Sehemu ya waandishi wa habari. |
Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda akizungumza na waandishi wa habari. |
MAKAMBA
MGENI RASIMI WA KONGAMANO LA WAENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MWANZA.
KONGAMANO
la Umoja wa waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza la kujitambua na kupata elimu ya
huduma wanayoitoa kwa wananchi linatarajiwa kufanyika leo jijini Mwanza
Kufuatia kutengwa kwa wanapopata ajali pia kukosa huduma za matibabu ni mambo yanayopelekea kuwepo semina hiyo maalumu kwa
wanachama wao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wengine kujiunga na umoja na mfuko
wa Bima ya Afya Mkoani hapa.
Akizungumza
na vyombo vya habari jana Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoani hapa
Makoye Kayanda alisema kwamba kutokana na kuwepo matukio mengi ya ajali,
uporwaji wa Pikipiki, Wizi unaotokea kwa baadhi ya wateja unaofanywa na baadhi
ya waendesha pikipiki wachache wasio waaminifu, uvunjwaji wa sheria unaotokana
kutokuwepo elimu ya kutosha na Bima ya Afya umesababisha uongozi wake kuandaa kongamano hilo.
Kayanda
alieleza kuwa kufatia sababu hizo, Uongozi umeamua kuwashirikisha wanachama
wake kujitambua na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu, kanuni na
sheria za Usalama barabarani hali inayopelekea kuwepo uvunjifu wa sheria kwa
baadhi ya waendesha pikipiki hao na lawama kuwa za jumla hali ambayo imekuwa
ikiwakosesha taswila na muonekano mzuri kwa jamii.
“Tumepata
ajali nyingi sana za waendesha pikipiki kwenye maeneo mbalimbali na kupelekea
kukosa huduma pale wanapochukuliwa baada ya ajali kupelekwa kupatiwa matibabu
kwenye Hospitali na Vituo vya Afya ambapo wamekuwa wakipokelewa na kutelekezwa
kutokana na watoa huduma kuwaona kama watu ambao hawafuati sheria na wasiokuwa
na tawsila nzuri kwa jamii” alisema
Mwenyekiti
huyo alisema kwamba uamuzi wao wa kuitisha kongamano hilo kwa kuitisha
wanachama wao kutoka Wilaya zote za Mkoa huo ni kusaidia kutoa elimu
kuwahamasisha kujiunga na mfuko wa Bima ya afya, kutii sheria bila shuruti na kukemea
vitendo vya uharifu kwa wanachama na kuwabaini wanaofanya ili kuwafikisha
kwenye vyombo vya dola na kuzingatia kanuni na sheria zilizopo.
“Tangu
kuanzishwa rasimi kwa Umoja huo na
kupata usajili mwaka 2011 ukiwa sasa na wanachama wapatao 4461 Mkoani hapa na
kupata mafanikio ya kupungua matukio ya upolwaji pikipiki ambapo kipindi
kilichopita huko nyuma kabla ya umoja zaidi ya pikipiki 83 zilipolwa kwa
waendeshaji na watu walioziuza mikoa mingine na kusababisha wimbi hili kushika
kasi baadhi ya maeneo” alisema
Kayanda
ametoa wito kwa jamii kuwapatia ushirikiano ikiwa ni pamoja na wateja wao
kukubali kufuata sheria za kupanda pikipiki zao na kuvaa Kofia Ngumu za
kujikinga na ajali pindi zinapotokea, kuwaunga mkono kuwatambua wasio wanachama
na waendesha pikipiki waaminifu na wanaofanya vitendo vya uhalifu kuwatolea
taarifa na siyo kuwaacha wakitumia kivuli cha waendesha pikipiki.
Aidha
Kayanda, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuishi kwa mazoea na kukubali
kubadilika na kuzingatia pia sheria wakati wanapotumia huduma hiyo ambayo
imekuwa na kusasambaa maeneo mbalimbali nchini kwa kisingizio cha kukataa kofio
ngumu eti huambukiza majonjwa ya ngozi jambo ambalo halina uhakika na utafiti
unaosemwa kutokana na taarifa zake kutokuwepo.
“Kongamano
hilo la siku moja litafanyika katika uwanja wa nyamagana na kabla ya kuanza
kutaongozwa na maandamano ya amani ya waendesha pikipiki kuanzia ofisi za Chama
hicho zilizopo mtaa wa Mlango mmoja na yatapokelewa na mgeni rasimi ambaye ni
Januari Makamba ambaye ni Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia (MB) kesho
(leo) kisha kuwahutubia kabla ya kufungua kongamano hilo.
Ametoa
wito kwa washiriki na wanachama kujitokeza kwa wingi huku pia waendesha
pikipiki kuja kujiunga na umoja huo kwa lengo la kuboresha mambo mbalimbali ikiwepo
kupitisha mkakati wa kupata mafunzo kutoka kwa vyombo husika na kuwasaidia kupata
leseni na kuwa na utambuzi kwa wahusika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.