ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 11, 2014

RAIS KIKWETE AFUNGUA DARAJA LA KISASA LA MABATINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la ufunguzi wa daraja la Kisasa la mabatini Mwanza.
* Amfagilia Meya wa Jiji la Mwanza kwa kueleza mipango ya maendeleo na kusema anglipata Mameya kama yeye nchi ingepiga hatua.
*Azindua miradi miwili ya Daraja la kisasa la Mabatini.

*Aweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami ya Usagara-Kisesa yenye urefu wa kilomita 16 

Rais Dk Kikwete amagiza viongozi wa serkali ya Mkoa, Wilaya na wananchi kwa kushirikana na vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua kali watu wanaohujumu miundombinu ya daraja hilo wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa polisi Mabatini.

“Haiwezekani watu waachwe wakiharibu ili kurudisha nyuma maendeleo ikiwemo kukamilika ka daraja hili la kisasa kabisa nchini kote chukueni hatua mara moja kwani kero ya majanga ya ajali, vifo na msongamano ndo kulipelekea serikali kujenga daraja hili,”alsisitiza.

Pia amewaagiza madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela ndani ya Jiji kweka mipango ya maendeleo na kuanza kufikiria ujenzi wa shule za awali, msingi na sekondari kwa kwenda juu ikiwa ni majengo ya gorofa ili kuondokana na uhaba wa maeneo.
“Make kwa pamoja kwa kushirikiana ili kuona njinsi gani mtatekeleza ujenzi huo na mkubaliane maeneo ya kutekeleza ujenzi wa majengo ya shule hizo kwa manufaa ya wanafunzi na Jiji hili ambalo linakuwa kwa kasi”alisema.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea daraja la kivuko cha juu lililojengwa eneo la Mabatini jijini Mwanza akiwa ameambatana na waziri wa Ujenzi, mkuu wa mkoa wa Mwanza, Meya wa jiji, Meya wa Manispaa ya Ilemela na wakuu wengine.
Juu kwa juu daraja la Mabatini Mwanza.
Umati uliofurika kushuhudia uzinduzi huo wa daraja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia.
Rais Dk Kikwete alisema kufunguliwa kwa daraja hilo kumesaidia kumaliza kero ya ajali za kugongwa watu lakini pia msongamano umepungua na sasa TANROAD wanaendelea na upanuzi wa njia tatu kuanzia eneo la Natta hadi eneo la stendi ya mabasi Buzuruga.

“Tunzeni viwatunze na daraja hili litawezesha kulitangaza Jiji hili na Mkoa wa Mwanza hivyo ni vyema mkashirikiana katika utunzaji kwa wanaofanya uaribifu wa miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kupitisha pikipiki, kuvunja taa na wengine kupanda na mawe kwa lengo la kuponda magari yanayopita chini hivyo vyombo vya ulinzi na usala vipo wachukulieni hatua kali,”alisisitiza.

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuri akihutubia.
Naye Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuri alisema tayari Mkandarasi ameisha pewa kazi ya kusanifu daraja la kisasa na kubwa zaidi eneo la Furaisha ambapo Wizara imeisha toa fedha na litatumia shilingi bilioni moja ili kuwezesha eneo hilo kuwa na daraja pia.

“Tangu umeingia madarakani na kuona inafaa kukusaidia ambapo sikukuhonga ili unipe uwaziri bali kwa kuona inafaa zaidi, umeweza kujenga mtandao wa barabara za lami kwa kilomita 11,154 nchini kote ili kurahisisha watanzania kufika kila mahali hakika umetimiza wajibu wako kilichobaki ni kukuombea kwa mwenyezi mungu utakapo maliza muda wako na tutakukumbuka sana,”alisema.
Dk Magufuri pia alisema tayari Wizara yake imishatoa fedha kwenye Halmashauri ,mbalimbali nchini kwa ajili ya ujenzi wa barabara za vijijini ambapo Jiji la Mwanza limepata Sh. bilioni 1.1 na Manispaa ya Ilemela Shilingi bilioni 1.0.

“Nimshauri Mbunge Wenje auhudhulie vikao vya Baraza la Madiwani ili kupanga maendeleo badala ya kuhamasisha vijana kufanya maandamano na vurugu na kwa kupita kwenye barabara zilizojengwa na Rais Dk Kikwete, serikali ya CCM na hata kwa ujenzi wa daraja hili litasaidia kupunguza maandamano,”alisema huku akishangiliwa kwa nguvu kwa vijembe hivyo.

Aliongeza kuwa Mbunge Wenje leo amesema mwenyewe kuwa yeye si tikiti maji lakini inaonyesha kuwa ni tikitimaji kwani amekuwa na busara ya kuomba kwa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutambua hilo hata wenzake ndani ya CHADEMA kungelikiwa hakuna maandamano

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akihutubia mbele ya Rais Jk na wananchi waliofurika uwanja wa Polisi Mabatini Mwanza.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akitoa salamu za jiji hilo alianza kwa kunukuu maandiko ya vitabu vitakatifu kuwa “watuwangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” akimaanisha vijana kutumika vibaya na baadhi ya wanasiasa kwa kuwa mstari wa mbele kufanya maandamano na vurugu kwa matarajio makubwa.

“Maendeleo ni Mipango na Jiji la Mwanza, Mhe. Rais Dk Kikwete limekuwa likiitekeleza ikiwa ni Ilani ya CCM ya uchaguzi ya mwaka 2010 lakini kupita Baraza lake la Madiwani ambapo limejenga barabara za km 9 kwa bilioni 15.2 za lami, barabara za mawe km 2.9 kwa bilioni 1.6,”alisisitiza.

Aidha Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeendelea na ujenzi wa  vyumba 68 wa Maabara ambapo kila vyumba vitatu vinajengwa kwa kila sekondari moja ya Kata katika Kata 12 za Jimbo hili, Hlmashauri pia imetoa fedha za kusaidia ujenzi huo ambapo kila chumba kimoja imetoa shilingi milioni 20 na hivyo kila Kata itapewa milioni 60 kwa maabara tatu , awamu ya kwanza zimetolewa milioni 20.

“Tunatarajia ifikapo tarehe 21 Novemba tutakuwa tumemaliza ujenzi japo kuna baadhi ya watu na wanasiasa wanapita huko wakiwaambia wananchi wasichangie maendeleo lakini kiongozi mzuri ni yule anayewahamasisha wananchi wake anaowaongoza kuchangia shughuli za maendeleo ili kupatikana huduma bora za kijamii,” alishangiliwa na umati wa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza akitoa salamu zake.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza wamefika uwanja wa Polisi Mabatini kumsikiliza Mhe. Rais Jk.
Kwaya iliyotia fora kwa ujumbe madhubuti kiasi cha kupata mwaliko siku chache zijazo kwenda jijini Dar es salaam kwenye dhifa ya kitaifa... AIC Vijana Makongoro Choir 'Wana Kekundu' ambao kwa sasa wanavuma kwa album yao iitwayo 'Keusi' wakitumbuiza.
Kiasili zaidi.
Shangwe zikilipuka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza wanakwaya wa AIC Vijana Makongoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya pamoja na AIC Vijana Makongoro Choir.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya pamoja na viongozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANROAD Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wake.
Eneo la tukio daraja la Mabatini jijini Mwanza. 

 Awali Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Ezekial Wenje, alipopewa nafasi ya kusalimia alianza kwa kuwapongeza wananchi, walimu, askari na watumishi wengine kwa kukatwa kodi na kufanikisha ujenzi wa barabara, daraja na huduma mbalimbali za kijamii.

“Bila wananchi kulipa kodi, bila kuchangia kununua bidhaa hakika hakuna ujenzi wa daraja wala barabara za kiwango cha lami hivyo ni vyema wananchi mkajipongeza kwa hilo kwani fedha zilizojengwa hapa niza kwenu na si za CCM,” na kushangiliwa na vijana wafuasi wa CHADEMA.

Wenje alisema kuwa nawapongezeni kwa kufanikisha kutokana na kulipa kodi zenu ambazo matunda yake mnayashuhudia leo lakini nikuombe Rais uweze kutujengea barabara ya kutoka Igoma hadi Buhongwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 12.2 likiwemo daraja la Fumagila Igoma.

Awali Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Charles kitwanga “Mawe matatu” Mbunge wa Jimbo la Misungwi alimpiga kijembe Mbunge Wenje kwa kusema kuwa vijana msitumike na sasa ni vyema mkajitambua kuliko kutumika kwani dunia ya leo niya Sanyansi na Teknolojia hivyo wajitambue ili kuendana na wakati.

“Acheni kutumika kwa maandamano na vurugu kwani havitawasaidia wala kuwaongezea maarifa hivyo ni vyema mkawa  vijana wenye kuelezwa kisha nanyi mkachanganya akili za kuambiwa na zenu ili msiwe kama Bayuwayi,”alisisitiza.

VIAGRA HUSABABISHA UPOFU

CHANZO:BBC SWAHILI
Watafiti nchini Australia wanadai kwamba dawa inayotumiwa kuongeza nguvu za kiume VIAGRA husababisha upofu baada ya mda mrefu.
Kulingana na Watafiti hao kutoka Australia, kiungo fulani katika dawa hiyo inayotumiwa kukabiliana na ukosefu wa nguvu za kiume,huathiri uwezo wa kuona miongoni mwa wanaume ambao wana ugonjwa wa macho.
Kulingana na gazeti la Nation nchini kenya, Madaktari nchini Australia wamebaini kwamba kiungo fulani katika dawa hiyo kinaweza kusababisha upofu miongoni mwa wanaume wenye tatizo la ugonjwa wa macho.
Vilevile inadaiwa kuwa dawa hiyo pia inaweza kuwaathiri watumiaji ambao wanaona vizuri.
Utafiti huo uliofanywa katika panya,ulibaini kwamba hata watu wasio na ugonjwa wa macho wanaweza kuathirika.

KAMPENI YA UTOAJI WA CHANJO YA SURUA-RUBELLA WILAYA ZA MKOAWA MWANZA


TANGAZO

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA KUTAKUWEPO NA KAMPENI YA UTOAJI WA CHANJO YA SURUA-RUBELLA KWA WATOTO WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA 15, ITAKAYOANZA TAREHE 18 HADI 24 OCTOBA, 2014 KWENYE VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA, SHULENI NA VILE VITAKAVYOANDALIWA NA HALMASHAURI HUSIKA.

PAMOJA NA CHANJO HII, WATOTO PIA WATAPATA CHANJO YA POLIO, MATONE YA VITAMINI A PAMOJA NA DAWA ZA MINYOO.

CHANJO HII NI SALAMA NA ITAMKINGA MTOTO DHIDI YA MAGONJWA YA SURUA NA RUBELLA NA MADHARA YAKE.

CHANJO HIZI ZITATOLEWA BILA MALIPO. EWE BABA, MAMA, MLEZI HAKIKISHA MTOTO WAKO ANAPATA CHANJO.

KAULI MBIU: LINDA, OKOA MAISHA ZUAI ULEMAVU-KAMILISHA CHANJO.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA WIZARA YA AFYA NA    USTAWI WA JAMII KUPITIA MPANGO WA TAIFA WA CHANJO PAMOJA NA LIONS CLUBS

Friday, October 10, 2014

WATU 11 WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KIGOMA.

 ONYO PICHA ZIFUATAZO ZINATISHA
TUNAOMBA RADHI...


WATU kumi na moja wameuawa kwa kuchomwa na moto wakiwa ndani na nje ya nyumba baada ya wananchi wenye hasira kali kuwatuhumu watu hao kuwa ni washirikina.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi na moja alfajiri mkoani Kigoma baada ya watu hao kuvamiwa na wananchi hao na kuanza kuchomewa nyumba zao moja baada ya nyingine huku wengine licha ya kufanikiwa kutoka ndani ya nyumba hizo zilizokuwa zimetanda moshi mzito, walipokelewa na wananchi hao wavamizi waliokuwa na majani makavu na matairi ya magari na kuanza kuwawasha moto kuwachoma mithili ya kuni. 

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ambalo ndilo chanzo cha habari hii lilifika eneo la tukio majira ya saa kumi na mbili asubuhi ikiwa ni saa moja mara baada ya tukio nakukuta mifupa sanjari na majivu ya miili, huku miili mingine ikifuka moshi na kuendelea kuteketea, miili mingine ikiwa kama ilisulubiwa kwa kupondwa mawe hadi kifo, ile hali waliofanya tukio hilo wakiwa wametokomea pasipojulikana.  
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku likiwasaka kwa udi na uvumba watu waliohusika na kutenda unyama huo ulio kinyume na haki za binadamu.
WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI KUEPUKA KABISA MATUKIO YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA KURIPOTI HARAKA PINDI WANAPOHISI DALILI ZA HALI YA UVUNJIFU WA AMANI ZINAPOJITOKEZA AU MATUKIO KAMILI YA MAASI.

By Magege H Athanas

JK AZINDUA UJENZI WA BARABARA NA MIRADI YA MAENDELEO MWANZA

* RAIS Dk Jakaya Kikwete atamka waziwazi kuwa wanaokula fedha za miradi ya maendeleo na barabara kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
*Asema ujenzi wa barabara za lami nchini ni sawa na Damu katika mshipa wa binadamu ili kuwa kuimarisha uchumi na maendeleo.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete, amesema kwamba wanaotafuna fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kufikishwa katika chombo cha sheria na amnewataka kuacha mara moja alioufananisha na "Mchwa".

Aidha alisema kuwa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami nchini ni kama damu kwenye mishipa ya binadamu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya uchumi na kusaidia watanzania kufika kila mahali kwa urahisi zaidi
Pia kutawezesha kufika mahali na kusaidia kupatikana maendeleo ya uhakika na kukuza uchumi na pato la taifa ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora katika sekta zote zinazotoa huduma kwa jamii.

Akihutubia wananchi wa Mji wa mdogo wa Kisesa wilayani Magu, leo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Usagara-Kisesa yenye urefu wa km 16 utakaogharimu shilingi bilioni 19.4 ambapo ukikamilika utasaidia kuondoa msongamano wa magari kuingia Jijini Mwanza.

Dkt Kikwete alisema serikali kuendelea kujenga barabara hizo ni sawa na mishipa ya damu kwa binadamu ambapo bila kufanya kazi hakika hupoteza maisha hivyo ujenzi huo utalahisisha usafiri kwa watokao nchi jirani ya Kenya kupitia mkoani Mara kupitia barabara hiyo kuelekea Usagara-Busisi hadi mkoani Geita na nchi za Burundi, Rwanda, DRC Kongo na Uganda.

“Niwasihi wananchi kuacha kuuza kiholela maeneo yenu kwani sasa thamani ya ardhi itaongezeka thamani baada ya kukamilika ujenzi wake, pia kutapatikana fursa za kimaendelo na kiuchumi kwa wananchi wa maeneo ya Kisesa Wilaya ya Magu na wananchi wa usagara Wilaya ya Misungwi,”alisema.
Rais Dkt. Kikwete alisema ujenzi wa barabara nchini utaendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuimarisha Miundombinu kuwa ya uhakika hivyo kama kuna barabara hazijajengwa serikali imeziweka katika mipango yake ya kuzijenga ili kusaidia uboreshaji wake na kufungua njia za kufika kila mahali hapa nchini.

“Tutahakikisha tunakamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mkoa wa Rukwa-Sumbawanga, Mpanda-Sikonge hadi Tabora, Mpanda –Uvinza, Tabora –Manyoni na maeneo ya Kariua-Tabora mjini, Manyoni hadi Chaya na Tabora-Urambo na kuendelea kupanua barabara ya Musoma-Lamadi hadi Mwanza na ujenzi wa barabara kutoka Lamadi-Bariadi hadi Maswa hadi Mwigumbi,”alisisitiza.

Pia serikali itaendelea kujenga barabara ya lami ya kutoka Makutoano- Musoma hadi Mugumu-Serengeti na Loliondo hadi Karatu mkoani Arusha kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa wamu ili kuwezesha kukamilika kwa wakati na kutoa huduma ikiwa ni kujenga miundombinu ya uchumi kwani bila barabara imala nchi haiwezi kuwa na uchumi imara na madhubuti.



Aliagiza uongozi wa Mkoa na Halmashauri za Wilaya za Magu na Misungwi kuanza kuweka utaratibu wa kupima maeneo ya makazi, viwanda na uwekezaji kwa kuzingatia taratibu za Mipango Miji ili kuondoa usumbufu badae kwa kuvunja nyumba za wananchi kutokana na Mji wa Kisesa kukua kwa kasi pia Usagara.

“Msiwe viongozi wa kusubiria kuomba barabara bali muwe viongozi wabunifu na mlio na mtazamo wa mbele zaidi kwa kuanza kuliona hili kuwa ni jambo la kuanza kushugulikiwa kwa haraka ili kuhakikisha badae hakuna malalamiko na migogoro ambayo bila kupima itakuja kuwa kero,”alisema. 
Rais Dkt.Kikwete alionya watu wanaotafuna fedha za maendeleo kama “Mchwa” jambo hili liko hata kwenye fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami za TANROAD, Halmashauri za Wilaya kwenye mitaa na vijijini jambo ambalo halikubariki kamwe.

“Mtu mmoja anaamua kuhamisha fedha na kuziondoa huku na kupeleka kule hivyo kusababisha miradi kukwama na kutekelezeka chini ya kiwango hili napenda kutoa rain a koonya kuacha upuuzi huo na mara moja na serikali haita sita kuwachukulia hatua kali kwa watu walio na mchezo huo bila kusita,”alisisitiza.


Awali kabla ya kumkaribisha Rais Dkt. Kikwete, kuhutubia wananchi katika viwanja vya Mji mdogo wa Kisesa Wilayani Magu, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuri alimweleza kuwa ujenzi huo unafanywa na Kampuni ya Kizalendo ya Nyanza Road Works ya jijini Mwanza na hivyo kukamilika kwake kutafungua fursa kwa wananchi wa maeneo hayo na kuondoa msongamano wa magari.

Dkt. Magufuri alisema hadi sasa Mkandarasi amekamilisha kazi ya kusafisha barabara kwa asilimia 87, huku wananchi 340 wakiwa tayari wamelipwa fidia kiasi cha shilingi milioni 922 na serikali ndiyo mfadhili kwa asilimia 100 ya ujenzi wa mradi huo kwa kutoa fedha zote.

“Nimesikia kuwa sasa wananchi wanarubuniwa na baadhi ya watu wachchache kuuza maeneo yao kwa bei ya chini hivyo waache kufanya hivyo zaidi ya kuchangamkia fursa ya kujipanga katika ujenzi wa nyumba bora na kuyapima ili kongeza thamani ya ardhi ili kunufaika na ardhi yao,”alisisitiza.

Dkt. Magufuri, liwataka wananchi kuacha tabia ya kuiba vifaa vya ujenzi wa barabara hizo ikiwa ni mafuta ya mitambo, saruji na nondo ili kutochelewesha ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na hivyo wampe ushirikiano wa kutosha Mkandarasi Kampuni ya Nyanza Road Works kwani serikali pia itaendelea kukamilisha ujenzi wa km 11,152 za kiwango cha lami nchini kote.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROAD makao makuu, Christian Annko alisema barabara hiyo itawekewa alama za barabarani, ujenzi wa daraja kubwa eneo la Nyashishi na Mkandarasi yuko katika muda ambao utamuwezesha kukamilika kwa ujenzi huo kwa muda uliopangwa.

MWALIMU AKUTWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE

CHANZO: PRINCE MEDIA
MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Muungano iliyopo mji mdogo wa Himo wilayani Moshi, Richard Ndoile (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za kukutwa gesti na mwanafunzi wake wakifanya mapenzi. 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema jana ofisini kwake, kuwa tukio la kukamatwa kwa mwalimu huyo lilitokea Oktoba 4, saa 5.00 asubuhi, katika gesti ya Kilimanjaro iliyopo Himo. 

Moita alisema mwalimu na mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) ambaye anasoma Shule ya Sekondari Muungano Kidato cha Tatu, walikamatwa baada ya wazazi wa mwanafunzi kumuona binti yao akiwa amepakiwa kwenye pikipiki ya mwalimu wake, kuelekea mahala kusikojulikana. 

Alisema hatua hiyo iliwafanya kuhamaki na hivyo kuanza kufuatilia mwelekeo wa pikipiki ili kujua hatma ya safari yao hiyo. 

Alisema baada ya kuwafuatilia, pikipiki hiyo ilielekea kwenye gesti hiyo na baada ya kuteremka mtuhumiwa na binti yao waliingia ndani na kuchukuwa chumba, kwa lengo la kutimiza haja zao. 

Kwa mujibu wa Kamanda Moita, wazazi waliamua kupiga simu katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Himo kwa lengo la kutoa taarifa, ambapo polisi walifika lakini hadi mtuhumiwa anakamatwa tayari walikuwa wameshatekeleza tendo la kujamiiana. 

Alisema mwalimu huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha Himo, kwa ajili ya kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI CHA HISANI KUCHANGIA MFUKO WA KAMPENI WA JITOLEE KWA AJILI YA KINAMAMA WA AFRIKA, JIJINI DAR.

Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 9, 2014 jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile, Freddie Manento, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Meneja Masoko Msaidizi wa Kampuni ya TOYOTA Tanzania, Eliavera Timoth, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa  mradi wa Uzazi Uzima, Dkt. Benatus Sambili (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa  Mpango wa Kujenga Uwezo katika mradi wa Uzazi Uzima wa Amref, Dkt. Pius Chaya (kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika, Dkt. Festus Ilako. Picha na OMR
Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika, Dkt. Festus Ilako.
Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo
Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo
Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya kinamama wakiserebuka kucheza muziki maalum unaomtukuza mama, wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR
Baadhi ya kinamama wakiserebuka kucheza muziki maalum unaomtukuza mama, wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR