Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa (katikati) akirusha mpira juu kuashiria kuanza kwa mchezo wa fainali kati ya Dar es salaam na Unguja (Wanawake) wa mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Bandari Jijini Tanga. Watatu Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa (mwenye fulana yenye bedera ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Tanga, Viongozi wa Benki ya CRDB pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini wakati wa fainali ya mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Bandari Jijini Tanga.
Ukaguzi wa timu.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga kulikofanyika fainali ya mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akizungumza wakati akifunga mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.