ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 17, 2020

CCM Imesema haitakuwa tayari kuwavumilia wanasiasa ambao watakiuka kanuni za Uchaguzi.

Na Thabit Madai,Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Abdallah Juma Sadala  alimaarufu  Mabodi  amesema chama Cha Mapinduzi CCM hakitawavumilia wanasiasa ambao watakiuka kanuni na utaratibu wa uchaguzi.

Pia Mabodi ameiomba Ofisi ya Msajiri wa Vyama vya Siasa kuwachukulia hatua viongozi wa vyama vya Siasa ambao wanakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifungua Kongamano la Mafunzo maalumu kwa viongozi wa ngazi zote  Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi CCM.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi wa ngazi mbali za chama  ambapo limefanyika  katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakili kikwajuni Mjini Unguja.

Naibu katibu Mkuu Mabodi alisema kwamba huu ni wakati wa kuzungumza Sera na si wakati wa kubishana na kutishiana.

Alisema CCM haitaki Ugomvi na Chama wala mtu yoyote, CCM inashindana na Sera na maendeleo waliyoyafanya kwa kipindi chote cha uongozi wake.

“CCM hatuatamvumlia yule yoyote ambaye atakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa za uchaguzi, akati ukifika tubishane kwa hoja na Sera lakini si kubishana kwa vituko na kutoleana kauli na vitisho” Alisema Naibu katibu Mkuu Mabodi.

Alieleza kwamba katika kipindi hichi kuelekea Uchaguzi Mkuu tayari baadhi ya vyama vya upinzani kupitia viongozi wao wameshaanza kutoa kauli ambazo hazina niya njema za kulina amani ya Nchi.

Alisema kama chama cha Mapinduzi hawaridhishwi na kauli hizo ambazo zinatolewa na kuoba vyombo vya dola kuwachukulia hatua.

“Wao waache wahubiri fujo, vurugu sisi tutahubiri Sera zetu, tunanadi maendeleo ambayo tumeyafanya lakini watakapo kiuka taratibu zilizowekwa tunawaambia hatupo tayari kuwavumilia” Alisema Naibu katibu Mkuu Mabodi.

Mabodi aliiomba  ofisii ya Msajiri wa Vyama Siasa kusimamia vyema Sheria na kanun zake pamoja na kuwachukulia hatua  viongozi wa vyama vya siasa ambavyo wanakwenda kinyume na  kanuni na taratibu zilizowekwa.

“CCM Oyee, Kupitia nafasi hii leo nataka niseme wazi kuwa CCM haturidhishwi na yanayofanyika maana tunaona muelekeo waeo haupo vizuri , tunaona mapema” alisema Mabodi.

Hata hivyo katibu huyo  aliwafahamisha wana CCM  kwamba kuelekea uchaguzi Mkuu wanawajibu wa kuzingatia maadili na atakae kwenda kinyume na maadili CCM itawachukulia hatua.

“Tunakwenda kwenye uchaguzi wana CCM lazima mutambue hakuna mtu ambaye yupo juu ya Chama cha Mapinduzi  lakini mutambue kuwa tunaongozwa na kanuni na katiba ya chama chetu atake kwenda kinyume basi tutamchukulia hatua” alieleza Mabodi.

Alisema CCM ipo mbioni kutoa jarida maalumu ambal litatoa muongozo kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Alifahamisha kuwa ni vyema kufuata maadili ya uchaguzi katika kipindi Cha uchaguzi ili kudumisha amani na utulivu nchini ili  kuepuka migogoro na uchafuzi wa mazingira.

Hata hivyo mabodi aliwataka Jumuiya ya Wazazi ndani ya Chama hicho kuchukua fursa ya kuwaelimisha vijana kuhusu kufuata maadili kuelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Pia aliwaomba Jumuiya hiyo kuhakikisha wanaweka mipango kwa kushirikianna na Jumuiya nyingine ndani ya CCM kukiletea Ushindi Chama hicho.

Wakati huo huo Mabodi alisisitiza Wazazi kupiga Vita maswala ya unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili kuondosha vitendo hivyo nchini.

Nae katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa Shemsa Simon alisema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kuwajengea uwezo viongozi wa CCM katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kongamano hilo lilijadili mada tatu ambazo ni udhalilishaji wa kijinsia,maadili ya uongozi na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.