ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 18, 2014

MTANGAZAJI WA BBC KOMLA DUMOR AFARIKI DUNIA.

Yatupasa kuamini kwamba mtangazaji huyu hatuto muona tena katika ulimwengu huu wa nyama kwa hivi sasa ni marehemu aliitwa Komla Dumor aliyekuwa mtangazaji wa BBD Focus On Africa.


BBC presenter Komla Dumor dies at 41

Akiwa na umri wa miaka 41, Mtangazaji Televisheni ya BBC Focus on Africa, Komla Dumor anaripotiwa kufariki dunia ghafla akiwa nyumbani kwake mjini London nchini Uingereza.
He was 41.
Komla joined the BBC African Service in 2007, after more than a decade working as a radio presenter in his native Ghana. He recently became the lead presenter of the BBC's first daily television programme for Africa.
He had a wide-ranging career as an interviewer and presenter - his interviewees included former US President Bill Clinton and the grandson of Nelson Mandela, Ndaba Mandela.

KANUSHO LA Dkt. CHAMI KUHUSIANA NA YALIYO POSTIWA FACE BOOK

Naitwa Cyril August Chami (PhD) Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini na Mjumbe wa NEC-CCM kupitia Wilaya ya Moshi Vijijini.

Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na mtu au watu waliotengeneza akaunti kwa jina langu kwenye  Mtandao wa Kijamii wa Facebook na kujifanya yeye au wao ndio mimi.

Wamepachika hata picha zangu zinazopatikana kirahisi kwa sababu ya majukumu ambayo nimeshawahi kuwa nayo kama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, na Waziri wa Viwanda na Biashara.

Hilo lenyewe, yaani kutengeneza akaunti kwenye Facebook kwa jina la mtu na kuweka picha zake bila ridhaa yake, ni kosa la jinai.

Lakini ubaya zaidi ni kwamba mtu huyo au watu hao wanawasiliana na wapiga kura wangu kule Moshi Vijijini na walio nje ya jimbo na kuwauliza kero zinazowakabili. Wanawajibu hao wananchi kana kwamba wao ndio mimi. Kwa vile wao sio mimi, majibu yao siyo sahihi. Lakini kwao hilo halina tatizo maana nia yao ni kunichafua.

Wanaenda mbali zaidi na kukitukana Chama changu cha Mapinduzi wakionyesha kuwa mimi ni shabiki na/au sympathiser wa CHADEMA.  Wanatukana wanachama wenzangu wa CCM na kwa maana hiyo, viongozi wangu wa CCM.

Naamini wanajua kuwa nia yao hii ni ovu lakini nawaomba watambue kuwa hawatafanikiwa katika malengo yao kwa sababu mtetezi wangu ni mkubwa kuliko nia hiyo yao.

Siyo siri kuwa asilimia kubwa ya mawasiliano kwenye mitandao yanafanyika kwa anwani feki, hivyo wajue kuwa hata wasomaji wangenishangaa sana kama ningejiundia akaunti ya Facebook,  niweke picha zangu, halafu NIANZE KUWATUKANA VIONGOZI, WANACHAMA NA CHAMA CHANGU CHA MAPINDUZI.

Ifahamike kuwa wakati wao wanawauliza wananchi wangu kero zao kwa Facebook wakiwa kwenye viyoyozi mimi nilikuwa naongea na wananchi hao ANA KWA ANA, siyo tu kuzijua kero zao bali kuzitatua.

Kwa mfano, kuanzia December 20 hadi Januari 17 nimetembelea Kata za Uru Kusini, Uru Kaskazini, Mbokomu, Old Moshi Mashariki, Old Moshi Magharibi, Kimochi, Kibosho Kati, Okaoni, Kibosho Magharibi, Kibosho Mashariki,  Mwika Kaskazini na Mwika Kusini. Nimefika pia TPC kumuonyesha DED wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi sehemu ya kujenga daraja la Samanga litakalounganisha vijiji vya Mikocheni na Chemichemi kwa shs 250 millioni na pia tumetembelea Kata ya Uru Mashariki kukagua barabara inayoanzia Kishumundu Parish hadi Materuni, na ambayo tuko mbioni kui-grade kwa shs 700 milioni na harakati za kuipata hiyo fedha zinakwenda vizuri.

Nimeshiriki fundraising ya kujenga ukumbi wa kisasa Mawella Parish Kata ya Uru Kusini, fundraising ya kujenga bwalo Mangi Meli Sekondari Kata ya Old Moshi Mashariki na fundraising ya kuvijengea uwezo vikundi 16 vya WEKEZA kata za Okaoni na Kibosho Kati. Kabla ya hapo nilishiriki fundraising ya kujenga jengo la utawala Uru Seminari katikati ya Novemba 2013.

Ningekuwa mtumiaji wa Facebook  ningepost events hizi zote na hata kutaja kiasi tulichopata na kiasi cha michango yangu na rafiki zangu.

Hilo sikufanya.

Kwa nini?
Ni kwa sababu asilimia 98 ya wananchi hawa niliowatembelea hawatumii Facebook, nalijua hilo, ndiyo maana nawatembelea kituo kwa kituo nikitambua nikiwasiliana nao kwa Facebook nitapata majibu kutoka kwa asilimia 2 ya wapiga kura, tena walio nje ya jimbo. Na katika kipindi chote hicho sikuweza kwenda kwenye mitandao kwa sababu nilikuwa vijijini kwenye ziara kama Katibu Mwenezi wa CCM Moshi Vijijini, Ndugu Hussein Jamal alivyopost siku chache zilizopita.

Watambue kuwa rekodi yangu ndani ya Bunge, CCM na Serikali inafahamika kuwa mimi si mpayukaji, sina ushabiki na upinzani, na ni kati ya makada wanaoipenda CCM kwa vitendo zaidi kuliko maneno. Kwa maana hiyo wengi wa wasomaji waliosoma hayo wanayonipandikizia wameshaanza kutia shaka kama huyo ndiye Chami wanayemfahamu, na katika hili wako sahihi.

Watambue pia kuwa kama nia yao ni kuniharibia ndani ya CCM na jamii wameshashindwa kwa sababu maneno ya kupandikiziwa kwa wiki moja hayawezi kuaminika zaidi ya rekodi yangu inayofahamika tangu Uru Seminari nilikokuwa Mwenyekiti wa UVCCM kwa miaka 3, Chuo Kikuu cha Dar nilikokuwa Rais wa Wanafunzi Kampasi ya Mlimani, Ikulu nilikokuwa msaidizi wa Rais masuala ya Uchumi, Mbunge, Naibu Waziri na Waziri.

Bila shaka wote nilioishi nao katika maeneo haya na kwingineko watakiri kuwa mimi si mwepesi wa kujisifu, kupayuka na wala si mtu wa matusi kwa mtu binafsi, viongozi wa dini, wa Chama au wale wa Serikali.

Wakati nawaonya waache siasa hizi chafu, nawatahadharisha pia kuwa za mwizi ni arobaini! Ipo siku mtu huyu au watu hawa wataumbuliwa na jamii.

Dr Cyril August Chami.
Mbunge wa Moshi Vijijini.

RAIS KIKWETE ATEUA MAKATIBU TAWALA WAPYA MIKOA MITANO NA KUHAMISHA WENGINE WAKIWEMO WAKURUGENZI WA MAJIJI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Januari 18, 2014,  amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wapya wa mikoa mitano na kuhamisha makatibu tawala wengine na Wakurugenzi wa Majiji nchini.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue iliyotolewa jioni ya leo, Ikulu, Dar Es Salaam inasema kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza leo hii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  Makatibu Tawala wapya ni Ndugu Wamoja A. Dickolangwa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa ambako alikuwa Kaimu Katibu Tawala; Ndugu Abdallah D. Chikota ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Newala na Ndugu Symthies E. Pangisa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Pangisa alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.

Wengine ni Ndugu Alfred C. Luanda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi wake,  alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Ndugu Jackson L. Saitabau ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Kabla ya hapo, alikuwa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha.

Taarifa hiyo iliwataja waliohamishwa kuwa ni Ndugu Beatha Swai aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na sasa anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Sipora J. Liana ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Benedict Ole Kuyan ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga anahamishiwa Mkoa wa Mara na Ndugu Salum M.Chima ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa anahamishiwa Mkoa wa Tanga.

Wengine waliohamishwa ni Ndugu Mgeni Baruani ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe anahamishiwa Mkoa wa Pwani; Ndugu Juma R. Iddi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya anahamishiwa Jiji la Arusha kama Mkurugenzi; Eng. Omari Chambo ambaye alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi anahamishiwa Mkoa wa Manyara kama Katibu Tawala wa Mkoa huo na Dkt. John Ndunguru aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi anahamishiwa Mkoa wa Kigoma kama Katibu Tawala wa Mkoa huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

18 Januari, 2014

ILI TAIFA LETU LIENDELEE LINAPASWA KUWA NA MATAJIRI WAKE WENYEWE NA SI WAWEKEZAJI WAGENI: KIGWANGALLA

Mbunge wa Nzega Hamisi K igwangalla akiwasilisha mada ndani ya kongamano lililokuwa na Ujumbe The impact of socialization for socio-economic development in our saciety.
SIKILIZA ALICHOSEMA KWA KUBOFYA PLAY.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hili lililofanyika chuo cha SAUT Mwanza.
Dr. Joseph Mwanga akiwasilisha ndani ya kungamano.
qI suggest that:
The family should be restored to its status as a strong bio psycho social unit;
Parents must balance work and family life for proper socialization of the children. We must not sacrifice our homes on the altar of our careers;
Family life education should be part of school curriculum at all levels with special emphasis on sexuality education;
Parents, counselors in schools, youth centers, churches, mosques and clinics should be youth friendly and accessible so that the youth can confide in them;
There should be adequate recreational facilities in schools and in the community to positively engage the youth;

The print and electronic media  should be censored so that immorality and violence will not be propagated in the name of entertainment and advertisement. By Dr. Joseph Mwanga.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo, aliwasilisha mada ya jinsi mawasiliano ya mitandao ya kijamii yalivyo muhimu katika karne ya sasa hasa yanapo tumiwa vizuri.
Mbunge wa Nzega Hamisi K igwangalla akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo.

"Where did we go wrong" "Kwanini tu masikini wakati huo huo tu matajiri" Ni swali la uwasilishaji wa mada wa Dr. Charles Kitima katika kongamano hili. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY

Dr. Makuri.
Mr. Kazeli Bituro 
Meza kuu ya wawasilishaji mada katika kongamano hilo lililofanyika Chuo cha SAUT likihusisha wasomomi wa chuo hicho, kutoka kushoto ni Rev. Dr. Charles Kitima, Dr. Hamisi Kigwangalla, Dr. Anthony Diallo na Dr. Gdrry Mshana.
Wasomi wa Chuo cha SAUT cha jijini Mwanza wakisikiliza kwa umakini uwasilishaji mada katika kongamano la The impact of socialization for socio-economic development in our society.
Mbunge wa Nzega Hamisi K igwangalla akiwasilisha mada ndani ya kongamano lililokuwa na Ujumbe The impact of socialization for socio-economic development in our saciety.

Tuwajenge wananchi kusimama katika misingi ya uwajibikaji.  MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.
Elimu ya dini ni msingi muhimu wa mawasiliano, Fedha yaweza kununua vitabu lakini siyo ufahamu,  fedha yaweza kununua chakula lakini siyo hamu (appetite), fedha yaweza kununua kitanda lakini siyo usingizi, fedha yaweza kukupa mashabiki lakini siyo marafiki, fedha yaweza kukupa dunia lakini siyo akhera. says Fr. Maziku L
MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.
Kwa umakini wasomi wa SAUT Mwanza.

NDANI YA LIBRARY YA HISTORIA MWANZA.

Kuna mengi yamehifadhiwa ndani ya Maktaba hii ya historia iliyojengwa kwa ushirikiano wa jamii ya watu toka taifa la India na Watanganyika (kabla ya uhuru) ni maktaba iliyoko barabara ya Posta katika kiunga cha Pizeria jijini Mwanza.
Jengo hili lilipewa jina la kiongozi huyu kutokana na mchango mkubwa alioutoa kuanzia wazo la ujenzi, fedha alizoweka kama mchango wake, ushauri na kadhalika.
Vitabu vinavyopatikana ndani ya maktaba hii vimeshiba busara na historia ya kujenga viongozi wa sasa na kesho.
Sehemu ya majina ya waliochangia ujenzi wa maktaba hii sanjari na viwango vyao vya fedha, katika ukumbi huu hapa ndipo Mkutano wa Kwanza wa Viongozi wa Chama cha kupigania Uhuru wa Afrika ulifanyika.
Kiwango cha chini kilikuwa ni shilingi 51 na centi 25
An angle.
Table.

HISTORY
Pan-African Leaders
       W.E.B. DuBois was one of the first African-Americans to support the idea of Pan-Africanism.  He attended the first Pan-African Conference in London in 1900.  He later organized the conferences held in Europe and in America.

       Although Dubois was a significant leader in the  origins of the Pan-African  Movement, it is imperative to understand why the imperialist powers were able to continue to exploit Africa.  We can begin with the relationship between the Western world and leaders like Julius Nyerere and Kwame Nkrumah.  Western governments encouraged them to provide limited welfare measures, particularly health care and education.

 The World bank underwrote their schemes for industrialization and agricultural development.  The colonial authorities ha, in many cases, drawn up plans for these projects before independence was granted.  Tanzania under Nyerere became on of the world's largest recipients of the World Bank loans.  Without this support, the Pan-Africanists' administration would not still  be existent.

        Nkrumah was the first of the Pan-African leaders to come to power.  His journey from prison cell to government was a pattern that was to be followed in an increasing number of colonies, as the British sought to maintain their power in Africa.  The more Nkrumah cooperated, however, their suspicion of Pan-Africanists resided.

       Joseph Stalin was the next great influence during the time of World War II.  To continue the progress of the movement, he disarmed the worker's movement.  After Stalin had done this, he attempted to make an alliance with other world powers by selling oil to Mussolini when he invaded Ethiopia and signed a pact with Hitler.  When Stalin tried to make an alliance with Great Britain, he ordered members of the communist party to drop their support for anti-colonial movements.  This discredited socialism in the eyes of many supporters, impacting India the most.

       The betrayal of the Indian anti-colonial struggle had indirectly affected the Pan-African movement (at this time, the organization was still American based.)  George Padmore, a leading West Indian communist party member decided to leave the communist party and join the Pan-African movement.  He successfully turn this organization into an African based movement by portraying it as the only combat to the imperialistic struggle.

       Pan-Africanist leaders were able to maintain the ability to do as they see fit, mainly because of the Cold War.  If they decided to step over their boundaries, however, they could have been become an enemy to the western world.  Actually, the Belgian, British, and U.S. governments all concluded that Patrice Lumumba had to be murdered when he called on the Soviet troops to support his government in the Congo.  On the other hand, others like Nyerere survived because of the support he gave the Western governments during the Cold War.

 A very persuasive quote by Marcus Garvey states:
     UP!UP! You Mighty Race! You can Accomplish What you will! I repeat that God created you masters of your own destiny, masters of your own fate, and you can pay no higher tribute to your Divine Master than function as man, as He created you. "A people without knowledge of their past and history is like a tree without roots!" AFRICA FOR THE AFRICANS!

       Even today, some experts partly blame the Pan-Africanists for the continued exploitation of Africa.  This is concluded because they continued to pursue economic and political policies that has kept Africa bound by the world powers.

Friday, January 17, 2014

MKENYA WA KWANZA KUTINGA OSCAR

>Orodha ya walioteuliwa kuwania tuzo za Oscar, imetolewa.
>Mkenya wa kwanza kuwahi kuwa katika Orodha hiyo pia ametajwa.
Lupita mwenye umri wa miaka 30 amepata uteuzi wa kuwa muigizaji msaidizi bora zaidi katika filamu za mwaka 2013. Si Mwingine bali ni Lupita Nyong'o nyota wa filamu liyowagusa wengi yenye mada utumwa, 12 years a Slave'.
Atamenyana na magwiji wa uigizaji Julia Roberts na Jennifer Lawrence katika tamasha la tuzo za Oscars mwaka 2014.
Babake Lupita ambaye ni mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya ameelezea kufurahishwa sana na taarifa hizo na kumtakia kila la heri binti yake.
Kwenye filamu ya '12 years a Slave', Lupita aliigiza kama mtumwa aliyetumiwa kama mtumwa wa kingono na mkubwa wake.
Tangu filamu hiyo iliyotengezwa mwaka 2013, na kutolewa, nyota ya Lupita imekuwa iking'aa kwani amejipata akiwa katika kumbi moja na wagizaji maarufu kama Brad Pitt, Julia Roberts na wengineo hali ambayo kwa wengi itasalia kuwa ndoto.
Alipata uteuzi katika tuzo za Golden Globes za Uingereza ingawa hakuweza kushinda 
THANX TO BBC SWAHILI.

SKYLIGHT BAND HARIiiiiii....!!!

DSC_0178
Kutokana na mapenzi kwa makubwa kwa mashabiki wa Skylight Band Mmiliki wa Band hiyo Dr. Sebastian Ndege a.k.a JEMBE aliamua kutoa kinywaji chake hicho kama zawadi kwa mwanadada atakayecheza vizuri staili za bendi hiyo.
DSC_0118
Hashim Donode mzee wa Oldies akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band sambamba na Digna Mbepera pamoja na Winnie kwenye show yao ya Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0049
Divas: Mary Lucos na Winnie wakiwapa raha fans wa Skylight Band.
DSC_0061
Sam Mapenzi akifanya yake jukwaani.
DSC_0075
Happy Birthday to you...... Happy Birthday dear Joti..........Happy Birthday to you....Shabiki wa Skylight Band anafahamika kwa jina la Joti (mwenye shati la kaki) alijumuika na marafiki zake kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0085
Skylight Band wakiendelea kutoa burudani na staili yao ya "Yachuma chuma".
DSC_0090
Birthday boy Joti akijimwaga na marafiki zake na sebene la Skylight Band.
DSC_0094
Warembo wakionekana kuchizika na Skylight Band.
DSC_0088
Rappa Joniko Flower akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0135
Ilikuwa full mzuka kwa mashabiki wa Skylight Band....Usipime na sio ya kukosa leo jioni pale pale muda ule ule....,mpango mzima.
DSC_0175
Rappa Joniko Flower akioyesha zawadi ya kinywaji cha PATRON kwa mashabiki wa Skylight Band ambapo mwanadada atakaye sebeneka vizuri atajishindia kinywaji hicho.
DSC_0180
Mzigo huu hapa kazi kwenu....Vijana mate yanawatoka.
DSC_0186
Vijana wa Skylight Band wakionyesha staili zao kwa mashabiki wao.
DSC_0199
Warembo wakionyesha makeke yao kwenye jukwaa la Skylight Band.
DSC_0213
DSC_0230
Wakaona hawaelekei ikabidi Aneth Kushaba AK 47 awaonyeshe manjonjo yake.
DSC_0224
Mchujoooooo....
  Mchujo ukiendelea....    
DSC_0237
Hapo je.....vijana wameiva sasa....
DSC_0239
Mashabiki wa Skylight Band ambao ghafla waligeuka kuwa mashabiki wa kuamaua nani mshindi..kwa umakini wakifuatilia burudani hiyo.
DSC_0262
Sony Masamba akionyesha staili mpya ya Skylight Band kwa mashabiki.
DSC_0263
Warembo wakifanya yao jukwaani.
DSC_0300
Mwishowe hawa ndio waliotinga fainali......na kutoka ngoma droo..tofauti ni maumbile tu lakini wote wakali.
DSC_0317
Walipatikana washindi wawili waliotoka ngoma droo kutokana na majaji ambao ni mashabiki...Pichani Sony Masamba akipata Ukodak na washindi hao huku Aneth Kushaba AK 47 (aliyeipa mgongo camera) akiwa hana mbavu.
DSC_0322
Baada ya zoezi hilo burudani iliendelea ni mwendo wa mduara tu....mambo ya kuzungusha nyonga wadada mpooo pale kati...???
DSC_0151
Aneth Kushaba AK47 na shabiki wake.
DSC_0156
Petit Man na Winnie wakishow love ndani ya kiota cha Thai Village.