ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 6, 2019

RC MONGELLA AAMURU KUBOMOLEWA KWA MSINGI WA KITUO CHA POLISI ULIOKOSEWA.


MAPEMA asubuhi ya leo Jumamosi ya tarehe 06/April/2019 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amefanya ziara fupi ya kukagua shughuli za ujenzi wa kituo cha polisi pamoja na nyumba 12 kwa makazi ya askari hao na kuamuru kubomolewa kwa msingi ulio kwisha anza kujengwa kutokana na ramani yake kuwa ya kizamani yenye mapungufu yasiyokidhi mahitaji ya sasa.

Mongella ameamuru kubomolewa haraka iwezekanavyo kwa msingi huo ulio anza kujengwa na kufikia pakubwa ili kupisha ramani ya kisasa inayo kidhi mahitaji yenye changamoto za kila uchwao..

Mnamo mwezi April mwaka jana (1918) Rais Magufuli  akiwa mjini Arusha alisema Serikali yake imetenga bilioni 10 kwaajili ya ujenzi na na kuboresha vituo vya polisi nchini ambapo shilingi milioni 150 zimetengwa kwaajili ya kukamilisha mradi huo mkoani hapa.

Ni katika eneo la Mtaa wa Ilamba A Kata ya Nyamhongolo, wilayani Ilemela mkoani Mwanza, mahala panaporipotiwa kuwa na matukio ya wizi, unyang'anyi na uporaji wa kupitiliza lakini sasa huwenda wakazi wa eneo hilo wakafikia hatua ya kusahau adha waliyokuwa wakiipata awali, kabla ya ujenzi huo ambao ni ndani ya miezi miwili tu unapaswa kuwa umekamilika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.