ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 6, 2019

RC MONGELLA AAMURU KUBOMOLEWA KWA MSINGI WA KITUO CHA POLISI ULIOKOSEWA.


MAPEMA asubuhi ya leo Jumamosi ya tarehe 06/April/2019 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amefanya ziara fupi ya kukagua shughuli za ujenzi wa kituo cha polisi pamoja na nyumba 12 kwa makazi ya askari hao na kuamuru kubomolewa kwa msingi ulio kwisha anza kujengwa kutokana na ramani yake kuwa ya kizamani yenye mapungufu yasiyokidhi mahitaji ya sasa.

Mongella ameamuru kubomolewa haraka iwezekanavyo kwa msingi huo ulio anza kujengwa na kufikia pakubwa ili kupisha ramani ya kisasa inayo kidhi mahitaji yenye changamoto za kila uchwao..

Mnamo mwezi April mwaka jana (1918) Rais Magufuli  akiwa mjini Arusha alisema Serikali yake imetenga bilioni 10 kwaajili ya ujenzi na na kuboresha vituo vya polisi nchini ambapo shilingi milioni 150 zimetengwa kwaajili ya kukamilisha mradi huo mkoani hapa.

Ni katika eneo la Mtaa wa Ilamba A Kata ya Nyamhongolo, wilayani Ilemela mkoani Mwanza, mahala panaporipotiwa kuwa na matukio ya wizi, unyang'anyi na uporaji wa kupitiliza lakini sasa huwenda wakazi wa eneo hilo wakafikia hatua ya kusahau adha waliyokuwa wakiipata awali, kabla ya ujenzi huo ambao ni ndani ya miezi miwili tu unapaswa kuwa umekamilika.

Friday, April 5, 2019

"ZIARA YA BUNGENI DODOMA IMENIJENGA" ASEMA PIERRE WAKATI AKIBUSU ARDHI YA MWANZA


MKALI anaye-trend hivi sasa kwa vituko na burudani katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii Pierre Gumbo aka 'Konki Liquid' amesema kuwa ziara yake aliyoifanya hivi karibuni Bungeni Jijini Dodoma imemjenga sana.

Pierre ameyasema hayo mapema asubuhi ya leo wakati alipotua jijini Mwanza majira ya saa 1 na dakika 30 kwaajili ya kujoin na wana wa jiji hilo la miamba kula weekend, ingawa ameficha kipi alichong'amua kwamba atakwenda kukifanyia kazi lakini amekiri kuwa ni moja kati ya matembezi yenye faida aliyoweza kuyafanya maishani.

Huku akikwepa maswali ya siasa Pierre amejibu swali alipoulizwa 'Iwapo akikutana na Mhe. Rais Magufuli ni kitu gani atakachomwambia' 

Jeh Pierre Konki ni shabiki wa timu gani, jamaa gani anayemchukia na Jeh kuna vitu asivyovipenda kwenye maeneo ya bata?

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA MGENI RASMI HARAMBEE YA KUICHANGIA LIPULI FC JUMAPILI HII

Kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo akiwa mbele ya waandishi wa habari akielezea lengo la kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo ili kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu Tanzania bara.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa wakiwasikiliza viongozi wa timu ya Lipuli fc juu ya mipango na mikakati ya Harambee ya kuichangia timu hiyo.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

UONGOZI wa timu ya mpira wa migu inayoshiliki ligi kuu Tanzania bara Lipuli Fc ya mkoani Iringa umepanga kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo kwa lengo la kuimarisha uchumi kutatua changamoto za mishahara pamoja ada za wachezaji ambazo hadi hii leo bado wanadaiwa na wachezaji wa klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoa Iringa kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo alisema kuwa lengo la kuitisha harambee hiyo ni kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu Tanzania bara.

“Ni kweli hatujalipa wachezaji miezi miwili hadi hivi sasa nab ado tunadaiwa pesa za usajili kwa wachezaji wetu hiyo tumeamua kufanya hivyo kwa lengo la kuinusu timu kwa msimu ujao kuondokewa na wachezaji wetu ambao ni wazuri kweli kweli na wanaujua mpira sana” alisema Kihwelo

Kihwelo aliongeza kuwa harambee hiyo itafanyika siku ya jumapili tarehe 7 / 4 / 2019 siku ya jumapili katika ukumbi wa kichangani uliopo manispaa ya Iringa ambapo wanatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo  Pinda kuwa mgeni Rasmi

“Siku ya harambee hii tunatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda kuwa mgeni Rasmi akiambatana na wadau mbalimbali akiwepo mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huu ambao tunategemea watachangia timu yao ambayo inafanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara” alisema Kihwelo

Kihwelo  alisema wanatarajia kupata zaidi ya shilingi milioni miatatu kwenye Harambee hiyo ambazo zitasaidia kuendesha timu bila kuwa na deni lolote kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo na kuweza kupata usajili mpya wa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara

“Tunalipa zaidi ya milioni ishirini na nne kila mwezi kwa ajili ya mishahara tu ya wachezaji wa timu na tunagharamia zaidi ya laki tatu kwa siku kwa ajili ya kambi ya timu hivyo utaona kwa namna gani timu inavyogharimu kiasi kikubwa cha fedha na timu hadi hivi sasa haina mdhamini yeyeote yule” alisema Kihwelo

Aliezea kuwa mikakati ya msimu ujao ni kuhakikisha timu inapata mdhamini wa kudumu kwa kuwa timu yetu ya Lipuli imekuwa ikipata matokeo mazuri kila msimu hivyo itatusaidia kupata mdhamini ambaye ataamini kuwa timu hiyo inauwezo wa kuitangazia bidhaa yake.

Kwa upande wake katibu mkuu wa klabu hiyo ya Lipuli Julius Leo ameomba wananchi,wadau wa soka na wapenzi wa klabu ya Lipuli kuichangia timu hiyo kwa kutumia akaunti ya benk ya CRDB  01J2072252000 na kwenye namba ya simu ya MPESA ya timu hiyo ambayo ni 0744 16 24 46 inayojulikana kwa jina la LIPULI FC

RAIS MAGUFULI: HATUNA MPANGO WA KUONGEZA MIKOA MIPYA.

Na Mwandishi Wetu
MAELEZO
DAR ES SALAAM

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo ya utawala ikiwemo kuanzisha mikoa mipya na badala yake imejipanga kuimarisha huduma na mahitaji ya miundombinu iliyopo ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru yenye urefu wa kilometa 193 leo (Ijumaa April 5, 2019), Rais Magufuli alisema Serikali imekusudia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, maji, elimu n.k katika maeneo waliopo.
Aliongeza kuwa katika awamu yake yake ya Uongozi, suala la kuongeza maeneo ya utawala halipo na badala yake kuwataka Viongozi wa maeneo hayo wajipange katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya fedha zilizopo kwenda katika kujenga ofisi mpya za Wakuu wa Mikoa mipya na kuwalipa mishahara viongozi hao.
“Tumepanga kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu, tumechelewa kuleta Maendeleo hususani kwa wananchi wetu wa mikoa ya kusini, Serikali ninayoiongoza haina mpango wa kuanzisha mikoa mipya , badala yake pesa hizo tutazielekeza katika ununuzi wa madawa na kuboresha miundombinu ya barabara, elimu na nishati’ alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli alisema bado yapo baadhi ya maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo barabara za lami, hivyo Serikali haitoweza kuleta Maendeleo katika sehemu moja kwa kuwa fedha hizo hazipo kwa kuwa ina na mahitaji makubwa katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa huduma muhimu na za msingi kwa Maendeleo ya wananchi zinapewa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati, kwa kuwa kukamilika kwake kutasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo katika miaka ya nyuma vimekuwa vikisababisha vifo vya makundi hayo ya kijamii.
Akizumgumzia kuhusu Sekta ya Maji, Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa kuwasimamia wakandarasi wa miradi ya maji nchini, kwani Serikali imekuwa ikitenga kiasi kikubwa cha cha fedha katika miradi ya Maendeleo pasipo na kupata matokeo yaliyotarajiwa, na hivyo kuisababishia hasara Serikali.
“Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Fedha na Mipango, miradi mingi ya maji imekuwa ikitumia fedha nyingi pasipo na kupata matokeo yoyote na wataalamu wetu hasa wakandarasi wamekuwa wazito kutoa tafsiri za nadharia za utaalamu na kuzileta katika nadharia halisi, na mataifa ya nje yanashangwa tunaposhindwa kuvitumia vyanzo tulivyonazo ili kuweza kuzalisha maji ya kutosha’ alisema Rais Magufuli.
Awali akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema kujengwa kwa barabara hiyo kutaimarisha mawasiliano katika ukanda wa kusini unaojumuisha Mtwara, Mingoyo, Masasi, Mangaka, Tunduru hadi Mbamba Bay na hivyo kuzidi kufungua fursa za kiuchumi nanchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Alisema hadi kukamilika kwake barabara hiyo imegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 173, ambapo Shirika la Misaada la Japan limetoa asilima 23.24, Benki ya Maendeleo ya Afrika asilimia63.32 na Serikali ya Tanzania asilimia 13.35 ikiwemo kodi na kulipa fidia kwa wananchi wanaostahili kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 2007.
Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania, Shinichi Goto alisema Serikali ya Japan imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru na itaendelea kusaidia miradi mingine ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa umaskini kwa wananchi wake yanafikiwa.

Thursday, April 4, 2019

GSENGO TV NA VICTORIOUS BATA POINT WAMTAKIA BIRTHDAY NJEMA MTANZANIA DAKTARI ANAYEISHI MAREKANI



Gsengo TV na Victorious wamtakia siku na heri Mtanzania anthonrtha anayeishi Marekani

Akizungumza na gsengo ,Anthonetha amesema ,Siku yake hi ameamua kuitumia kwa mapunziko machache ,

Pamoja na kuwa Daktari nchini Marekani lakini, Bado mwanadada huyu ni Designer ambaye amekuwa akiwapa tabu sana baadhi ya Wadada wengi ambao wamekuwa wakitamani kuwa Kama  yeye,na Kila vazi analovaa kwakwe uwa pahala pake 

aaa

MAPENDEKEZO BAJETI YA SERIKALI 2019/2020 KUZINGATIA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA.

Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa mapendekezo ya Bajeti ya Serikali yanazingatia Mpango wa Maendeleo wa Taifa sanjari na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.

Amesema hayo leo Bunge jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Hotuba ya Mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020.

"Mpango wa Maendeleo wa  Taifa unatekelezwa sanjari na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 - 2020, ahadi za Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na zile alizozitoa katika hotuba yake ya kuzindua Bunge hili mwezi Novemba, 2015." amesema  Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesema, vipaumbele vya mpango wa mwaka 2019/2020 ni kuendelea kuimarisha msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu, kuendelea kuboresha mazingira wezeshi kwa uendeshaji  wa biashara na uwekezaji na kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mpango.

Aidha amesema kuwa, katika Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea kutekeleza Mradi wa Umeme wa Maji wa Mto Rufiji (Stiegler's Gorge), ujenzi wa miundombinu ya reli ya kisasa (SGR), barabara pamoja na kukuza sekta ya anga.

Utekelezaji wa miradi hiyo ya miundombinu wezeshi ya kiuchumi una lengo la kufungamanisha ukuaji wa sekta hizo na sekta nyingine hususan za biashara, kilimo na utalii.

Waziri Mkuu amesema kuwa, kuimarika kwa sekta hizo kutachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Wananchi kwa ujumla
Ameendelea kusema, katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli yamepatikana mafanikio mengi ambayo wananchi wanapaswa kufahamishwa.

Amesema, Mhe. Rais Magufuli ameonesha dhamira ya dhati ya kisiasa katika kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea. Halikadhalika, ameweza kuhakikisha dhamira hiyo ya kujenga uchumi imara usiyo tegemezi inaenea kwa viongozi wengine, watendaji na wananchi kwa ujumla.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni kuendelea kukua na kuimarika kwa uchumi ambao unachochewa na jitihada za Serikali za kuwekeza kwenye miundombinu ya usafirishaji ikiwemo ujenzi wa barabara, reli, viwanja vya ndege sanjari na kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme.

Ameongeza kuwa kuimarika kwa Shirika la Ndege Tanzania ni sehemu ya mafanikio hayo, ambapo Serikali imefanikisha ununuzi wa ndege saba mpya ikiwemo Dreamliner Boeing 787.

Ununuzi wa ndege hizo umesaidia kuitangaza nchi, kuongeza mapato ya Serikali, fursa za ajira kwa vijana na kuwa kichocheo kwa Sekta za ajira kwa vijana na kuwa kichocheo kwa sekta nyingine kama vile kilimo, utalii, mifugo na uvuvi.

Vilevile, mpango wa elimu msingi bila malipo umesaidia kuongezeka idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kutoka wanafunzi milioni 1.57 mwaka 2015 hadi milioni 2.08 mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 35.2 kwa mwaka  2019 uandikishaji ulikuwa milioni 1.58.

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuimarisha uchumi na mafanikio yanayoonekana, ambapo katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2018, Pato la Taifa lilikuwa kwa asilimia 6.7 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2017.

Ukuaji huo wa uchumi umechangia kutoa ajira na kuongeza mapato ya Serikali yaliyowezesha ujenzi na uboreshaji wa miundombinu kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii. 

'HATUTOCHOKA KUWALETEA MAENDELEO WATANZANIA' ASEMA RAIS MAGUFULI.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kuacha kulalamika na badala yake imewataka wananchi wa mikoa ya kusini kutambua kuwa Serikali itaendelea kuwatumia na kuwaletea maendeleo katika sekta za kijamii na kiuchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Tunduru-Nakapanya-Mangaka- Mtambaswala yenye urefu wa kilometa 202.5, Rais Magufuli alisema Serikali yake itaendelea kuwajibika na kusimamia miradi ya maendeleo inayobeba manufaa kwa Watanzania walio wengi.

Alisema kuwa Wananchi wa mikoa ya Kusini wanapaswa kutambua historia ya ujenzi wa barabara hiyo ulianzia katika Serikali za Awamu zilizopita ambapo kulikabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa kuomba fedha kutoka wafadhili na wadau wa maendeleo.

Aidha Rais Magufuli aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuiunga mkono Serikali katika juhudi mbalimbali inazofanya za kuimarisha miundombinu ya barabara katika ukanda wa kusini ikiwemo Mtwara kwani hapo awali hali ya miundombinu hiyo haikuwa ya kuridhisha ukilinganisha na ilivyo sasa.

"Mtakumbuka kuwa wakati tulipokuwa tukiomba fedha za ujenzi wa daraja la Umoja lilnalounganisha Tanzania na Msumbiji ambalo ndio kiungo muhimu baina ya mataifa haya, wafadhili wote walikataa kutoa fedha kwani daraja hili linaingia porini katika kila nchi, lakini tulisimama imara na kujenga daraja hili," alisema Rais Magufuli.

Alisema kutokana na Mkoa wa Mtwara kuwa katika ukanda muhimu katika usafirishaji wa bidhaa muhimu za kiuchumi kupitia bandari, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) na Benki ya Mandeleo ya Afrika (AfDB) zilikubaliana kujenga barabara hiyo ambayo kwa sasa itakuwa imefungua fursa za ukanda wa kiuchumi kwa kushirikiana na nchi ya Msumbiji.

"Ukitazama fedha hizi, si ndogo kwa mfano kipande cha Tunduru-Nakapanya-Mangaka yenye urefu wa kilometa 137 kimetumia wakandarasi watatu na washauri 3 na jumla ya Tsh Bilioni 182 zimetumika, na kipande cha Mangaka- Mtambaswala chenye urefu wa kilometa 56 pia kiasi cha Tsh Biloioni 56 kimetumika," alisema Rais Magufuli.

Alisema kuwa kitendo cha wadau hao wa maendeleo kuiunga mkono Tanzania kinatokana na imani waliyonayo kwa Serikali ya Awamu ya Tano, kwani yapo mataifa mbalimbali ya Bara la Afrika yanayohitaji kujengewa barabara na kupatiwa misaada mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Kuhusu Kipande cha barabara ya Masasi-Mtwara chenye urefu wa kilometa 150, Rais Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Waziri wa Fedha na Mipango kuandika barua ya mchanganuo wa maombi ya fedha kwa Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) NA Benki ya Maendeleo ya Afrika ili kuanza mara moja ujenzi wa barabara hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kumeweza kutimiza malengo ya Serikali ya kuiunganisha ushoroba wa kusini katika kiwango cha lami.

Aliongeza kuwa katika ujenzi huo, Shirika la Maendeleo ya Japan ilichangia asilimia 32.83, Benki ya Maendeleo ya Afrika 64.79 na Serikali ya Tanzania ilitoa asilimia 2.38 ikiwemo malipo ya fidia kwa wananchi pamoja na kodi.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Alex Mubiru alisema kufunguliwa kwa barabara hiyo kumeweza kutimiza ndoto ya waasisi wa Mataifa ya Tanzania na Msumbiji Samora Machel na Julius Nyerere, ambapo walitaka mataifa hayo kuweza kuunganisha na Daraja la Umoja ambalo kwa sasa litatoa fursa kwa wananchi wote kuweza kuimarisha shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

IKULU YAOMBA TAARIFA HII KUHUSU CAG KUPUUZWA.


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inapenda kuutarifu umma kupuuza taarifa hii kuhusu kusikitishwa na azimio la Bunge kutofanya kazi na CAG.


Wednesday, April 3, 2019

PEMBE ZA NDOVU ZAMPONZA ASKARI MAGEREZA.


Askari Mageraza wa gereza la Msalato A.8070 SSGT Cosmas Ndasi (51) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa na pembe za ndovu vipande  sita vyenye thamani ya sh 103.5 milioni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa April mosi mwaka huu katika mtaa wa Kilimani  akiwa na vipande hivyo vya pembe vyenye uzito wa kilogramu 13 sawa na tembo watatu.

“Tulitengeza mtego na Askari huyo akanasa na  kumkamata akiwa ameficha kwenye mfuko vipande vya pembe za ndovu kwa ajili ya kumsubiri mteja ili kufanya mauzo,” amesema Muroto.

Katika tukio jingine  Muroto amesema kuwa  wanamshikilia Ambokile Mwampulo (32) kwa tuhuma za kujifanya afisa usalama wa Taifa na kudanganya watu ili kujipatia fedha.

WAPITISHA SHERIA KALI KUPAMBANA NA USHOGA, WATAKAOTHIBITIKA KUPIGWA MAWE HADI KUFA.



Taifa la Brunei limeazisha sheria, itakayoruhusu wale watakaobainika kushiriki mapenzi ya jinsia moja kuuawa kwa kupigwa mawe. Sheria ambayo imekosolewa na wanaharakati wa haki za binadamu.

Sheria hiyo inaanza kutekelezwa leo Jumatano, lakini pia wale watakaobainika kuhusika na makosa mengine kama wizi, watakatwa mikono.

Uongozi wa taifa hilo dogo la Asia Mashariki limesema limeamua kutekeleza sheria ya Kiislamu (Sharia) hatua ambayo imeshtumiwa na Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za kibinadamu.

Wakati huo huo Ufaransa imeomba Brunei kufuta adhabu ya kifo kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja ikibaini kwamba sheria hiyo inakiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu.

BILA UBUNIFU NA KUJIONGEZA TAIFA LITAENDELEA KUTESWA NA VIFO VYA MAMA NA MTOTO.


Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Afya na Ustawi wa Jamii Mkoani Mwanza wamezindua Kampeni   ya Uzazi Salama ijulikanayo kama "Jiongeze Tuwavushe Salama".

Kampeni hiyo imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ikiwa na kauli mbiu ya "Kila mmoja wetu anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi.Maneno basi, sasa vitendo."

Akiongea katika uzinduzi huo Mhe.Mongella amesema vifo hivyo vinaepukika hivyo jamii ina jukumu kwa kuhakikisha inatambua dalili hatarishi na kuwasaidia wazazi na watoto wachanga.

"Katika kuhakikisha kuwa Vifo hivi vinapungua Serikali ya awamu ya  tano ya Mhe. Dkt.John Magufuli imejenga vituo vya afya 352 Nchi nzima na kuongeza upatikanaji wa dawa ili kusaidia wazazi na kiwavusha salama," aliaema Mongella.

Naye Katibu Tawala Msaidizi kwa upande wa Afya Dkt.Thomas Rutachunzibwa amesema kampeni hii  ina maana kuwa viongozi mbalimbali wakitumika  ipasavyo watachangia kumvusha mzazi salama na haipaswi kuachiwa wadau wa afya pekee.

"Swala la vifo bado ni tatizo tusiwaachie wadau wa afya pekee tubadirishe mtazamo kuhusiana na vifo vya wazazi na watoto wachanga kila mdau ana wajibu wa kumvusha mzazi  salama,"  alisema Dkt. Rutachunzibwa.

Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amesisitiza kuhusu Afya ya uzazi na kumtaka kila kiongozi kuwajibika katika kufanikisha Kampeni hii ya kumvusha mzazi  salama, hii inaweza kufanyika katika ngazi mbalimbali katika maeneo yetu ya kazi.

"Sisi tuliopo humu ndani tujiulize, umefanya nini katika kupunguza vifo vya wazazi na watoto wachanga hasa katika maeneo tuliyopo?" Alisema Kadio.

Mkoa wa Mwanza ni Mkoa wa nne kutekeleza uzinduzi wa kampeni hii ambayo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan aliizindua Kitaifa mwaka 2018 kwa lengo la kutokomeza kabisa vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kujiongeza na kuwavusha salama.

MWANZA YAZINDUA KAMPENI YA UZAZI SALAMA


Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Afya na Ustawi wa Jamii Mkoani Mwanza wamezindua Kampeni   ya Uzazi Salama ijulikanayo kama "Jiongeze Tuwavushe Salama".


Kampeni hiyo imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ikiwa na kauli mbiu ya "Kila mmoja wetu anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi.Maneno basi, sasa vitendo."
Akiongea katika uzinduzi huo Mhe.Mongella amesema vifo hivyo vinaepukika hivyo jamii ina jukumu kwa kuhakikisha inatambua dalili hatarishi na kuwasaidia wazazi na watoto wachanga.
"Katika kuhakikisha kuwa Vifo hivi vinapungua Serikali ya awamu ya  tano ya Mhe. Dkt.John Magufuli imejenga vituo vya afya 352 Nchi nzima na kuongeza upatikanaji wa dawa ili kusaidia wazazi na kiwavusha salama," aliaema Mongella.

Naye Katibu Tawala Msaidizi kwa upande wa Afya Dkt.Thomas Rutachunzibwa amesema kampeni hii  ina maana kuwa viongozi mbalimbali wakitumika  ipasavyo watachangia kumvusha mzazi salama na haipaswi kuachiwa wadau wa afya pekee.
"Swala la vifo bado ni tatizo tusiwaachie wadau wa afya pekee tubadirishe mtazamo kuhusiana na vifo vya wazazi na watoto wachanga kila mdau ana wajibu wa kumvusha mzazi  salama,"  alisema Dkt. Rutachunzibwa.

Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amesisitiza kuhusu Afya ya uzazi na kumtaka kila kiongozi kuwajibika katika kufanikisha Kampeni hii ya kumvusha mzazi  salama, hii inaweza kufanyika katika ngazi mbalimbali katika maeneo yetu ya kazi.
"Sisi tuliopo humu ndani tujiulize, umefanya nini katika kupunguza vifo vya wazazi na watoto wachanga hasa katika maeneo tuliyopo?" Alisema Kadio.

Mkoa wa Mwanza ni Mkoa wa nne kutekeleza uzinduzi wa kampeni hii ambayo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan aliizindua Kitaifa mwaka 2018 kwa lengo la kutokomeza kabisa vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kujiongeza na kuwavusha salama.

TANZANIA YAWA MFANO WA KUIGWA KATIKA UDHIBITI WIZI NA UNYONYAJI SEKTA YA MADINI.


WAZIRI wa Nishati na Madini wa nchi ya Uganda Peter Lokeris, mwanzoni mwa wiki hii amewasili jijini Mwanza akiwa na wajumbe wake kwaajili ya kujifunza namna Tanzania ilivyoweza kudhibiti wizi na unyonyaji Sekta ya Madini.


Wenyeji wa ujumbe huo ni Naibu Waziri wa Madini nchini Tanzania Stanslaus Nyongo, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Monday, April 1, 2019

MBUNGE LEMA USO KWA USO NA RAIS MAGUFULI.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amehudhuria kutoa heshma za mwisho kwenye msiba  wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. Katika kuhudhuria msiba huo amekutana na kuzungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati akitoka.

DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpongeza mwenyekiti wa halmshuri ya wilaya ya Iringa Vijijini Stephen Mhapa kumpa tuzo ya ngao kwa kufanya vizuri katika utunzaji wa mazingira pamoja na kuwa na vyoo safi na bora.
 Baadhi ya washiriki waliofika katika kikao hicho cha utoaji tuzo kwa utunzaji bora wa mazingira na kuwa na vyoo bora
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa sambamba na mkurugeni wa halmashauri ya Iringa vijijini Robert Masunya wakinywa maziwa ya asas

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wananchi,viongozi,taasisi na jumuiya mbalimbali kwa kutekeleza vizuri kampeni ya kuwa na vyoo bora ambavyo vimeipa ushindi halmasahuri ya Iringa Vijijini kwa kupata tuzo ya usafi hapa nchini.

Kasesela alisema kuwa ofisi ya afya katika halmasahuri ya Iringa Vijijini wamekuwa wakisimamia vizuri swala la afya na kuwa na vyoo bora ambapo wanataraji kuwa halmashauri ya kwanza kwa kuwa na vyoo bora kuliko halmashuri zote za mkoa wa Iringa hadi taifa.

“Nampengeza bibi afya wa hapa amekuwa mkali kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kukwamisha zoezi lolote la kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha afya za wananchi wa wilaya hii wanakuwa na afya njema” alisema Kasesela

Aidha Kasesela amepiga marufuku wa wazazi kujifungulia majumbani kwa kuwa sio sehemu salama kwa uzazi wa mtoto wakati serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ambayo ndio kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano.

“Jukumu la kwanza kwa baba ni kuhakikisha amempeleka mama kliniki kupata huduma ili kuwa na malezi mazuri ya mtoto,hivyo tutaondoa ile njia ya akinamama kujifungulia majumbani kwa kuwa tayari baba atakuwa anajua wajibu wake” alisema Kasesela

Kasesela amewataka watendaji wa kata,vijiji na maafisa tarafa kuhakikisha hakuna mama anajifungulia nyumbani na nitamshughulikia mtendaji yeyeto Yule ambaye hata wachukulia hatua akibaba watakao fanikisha mama kujifungulia numbani.

Awali akitoa hutuba kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa halmasahuri ya Iringa Vijijini Robert Masunya aliwataka  watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wameendeleza juhudi hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na vyoo bora ili kupunguza na kumaliza tatizo la milipuko ya magonjwa.

“Niwaombeni tena tuendelee kushirikiana vyema katika kuhakikisha halmasahuri ya Iringa Vijijini inaongoza kwa kuwa na mazingira bora na safi kuliko halmashuri zote hapa nchini kwa kuwa tuna mikakati ambayo ni bora sana” alisema Masunya

NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AMEWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

 Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata amewataka wanafunzi wa manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani
Mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.
 Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiongea na wanafunzi walijitokeza kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

NAIBU MEYA wa manispaa ya Iringa amewataka wanafunzi wa manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani.

Akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mwembetogwa,Lugalo,Tagamenda na Mawelewele  naibu meya Joseph Lyata aliwataka wanafunzi hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha pekee ya kuhakikisha tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.

Kuthamini vitu vilivyopo katika nchi yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za nchi na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo” alisema Lyata

Lyata alisaema kuwa nchi nyingi ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana uongozi bila kutumia mabavu,hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.

“Angalieni nchi kama Somalia tu hapo jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo wa wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu” alisema Lyata

Lyata aliongeza kwa kusema kuwa uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa wazalendo na nchi yao.

“Lazima tuambizane ukweli kabisa maana sisi kama manispaa tunahakikisha manispaa inaendelea kuongoza kwenye usafi,kuhakikisha wanafunzi mnasoma vizuri bila kuwa na woga na kuhakikisha tunailinda mipaka ya nchi yetu huo ndio uzalendo wa nchi yetu” alisema Lyata

Lyata aliwata wanafunzi kuanza kuwa na uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda nchi hii kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa watakuwa na lengo la kulinda amani ya nchi.

“Uzalendo pia huanzia pale unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara kuna mambo ya msingi utajifunza tu” alisema Lyata

Naye mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.

“Wananchi wanasababisha umasikini wenyewe kutokana na kuchagua viongozi ambao hawana uwezo ndio hupelekea umaskini katika  kwa wananchi waliomchagua kiongozi waliyekuwa na imani naye,hivyo kukosea kuchagua kiongozi bora ni kujitafutia matatizo wenyewe” alisema Ngerera

Ngerera aliongeza kwa kuwaambia wanafunzi hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri huo waliona wanafunzi kwa kuwa ndio kipendi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa wa maisha ni nini.

“Jamani lazima mjifunze mnapotaka kumlaumu kiongozi mlimchagua wenyewe ni lazima mjipie wenyewe kwanza mlikosea wapi na sasa mnatakiwa mfanye nini ili kuhakikisha mfanya kazi huku mkiwa mmetawaliwa na uzalendo wenu” alisema Ngerera

SERIKALI YAKABIDHI NDEGE YAKE YA FOKKER 50 KWA ATCL.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amemkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. LeonardChamriho ndege ya serikali aina ya Fokker 50 ili aikabidhi kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida  kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufulikwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JuliusNyerere leo Aprili 1, 2019.






ILIVYOFANA LIFT HIM HIGHER CONCERT 2019 SEASON ONE NDANI YA MWANZA - PART 1


Hii ni sehemu ya kwanza ya tamasha la muziki wa injili lililofanyika Jijini Mwanza katika ukumbi wa Hotel Belmont Fearmont likiandaliwa na waimbaji wa Muziki huo wa jiji hilo la miamba kwa kushirikiana na kipindi cha muziki wa injili toka Radio Jembe Fm kiitwacho Jembe Gospel, kinachoruka kila Jumapili saa moja asubuhi hadi saa nne kamili asubuhi chini ya watangazaji Adolf Nzwalla na Albert G. Sengo.