Hafla ikiendelea katika ukumbi wa Victoria Palace Hotel jijini Mwanza. |
Meneja wa The Great Zone Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa matarajio ya Kampuni. |
Baadhi ya Maaskofu. |
Bahati Bukuku naye alikuwa sehemu ya waalikwa kwenye hafla hiyo. |
Sala ya kuhitimisha hafla. |
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika hafla hiyo. |
MWANZA:Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema taifa lipo katika kipindi Kigumu hivyo kuwataka maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali nchini kuiombea nchi yetu ili ipate kiongozi mwenye sifa zinazotajwa katika Biblia.
Akizungumza kwenye Hotel ya Victoria Palace katika Hafla ya chakula cha usiku kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayoshughulika na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, alisema ameamua kusema haya kwa mbele ya Maaskofu na Wachungaji ambao aliwaita watu wazito wenye kuaminiwa na kuheshimiwa katika jamii.
Hafla hiyo iliudhuriwa na Askofu Zenobius Isaya ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo mkoa wa Mwanza, Askofu Alex Mwakisumbwa mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentokosti (P.C.T) pamoja na Askofu Charles Sekelwa ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa makanisa ya Kikristu mkoani Mwanza.
“Taifa linapita katika kipindi kigumu, linajaribiwa linapita kwenye wakati mgumu, ….Ndugu zangu yakusema yapo mengi, lakini nadhani tuzungumze machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu wote ni watanzania hapa na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu,” alieeleza.
Alisema nchi yetu inahitaji kuponywa, ili ianze upya (Reset) na kubainisha kuwa katika kuanza upya kama Taifa linahitaji aina ya viongozi wenye sifa za kama za viongozi wa dini ambazo zimebainishwa ndani ya Biblia na jukumu hilo kuhakikisha akiongozi wa sifa hizi anapatikana wqanalo wachugaji.
“Taifa lipo katika changamito kama rushwa, wizi, ubakaji, kumomonyoka kwa maadili na ninyi viongozi wa dini mnaziona na kukabiliana nazo kila siku, jamii yetu hii kwa sasa uongo umzidi, ubakaji umezidi, wizi umezidi mauaji yamezidi sasa nini kinaendelea na kutokea na kwa nini maovu yanaongezeka juu yetu?” alihoji Makamba.
Alisema katika hali kama hii kuna kipindi Mungu hukasirika na kutoa adhabu, hivyo kutaka Gharika pamoja na Sodoma na Gomola zilikuwa ni adhabu za Mungu kutokana na watu kupitiliza katika maovu hivyo adhabu ya kwanza ilikuwa ya Maji na ya pili ilikuwa Moto, hatujui inayofuata kwa nchi yetu itakuwa ya nini, japo kama Taifa hatutegemei kufuka huko.
Alieleza kwamba moja kati ya ujumbe wake kwa viongozi hao ni kama kizazi cha sasa ama taifa tunahitaji uponyaji wa hali ya juu na kwamba katika uponyaji huo viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa sana ya kuiponya nchi hii ili iepuke adhabu kama za nyakati hizo zilizotolewa na Mungu.
“Shughuli za siasa zimeingiliwa na Matapeli, lakini hata shughuli yenu pia imeingilia na matapeli vilevile sasa tunapotafuta uponywaji wan chi yetu ninyi mnanafasi kubwa sana kwani uponyaji tunaoongea ni wa maovu ya kiroho, uongo ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mnanafasi kubwa sana. Viongozi wa siasa pia tunayo nafasi wote tunanafasi lakini ili tufanikiwe na nchi ipone lazima viongozi wa siasa wawe wasafi,” alieleza.
Alisema Askofu ama mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi, na hata katika uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya wananchi ama yeye ni nyezo ya matatizo ni vizuri kumtazama sura yake kama ameacha (maovu).
Tunapoomba uongozi wa kisiasa zipo sifa kwani tunaomba kuongoza watu wa mungu ambao ni wale wale wanaokuja Makanisani ndiyo wanaokuja katika siasa, kuongoza watu wa mungu siyo kitu kidogo maana hata mamlaka ya serikali yametambuliwa hivyo lazima vigezo vya kuongoza watu hawa view vikubwa sana.
“Katika Biblia zinataja sifa za mtu atendae kazi ya Askofu ngoja nizisome (1 Timotheo 3.1) zinasema … mtu akitamani kazi ya Askofu, atamani kazi nzuri. Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. Asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha,” alisema na kuongeza katika siasa hatutafuti askofu lakini ni lazima sifa zifanane na hizi za askofu na kuwataka viongozi hao wa makanisa kuzisoma sifa hizo kila watu wanapopita kwao kutafuta uongozi wa nchi na kila mtu anayetafuta uongozi lazima ajipime kwa sifa hizi.
Alisema hata hivyo kumekuwa na mjadala mkubwa wa sifa za uongozi kuhusu kijana, uzoefu na kubainisha kwamba amekuwa akitoa mwito kwa vijana ambao hawana makandokando washiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.
Makamba aleleza vijana wengi wamekuwa waoga waoga, wengi wamekuwa wakidai kutokuwa na fedha, uzoefu lakini maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo na siwezi.
“Yeremia alipopewa unabii alilalamika mimimi mdogo mimi siwezi, lakini mungu alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) ….Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa,” alifafanua na kuongeza kuwa bwana alimwambia “Usiseme, ‘mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe.”
Kutokana na kauli hiyo ya Januari Makamba Askofu Jacoub Lutabija alisema amepokea ujumbe mzito ambao atakwenda kuutangaza kwa waumini wake Musima na kubainisha kwamba kwa ujumbe huo watu wenye hekina zao wametambua nini wanapaswa kufanya.
“Haya ni maneno mazito, mimi nimefurahi sana na nimueleze mgeni wetu nitakwenda Musoma kuwaeleza watu wangu juu ya ujumbe huu wenye maana sana kwa mustakabali wan chi yetu,” alisema.
Kwa upande wake Bahati Bukuku msanii wa Nyimbo za Injili, yeye aliwaasa wachungaji kuacha kuomba na kufunga mambo yanapokuwa mabaya kwani tatizo linaanzia pale maono yanapopuuzwa hivyo kuwataka kuangalia namna ya kuunga mkono kauli zenye maono kama hayo ambayo yanasaidia kuokoa nchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.