ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 17, 2020

MONGELLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NIDA MWANZA AKUTANA NA OMBI KWENDA KWA MHE RAIS.


Wakati Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA ikiendelea na zoezi la usajiri na utambuzi wa raia, nao kupata namba zinazotumika kusajili laini zao za simu kwa alama ya vidole ili kuepuka kuzimiwa mawasiliano, nazo siku za ukomo wa zoezi hilo zikiwa zinatosha hata kuhesabika kwa vidole vya kiganja kimoja, kasi ya uzalishaji wa namba za utambulisho wa Taifa na vitambulisho sanjari na ugawaji wake kwa wananchi umeendelea kuathiri shughuli za ujasiliamali na uzalishaji kwa baadhi yao.

Alhamisi ya tarehe 16 Januari 2020 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella anafanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Mamlaka hizo mkoani hapa ambapo anakutana na misururu ya wananchi wakiwa wamesongamana kwenye mistari kulivaa lango kuu la ofisi hizo kwaajili ya kupatiwa huduma.


CCM Imesema haitakuwa tayari kuwavumilia wanasiasa ambao watakiuka kanuni za Uchaguzi.

Na Thabit Madai,Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Abdallah Juma Sadala  alimaarufu  Mabodi  amesema chama Cha Mapinduzi CCM hakitawavumilia wanasiasa ambao watakiuka kanuni na utaratibu wa uchaguzi.

Pia Mabodi ameiomba Ofisi ya Msajiri wa Vyama vya Siasa kuwachukulia hatua viongozi wa vyama vya Siasa ambao wanakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifungua Kongamano la Mafunzo maalumu kwa viongozi wa ngazi zote  Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi CCM.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi wa ngazi mbali za chama  ambapo limefanyika  katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakili kikwajuni Mjini Unguja.

Naibu katibu Mkuu Mabodi alisema kwamba huu ni wakati wa kuzungumza Sera na si wakati wa kubishana na kutishiana.

Alisema CCM haitaki Ugomvi na Chama wala mtu yoyote, CCM inashindana na Sera na maendeleo waliyoyafanya kwa kipindi chote cha uongozi wake.

“CCM hatuatamvumlia yule yoyote ambaye atakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa za uchaguzi, akati ukifika tubishane kwa hoja na Sera lakini si kubishana kwa vituko na kutoleana kauli na vitisho” Alisema Naibu katibu Mkuu Mabodi.

Alieleza kwamba katika kipindi hichi kuelekea Uchaguzi Mkuu tayari baadhi ya vyama vya upinzani kupitia viongozi wao wameshaanza kutoa kauli ambazo hazina niya njema za kulina amani ya Nchi.

Alisema kama chama cha Mapinduzi hawaridhishwi na kauli hizo ambazo zinatolewa na kuoba vyombo vya dola kuwachukulia hatua.

“Wao waache wahubiri fujo, vurugu sisi tutahubiri Sera zetu, tunanadi maendeleo ambayo tumeyafanya lakini watakapo kiuka taratibu zilizowekwa tunawaambia hatupo tayari kuwavumilia” Alisema Naibu katibu Mkuu Mabodi.

Mabodi aliiomba  ofisii ya Msajiri wa Vyama Siasa kusimamia vyema Sheria na kanun zake pamoja na kuwachukulia hatua  viongozi wa vyama vya siasa ambavyo wanakwenda kinyume na  kanuni na taratibu zilizowekwa.

“CCM Oyee, Kupitia nafasi hii leo nataka niseme wazi kuwa CCM haturidhishwi na yanayofanyika maana tunaona muelekeo waeo haupo vizuri , tunaona mapema” alisema Mabodi.

Hata hivyo katibu huyo  aliwafahamisha wana CCM  kwamba kuelekea uchaguzi Mkuu wanawajibu wa kuzingatia maadili na atakae kwenda kinyume na maadili CCM itawachukulia hatua.

“Tunakwenda kwenye uchaguzi wana CCM lazima mutambue hakuna mtu ambaye yupo juu ya Chama cha Mapinduzi  lakini mutambue kuwa tunaongozwa na kanuni na katiba ya chama chetu atake kwenda kinyume basi tutamchukulia hatua” alieleza Mabodi.

Alisema CCM ipo mbioni kutoa jarida maalumu ambal litatoa muongozo kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Alifahamisha kuwa ni vyema kufuata maadili ya uchaguzi katika kipindi Cha uchaguzi ili kudumisha amani na utulivu nchini ili  kuepuka migogoro na uchafuzi wa mazingira.

Hata hivyo mabodi aliwataka Jumuiya ya Wazazi ndani ya Chama hicho kuchukua fursa ya kuwaelimisha vijana kuhusu kufuata maadili kuelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Pia aliwaomba Jumuiya hiyo kuhakikisha wanaweka mipango kwa kushirikianna na Jumuiya nyingine ndani ya CCM kukiletea Ushindi Chama hicho.

Wakati huo huo Mabodi alisisitiza Wazazi kupiga Vita maswala ya unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili kuondosha vitendo hivyo nchini.

Nae katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa Shemsa Simon alisema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kuwajengea uwezo viongozi wa CCM katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kongamano hilo lilijadili mada tatu ambazo ni udhalilishaji wa kijinsia,maadili ya uongozi na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.

NYONGO AWAONYA WANAOWASUMBUA WAFANYABIASHARA WA MADINI


Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza kwenye mkutano na wadau wa madini katika ukumbi wa Mount Meru jijini Arusha.

Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki akizungumza jambo kwenye mkutano na wadau wa madini mwanzoni kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo anaefata ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akipewa maelezo na mfanyabiashara wa madini katika soko la madini jijini Arusha.
Balozi wa China nchini Tanzania Wang ke akizungumza kwenye mkutano na wadau wa madini katika ukumbi wa Mount Meru jijini Arusha
Balozi wa China nchini Tanzania akikabidhiwa zawadi kutoka kwa mfanyabiashara wa Madini.
 Baadhi ya Wajumbe walioshiriki katika mkutano wa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo jijini Arusha

NAIBU wa Madini Stanslaus Nyongo akitoa maelekezo kwa wafanyabiashara wa Madini jijini Arusha, mbele kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula na wapili kutoka kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha Mhandisi Khamis Kamando.
Na Tito Mselem Arusha,

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, ameonya tabia ya  baadhi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwakamata wafanyabiashara wa madini wenye vibali na wanaofata Sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali katika shughuli hiyo.

Kauli hiyo ameitoa  Januari 15,  jijini Arusha wakati  akifungua Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki na Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke pamoja na wadau wa madini uliolenga kujadili fursa za biashara katika sekta ya Madini.

“kumeibuka tabia ya kuwakamata na kuwasumbua wafanyabiashara wa madini ambao wengi wao wanavibali halali vya kumiliki madini hii ni kunyanyasa wafanyabiashara wasio na hatia, tumefungua 
masoko ya madini mikoani ili wafanyabiashara wetu wasinyanyasike”, alisema Nyongo.

Aidha, Nyongo, amewataka Polisi watakao kamata wafanyabiashara wakiwa na madini majumbani mwao, kuhakikisha wanawatumia Maofisa Madini ili kujua kama madini hayo yanavibali kwa kuwa sheria inaruhusu wafanyabiashara kukaa na madini ilimradi wanavibali na wafuate sheria.

Alisema ili kuondoa mkanganyiko huo, Wizara imejipanga kuelimisha wadau wa madini vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu sheria za madini ikiwemo inayoruhusu wafanyabiashara hao kushikilia madini kabla ya 
kuyauza katika masoko ya madini.

Pia, Nyongo aliwasisitiza Mabalozi wa China nchini Tanzania Wang Ke na yule wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki kuendelea kuhamasisha wawekezaji  kuwekeza nchini hususan  kwenye masuala ya uongezaji thamani madini chini ya gramu mbili ambayo yanaruhusiwa kwenda nje ya  nchi bila kuongezwa thamani.

"Kama mnateknolojia ya kuongeza thamani madini haya tunawaalika mje kuwekeza ili tusiyatoe nje bila kuongeza thamani,” alisema Nyongo.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Nyongo, amewahakikishia wawekezaji waliowekeza katika Sekta ya Madini mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuhakikisha anasimamia kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema mchango wa Sekta ya Madini katika pato la taifa bado ni mdogo hivyo ipo haja kuendelea kuyatangaza madini yetu na kushiriki maonyesho mbalimbali ya kimataifa.

Amesema serikali imeamua kutumia balozi zake katika kutangaza madini  yanayopatikana hapa nchini ikiwemo madini adimu ya Tanzanite.

Aidha, katika hatua nyingine Gambo, amewahakikishia wawekezaji kutoka China waliowekeza katika Mkoa wa Arusha, mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuwaahidi kwamba atasimamia kuondoa kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji hao.

Alisema nchi ya Tanzania ina madini mengi lakini mchango wake kwa pato la Taifa ni asilimia 5.07 tofauti na pato la Sekta ya Utalii asilimia 17 na asilimia 25 katika kulingizia Taifa fedha za kigeni.

"Mchango huu hautoshi hivyo tumeamua kutumia mkutano huu ili tuongeze fursa katika madini na kukuza zaidi pato la sekta hii," alisema Gambo.

Kuhusu ukusanyaji wa maduhuli ya serikali Gambo alisema yanatokana na soko la madini Namanga ambapo lilikusanya Shilingi bilioni 1.7 na soko la Arusha limekusanya Shilingi bilioni 34.46 katika kipindi cha Juni 2019 hadi Desemba 2019.

Naye, balozi wa Tanzania Nchini China, Mbelwa Kairuki amewataka wafanyabiashara wa madini nchini kujipanga kwa kutafuta viza mapema ili kushiriki soko la madini nchini china linalotarajiwa kufanyika Novemba 10 hadi 15 mwaka huu.

"China ni wanunuzi wakubwa wa dhahabu kama mwaka jana 2019 walinunua dhahabu tani 1506 hiki sio kiwango kidogo na hata madini mengine wananunua sana hivyo tujitahidi kuongeza fursa za soko nchini China,” alisema Kairuki.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula amewataka  Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa yote nchini kukaa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuelimishana kuhusu sheria za madini ili  wawe na namna bora ya pamoja ya kudhibiti utoroshaji wa madini nchini.

NAMBA ZA UTAMBULISHO NIDA MILIONI 6.8 HAZIJATUMIKA KUSAJILI LAINI ZA SIMU.


Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA inaendelea na zoezi la usajiri na utambuzi wa watu, uzalishaji wa namba za utambulisho wa Taifa na vitambulisho na ugawaji wake kwa wananchi zinazotumika kusajili laini za simu kwa alama za vidole na huduma nyingine zinazohitaji utambulisho.

NIDA imezalisha idadi kubwa ya namba za utambulisho wa Taifa kati ya hizo, namba za utambulisho wa Taifa 6,806,096 hazijatumika kusajili laini za simu kwa alama za vidole.



Tuesday, January 14, 2020

JAMBO FOOD PRODUCT CO LTD WAINGIZA BIDHAA 3 SOKONI KWA MPIGO


Jambo Apple Crush Soda, Jambo Ubuyu na Jambo Ukwaju ni bidhaa tatu zilizoingizwa sokoni hivi karibuni na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji baridi cha Jambo Food Products chanya maskani yake mjini Shinyanga nchini Tanzania. Hamis Salum ni mmoja kati ya Wakurugenzi waandamizi wa kiwanda hicho akiwa ameambatana na Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo hapa wanakupa taarifa zaidi. KUHUSU KIWANDA Kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda, juisi na maji kimejichukulia umaarufu wa bidhaa zake bora ambazo zinapendwa na watu wa rika zote kutokana na uhalisia wake. Kiwanda hicho ambacho kilizinduliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mnamo Januari 13, mwaka 2017, hadi sasa kimekuwa moja wa viwanda vya uzalishaji bidhaa bora za viwango vya kimataifa toka hapa nchini, vywenye radha murua kukufanya ujisikie fresh kabisa muda wote, kuupa mwili nguvu na mzuka zaidi, afya bora na kukuburudisha. Jambo wanazalisha na kusambaza vinywaji aina mbalimbali kwa jumla na rejareja. Vinywaji kama, Jambo Malta Lemon, Jambo Apple, Jambo Embe, Jambo Energy, Jambo Malta Pineapple, Jambo Lemon, Jambo Vito, Jambo Orange, Jambo Drinking Water na nyingine kibaooooo! Kiwanda cha Jambo kipo Shinyanga Mjini. Simu: +255622666692 au +255622666680 Email: info@jambogrouptz.net. Website: https://jambogroup.co.tz

DC MASASI ASEMA ATAKAYEPIGA KAMPENI KABLA YA WAKATI KUKIONA.



Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Selamani Mzee amepiga marufuku kwa kiongozi yeyote wa siasa wilayani humo kufanya kampeni za kisiasa kabla ya wakati kufika kwa ajili ya kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2020 badala yake wasubiri muda ufike ndipo wafanye hivyo.


Aidha, Mkuu huyo wa wilaya amewapa rungu viongozi wa Serikali za mitaa wilayani humo kutofumbia macho vitendo vya baadhi ya wanasiasa wilayani  ambao watajitokeza na kupinga agizo hilo na kwamba vyombo husika vya sheria vitafanya kazi yake.

Mzee alitoa agizo hilo jana wilayani Masasi  wakati alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa serikali ya mtaa wapiwapi-A mara baada ya mkuu huyo wa wilaya kujitokeza katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 wa raisi, wabunge na madiwani wapo baadhi ya wanasiasa wilayani Masasi wameanza kufanya kampeni kwenye maeneo yao wakati wakifahamu muda wa kufanya hivyo bado haujafika.

Alisema wenyeviti, watendaji na wajumbe wa serikali za mitaa wilayani Masasi katika kutekeleza majukumu yao wasisite kutimiza wajibu wao kwa kudhibiti vitendo vya aina hiyo kwa baadhi ya wanasiasa ambao wameanza kujitokea kwenye maeneo mitaa yao na kufanya kampen za kisiasa za uchaguzi kabla ya wakati kufika.

Mzee alisema viongozi wa serikali za mitaa kwenye maeneo yao washirikiane kwa nguvu moja kuhakikisha wanasiasa hao wanawadhibiti kisha wanawachisha tabia hiyo na badala yake wanatakiwa kusubiri muda ufike ndipo wafanye kampeni hizo kupitia taratibu husika ikiwemo za vyama vyao.

Alisema kitendo cha kufanya kampeni kabla ya muda muhafaka kufika ni kujiondolea sifa stahiki ya kugombea pindi muda wa kufanya hivyo utakapokuwa tayari umefika.

Mzee alisema kufanya hivyo ni kuvunja taratibu husika za uchaguzi na kwamba vyombo husika vitawachukulia hatua stahiki za kisheria.

Aidha, Mkuu wa wilaya huyo, ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa wilaya ya Masasi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya kurekebisha taarifa zao kama zinauhitaji wa kufanya hivyo.

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo hicho cha Mtaa wa Wapiwapi-A , Kulwa Mchelezo alisema zoezi hilo limeanza jana Januari 12 na hamasa ya watu kujitokeza kujiandikisha ni kubwa.

Alisema tangu zoezi hilo limeanza jumla ya watu 65 wamejitokeza huku zaidi ya wananchi 30 wakiwa ni wapya ambao umri wao kwa sasa unaruhusu kupiga kura.


Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni kwa ajili ya wale wanaotaka kurekebisha taarifa zao kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupotelewa kadi zao, kuharibika na wale ambao kwa sasa wamefikisha umri wa kupiga kura na wanahitaji vitambulisho hivyo ili kuweza kupiga kura.

JAMBO FOOD PRODUCT CO. LTD MWEKEZAJI MKUBWA SEKTA YA VIWANDA ALIYEAMUA KUJIKITA MKOANI SHINYANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amejipambanua kuwa na Sera ya Serikali ya Viwanda, Jeh kwa wawekezaji wa ndani, sera hii inawashika mkono kwa kasi gani na kuwavusha? Uchumi wa Viwanda ukiimarika, Uchumi wan chi utakuwa kwa kasi na matokeo yake yataonekana hasa kwenye kuongeza wigo wa soko la ajira. Jeh kuna usawa kati ya udhibiti bidhaa za nje ili kulinda viwanda vyetu vya ndani? Kwa majibu ya maswali haya na mengineyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Company Limited, Bwana Salum Hamis anafunguka zaidi…… KUHUSU KIWANDA Kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda, juisi na maji kimejichukulia umaarufu wa bidhaa zake bora ambazo zinapendwa na watu wa rika zote kutokana na uhalisia wake. Kiwanda hicho ambacho kilizinduliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mnamo Januari 13, mwaka 2017, hadi sasa kimekuwa moja wa viwanda vya uzalishaji bidhaa bora za viwango vya kimataifa toka hapa nchini, vywenye radha murua kukufanya ujisikie fresh kabisa muda wote, kuupa mwili nguvu na mzuka zaidi, afya bora na kukuburudisha. Jambo wanazalisha na kusambaza vinywaji aina mbalimbali kwa jumla na rejareja. Vinywaji kama, Jambo Malta Lemon, Jambo Apple, Jambo Embe, Jambo Energy, Jambo Malta Pineapple, Jambo Lemon, Jambo Vito, Jambo Orange, Jambo Drinking Water na nyingine kibaooooo! Kiwanda cha Jambo kipo Shinyanga Mjini. Simu: +255622666692 au +255622666680 Email: info@jambogrouptz.net. Website: https://jambogroup.co.tz

MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA AANAYEMALIZA MUDA WAKE BI.BELLA BIRD APONGEZA TASAF KWA MAFANIKIO YA KUPUNGUZA UMASKINI NCHINI.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga  (picha ya juu na chini ) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake nchini Bi. Bella Bird katika hafla ya kuagana naye .
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuagana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia aliyemaliza muda wake, Bi. Bella Bird alipofika kwenye ofisi ndogo za Mfuko huo jijini Dar es Salaam kuagana na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (hayupo pichani ) wakati alipofika katika taasisi hiyo kuagana nao baada ya kumaliza muda wake nchini.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bw.Ladislaus Mwamanga (aliyevaa tai) akimwongoza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake bi. Bella Bird kuingia katika ukumbi wa mikutano wa TASAF katika ofisi ndogo jijini Dar es Salaam.


Na Estom Sanga- TASAF- DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake Bi.Bella Bird amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF- kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kukabiliana na umaskini nchini.

Bi.Bella Bird amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa katika azma ya kuwaondolea wananchi wake kero ya umaskini jambo ambalo amesema limeijengea heshima kubwa serikali na hivyo kufanya mataifa mengine hususani ya bara la Afrika kuwavutiwa nayo. 

Mkurugenzi Mkazi huyo wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake ameyasema hayo alipokutana na Wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- katika Ofisi ndogo ya Mfuko huo jijini Dar es salaam ambako alikwenda kuagana nao baada ya kumaliza kipindi chake cha takribani CHA utumishi wa miaka minne hapa nchini. 

‘’ mataifa mengine ya Afrika yamekuwa yakija Tanzania kujifunza namna TASAF ilivyofanikiwa kuwafikia watu maskini kabisa kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini’’ amesisitiza Bi. Bella Bird. 

Amesema tafiti huru za ndani na nje ya nchini zilizofanywa zinaonyesha kuwa umaskini nchini Tanzania umepungua katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kuwa kinachotakiwa sasa ni kuhakikisha kuwa mafanikio hayo yanalindwa, kuboreshwa na kuendelezwa. 

Bi.Bella Bird amesisitiza kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF ni miongoni mwa miradi hiyo. 

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira yaliyosaidia Benki ya Dunia kukubali kufadhili shughuli za Mpango was Kunusuru Kaya Maskini. 

Bwana Mwamanga amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya sehemu ya kwanza yamewezesha Serikali kukubali kutekeleza sehemu ya pili ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameahidi kuwa taasisi hiyo imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali huku Mkazo ukiwekwa katika kuwashirikisha Walengwa katika kutekeleza miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira kama sehemu ya kuwaongezea kipato . 

Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ulianzishwa na Serikali kwa lengo la kusaidia wananchi kupitia utaratibu wa Kaya Maskini sana ili ziweze kujikimu kwa kupata mahitaji muhimu yakiwemo lishe, elimu na afya huku mkazo ukiwekwa katika kuziwezesha kaya za Walengwa kutumia sehemu ya ruzuku kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji mali ili kuinua kipato chao na kuboresha maisha yao. 

Monday, January 13, 2020

BODABODA WAFURAHIA SERIKALI KUWAKUMBUKA KUINGIZWA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)


Jumuiya za Wajasiriamali wadogowadogo na Waendesha Bodaboda nchini wamepongeza hatua ya kuanzishwa kwa vifurushi vya bima ya afya ambavyo vimewawezesha katika kupata matibabu ya uhakika pindi wanapoumwa. Wakiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya viongozi wa jumuiya hizo wamesema ilikuwa ni hitaji lao la muda mrefu la kuhakikisha wanachama wao wanakuwa na uhakika wa matibabu kwa kuwa na bima za afya. Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema mpango wa vifurushi umekuja kwa ajili ya kuwajumuisha watanzania wote.