ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 28, 2011

SHOGA MAARUFU NCHINI UGANDA AUAWA .

Mwanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wa Uganda ambaye mwaka jana alilishtaki gazeti lililomtoa kwa jinsia yake hiyo amepigwa mpaka kufa. Polisi wamethibitisha kifo cha David Kato (pichani kulia) na kusema wamemkamata mshukiwa mmoja.
Gazeti la Uganda la Rolling Stone lilichapisha picha za watu kadhaa ambao walisema ni wapenzi wa jinsia moja na huku pembeni kukiwa na kichwa cha habari "WANYONGENI"

Kumekuwa na wimbi la matukio ya "mauaji kutumia chuma" huko Mukono, alipokuwa akiishi Bw Kato, ambapo watu wamekuwa wakiuliwa na vipande vya chuma. Walioshuhudia wanasema kwamba mtu mmoja aliingia nyumbani kwa Bw Kato karibu na Kampala, na kumpiga mpaka kumwuua kabla hakuondoka. Polisi wamesema licha ya kumkamata mshukiwa mmoja, mshukiwa mkuu- ambapo wanasema alikuwa akiishi naye amekimbia.


GAZETI LILILO MWAGA DATA:-Kundi lake liitwalo (Smug) limesema Bw Kato alikuwa akipata vitisho tangu jina, picha na anwani yake kuchapishwa na Rolling Stone mwaka jana. Nae Frank Mugisha, mkurugenzi mtendaji wa kundo hilo, amesema kuwa "ameshtushwa" kupata habari hizo kutoka New York. "Marehemu alikuwa na wasiwasi na vitisho alivyokuwa akivipata hivi karibuni".

Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria Uganda, na adhabu ya miaka 14 jela. Hivi karibuni mbunge mmoja alijaribu kuongeza adhabu kwa kuwepo kwa hukumu ya kifo kwa baadhi ya makosa.

Shirika la kutetea haki za binadamu (HRW) lilitoa wito wa kufanyiwa uchunguzi kwa kifo chake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.