TIMU YA TAIFA YA UGANDA IMEWASILI JANA JIJINI MWANZA KWA NDEGE YA PRECISION MAJIRA YA SAA 12 JIONI IKITOKEA ENTEBE IKIWA NA KIKOSI CHA WACHEZAJI 18 NA VIONGOZI 10 HUKU IKIMWAGA TAMBO NYINGI ZA USHINDI.
PAMOJA NA KUKIRI KUWA STARS NI NGUMU NA KUTAMBUA MAKALI YA KOCHA WA TIMU HIYO MARCIO MAXIMO KOCHA WA TIMU YA UGANDA RAIA WA SCOTLAND BOBBY WILLIAMS AMESEMA AMEFANYA MAANDALIZI YA KUSHINDA MCHEZO HUO PIA ANAJIVUNIA KIKOSI CHAKE CHENYE CHIPUKIZI WAPYA WATATU AMBAO NI SULA MATOVU, PATRICK EDEMA NA IBRAHIM 'SADAM' JUMA.

TAIFA STARS YA TANZANIA LEO INAJIPIMA UWEZO NA CRANES YA UGANDA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA. MECHI HIYO YA KIMATAIFA IMO KATIKA KALENDA YA FIFA.
PAMBANO HILO LINACHEZWA KUZIANDAAA TIMU HIZO NA MECHI ZIJAZO ZA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA UBINGWA WA MATAIFA YA AFRIKA (CHAN)
STARS ITAANZA MECHI ZA CHAN KWA KUKIPUTA NA SOMALIA, NAYO UGANDA DHIDI YA BURUNDI.
MECHI ZA CHAN ZIMEPANGWA KUANZA MARCH 12.
WAKATI HUO HUO NAHODHA WA STARS SALUM SWEDI LEO KUAGA RASMI KUITUMIKIA TIMU HIYO.
NDANI YA STUDIO ZA CLOUDS FM MWANZA 88.1 KUTOKA KULIA NI MJUMBE WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA DR.AMOS MWAKILASA, MWENYEKITI BIBI MARIA KASHONDA, MJUMBE WA KAMATI HIYO BW. WALTER BGOYA NA WENGINEO.
MIE NIKITOA UFAFANUZI KWA WADAU WA TCRA WALIPOTEMBELEA 88.1 MWANZA. PEMBENI ANAONEKANA BW. SAMADU ABDUL NA MENEJA WA TCRA KANDA YA ZIWA BW. ERASTO MBILINYI.