ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 4, 2023

Benki ya CRDB yakabidhi kituo cha mawasiliano Ocean Road

 

  
Benki ya CRDB imekabidhi kituo cha mawasiliano katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ikiwa ni matokeo ya fedha zilizokusanywa katika mbio za CRDB Bank Marathon 2021. Kituo hicho cha kisasa na cha kwanza kwa hospitali hapa nchini kimekabidhiwa kwa uongozi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla aliekua Mgeni Rasmi katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela amesema Benki ya CRDB ni mdau mkubwa wa maendeleo ya sekta ya afya nchini kupitia Sera ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI Policy) ambayo inaelekeza Benki kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka kwa ajili ya kutatua changamoto katika sekta ya afya, elimu, mazingira, na uwezeshaji kwa wanawake na vijana.
Katika sekta ya afya Benki ya CRDB imejikita zaidi katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto na pia huduma za kibobezi (specialist services), ikiwa ni pamoja na ufadhili wa ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya, wodi za wagonjwa pamoja na utoaji wa vifaa tiba katika vituo vya afaua , zahanati na hospitali mbalimbali nchini.

“Mwaka 2020 Benki ya CRDB ilianzisha mbio za hisani zilizopewa jina la CRDB Bank Marathon kwa lengo la kusaidia jamii kwa kushirikisha wadau mbalimbali. Kupitia mbio hizi mnamo mwaka 2021, tukishirikiana na washirika wetu ambao baadhi tupo nao hapa tulifanikiwa kukusanya takribani Shilingi Milioni 500 ambapo kati ya hizo tulitenga kiasi cha Shilingi Milioni 102 kufadhili ujenzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja chini ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kurahisisha ufikishwaji wa huduma, elimu na ushauri juu ya Saratani kwa watanzania wengi” aliongeza Nsekela.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage ameishukuru Benki ya CRDB kwa kusaidia ujenzi wa kituo hiko cha mawasiliano ambacho kinakwenda kuisaidia katika kutekekeleza malengo ya kuanzishwa kwake hususan upande wa kuongeza uelewa wa ugonjwa wa Saratani jambo ambalo ni muhimu katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

“Tunaishukuru Benki ya CRDB sambamba na washirika wake Sanlam, Strategis na Alliance Insurance pamoja na wakimbiaji zaidi ya elfu 5 ambao kwa kushiriki kwao katika marathon ile ya mwaka 2021 leo tumeweza kuwa na kituo hiki cha kisasa ambacho kinakwenda kuokoa maisha ya Watanzania” alsema Dkt. Mwaiselage.
Makabidhiano hayo yalitanguliwa na matembezi ya hisani yalioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe, Amos Makalla yamefanyika katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam yakilenga kuongeza ufahamu wa ugonjwa wa saratani. 
 
Sehemu ya washiriki wa matembezi hayo walikua ni mashujaa waliopona ugonjwa wa Saratani ambapo walisisitiza umuhimu wa kupima saratani mara kwa mara kwani kugundulika kwa mapema kwa saratani kuna mchango mkubwa katika matibabu yake.
Akizungumza katika halfa hiyo Mhe. Makalla amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetenga fedha za kutosha kwenye sekta ya afya na kuhakikisha kunakua na mgawanyo mzuri wa vituo vya afya katika ngazi zote ili kuhakikisha wananchi kutoka maeneo yote ya nchi wanapata huduma bora za afya.

Kwa upande mwingine Mhe. Makalla aimeipongeza Benki ya CRDB na washirika wake kwa kufanikisha ujenzi wa kituo hiko kama walivyoahidi wakati wakihamaisha ushiriki wa mbio za CRDB Bank Marathon na kuahidi kuwa ataendelea kuwa mshiriki wa mbio hizo kama ambavyo amefanya katika miaka miwili iliyopita.
“Mimi ni shahidi mzuri wa mbio hizi na naamini CRDB Bank Marathon ya mwaka huu itakua bora zaidi ya zilizopita na natoa wito kwa wadau kushiriki kwa wingi katika mbio hizi kwani fedha zinazopatikana katika mbio hizo zinarejeshwa kwenye jamii hususan kwenye sekta ya afya” aliongeza Mhe. Makalla.

Pamoja na ujenzi wa kituo hiko, mbio za CRDB Bank Marathon kwa mwaka 2021 ziliweza kusaidia matibabu ya watoto zaidi ya 100 wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo pia kwa mwaka jana kupitia mbio hizo jumla ya Shilingi Milioni zilipelekwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Shilingi zilipelekwa katika Hospitali ya CCBRT kusaidia wanawake ambao wana ujauzito hatarishi.


















CCM IRINGA KUWACHUKULIA HATUA KALI WATENDAJI WAZEMBE KAZINI.

 

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin akiongea wakati wa uapisho wa mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa

Na Fredy Mgunda, Iringa.

CHAMA cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kimesema hakitamfumbia macho mtendaji yoyote wa serikali atakayetekeleza miradi chini ya kiwango.

Akizungumza wakati wa uapisho wa mkuu wa wilaya ya Mufindi, mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin alisema kuwa chama kitaendelea kuisimamia serikali kila Kona ili kuhakikisha wanatekeleza miradi inavyotakiwa.

Yassin alisema kuwa watakuwa wakali kwenye miradi ambayo itakuwa imetekelezwa chini ya kiwango au hailingani na thamani ya fedha ambazo serikali imetoa kwenye mradi husika.

Alisema kuwa wataendelea kusimamia serikali ili kuhakikisha wanatekeleza vilivyo Ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2020/2025 kama ambavyo inasema.

Yassin alisema kuwa watahakikisha wanaisimamia serikali kutatua changamoto za wananchi kama ambavyo inatakiwa ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kimaendeleo bila kuwa na changamoto zozote zile.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kimejipanga kuhakikisha wanashinda uchaguzi wa serikali za mitaa,udiwani,ubunge na urais kwa asilimia 100 hivyo wapinzani hawawezi kupata hata kiti kimoja mkoani Iringa.

Yassin alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kinampongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego kwa utekelezaji wa Ilani mzuri hivyo jukumu la chama hicho kuhakikisha wanafikisha elimu kila kona ya mkoa wa Iringa.


Aliwataka viongozi wa wilaya kutoa ushirikiano mkubwa kwa viongozi wa chama cha CCM wilaya kama ambayo mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego anafanya.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin alimazia kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga nchi kiuchumi na kutekeleza vizuri Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.

Friday, February 3, 2023

"WANASIASA SOMENI KWANZA MIKATABA YA MIRADI KABLA YA KUFANYA MAAMUZI ILI KUIEPUSHA HASARA SERIKALI"

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Mafunzo kwa Wakandarasi na wadau wa Sheria kwa taasisi za Serikali juu ya usimamizi wa mikataba ya ujenzi ili kuboresha utendaji na kusimamia miradi imalizike kwa wakati pamoja na kuiepusha Serikali na hasara kwa kesi zinazozuilika yaliyofanyika kwa muda wa siku 5 yamemalizika leo jijini Mwanza. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambalo tangu kuanzishwa kwake moja ya majukumu yake katika sheria yake ni kusimamia ukuaji wa sekta ya ujenzi nchini ili kwenda sambamba na maendeleo na ushindani wa kimataifa. Majukumu mengine ni pamoja na Kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayohusu sekta ya ujenzi na kutayarisha mapendekezo, maelekezo na utekelezaji wake; Kutoa ushauri wa kiufundi kwa wadau wa sekta ya ujenzi, Kukuza na kuratibu mafunzo bora kwa watu wanaojihusisha au watakaojihusishana sekta ya ujenzi na Kukuza, kuendesha na kuratibu utafiti katika masuala yanayohusiana na sekta ya ujenzi. Jeh yapi yamejiri ndani ya mafunzo hayo........

Wednesday, February 1, 2023

JE ULIWAHI KUJIULIZA KWA NINI MATAIRI YA GARI YANA RANGI NYEUSI NA SI RANGI YOYOTE?

Kwa Sababu rangi nyeusi ni nyepesi kushika joto alafu inauwezo wa kuhimiri joto kwa muda mrefu tofauti na RANGI nyingine.

Kuna sababu kwanini matairi ya magari duniani huwa na rangi nyeusi na si rangi nyingini. Sababu kubwa ni kuweza kuwa na ubora zaidi wa kutumika.

Kwa makusudi kabisa matairi ya magari ni ya rangi nyeusi ili yaweze kufanyakazi vizuri na kuyafanya yaweze kutumika kwa muda mrefu zaidi kwa kuongeza kemikali kwenye mpira inayojulikana kitaalamu kwama ‘Carbon Black’ ambayo ndiyo hubadilisha rangi ya matairi.
Kwanini Carbon Black? Kemikali ya Carbon Black hufanya kazi kubwa ya kuongeza uwezo wa mpira wa tairi kufanya kazi kwa ubora wa hali ya ju kiasi kwamba duniani kote wakawa wanaitumia kemikali hiyo.

Asilimia 70 ya kemikali hiyo inayozalishwa dunia, hutumika kutengenezea matairi mbalimbali.

Carbon black huongeza uwezo wa raba kuweza kutumika muda mrefu zaidi pamoja na kuipa uimara ili kuzuia kutoisha kirahisi ikiwa juu la lami.

Aidha Carbon black husaidia kuipa tairi muda mrefu wa matumizi kwa kuondoa joto na hivyo tairi haiwezi kuathiriwa na joto kirahisi. Kabla ya vita ya kwanza ya dunia, Zinc Oxide (iliyofanya matairi kuwa meupe) ilitumika kwenye matairi badala ya carbon black ili kuzuia tairi kupata joto na kuwa ngumu.

Lakini baada ya matumizi ya carbon black kushika kasi, ilianza kutumika sehemu ya juu ya tairi (tire tread) na zinc oxide kutumika kwenye kuta za tairi (tire sidewalls)


Carbon black pia huisaidia tairi kujikinga dhidi ya madhara ya gesi ya ozone (corrosive effects of ozone). Gesi ya ozone ni moja ya vitu ambavyo huchangia kuharibika sana kwa tairi, hivyo kemikali hiyo ni ya muhimu sana kwa watengenezaji na watumiaji, bila hiyo tairi zingekuwa zinaharibika haraka sana. Madhara ya gesi ya ozone ndiyo sababu haushauriwi kuhifadhi tairi zako karibu na mota za kielektroni ambazo huto gesi hiyo.

Kwa kuhitimisha unaweza kusema kuwa, sababu kubwa ya tairi za magari na vifaa vingine kuwa nyeusi ni kwa sababu ya matumizi ya kemikali ya carbon black ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uimara wa mpira unaotumika kutengenezea tairi.

♡♡♡ USISAHAU KUSHARE NA KULIKE PAGE ILI UZIDI KUPATA MAUJANJA ZAIDI

MANISPAA YA IRINGA WATOA MKOPO WA MILIONI 328,680,000 KWA VIKUNDI 44

 

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiwakabidhi pikipiki zaidi 20 kwa moja ya kikundi ambacho kimepata mkopo wa asilimia 10 unaotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akimkabidhi bajaji moja ya kikundi cha mtu  kimepatmlemavu ambacho mkopo wa asilimia 10 unaotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo

Na Fredy Mgunda, Iringa.


HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imetoa mkopo wenye thamani ya kiasi cha shilingi millioni 328,680,000 kwa vikundi 44 kutokana na mapato ya ndani ya asilimia 10 ya madirio ya makusanyo.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa mikopo hiyo Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda alisema kuwa wametoa mikopo kwa vikundi 18 vya wanawake, vikundi 15 vya vijana na vikundi 11 ya watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa 4:4:2.

Ngwanda alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imepanga kuanza kutoa mikopo kuanzia Milioni 20 na kwenda juu lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi wenye vikundi hivyo kuwa na tija kwenye mitaji yao.

Alisema kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wametoa zaidi ya bodaboda 20, Bajaji mbili na mikopo mingine mikubwa kwa ajili ya kilimo.

Ngwanda alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inatarajia kuanza kutoka mikopo kwa ajili ya vikundi ambavyo vinataka kuanzisha viwanda mbalimbali kwa lengo la kuifanya Manispaa hiyo kuwa ya viwanda kwa kuwa malighafi za viwanda mbalimbali zinapatika kirahisi.

Alisema kuwa vikundi hivyo hupatikana kuanzia ngazi ya mtaa,kata hadi ngazi ya Manispaa ya Iringa hivyo uhakiki wa vikundi hivyo umekuwa unafuata taratibu zote kama ambavyo serikali imeagiza.

Aidha Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda alisema kuwa bado kunachangamoto ya urejeshaji wa mikopo sio nzuri hivyo wanatafuta njia mbadala ya kuhakikisha vikundi vyote vinarejesha kwa wakati mikopo hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya wanaufaika wa mikopo hiyo walisema kuwa wanaushukuru uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa unaongozwa na Meya Ibrahim Ngwanda kwa kuwakopesha wananchi mikopo ambayo haina riba kama taasisi nyingine za kifedha.

Walisema kwa kuwa wamepata mikopo mikubwa hivyo wapo tayari kurejesha mikopo kwa wakati ili kusaidia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwakopesha wananchi wengine kwa kukuza uchumi na maendeleo ya Manispaa hiyo.

MNEC ASAS KUJENGA BWENI SHULE YA SEKONDARI KIYOWELA

 

Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas akiongea na wananchi wa Mkoa wa Iringa wakati wa uzinduzi wa miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi na kutoa ahadi ya ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Kiyowela.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas.



Na Fredy Mgunda, Iringa.


CHAMA cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kimepanga kutatua changamoto uhaba wa bweni katika shule ya sekondari ya kiyowela ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa kwa Watoto wa kike.


Akizungumza wakati uzinduzi wa maazimisho ya miaka 46 ya chama hicho,Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas alisema kuwa amesikia kero iliyosemwa na Diwani wa kata ya kiyowela ya uhaba wa bweni la shule ya sekondari Kiyowela.

Asas alisema kuwa yupo tayari kuchangia ujenzi wa bweni hilo hata kwa asilimia 90 ilimradi kuwawezesha wanafunzi hasa wa kike kusoma wakiwa bwenini.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa kimepanga kuboresha sekta ya elimu hivyo uongozi wa kata na shule hiyo wanatakuwa kutuma haraka michoro ya ujenzi wa bweni hilo ili waanze ujenzi mara moja.

Asas alimpongeza MNEC Qwihaya kwa kujitolea Tripu 20 za tofari kwa ajili ya ujenzi wa bweli la shule ya sekondari Kiyowela jambo ambalo linatakiwa kuigwa na wanaccm na wananchi wote.

Alisema kuwa anachangia ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Kiyowela ili kuwanusuru wanafunzi wa kike wanaotembea zaidi ya kilometa saba kwenda shuleni.

Awali Diwani wa Kata ya Kiyowela, Steven Muhumba alisema katika mkutano huo kwamba ukosefu wa bweni katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 400 unawaweka wanafunzi hasa wasichana katika mazingira hatarishi na akaomba msaada wa ujenzi wa bweni litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 200.

Kwa upande wake Qwihaya aliahidi kuchangia tripu 20 za tofari kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo huku Mkuu wa Mkoa akisema serikali itaweka pia mkono wake katika shughuli hiyo.

“Qwihaya ameahidi tripu 20 na serikali ya mkoa imesema itaweka mkono wake; mimi naahidi sehemu yote itakayobaki katika ujenzi wa bweni hilo, nitaikamilisha,” Asas alisema na kuamsha vigelegele kutoka kwa wananchi.


Tuesday, January 31, 2023

WATOTO WENGI WANAZALIWA NA BABA WALIOJIFICHA.

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Historia yako na mumeo au mkeo jeh unaweza kumwadithia mwanao, kumkumbushia au unaifisha kwasababu inaukakasi ndani yake? Kila kinachofanyika ndani ya familia yako kina chukuliwa na watoto wako kama ndiyo maisha ambayo kwayo wao wanapaswa kuishi pindi wanapotengeneza familia zao. Japo kwa ufupi kile kilichofanyika ndani ya kipindi cha Sega La Leo ukiwa na mtangazaji wako Florencia Peter.