ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 10, 2014

JK AZINDUA UJENZI WA BARABARA NA MIRADI YA MAENDELEO MWANZA

* RAIS Dk Jakaya Kikwete atamka waziwazi kuwa wanaokula fedha za miradi ya maendeleo na barabara kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
*Asema ujenzi wa barabara za lami nchini ni sawa na Damu katika mshipa wa binadamu ili kuwa kuimarisha uchumi na maendeleo.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete, amesema kwamba wanaotafuna fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kufikishwa katika chombo cha sheria na amnewataka kuacha mara moja alioufananisha na "Mchwa".

Aidha alisema kuwa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami nchini ni kama damu kwenye mishipa ya binadamu kwa lengo la kuboresha miundombinu ya uchumi na kusaidia watanzania kufika kila mahali kwa urahisi zaidi
Pia kutawezesha kufika mahali na kusaidia kupatikana maendeleo ya uhakika na kukuza uchumi na pato la taifa ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora katika sekta zote zinazotoa huduma kwa jamii.

Akihutubia wananchi wa Mji wa mdogo wa Kisesa wilayani Magu, leo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Usagara-Kisesa yenye urefu wa km 16 utakaogharimu shilingi bilioni 19.4 ambapo ukikamilika utasaidia kuondoa msongamano wa magari kuingia Jijini Mwanza.

Dkt Kikwete alisema serikali kuendelea kujenga barabara hizo ni sawa na mishipa ya damu kwa binadamu ambapo bila kufanya kazi hakika hupoteza maisha hivyo ujenzi huo utalahisisha usafiri kwa watokao nchi jirani ya Kenya kupitia mkoani Mara kupitia barabara hiyo kuelekea Usagara-Busisi hadi mkoani Geita na nchi za Burundi, Rwanda, DRC Kongo na Uganda.

“Niwasihi wananchi kuacha kuuza kiholela maeneo yenu kwani sasa thamani ya ardhi itaongezeka thamani baada ya kukamilika ujenzi wake, pia kutapatikana fursa za kimaendelo na kiuchumi kwa wananchi wa maeneo ya Kisesa Wilaya ya Magu na wananchi wa usagara Wilaya ya Misungwi,”alisema.
Rais Dkt. Kikwete alisema ujenzi wa barabara nchini utaendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuimarisha Miundombinu kuwa ya uhakika hivyo kama kuna barabara hazijajengwa serikali imeziweka katika mipango yake ya kuzijenga ili kusaidia uboreshaji wake na kufungua njia za kufika kila mahali hapa nchini.

“Tutahakikisha tunakamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mkoa wa Rukwa-Sumbawanga, Mpanda-Sikonge hadi Tabora, Mpanda –Uvinza, Tabora –Manyoni na maeneo ya Kariua-Tabora mjini, Manyoni hadi Chaya na Tabora-Urambo na kuendelea kupanua barabara ya Musoma-Lamadi hadi Mwanza na ujenzi wa barabara kutoka Lamadi-Bariadi hadi Maswa hadi Mwigumbi,”alisisitiza.

Pia serikali itaendelea kujenga barabara ya lami ya kutoka Makutoano- Musoma hadi Mugumu-Serengeti na Loliondo hadi Karatu mkoani Arusha kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa wamu ili kuwezesha kukamilika kwa wakati na kutoa huduma ikiwa ni kujenga miundombinu ya uchumi kwani bila barabara imala nchi haiwezi kuwa na uchumi imara na madhubuti.



Aliagiza uongozi wa Mkoa na Halmashauri za Wilaya za Magu na Misungwi kuanza kuweka utaratibu wa kupima maeneo ya makazi, viwanda na uwekezaji kwa kuzingatia taratibu za Mipango Miji ili kuondoa usumbufu badae kwa kuvunja nyumba za wananchi kutokana na Mji wa Kisesa kukua kwa kasi pia Usagara.

“Msiwe viongozi wa kusubiria kuomba barabara bali muwe viongozi wabunifu na mlio na mtazamo wa mbele zaidi kwa kuanza kuliona hili kuwa ni jambo la kuanza kushugulikiwa kwa haraka ili kuhakikisha badae hakuna malalamiko na migogoro ambayo bila kupima itakuja kuwa kero,”alisema. 
Rais Dkt.Kikwete alionya watu wanaotafuna fedha za maendeleo kama “Mchwa” jambo hili liko hata kwenye fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami za TANROAD, Halmashauri za Wilaya kwenye mitaa na vijijini jambo ambalo halikubariki kamwe.

“Mtu mmoja anaamua kuhamisha fedha na kuziondoa huku na kupeleka kule hivyo kusababisha miradi kukwama na kutekelezeka chini ya kiwango hili napenda kutoa rain a koonya kuacha upuuzi huo na mara moja na serikali haita sita kuwachukulia hatua kali kwa watu walio na mchezo huo bila kusita,”alisisitiza.


Awali kabla ya kumkaribisha Rais Dkt. Kikwete, kuhutubia wananchi katika viwanja vya Mji mdogo wa Kisesa Wilayani Magu, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuri alimweleza kuwa ujenzi huo unafanywa na Kampuni ya Kizalendo ya Nyanza Road Works ya jijini Mwanza na hivyo kukamilika kwake kutafungua fursa kwa wananchi wa maeneo hayo na kuondoa msongamano wa magari.

Dkt. Magufuri alisema hadi sasa Mkandarasi amekamilisha kazi ya kusafisha barabara kwa asilimia 87, huku wananchi 340 wakiwa tayari wamelipwa fidia kiasi cha shilingi milioni 922 na serikali ndiyo mfadhili kwa asilimia 100 ya ujenzi wa mradi huo kwa kutoa fedha zote.

“Nimesikia kuwa sasa wananchi wanarubuniwa na baadhi ya watu wachchache kuuza maeneo yao kwa bei ya chini hivyo waache kufanya hivyo zaidi ya kuchangamkia fursa ya kujipanga katika ujenzi wa nyumba bora na kuyapima ili kongeza thamani ya ardhi ili kunufaika na ardhi yao,”alisisitiza.

Dkt. Magufuri, liwataka wananchi kuacha tabia ya kuiba vifaa vya ujenzi wa barabara hizo ikiwa ni mafuta ya mitambo, saruji na nondo ili kutochelewesha ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na hivyo wampe ushirikiano wa kutosha Mkandarasi Kampuni ya Nyanza Road Works kwani serikali pia itaendelea kukamilisha ujenzi wa km 11,152 za kiwango cha lami nchini kote.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROAD makao makuu, Christian Annko alisema barabara hiyo itawekewa alama za barabarani, ujenzi wa daraja kubwa eneo la Nyashishi na Mkandarasi yuko katika muda ambao utamuwezesha kukamilika kwa ujenzi huo kwa muda uliopangwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.