PAMOJA NA KUKIRI KUWA STARS NI NGUMU NA KUTAMBUA MAKALI YA KOCHA WA TIMU HIYO MARCIO MAXIMO KOCHA WA TIMU YA UGANDA RAIA WA SCOTLAND BOBBY WILLIAMS AMESEMA AMEFANYA MAANDALIZI YA KUSHINDA MCHEZO HUO PIA ANAJIVUNIA KIKOSI CHAKE CHENYE CHIPUKIZI WAPYA WATATU AMBAO NI SULA MATOVU, PATRICK EDEMA NA IBRAHIM 'SADAM' JUMA.
TAIFA STARS YA TANZANIA LEO INAJIPIMA UWEZO NA CRANES YA UGANDA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA. MECHI HIYO YA KIMATAIFA IMO KATIKA KALENDA YA FIFA.
PAMBANO HILO LINACHEZWA KUZIANDAAA TIMU HIZO NA MECHI ZIJAZO ZA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA UBINGWA WA MATAIFA YA AFRIKA (CHAN)
STARS ITAANZA MECHI ZA CHAN KWA KUKIPUTA NA SOMALIA, NAYO UGANDA DHIDI YA BURUNDI.
MECHI ZA CHAN ZIMEPANGWA KUANZA MARCH 12.
WAKATI HUO HUO NAHODHA WA STARS SALUM SWEDI LEO KUAGA RASMI KUITUMIKIA TIMU HIYO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.