ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 18, 2022

BENKI YA CRDB YAZINDUA MFUMO MPYA WA MAWAKALA , SASA WATAWEZA KUFUNGUA AKAUNTI NA KUTOA KADI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) pamoja na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, wakipiga makofi wakati wa uzinduzi rasmi mfumo mpya na wakisasa utakaowawezeza mawakala wa benki hiyo kutoa huduma kwa urahisi zaidi kupitia simu janja zao, uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam, Novemba 15, 2022.
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati wa uzinduzi rasmi wa mfumo mpya na wakisasa utakaowawezeza mawakala wa benki ya CRDB kutoa huduma kwa urahisi zaidi kupitia simu janja zao, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam, Novemba 15, 2022. Kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
 
Benki ya CRDB imekamilisha na kuuuzindua mfumo mpya na wakisasa utakaowawezesha mawakala wake zaidi ya 25,000 waliopo nchi nzima kumfungulia mteja akaunti na kumpa kadi ndani ya muda mfupi ili afurahie huduma za benki, imefanya hivyo kwa kutambua mchango wa mawakala katika kusogeza huduma za benki karibu zaidi na wananchi hususani waliopo maeneo ambayo hayana matawi ya benki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema sekta ya fedha ina mchango mkubwa katika ukuaji na maendeleo ya uchumi, kujenga uchumi jumuishi, na kupunguza umasikini ndio maana Serikali nyingi duniani kote zinatilia mkazo suala la ujumuishi wa kifedha (financial inclusion).
"Hapa nchini Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kisera ili kukuza ujumuishi wa kifedha kwa wananchi, Baadhi ya jitihada za kisera na kimkakati ambazo zimefanyika ni pamoja na kuanzishwa kwa Mpango wa Elimu ya Kifedha (Financial Education Program 2021/22 – 2025/26) na mwaka 2020, Serikali ilizindua Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (Financial Sector Development Master plan - 2020/21 -2029/30)," alisema Nnauye.

Pamoja na juhudi hizo, Waziri Nnauye alisema bado idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za benki ni ndogo akikumbusha utafiti wa kwanza wa Finscope wa mwaka 2006 ulioonyesha kuwa ni asilimia 46 tu ya watu wazima walijumuishwa kifedha, ambapo asilimia 11 tu walikuwa wakitumia huduma rasmi za kifedha.
Sababu kuu za watu wengi kuwa nje ya mfumo wa fedha, alisema ni ufikiwaji mdogo wa huduma za benki kupitia matawi katika maeneo ya vijijini na gharama kubwa za ufikiaji wa huduma za kifedha ikiwemo hitaji la kusafiri umbali mrefu katika maeneo yenye matawi ya benki kwani nyingi zilikuwa maeneo ya mkoani au wilayani.

Kwa kutambua mchango wa teknolojia kutatua changamoto hiyo, alisema Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Februari 2013 ilitoa Mwongozo wa Huduma za benki kupitia wakala na leo hii Benki ya CRDB ina zaidi ya mawakala 25,000 ambao ni sawa na asilimia 46 ya mawakala wote 55,000 wa benki waliopo nchini wanaofanikisha zaidi ya miamala milioni 100 yenye thamani ya shilingi trilioni 50 zikiwamo shilingi trilioni 1.3 za mapato ya Serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema, CRDB ndiyo ilikuwa Benki ya kwanza nchini kuanzisha huduma kupitia mawakala mwaka 2013 ikiwasajili mawakala 500 na leo hii inajivunia kuwa nao zaidi ya mawakala 25,000 ambao wamesambaa kote nchini hivyo kuifanya iongoze nchini na kuwa ya tatu Afrika Mashariki.

"Mfumo wa CRDB Wakala umekua na mchango mkubwa katika ufikishaji wa huduma za fedha kwa wananchi, taarifa zetu za utendaji zinaonyesha zaidi ya miamala milioni 100 yenye thamani ya shilingi Trilioni 50 imekua ikifanyika kupitia CRDB Wakala kwa Mwaka, mfumo huu pia umekua ukisaidia katika ukusanyaji wa mapato ya serikali ambapo takribani Trilioni 1.3 hukusanywa kwa mwaka," alisema Nsekela.
Aidha, Nsekela alifafanua kwamba mfumo huo wa CRDB Wakala unatoa huduma za fedha kwa watanzania milioni 3 kwa mwezi ambapo asilimia 40 ni wateja wa Benki na asilimia 60 ni wananchi wengine.

Mfumo wa CRDB Wakala, alisema umetoa zaidi ya ajira 35,000 kwa vijana wanaopokea kamisheni kwa miamala wanayoifanya.

CRDB Wakala App ni mfumo mpya wa kisasa, salama na wa kidijitali unaotumika kwenye simu janja kutoa huduma za kibenki kwa ufanisi wa hali ya juu hivyo kuongeza ufanisi, kasi ya utoaji huduma na kupunguza gharama za uendeshaji kwa watoa huduma hasa kwa mawakala wa Benki.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akibonyeza sehemu yenye ujumbe wa Ubora wakati wa uzinduzi rasmi wa mfumo mpya na wakisasa utakaowawezeza mawakala wa benki ya CRDB kutoa huduma kwa urahisi zaidi kupitia simu janja zao, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam, Novemba 15, 2022. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (watatu kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda.




Thursday, November 17, 2022

VITA VYA UKRAINE: NINI KILICHOTOKEA KATIKA MLIPUKO WA KOMBORA POLAND?

. Eeneo lililoathirika na mlipuko wa bomu Poland

Jeshi la Poland liliwekwa katika hali ya tahadhari siku ya Jumanne jioni baada ya kombora kutua katika eneo lake na kuua watu wawili.

Hatua hiyo ilijiri wakati Urusi iliporusha makumi ya makombora huko Ukraine na vikosi vya Ukraine vilijaribu kuyaangusha kwa makombora yake – ikiwa sehemu ya mfumo wake wa ulinzi wa anga.

Wakati mamlaka ya Poland - pamoja na washirika wa Nato - walipojaribu kubaini ukweli, timu ya uchunguzi ya BBC imekuwa ikichambua ripoti na kusoma picha kwenye mitandao ya kijamii ili kujaribu kufichua maelezo zaidi kuhusu tukio hilo.

Mlipuko huo ulikuwa wapi?

Mlipuko huo uliripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye vyombo vya habari vya Poland Jumanne jioni, vikielezea mlipuko karibu na kijiji cha Przewodow, nchini Poland, takriban kilomita 6 kutoka mpaka wa Ukraine.

RIPOTI za awali zilisema kuwa kombora hilo lilitua karibu na eneo la shamba ambalo wafanyikazi hupakia na kupima nafaka, na kuharibu jengo la karibu.

Tulikagua picha za satelaiti (ambazo zilionyesha shamba moja pekee katika kijiji) na kuzirejelea kwa njia tofauti na picha zilizopigwa eneo hilo Jumatano asubuhi ili kupata tovuti - ambayo imethibitishwa na mamlaka ya Poland.

.
Maelezo ya picha,

Ramani ya eneo lililoshambuliwa

Pia tulikagua video ambayo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii jioni ya Jumanne.

Inadai kuonyesha matokeo ya mara moja ya mlipuko kama kombora "lililoanguka kwenye eneo la Poland". Eeneo linalofuka moshi  linaweza kuonekana .

Kuna vidokezo vya kuona kwenye video ambavyo vinafanana na tovuti katika Przewodow.

Mchoro unaoonyesha picha ya skrini ya video na ramani ya eneo karibu na mlipuko

Barabara inayoonekana kwenye video (iliyoangaziwa na sisi kwa rangi nyekundu) ina muundo sawa na ile inayoonekana kwenye picha ya anga ya eneo hilo

Barabara mbele ya jengo la rangi nyepesi (iliyoangaziwa nasi katika machungwa).

Picha zilizopigwa ardhini siku ya Jumatano (zinazoonekana kwenye mchoro wa kwanza) zinaonyesha nyumba ya rangi nyepesi karibu na shamba hilo.

Na mimea na mistari ya miti inaonekana .

Tumejaribu kuwasiliana na mtu aliyechapisha video hii ili kuithibitisha zaidi lakini bado hatujapata jibu.

Picha kutoka kwa tovuti ya mlipuko pia zilianza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii jioni ya Jumanne, zikionyesha moto na trekta na trela ilioharibika.

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Shimo lililosababishwa na shambulio la kombora (picha: Tue 15 Nov)

Ilikuwa vigumu kupata hizi peke yao kwa sababu ya giza na ukosefu wa dalili pana za kuona.

 

Lakini picha iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii na polisi wa Poland Jumatano asubuhi inaonyesha maafisa wakichunguza eneo la tukio. Trela ​​, nafaka zilizomwagika na uchafuuinaweza kuonekana kwenye picha zote mbili.

MUSOMA, GEITA, UKEREWE KUPIGA MAKASIA KISHA FAINALI MBIO ZA MITUMBWI 11 DEC 2022 MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

ZAIDI ya wanamichezo 300 wanatarajiwa kushiriki mashindano ya mbio za mitumbwi yatakayofanyika katika mikoa ya Mara, Geita na Mwanza huku washindi wakiondoka na mamilioni ya fedha. Mashindano hayo yanayoandaliwa na The Scope Experience yanafanyika kwa mwaka wa 14 mfululizo yataanza wilayani Ukerewe Oktoba 27, Musoma Desemba 4 na fainali kuhitimishwa Desemba 11 jijini Mwanza katika eneo la Mwaloni (soko la Kirumba). Muandaaji wa mashindano hayo, Ayoub Sossy, amesema msimu huu wamepanua wigo na wanatarajia kufanya makubwa ambapo Musoma yatafanyika Kwenye mwalo wa Mwigobelo, Ukerewe (Monarch beach) na Mwanza (Mwaloni) kila kituo kutakuwa na wiki moja ya maandalizi na hamasa kwa wavuvi na wadau wengine lengo ni kuutambulisha mkoa na fursa zinazopatikana ili kuvutia wawekezaji na kufungua fursa za utalii. Meneja Mauzo wa TBL ambao ni wadhamini wa mashindano hayo, Yuda Ryaga amesema kila kituo kitashirikisha timu za wanaume na wanawake ambapo Ukerewe na Musoma washindi wa kwanza watapata Sh 500,000, wa pili Sh 300,000 na wa tatu Sh 200,000 kwa timu zote (Wanawake na wanaume). Amesema kwa upande wa fainali itakayofanyika Mwanza, kwa timu zote za wanawake na wanaume mshindi wa kwanza ataondoka na Sh 2 milioni, wa pili Sh 1.5 milioni na wa tatu Sh 1 milioni huku mshindi wa nne akipata Sh 800,000 na wa tano Sh 500,000 ambapo fedha hizo zitalipwa taslimu wakati wa mashindano. Naye Mwenyekiti wa mbio za Mitumbwi Mwanza, Ludovick Kanebuye amewataka wanamichezo wote waliosajiliwa kushiriki mbio hizo kwa kutumia vifaa (makasia na mitumbwi) ambayo imesajiliwa na mamlaka na kutambuliwa huku akisisitiza kila mtumbwi utakuwa na washiriki watano ambapo wanategemea zaidi ya wanamichezo 300 watashiriki.

Wednesday, November 16, 2022

TRA YATAMBA KUCHUKUA UBINGWA WA MPIRA WA MIGUU MICHUANO YA SHIMUTA

 

Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga 
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga 
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga 


Na Oscar Assenga,TANGA.


MABINGWA Watetezi wa Michuano ya Shimuta kwa upande wa Mpira wa Miguu miaka miwili mfululizo timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetamba kuendeleza wimbi la kuchukua kombe hilo.


Tambo hizo zilitolewa na Katibu wa timu ya TRA Hamna Shomari mara baada ya kumalizika kwa mechi yao ya mpira wa miguu dhidi ya KCMC ambayo ilimalizika kwa timu hizo kugawana pointi mojamoja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.


Mchezo huo ulichezwa kwenye viwanja wa mizani ya zamani Jijini Tanga ambapo timu ya TRA ililazimika kusawadhisha bao lao kipindi cha Pili kupitia Datram Benzema ambaye alitumia uzembe wa mabeki kupachika wavuni bao hilo na hivyo kuamsha shangwe uwanja mzima.


Awali kabla ya timu TRA kuandika bao hilo timu KCMC ndio ilikuwa ikiongoza kufunga bao ambalo lilifungwa na Yusuph Madili aliyepiga faulu ya kona iliyotinga moja kwa moja.


Shomari alisema kwamba wanamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kupata Sare na wana mechi nyengine kesho hivyo wana matumaini watarekebisha mapungufu na kufanya vizuri Michezo ijayo.


Alisema kwamba wamepania kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi yao dhidi ya timu ya PSSF.

TPDC YALAZIMISHWA SARE NA TICD MICHUANO YA SHIMUTA TANGA

 

Mshambuliaji wa timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia akiwania mpira na mchezaji wa  timu ya  Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya Mkoani Arusha (TICD) leo wakati wa mechi ya mpira wa miguu ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Shimuta ambapo timu hizo zilitoka sare tasa ya kutokufungana 
Mshambuliaji wa timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia akiwania mpira na mchezaji wa  timu ya  Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya Mkoani Arusha (TICD) leo wakati wa mechi ya mpira wa miguu ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Shimuta ambapo timu hizo zilitoka sare tasa ya kutokufungana 
Mshambuliaji wa timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia akijaribu kumtoka  mchezaji wa  timu ya  Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya Mkoani Arusha (TICD) leo wakati wa mechi ya mpira wa miguu ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Shimuta ambapo timu hizo zilitoka sare tasa ya kutokufungana 





Na Oscar Assenga, TANGA.

TIMU ya Soka ya Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) imelazimishwa sare tasa kutokufungana na timu ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya Mkoani Arusha (TICD) katika mchezo wa mpira wa Miguu uliochezwa kwenye Dimba la Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Shimuta.

Katika mchezo huo ambao ulianza kwa kasi kwa kila upande kupambana kutaka kuvuna alama tatu ambapo walilazimika kushambuliana kwa zamu kila mmoja kwa kuonyesha umahiri wake.

Timu ya TPDC ambao walikuwa wakiongozwa na wachezaji wake mahiri Nahodha Dalushi Shija,washambuliaji wake Eugene Isaya,Kiungo mshambuliaji Mohamed Muya ,Joseph Samani na Dastan Masasi waliweza kusakata vema kabumbuku na kuwa mwiba kila walipokuwa wakigusa mipira uwanjani.

Hali hiyo ilipelekea timu ya TPDC kufika mara kwa mara langoni mwa wapinzani wao lakini bahati haikuwa yao ya kuweza kupata bao na hivyo kujikuta wakimbulia pointi moja.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo,Kocha Mkuu wa TPDC Matuka Bizoo alisema kwamba wanashukuru kwa kuanza na sare lakini sio kwamba wameridhika ila watakwenda kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili kuweza kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye michezo mengine.

Bizoo alisema tatizo kubwa ambalo aliliona lililosababisha sare tasa hiyo ni timu yake kukosa muunganiko hivyo nalo atahakikisha analifanyia kazi haraka.

“Kikibwa leo niwapongeze angalau tumepata pointi moja sio mbaya lakini niwatake mhakikishe mnatulia mnapokuwa uwanjani na kupunguza presha “Alisema

FAINALI YA CRDB BANK TAIFA CUP JIJINI TANGA

 

 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa (katikati) akirusha mpira juu kuashiria kuanza kwa mchezo wa fainali kati ya Dar es salaam na Unguja (Wanawake) wa mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Bandari Jijini Tanga. Watatu Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa  (mwenye fulana yenye bedera ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Tanga, Viongozi wa Benki ya CRDB pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini wakati wa fainali ya mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Bandari Jijini Tanga.
Ukaguzi wa timu.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga kulikofanyika fainali ya mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akizungumza wakati akifunga mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa fainali ya mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga.







Monday, November 14, 2022

TASAC YATOA ELIMU YA ULINZI, USALAMA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MOROGORO

 

AFISA Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin akimuonyesha mmoja wa watumiaji wa vyombo vya majini namna ya kuvaa jaketi okozi






Na Mwandishi Wetu,Morogoro


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imetoa elimu ya Usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira mkoani Morogoro pamoja na kuendesha zoezi la ukaguzi wa Vyombo vya usafiri majini.

Ukaguzi huo ni sehemu mikakati ya Shirika hilo kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa kuzingatia viwango. 

Zoezi hilo liliendeshwa na Maafisa Ukaguzi na Udhibiti wa Vyombo vya Majini  wa Shirika hilo, Bw. Gabriel Manase na Maulid Nsalamba katika wilaya ya Ifakara mkoani humo. Maafisa hao walitoa elimu ya usalama na ulinzi ikiwemo utunzaji wa mazingira wanapokuwa kwenye shughuli zao


Akizungumza wakati wa zoezi hilo Manase alisema elimu hiyo ina umuhimu mkubwa sana hivyo jamii inapaswa kuitambua na kuweza kuzuzungatia wakati wote wanapotekeleza shughuli zao za kila siku.


Zoezi hili lilianza tarehe 11 Novemba, 2022 ifakara katika maeneo ya Ngalimila, Ngapemba, Utengule, Chita na Mngeta na Mchombe na litaendelea katika mikoa ya  iringa na Dodoma lengo ni kuhakikisha jamii inapata elimu.


Zoezi hilo liliendeshwa pia kwa ushirkiano na Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin na Afisa Uhusiano Mwandamizi Amina Miruko ambapo waliitaka jamii kuhakikisha inazingatia usalama kwenye vyombo vya maji ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinazaweza kuwakuta wawapo safarini.