ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 8, 2019

KUTOSAJILI LAINI YA SIMU AU KUSAJILI KWA KUTUMIA JINA BANDIA NI 'SOO'



Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  imefanya Mkutano na wadau  wa huduma za mawasiliano  Mkoa wa Mwanza  ikiwa na lengo la kukumbushana taswira ya Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ya mwaka 2015,Matumizi bora ya mitandao ya kijamii, changamoto za watumiaji wa mawasiliano na kuelimisha Umma na utatuzi wa malalamiko hayo.

Akiongea katika kikao hicho Mkuu wa Kanda ya Ziwa Mamlaka ya Mawasiliano Mhandisi Fransis Mihayo amesema kutokana na ukuaji wa tekinolojia kumekuwa na uelewa mdogo wa watumiaji wa mitandao hivyo kifanya makosa ya kimitandao kuongezeka kila siku.
" Mamlaka inayo orodha ya watoa huduma mitandaoni wanaoendelea kurusha maudhui kwa kuvizia, inawataadharisha kuacha kuvunja sheria, bali wafuate taratibu za usajili,"alisema Mhandisi Mihayo.

Aidha amewaomba viongozi wa dini wakati wakiendelea kutujenga na kutuimarisha kiroho, watukumbushe pia uwepo wa changamoto ya matapeli mitandaoni na kamwe kila mtu hapaswi kutoa ushirikiano wa aina yoyote kwa kujibu ujumbe mfupi na kuendelea na mazungumzo na matapeli kupitia simu.

Naye Kamishna Msaidizi wa polisi Muliro J.MULIRO amesema maendeleo makubwa  ya kitekinolojia yameleta ongezeko kubwa la huduma mbalimbali mitandaoni, na kuleta msukumo mkubwa wa ukuaji katika Sekta ya mawasiliano.

"Mwaka 2000 kulikuwa na laini za simu 284,109 idadi hii imeongezeka hadi laini milioni 43 kwa sasa wakati huduma za intaneti wameongezeka  kutoka milioni 3 na laki tano kwa miaka 5 iliyopita hadi milioni 17 hivi leo," alisema Kamishna Muliro.

Kwa upande wao watoa huduma kutoka Vodacom wakiwakilishwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa Victoria, Ayubu Kalutya  amesema wao hufanya kazi hadi jumamoai hivyo wangependa hata Jeshi la polisi lingefanya hivyo hasa wanaohuaika na taarifa ya upotevu 'loss report' kwani wateja huchukua muda mrefu kupata taarifa hii, pia huwachelewesha kurudisha line zao.

"Kuwe na udhibiti wa simu ili makampuni yanayotoa huduma za simu yaweze kuendesha huduma kuwezs kuwa na mawasiliano mazuri na wateja wao,"alisema Kalutya.

Aidha Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha uhalifu wa kimtandao kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, ASP Joshua Mwangasa amesema, kuna changamoto kubwa ya kutoa taarifa za uongo hivyo jeshi la polisi linakabiliana na kila mvunjifu wa kosa hilo, hata hivyo ushirikiano mkubwa kati ya Jeshi la polisi na wananchi inasaidia kuleta amani.

"Ili kuepuka kufanya makosa ya mtandao  ni vema kufuata sheria,kuwa na hofu ya mungu, kuepuka kutuma taarifa udiyo na uhakika nayo na kuhakikisha kila mtu anatoa taarifa kwa jeshi la polisi pale ualifu unapotokea,"alisema ASP Mwangasa.

Aidha, ushirikiano unatakiwa ili kuleta amani kwani baadhi ya mitandao ya kijamii ipo nje ya nchi hivyo Mamlaka ya Mawasiliano haina mamlaka nayo.

Hata hivyo amesisitiza kuwa uvunjifu wote wa sheria uripotiwe polisi ili wahalifu wakabiliwe na sheria ifuate mkondo wake, pia ulinzi uanzie kwa mtu mwenyewe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.