mbunge wilaya ya Nyamagana.
Sifa na shukurani kupitia nyimbo.
Askofu Ruwa’ichi ambaye pia ni Rais wa TEC, alizaliwa Januari 30, 1954 katika Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro na alipata Daraja la Upadri Novemba 25, 1981 kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mbulu, Februari 9, 1999.
Kamati ya itifaki, mapokezi na usalama wa viongozi wa serikali ilisimamiwa barabara na wadau hawa:- kutoka kushoto Joseph Mlinzi ambaye ni afisa uhusiano wa jiji na Patrick Karangwa huyu ni mchumi wa jiji.
Wednesday, January 26, 2011
MICHEZO
Kampuni ya Sky imemtimua mara moja mchambuzi na mtangazaji wa soka Andy Gray.GRAY and KEYS.
Mchambuzi huyo ambaye tayari ameshapewa adhabu kwa matamshi yake yaliyolenga ubaguzi wa kijinsia dhidi ya mwamuzi mwanamke Sian Massey, kabla ya mchezo wa siku ya Jumamosi kati ya Wolves na Liverpool. Gray mwenye umri wa miaka 55 pamoja na mwenzake Richard Keys, waliondolewa kuchambua mechi ya Jumatatu kati ya Bolton na Chelsea. Na siku ya Jumanne, Sky walisema wanakatisha mkataba wa Gray kutokana na ushahidi mpya "usiokubalika wa matamshi ya utovu wa nidhamu."
Taarifa iliyotolewa na kampuni ya Sky imeendelea kueleza: "Ushahidi mpya, unaohusu matamshi yaliyotolewa kwenye televisheni mwezi wa Desemba mwaka 2010, yameunganishwa baada ya Andy Gray tayari kupewa adhabu ya utovu wa nidhamu kutokana na matamshi yake aliyoyatoa tarehe 22 mwezi wa Januari, 2011."
Mkurugenzi mtendaji wa Sky Sports, Barney Francis amesema: "Mkataba wa Andy Gray umesimamishwa kutokana na tabia yake isiyokubalika. Baada ya kutolewa onyo siku ya Jumatatu, tumeona hakuna haja ya kusubiri kuchukua hatua zaidi baada ya kupata taarifa mpya." Wakati huo huo Massey, ameondolewa kuwa msaidizi wa mwamuzi katika mechi ya siku ya Jumanne ya ligi daraja la pili kati ya Crewe na Bradford.
Tukio zima lilianza siku ya Jumamosi, wakati Keys na Gray, walipoamini vipaza sauti vyao vimezimwa, na wakanukuliwa wakisema mwamuzi huyo Massey na waamuzi wasaidizi wengine wanawake, "hawafahamu sheria ya kuotea". Keys alimpigia simu Massey, ambaye alikubali kuombwa radhi na mtangazaji huyo.
Hata hivyo picha nyingie iliyoneshwa katika televeshini, siku ya Jumatatu ambapo Gray alizungumza na mwandishi wa Sky Sports, Andy Burton kuhusiana na Massey.
Sky iliripoti watu hao wawili walikuwa wakizungumzia kuhusu mwamuzi Massey muonekano wake, huku Burton akimwita Massey "ni mrembo anayevutia" wakati Gray akihoji: "Wanawake wanafahamu nini juu ya sheria ya kuotea?"
Mapema siku ya Jumanne, ilitangazwa Burton "alizungumza na kuonywa" kuhusiana na matamshi yake na sasa hatahusishwa katika matangazo ya mpambano wa nusu fainali ya Kombe la Carling siku ya Jumatano, kati ya Birmingham na West Ham.
Tuesday, January 25, 2011
HABARI
TAREHE 22 majira ya saa 10:30 jioni. Watu wanne wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa katika ajali mbaya ya gari la abiria aina ya Toyota Costa lenye namba za usajiri T386 AMV lililoacha njia na kugonga mtu mmoja aliyekuwa pembezoni mwa barabara eneo la Msola kijiji cha Mwamagigisi wilayani magu, mkoani Mwanza.OCD NYAMAGANA LILIAN MATOLA.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza OCD Lilian Matola amewataja watu hao waliofariki dunia kuwa ni Visent Mashauri (54) mkulima, mkazi wa Nyakaboja Magu, na Ngokoli Eliasi (18) mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Busega wilaya ya Magu.
Wengine waliotajwa kufariki kwenye ajali hiyo ni pamoja na Diana Charles (34) mkulima, mkazi wa Nyalipungu Magu, na Magreth Busuma (28) mkazi wa Masanzakona wilayani Magu.
Aidha Kamanda Matola ameongeza kusema kuwa majeruhi watano kati ya tisa walionusurika na ajari hiyo wametoka hospitali ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu huku wengine wanne waliosalia wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo na hali zao zikiendelea vizuri
Nae dereva wa gari hilo Deonad Mashauri (26) mchana wa leo amefikishwa mahakamani kujibu shitaka ya kuendesha gari kwa mwendo kasi hata kusababisha ajali hiyo.
Tuesday, January 25, 2011
BANGO
Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi ambazo zina vifo vingi zaidi vya uzazi duniani. Zaidi ya wanawake elfu nane wanakufa kila mwaka kutokana na matatizo ya uzazi ( sawa na wanawake 22 kila siku).
-Pamoja na kupungua kwa kasi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano bado kila mwaka Tanzania watoto183,800 wanakufa, 45,000 kati ya hao ni watoto wachanga
-Kila siku watoto 500 chini ya umri wa miaka mitano wanakufa,123 kati yao ni watoto wachanga
-Kila saa watoto 20 chini ya umri wa miaka mitano anakufa
Vifo hivi vinasababishwa na malaria, utapiamlo,kuharisha, nimonia ,ukimwi na upungufu mkubwa wa damu na vile vinavyotokana na huduma duni ya uzazi.
Bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) imeonyeshwa kuchukizwa na upotevu wa shilingi milioni 340 na imekusudia kutomuongezea muda wa mkataba Mkurugenzi wake Justus Rwetebula baada ya kuelekea kumalizika .HUDUMA YA MAJI NYUMBA ZA VILIMA VYA mwanza.
Mmoja kati ya wajumbe ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa kwa ujumla Bodi imechukizwa na namna Mkurugenzi huyo alivyoshindwa kutoa taarifa kwa Bodi juu ya wizi huo uliofanywa na mhasibu wa MWAUWASA Moses Ndaki.
“Mara baada ya wizi huo kutokea Mkurugenzi aliamua kwenda likizo na kumwachia maelezo nusunusu aliyemwachia ofisi, unaweza kuona ni namna gani Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA asivyo makini na kazi yake ndiyo maana wajumbe wa Bodi kwa kauli moja tumeamua kutokumwongezea muda wa kazi baada ya kipindi chake kumalizika hivi karibuni wakati hatua nyingine za kiutendaji zikichukuliwa na mamlaka husika ambazo zimepewa jukumu la kuchunguza wizi huo na kuchukua hatua” alisema mjumbe.
Mjumbe huyo ameongeza kuwa kuna mtandao mkubwa wa wafanyakazi uliofanikisha wizi huo kwani fedha hizo inaonyesha zilikuwa zikiibiwa kwa awamu huku baadhi ya viongozi wakiwa kimya wakijua mchezo.
Kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Nonosius Komba amesema kuwa jeshi lake bado linamsaka mhasibu Moses ndaki aliyedaiwa kutoweka kazini baada ya kubainika wizi huo wa milioni 340.
Komba ameongeza kwa kusema kuwa polisi pia kwa kushirikiana na uongozi wa MWAUWASA bado wanachunguza kwa makini tukio zima ili wahusika waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi huo.
"Chandarua yangu ya chuma bwana"
Monday, January 24, 2011
BANGO
Monday, January 24, 2011
HABARI
Waziri Mkuu wa Tunisia, Mohammed Ghannouchi, amesema atastaafu shughuli za kisiasa haraka iwezekanavyo baada ya mhula wa mpito kumalizika na Tunisia kurejea katika mfumo rasmi wa kidemokrasia.MOHAMMED GHANNOUCHI.
Katika mahojiano na televisheni ya Tunisia siku ya Ijumaa, Bw Ghannouchi pia aliahidi sheria zote zisizoambatana na demokrasia nchini humo, zitafutwa katika kipindi hiki cha mpito.
Siku chache zilizopita, waandamanaji nchini Tunisia wamekuwa wakidai kuondoka kwa viongozi wote wa serikali ya zamani waliobaki madarakani. Serikali ya mpito nchini humo imesema imewaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa waliotiwa mbaroni wakati wa utawala wa Rais aliyetimuliwa, Zine El-Abidine Ben Ali.
Wakati huo huo vikosi vya usalama nchini Tunisia, vimejiunga na waandamanaji, katika mji mkuu Tunis. Wamesema wao ni sehemu ya watu kama walivyo wengine, na ni waathirika wa madhila kutoka kwa utawala wa zamani wa Rais ben Ali kama walivyo Watunisia wa kawaida. Hatua hii inaonekana ni maendeleo makubwa kufuatia wiki tano za harakati zilizomng'oa Rais Zine el-Abidine Ben Ali aliyeikimbia nchi wiki moja iliyopita.
Maafisa wa polisi binafsi, wanataka serikali ya mpito ijiuzulu kwa sababu imetawaliwa na viongozi waliokuwa katika utawala uliopita.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.