Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda akiwa na Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi alipokuwa kwenye mkutano na walimu wazalendo mkoani Iringa kujadili maswala ya uzalendo wa wananchi wa Tanzania kwa nchi yao
Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na naibu meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata
Baadhi ya walimu wazalendo walihudhulia mkutano huo uliongozwa na Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda
WAZIRI mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka
walimu wazalendo wa mkoa wa Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi
yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta
maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga
amani.
Akizungumza na baadhi ya walimu wa
shule za sekondari na shule ya msingi mkoani Iringa waziri mkuu mstaafu mizengo
panda aliwataka walimu hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha
pekee ya kuhakikisha tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.
Kuthamini vitu vilivyopo katika nchi
yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za nchi
na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na nchi yao
bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo” alisema Pinda
Pinda alisaema kuwa nchi nyingi
ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana
uongozi bila kutumia mabavu,hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya
kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.
“Angalieni nchi kama Somalia tu hapo
jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo wa
wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini
maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu” alisema Pinda
Pinda aliongeza kwa kusema kuwa
uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui
nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa
wazalendo na nchi yao.
Pinda aliwata walimu kuanza kuwa na
uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda nchi hii
kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa watakuwa
na lengo la kulinda amani ya nchi.
“Uzalendo pia huanzia pale
unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa
mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara
kuna mambo ya msingi utajifunza tu” alisema Pinda
Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi
aliwataka walimu kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio
chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na
uzalendo wan chi yao.
“Wananchi wanasababisha umasikini
wenyewe kutokana na kuchagua viongozi ambao hawana uwezo ndio hupelekea
umaskini katika kwa wananchi waliomchagua kiongozi waliyekuwa na
imani naye,hivyo kukosea kuchagua kiongozi bora ni kujitafutia matatizo
wenyewe” alisema Ngerera
Hapi aliongeza kwa kuwaambia walimu
hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri mdogo hasa wanafunzi
kwa kuwa ndio kipindi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa wa maisha ni nini.
“Jamani lazima mjifunze mnapotaka
kumlaumu kiongozi mlimchagua wenyewe ni lazima mjipie wenyewe kwanza mlikosea
wapi na sasa mnatakiwa mfanye nini ili kuhakikisha mfanya kazi huku mkiwa
mmetawaliwa na uzalendo wenu” alisema Hapi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi alimuakikishia waziri mkuu
mstaafu Mizengo Pinda kuwa walimu wazalendo wamekuwa wazalendo kweli kweli kwa
kuijenga Iringa mpya na kufanya kazi pamoja na serikali pamoja na chama tawala.
“Walimu unaowaona humu ndani wote ni
wanachama wa chama cha mapinduzi na wapo tayari kukitumikia chama tawala kwa
kuwa kinaongoza vizuri serikali kwa miaka yote” alisema Ngowi
Ngowi alisema kuwa walimu
wazalendo wamekuwa wakifanya kazi ya kuutangaza uzalendo kwa wanafunzi na
wananchi wote ambao wanatuzunguka kwa lengo la kufanya kazi pamoja na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
“Rais wetu amekuwa akifanya kazi kwa
kutunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja hivyo hata sisi walimu wazalendo
mkoa wa Iringa tunamuunga mkono kwa kila jambo jema ambalo anaifanyia nchi yetu”
alisema Ngowi
Ngowi alimazia kwa kumuomba waziri mkuu mstaafu
Mizengo Pinda kuwafikishia salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr
John Pombe Magufuli kuwa walimu wazalendo mkoa wa Iringa wapo makini na wapo
tayari kufanya kazi pamoja naye kwa kila jambo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.