ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 22, 2021

WANAFUNZI WA SEKONDARI WAHAMASISHWA KULIMA KILIMO CHA MBOGA NA MATUNDA

 


Na Woinde shizza , Arusha


Wanafunzi zaidi ya 300 wa shule ya Sekondari ya Nkoanekoli iliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha wamehamasishwa ulimaji wa kilimo Cha mboga na matunda Ili wajipatie kipato na ajira mara tu wanapomaliza masomo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari mratibu kutoka kitengo cha jinsia na lishe cha taasisi kilele inayojishughulisha na masuala ya maua ,mboga,mizizi,viungo na matunda (TAHA)Salome Stephen alisema kilimo hicho mbali na kujipatia ajira na kipato pia ni Cha muda mafupi.

Alisema Taha wameamua kuhamamasisha watoto kwenye shule mbalimbali juu ya muhimu wa kilimo hicho pamoja na kutumia vyakula mchanganyiko Katika kila mlo Ili kujenga afya bora .

Aidha alitaja lengo la TAHA la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha kila mwananchi anatambua kilimo hicho ,fursa zilizopo Katika kilimo hicho na pia kilimo hicho ni kinga ya magonjwa endapo mtu atazingatia ulaji wa vyakula mchanganyiko.

Alisema elimu hiyo wameanza kutoa zaidi ya miaka 10 Katika shule mbalimbali za Tanzania bara na visiwani na zaidi ya wanafunzi 5000 amenufaika ,ambalo akiongea kuwa mbali na kutoa elimu pia wametoa Miche ya matunda kwenye shule mbalimbali za maeneo wanaofanya nayo kazi Ili kila shule ihakikishe inawapatia watoto wapi matunda wakati wa chakula .

Kwa upande wake mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Respicius George waliishukiru TAHA kwa kuwapa elimu hiyo ya uhamasishaji wa kilimo Cha matunda na mboga pamoja na ulimaji wa mazao hayo Kama chanzo cha kuinua uchumi na ajira.

Mratibu wa jinsia na lishe kutoka (TAHA) Salome Stephen akiwapa  wanafunzi wa shule ya sekondari Nkwanikole iliopo Katika kata ya Nkwanikole wilayani Arumeru mkoani Arusha elimu ya lishe na kilimo Cha mboga na matunda  (Picha na Woinde Shizza, ARUSHA)