Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Aprili 06,2019 yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Aprili 06,2019 yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.
Raisi wa Chama cha Riadha nchini Mhe.Antony Mtaka akizungumza Jijini Arusha wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Aprili 06,2019 yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.Mrisho Gambo akitoa salamu za Mkoa huo wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Aprili 06,2019 yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja mshindi wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika April 06,2019 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akimvalisha
Medali mshindi wa kilometa tano wanaume
wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon
yaliyofanyika Aprili 06,2019 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi
hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye
alifariki miaka 35 iliyopita.Kushoto ni Rais wa Chama cha Riadha nchini
Mhe.Antony Mtaka.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akimvalisha
Medali mshindi wa kilometa tano wanawake
wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon
yaliyofanyika Aprili 06,2019 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi
hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye
alifariki miaka 35 iliyopita.
Waziri
Mkuu asisitiza Michezo ni Ajira
Na
Shamimu Nyaki –WHUSM
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka
vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali
kuendelea kuviendeleza kwakua Michezo katika Dunia ya leo ni ajira.
Mhe.Waziri
Mkuu ameyasema hayo Aprili 06,2019 Jijini Arusha katika Mashindano ya Riadha ya
Sokoine Memorial Marathon yaliyolenga kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani Hayati
Edward Moringe Sokoine aliefariki miaka 35 iliyopita ambapo ameeleza kuwa
marehemu Sokoine alikua anapenda sana michezo pamoja na kufanya kazi kwa bidii.
“Michezo
ni muhimu kwakua inaleta umoja,ushirikiano furaha lakini zaidi katika dunia ya
leo ni ajira ya kuaminika hivyo ni lazima vijana mkatumia vipaji mlivyonavyo
katika michezo mbalimbali ili muweze
kupata ajira na hatimaye mfanikiwe kama wengine waliofanikiwa kupitia
sekta hii”.alisema Mhe.Kassim Majaliwa.
Aliongeza
kuwa Michezo kwa sasa inatangaza Taifa letu ambapo ametolea mfano wa Timu ya
Taifa (Taifa Stars) ambayo hivi karibuni imefuzu kushiriki Michuano ya AFCON itakayochezwa
baadae mwezi juni huko nchini Misri,Timu ya Vijana chini ya Miaka 17 “Serengeti
Boys” itakayoshiriki Mashindano hayo ambayo yatafanyika hapa nchini kuanzia
April 14 -28 mwaka huu ambapo timu hiyo inatakiwa kushinda mechi mbili tuu ili
iweze kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia nchini Brazili.
Katika
hatua nyingine Mhe.Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali itaendelea kumuenzi
Hayat Edward Moringe Sokoine kutokana na mchango wake wa kuletea Taifa
maendeleo kwa kuhimiza wananchi kujituma, kuwa wazalendo pamoja na kudumisha
amani ya nchi.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
amesema kuwa mchezo wa riadha umeendelea kufanya vizuri kimataifa kwakua nchi
imepata wawakilishi watakaoshiriki mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa
kufanyika mwaka 2020 huko Tokyo Japan,mashindano ya riadha ya Dunia pamoja na
Jumuiya ya Madola.
Mhe.Shonza
ameongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na Chama cha Riadha nchini inaendelea na
maandalizi ya mashindano ya riadha ya kimataifa ya All Africa Games,World
Championship na African Cross Country Championship ambayo Tanzania ndio itakuwa
Mwenyeji.
“Mchezo
huu wa riadha umeitangaza vyema nchi yetu kupitia wanariadha mbalimbali
waliofanya vizuri kimataifa ambapo timu yetu ya Taifa ya mbio za nyika
ilishiriki mashindano nchini Dernmark na kumaliza katika nafasi ya 8,10 na 11
kupitia wanariadha Failuna Matanga,Emmanuel Ginik,Gabriel Geay na Aliphonce
Simbu”.alisema Mhe.Shonza.
Hata
hivyo Rais wa Chama cha Riadha nchini
Mhe.Antony Mtaka amewataka waandaaji wa mbio mbalimbali nchini kuzingatia
Sheria na taratibu hususan usajili wa
mbio hizo katika Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) kabla ya kuzitangaza ama kuhamasisha wadau na wananchi kushiriki.
Naye
mshindi wa mbio za Kilometa 21 kwa wanawake Bibi Failuna Matanga amesema kuwa
mafaniko anayopata kupitia riadha ni kutokana na kujituma kufanya mazoezi
pamoja na nidhamu katika mchezo huo.
Mbio
hizo za Soikone Memorial Marathon zilishirikisha mbio za Kilometa 2 na
nusu,Kilometa 05 na kilometa 21 ambapo Watoto,wasichana
na wavulana walishiriki na washindi kupewa zawadi ikwemo pesa pamoja na medali.
……MWISHO….
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.