ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 28, 2013

Friday, December 27, 2013

MAKAMBA AWASIHI BODABODA WA MWANZA: URAHISI NA UHARAKA WA UPATIKANAJI LESENI USIWE TIKETI YA VIFO VYA WANANCHI.

NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha kupata pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.

Kauli hiyo ya Makamba ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.

Makamba amesema kwamba upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo  kwa wananchi (ZAIDI MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)

Awali kabla ya kongamano hilo madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano toka makao makuu ya ofisi zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani Nyamagana jijini Mwanza hadi katika uwanja wa historia wa Nyamagana.
Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana.
Ndani ya uwanja wa Nyamagana madereva wa Bodaboda wamejitokeza kiasi cha kutosha.
Huku wengine wakizidi kumiminika viwanjani hapa kuhudhuria kongamano lao.
Naibu wa Sayansi na Teknolijia ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mhe. January Makamba akiingia katika uwanja wa Nyamagana kushiriki kongamano la Bima ya Afya kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa mkoa wa Mwanza.
Kila mmoja viwanjani hapa alikuwa na kiu ya kusalimiana ana kwa ana na Naibu waziri huyo.
Licha ya kutoa elimu ya uelimishaji kujitambua kwa Bodaboda wa jiji la Mwanza ili kuepukana na maisha magumu uzeeni kwa wadau hao wa usafiri, Mkuu wa mkoa waMwanza Evarist Ndikilo ndiye aliye mkaribisha Mhe. Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia kuhutubia maelfu ya wadau hao. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evaris Ndikilo kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi aliwaasa bodaboda kufuata sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa umakini na kwa amani na utulivu huku wakihakikisha usalama kwanza katika kazi zao kwa kuwa wanatumia vyombo vya moto.

Injinia Ndikilo aliwataka pia kufuata sheria za barabarani kutokana na kuwepo watumiaji wengine, kuwa waangalifu na abiria wengine wanaowachukua kutokana na baadhi yao kuwateka na kuwafanyia ukatili, kuwauwa na kuwanyanganya pikipiki zao nyakati za usiku na kuwataka kukataa kushiriki katika shughuli za uhalifu na badala yake wawabaini na kuwatolea taarifa kwa viongozi na jeshi la polisi.

Makamba alisema kuwa kupatikana kwa Bima za Afya kutatawezesha wanaopata ajali kupatiwa matibabu na kupata fidia pindi wanapopata ajali na kupata ulemavu na kifo jambo ambalo ni hakika lazima wakubali kukata bima kutoka Kampuni ya Ndege Insurance na Shirika la Bima la Taifa (NIC) yaliyokubali kuingia mkataba na wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza. 
Ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuachana na tabia ya manyanyaso kwa waendesha pikipiki ya kuwabambikia kesi na makosa bali washirikiane nao kuwabaini walio wachache wanaojipenyeza kujifanya ni bodaboda kumbe ni wanaofanya vitendo vya kihuni, uhalifu na wizi kwa kivuli cha bodaboda jambo ambalo litasaidia pia kuwabaini wanaovunja sheria taritibu zilizopo.
“Mimi leo nimekubali kuwa Mlezi wenu lakini kila kijana lazima amiliki pikipiki yake mwenyewe badala ya kuwa mtu wa kuajiliwa tunahitaji kila mmoja ajiajili kwa kuwa na chombo chake, kazi ya pikipiki iwe ya usalama isiwe leseni ya kifo na ulemavu, msije mkadanganywa na baadhi ya watu kuwa watawatetea bali sisi wa viongozi wa Serikali Taifa, Mkoa, Wilaya na Jiji na kuweni makini kwa kufuata sheria za usalama” alisisitiza
Tangu kuingia mkataba na Kampuni ya Tanzania China Dev Ltd wamefanikiwa kuwakopesha 1745 na awamu ya kwanza umoja umlikopesha pikipiki 265, awamu ya pili 450 na awamu ya tatu pikipiki 1000 na wanachama wapatao 1745 wamenufaika na kupata ajira .
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alikuwa ni mmoja kati ya viongozi walioshiriki zoezi la kuendesha bahati nasibu ya waendesha bodaboda 100 waliobahatika kuandikishwa Bima ya Afya bure katika kongamano hilo.
Zoezi la bahati nasibu ya Bima ya Afya linaendelea na waliobahatika ndiyo hawa waliokuwa wakifika mbele katika mstari.
Mwakilishi toka jeshi la polisi na bahati nasibu ya Bima ya Afya.
Kongamano hilo limelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya kufuata sheria za usalama barabarani, kusoma na kupata cheti na hatimaye leseni, kuhimiza kuvaa kofia ngumu, kuhimiza kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuhimiza waendesha pikipiki kufuata taratibu zote zilizowekwa na serikali kwa wanachama wa wilaya za Sengerema, Nyamagana, Ilemela , Kwimba, Ukerewe, Magu na Misungwi.
Ndikilo kusanyikoni.

Burudani ndani ya Kongamano hazikukosekana.
Wadau walikuja na vyombo vyao.
No Parking.

MAKAMBA AKUTANA NA MAASKOFU NA WACHUNGAJI MWANZA:AZITAJA SIFA ZA KIONGOZI WA TAIFA.

Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na baadhi ya Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa Mwanza katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa.
Bishop Alex Lwakisumbwa ambaye ni mwenyekiti wa P.C.T mkoa wa Mwanza akizungumza  katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba.  
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa jiji la Mwanza Bishop Charles Sekelwa akizungumza  katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba. 
Sehemu ya baadhi ya baadhi ya watumishi wa Mungu waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba. 
Hafla ikiendelea katika ukumbi wa Victoria Palace Hotel jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa The Great Zone Entertainment Fabian Fanuel (kulia) akitoa utambulisho wa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni yake, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba.
Meneja wa The Great Zone Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa matarajio ya Kampuni.
Katika hafla hiyo Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akiwa mbele ya Maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya jijini Mwanza wakiwemo wafanyabiashara, aliridhia ombi la kuwa mlezi wa Kampuni ya The Great Zone Entertainment.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa makanisa ya Kikristo mkoa wa Mwanza Askofu Zenobius Isaya (Pentecoste) akizungumza  namna umoja wake ulivyolipokea wazo la ukuzaji wa majukwaa ya waimbaji wa muziki wa injili na sanaa ya jiji la Mwanza toka kwa Kampuni ya The Great Zone Entertainment
Baadhi ya Maaskofu.
Bahati Bukuku naye alikuwa sehemu ya waalikwa kwenye hafla hiyo.
Sala ya kuhitimisha hafla.
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba katika picha ya pamoja na wadau ambao huvutiwa na utendaji wake kutoka kushoto ni Ahmed Ibrahim kutoka Musoma, Bi Helen Kaji ambaye ni Meneja Kampuni ya Kinengena Agro and Minerals Logistics ya jijini Dar es salaam na Pilly Mgori wa Clouds Fm Mwanza.
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika hafla hiyo.
MWANZA:Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema taifa lipo katika kipindi Kigumu hivyo kuwataka maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali nchini kuiombea nchi yetu ili ipate kiongozi mwenye sifa zinazotajwa katika Biblia.
Akizungumza kwenye Hotel ya Victoria Palace katika Hafla ya chakula cha usiku kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayoshughulika na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, alisema ameamua kusema haya kwa mbele ya Maaskofu na Wachungaji ambao aliwaita watu wazito wenye kuaminiwa na kuheshimiwa katika jamii.
Hafla hiyo iliudhuriwa na Askofu Zenobius Isaya ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo mkoa wa Mwanza,  Askofu Alex Mwakisumbwa mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentokosti (P.C.T) pamoja na Askofu Charles Sekelwa ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa makanisa ya Kikristu mkoani Mwanza.
“Taifa linapita katika kipindi kigumu, linajaribiwa linapita kwenye wakati mgumu, ….Ndugu zangu yakusema yapo mengi, lakini nadhani tuzungumze machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu wote ni watanzania hapa na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu,” alieeleza.
Alisema nchi yetu inahitaji kuponywa, ili ianze upya (Reset) na kubainisha kuwa katika kuanza upya kama Taifa linahitaji aina ya viongozi wenye sifa za kama za viongozi wa dini ambazo zimebainishwa ndani ya Biblia na jukumu hilo kuhakikisha akiongozi wa sifa hizi anapatikana wqanalo wachugaji.
“Taifa lipo katika changamito kama rushwa, wizi, ubakaji, kumomonyoka kwa maadili  na ninyi viongozi wa dini mnaziona na kukabiliana nazo  kila siku, jamii yetu hii kwa sasa uongo umzidi, ubakaji umezidi, wizi umezidi mauaji yamezidi sasa nini kinaendelea na kutokea na kwa nini maovu yanaongezeka juu yetu?” alihoji Makamba.
Alisema katika hali kama hii kuna kipindi Mungu hukasirika na kutoa adhabu, hivyo kutaka Gharika pamoja na Sodoma na Gomola zilikuwa ni adhabu za Mungu kutokana na watu kupitiliza katika maovu hivyo adhabu ya kwanza ilikuwa ya Maji na ya pili ilikuwa Moto, hatujui inayofuata kwa nchi yetu itakuwa ya nini, japo kama Taifa hatutegemei kufuka huko.
Alieleza kwamba moja kati ya ujumbe wake kwa viongozi hao ni kama kizazi cha sasa ama taifa tunahitaji uponyaji wa hali ya juu na kwamba katika uponyaji huo viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa sana ya kuiponya nchi hii ili iepuke adhabu kama za nyakati hizo zilizotolewa na Mungu.
“Shughuli za siasa zimeingiliwa na Matapeli, lakini hata shughuli yenu pia imeingilia na matapeli vilevile sasa tunapotafuta uponywaji wan chi yetu ninyi mnanafasi kubwa sana kwani uponyaji tunaoongea ni wa maovu ya kiroho, uongo ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mnanafasi kubwa sana. Viongozi wa siasa pia tunayo nafasi wote tunanafasi lakini ili tufanikiwe na nchi ipone lazima viongozi wa siasa wawe wasafi,” alieleza.
Alisema Askofu ama mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi, na hata katika uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya wananchi ama yeye ni nyezo ya matatizo ni vizuri kumtazama sura yake kama ameacha (maovu).
Tunapoomba uongozi wa kisiasa zipo sifa kwani tunaomba kuongoza watu wa mungu ambao ni wale wale wanaokuja Makanisani ndiyo wanaokuja katika siasa, kuongoza watu wa mungu siyo kitu kidogo maana hata mamlaka ya serikali yametambuliwa hivyo lazima vigezo vya kuongoza watu hawa view vikubwa sana.
“Katika Biblia zinataja sifa za mtu atendae kazi ya Askofu ngoja nizisome (1 Timotheo 3.1)  zinasema … mtu akitamani kazi ya Askofu, atamani kazi nzuri. Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. Asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha,” alisema na kuongeza katika siasa hatutafuti askofu lakini ni lazima sifa zifanane na hizi za askofu na kuwataka viongozi hao wa makanisa kuzisoma sifa hizo kila watu wanapopita kwao kutafuta uongozi wa nchi na kila mtu anayetafuta uongozi lazima ajipime kwa sifa hizi.
Alisema hata hivyo kumekuwa na mjadala mkubwa wa sifa za uongozi kuhusu kijana, uzoefu na kubainisha kwamba amekuwa akitoa mwito kwa vijana ambao hawana makandokando washiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.
Makamba aleleza vijana wengi wamekuwa waoga waoga, wengi wamekuwa wakidai kutokuwa na fedha, uzoefu lakini maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo na siwezi.
“Yeremia alipopewa unabii alilalamika mimimi mdogo mimi siwezi, lakini mungu alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) ….Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa,” alifafanua na kuongeza kuwa bwana alimwambia “Usiseme, ‘mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe.”
Kutokana na kauli hiyo ya Januari Makamba Askofu Jacoub Lutabija alisema amepokea ujumbe mzito ambao atakwenda kuutangaza kwa waumini wake Musima na kubainisha kwamba kwa ujumbe huo watu wenye hekina zao wametambua nini wanapaswa kufanya.
“Haya ni maneno mazito, mimi nimefurahi sana na nimueleze mgeni wetu nitakwenda Musoma kuwaeleza watu wangu juu ya ujumbe huu wenye maana sana kwa mustakabali wan chi yetu,” alisema.
Kwa upande wake Bahati Bukuku msanii wa Nyimbo za Injili, yeye aliwaasa wachungaji kuacha kuomba na kufunga mambo yanapokuwa mabaya kwani tatizo linaanzia pale maono yanapopuuzwa hivyo kuwataka kuangalia namna ya kuunga mkono kauli zenye maono kama hayo ambayo yanasaidia kuokoa nchi.

JANUARY MAKAMBA KUWA MGENI RASMI WA KONGAMANO LA KUJITAMBUA BODABODA MWANZA HII LEO.

Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda akizungumza na waandishi wa habari (wanaonekana katika picha nyingine) amesema kuwa kutokana na kuwepo matukio mengi ya ajali, uporwaji wa Pikipiki, Wizi unaotokea kwa baadhi ya wateja unaofanywa na baadhi ya waendesha pikipiki wachache wasio waaminifu, uvunjwaji wa sheria unaotokana kutokuwepo elimu ya kutosha na Bima ya Afya wamelazimika kuandaa kongamano hilo.
Sehemu ya waandishi wa habari. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda akizungumza na waandishi wa habari.

MAKAMBA MGENI RASIMI WA KONGAMANO LA WAENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MWANZA.

KONGAMANO la Umoja wa waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza la kujitambua na kupata elimu ya huduma wanayoitoa kwa wananchi linatarajiwa kufanyika leo jijini Mwanza 

Kufuatia kutengwa kwa wanapopata ajali pia kukosa huduma za matibabu ni mambo yanayopelekea kuwepo semina hiyo maalumu kwa wanachama wao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wengine kujiunga na umoja na mfuko wa Bima ya Afya Mkoani hapa.

Akizungumza na vyombo vya habari jana Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoani hapa Makoye Kayanda alisema kwamba kutokana na kuwepo matukio mengi ya ajali, uporwaji wa Pikipiki, Wizi unaotokea kwa baadhi ya wateja unaofanywa na baadhi ya waendesha pikipiki wachache wasio waaminifu, uvunjwaji wa sheria unaotokana kutokuwepo elimu ya kutosha na Bima ya Afya umesababisha uongozi wake kuandaa kongamano hilo.

Kayanda alieleza kuwa kufatia sababu hizo, Uongozi umeamua kuwashirikisha wanachama wake kujitambua na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za Usalama barabarani hali inayopelekea kuwepo uvunjifu wa sheria kwa baadhi ya waendesha pikipiki hao na lawama kuwa za jumla hali ambayo imekuwa ikiwakosesha taswila na muonekano mzuri kwa jamii.

“Tumepata ajali nyingi sana za waendesha pikipiki kwenye maeneo mbalimbali na kupelekea kukosa huduma pale wanapochukuliwa baada ya ajali kupelekwa kupatiwa matibabu kwenye Hospitali na Vituo vya Afya ambapo wamekuwa wakipokelewa na kutelekezwa kutokana na watoa huduma kuwaona kama watu ambao hawafuati sheria na wasiokuwa na tawsila nzuri kwa jamii” alisema

Mwenyekiti huyo alisema kwamba uamuzi wao wa kuitisha kongamano hilo kwa kuitisha wanachama wao kutoka Wilaya zote za Mkoa huo ni kusaidia kutoa elimu kuwahamasisha kujiunga na mfuko wa Bima ya afya, kutii sheria bila shuruti na kukemea vitendo vya uharifu kwa wanachama na kuwabaini wanaofanya ili kuwafikisha kwenye vyombo vya dola na kuzingatia kanuni na sheria zilizopo.

“Tangu kuanzishwa rasimi kwa Umoja huo  na kupata usajili mwaka 2011 ukiwa sasa na wanachama wapatao 4461 Mkoani hapa na kupata mafanikio ya kupungua matukio ya upolwaji pikipiki ambapo kipindi kilichopita huko nyuma kabla ya umoja zaidi ya pikipiki 83 zilipolwa kwa waendeshaji na watu walioziuza mikoa mingine na kusababisha wimbi hili kushika kasi baadhi ya maeneo” alisema

Kayanda ametoa wito kwa jamii kuwapatia ushirikiano ikiwa ni pamoja na wateja wao kukubali kufuata sheria za kupanda pikipiki zao na kuvaa Kofia Ngumu za kujikinga na ajali pindi zinapotokea, kuwaunga mkono kuwatambua wasio wanachama na waendesha pikipiki waaminifu na wanaofanya vitendo vya uhalifu kuwatolea taarifa na siyo kuwaacha wakitumia kivuli cha waendesha pikipiki.

Aidha Kayanda, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuishi kwa mazoea na kukubali kubadilika na kuzingatia pia sheria wakati wanapotumia huduma hiyo ambayo imekuwa na kusasambaa maeneo mbalimbali nchini kwa kisingizio cha kukataa kofio ngumu eti huambukiza majonjwa ya ngozi jambo ambalo halina uhakika na utafiti unaosemwa kutokana na taarifa zake kutokuwepo.

“Kongamano hilo la siku moja litafanyika katika uwanja wa nyamagana na kabla ya kuanza kutaongozwa na maandamano ya amani ya waendesha pikipiki kuanzia ofisi za Chama hicho zilizopo mtaa wa Mlango mmoja na yatapokelewa na mgeni rasimi ambaye ni Januari Makamba ambaye ni Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia (MB) kesho (leo) kisha kuwahutubia kabla ya kufungua kongamano hilo.


Ametoa wito kwa washiriki na wanachama kujitokeza kwa wingi huku pia waendesha pikipiki kuja kujiunga na umoja huo kwa lengo la kuboresha mambo mbalimbali ikiwepo kupitisha mkakati wa kupata mafunzo kutoka kwa vyombo husika na kuwasaidia kupata leseni na kuwa na utambuzi kwa wahusika.

LAND FORE SALE.



Location: Igoma Mwanza
Size:           5 acres (20,000 Square Meters)
Price:         Contact seller +255 757 556 935

Serious buyers only!

ILIVYOKUWA BURUDANI YA SKYLIGHT BAND NA X-MASS NDANI YA KIOTA CHA ESCAPE ONE.

DSC_1317
Vijana wa Skylight Band wakionyesha manjonjo yao kwa mashabiki wa Band hiyo wakati wa sherehe za X-MASS ndani ya fukwe za kiota cha Escape One walipotoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao.
DSC_1332
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani huku akipewa back up na Joniko Flower, Winnie pamoja na Digna Mbepera.
DSC_1352
Mary Lukos akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band katika kusheherekea sikukuu ya X-MASS ndani ya kiota cha Escape One.
DSC_1361
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakijisogeza kwa dancing floor.
DSC_1378
Joniko Flower akiwasogeza mashabiki kwa dancing floor kuwarusha na gwaride la aina yake.
DSC_1382
Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma....Ya chuma chuma nataka mukanda Ya chuma chuma.....!!! Hapo ni gwaride mwanzo mwisho...
DSC_1547
Mheshimiwa Bernard Bundala na mdau Emmanuel Francis wakionyesha umahiri wao katika kusakata sebene la Skylight Band kwenye sherehe za X-MASS.
DSC_1562
Hapo sasa twende kazi...!!
DSC_1578
Mdau Emmanuel Francis akifanya yake, njoo leo Thai Village akifundishe style hii mpya ya Skylight Band.
DSC_1402
Mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka na burudani ya kukata na shoka.
DSC_1406
Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akimpagawisha shabiki wake.
DSC_1410
Palinogaje wewe uliyekosa tunakupa pole tukutane leo pale Thai Village ufurahie Holiday yako na Skylight Band.
DSC_1412
Mpiga Solo wa Skylight Band Allen Kisso a.k.a Mundende akimchizisha shabiki na upigaji wake Gitaa.
DSC_1414
Mrs. Kisso akisebeneka na wifi yake Digna Mbepera.
DSC_1421
Kwa raha zao kwenye upepo mwanana wa Baharini ndani ya fukwe za kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
DSC_1426
Watu weweeeee....!
DSC_1431
Mpaka chini...
DSC_1385
Daudi Tumba akifanya yake jukwaani, ni kiungo muhimu sana kwenye Live Band.
DSC_1464
Lubea wa Skylight Band akishow love na Super Model Neema Mbuya na mdau kwenye kiota cga Escape One.
DSC_1356
Mdau Alois Ngonyani akishow love na mashemeji zake.
DSC_1593
Mdau Fredy Tony akishow love......!!!
DSC_1308
Wadau wa Skylight Band kutoka Kijitonyama nao walijumuika na Band hiyo kusheherekea X-MASS ndani ya fukwe za kiota cha Escape One jijini Dar.
DSC_1399
Fans wa Skylight Band.
DSC_1605
Mdau William Malecela a.k.a LEMUTUZ akishow love na Mbabes mkareeeee ndani ya kiota cha Escape One.
DSC_1461
Mdau nambari moja wa Skylight Band Alois Ngonyani akishow love na Sam Mapenzi wakisherekea sikukuu ya X-MASS Escape One jijini Dar.
DSC_1514
Wadau Batani na Skylight Band ndani ya kiota cha Escape One kilichopo Mikocheni jijini Dar.
DSC_1613
Aneth Kushaba AK47 akishow love na shabiki wake.
DSC_1443
Hapo sasa...
DSC_1452
Watu wa ukweli kwenye muziki wa wastaarabu.....!!
DSC_1454
Wenye mbeleko haya wenye vibwaya mulele twende kazi.....!!!
DSC_1478
Mduara ulihusika pia....!!
DSC_1505
Shazi la kumwaga usiipimie Skylight Band....!!! tukutane leo jioni Thai Village Masaki tufurahi pamoja.
DSC_1489
Beautiful colours...
DSC_1586
 Skylight Band ni line ya wajanja tuuuu...!
DSC_1625
Winnie wa Skylight Band akipata Ukodak na wifi yake Mrs. Kisso.