ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 5, 2012

"ILIKUWA KATIKA NINI NA NIKWANINI.......!!!!......?"

Mbunge Mteule wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji na ze-keki.

Mbunge Mteule wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji akipomkelekea keki Mbunge wa Kawe Halima Mdee..Ahaa mheshimiwa Shy-Rose unataka nitengwe nini??? mimi simooooo hata waandishi wakipiga picha sijaigusa maana hata rangi zake sizielewi elewi hazifanani naza kwetu...
Asante sana labda mpeleee mwenzangu yeye akiigusa sawa tu wala sina matatizo nae ila mimi nitaenda kumsemelea...

.Ehe alipofika kwa mwenzake ikabidi yeye asiiangalie kabisa maana alisema rangi zake zinamuumiza macho... hahahahaha
KUONDOA 'UTATA' BOFYA ANUANI IFUATAYO:-

HAPA NA PALE WILAYANI MULEBA MKOANI KAGERA

Mkoa wa Kagera ni moja kati ya mikoa hapa nchini inayoongoza kwa kutokuwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa malaria pamoja na hilo serikali haijabweteka kuhakikisha kuwa inaangamiza kabisa mazalia ya mbu.. pichani bwana Jovita N.Ngambeki akitoa elimu kwa moja ya kaya (haionekani pichani) ili aanze zoezi la kupulizia dawa maarufu kwa jina 'Dawa ya ukoko'

Shughuli hizo za unyunyiziaji hufanywa kwa umakini mkubwa huku 'timulida' (team leader)  wakikagua mara baada ya unyunyiziaji kufanyika.

Jovita N.Ngambeki tayari kwa kuanza zoezi katika kijiji cha Ilogelo tarafa ya Kamachumu wilayani Muleba.

Serikali yetu iling'aka sana mara baada ya mchizani Sauper kutengeneza filamu ya DARWIN’S NIGHTMARE ambayo ndani yake ilionyesha watanzania wakitumia mabaki ya samaki maarufu kama mapanki kama mboga tegemeo huku minofu ya samaki iklisafirishwa tani kwa tani kuelekea nchi za wenyenazo kwaajili ya biashara. Pichani ni mokono ya mteja ikichambua mabaki ya samaki toka viwandani mara baada ya minofu kutolewa (mapanki)  yakiwa sokoni kwaajili ya mboga, katika Gulio la Kilamba linalofanyika kila jumapili kijijini Rwigembe.

Panki
Mimi msimamo wangu ninasisitiza kuwa mapanki ni kitoweo kinachoonekana kawaida familia kadhaa cha kila siku katika familia hizo kanda ya ziwa sio Mwanza tu hata Kagera wanakula 'Mapanki' bwana.

Mapanki yakiwa kwenye meza ya mchuuzi.
"Mimi mwenyewe nimeanza kula mapanki kuanzia mwisho mwa miaka ya tisi, Leo hii watu wanashangaa kitoweo cha Mapanki ila nimejikuta nakula mapanki kutokana na uhaba wa sangara" alisema mmoja kati ya wadau wa kijiji cha Rwigembe kilichopo kata ya Ngenge wilayani Muleba.

Ingawa hukaushwa mabaki mengine hutoa harufu ya kuharibika
Wadau nawasihi tuitizame upya filamu ile na ifanyiwe utafiti ili ukweli ujulikane kama mtunzi ana makosa au la. Nakumbuka juu ya sakata lile la filamu kuna udanganyifu ulifanywa toka kwa viongozi kwenda kwa prezidaa' kama walivyozoea kuwapotosha viongozi wengine wa kitaifa, kwamba mapanki yanaliwa na watu maskini tu...

Wananchi katika pilikapilika gulioni Kilamba linalofanyika kila jumapili.
Picha na mdau wa G. Sengo Blog bwana Samadu Abdul 

VIBAO ELEKEZI...

Jeh! mwenzangu waelekea wapi?

Kutokana na wizi uliofumuka wa vyuma chakavu hata wezi hao kuiba hadi mabango wadau wa huduma mbalimbali imewabidi kuumiza vichwa kubuni mbinu nyingine za kuweka mabango.

Bango la ofisi za TBC maeneo ya Isamilo jijini Mwanza.
Victoria Palace...

Friday, May 4, 2012

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI MEI 2012 HILI HAPA

Rais Jakaya Kikwete hivi punde ametangaza Baraza jipya la Mawaziri likiwa na sura mpya wakati baadhi ya Mawaziri wakibaki katika nafasi zao. Ifuatayo ni orodha ya Mawaziri na Manaibu  walioteuliwa.
HII NDO ORODHA NZIMA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI) Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO) Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Ndugu Mary M. Nagu, Mb., Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4. WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi Dr. John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5. NAIBU MAWAZIRI OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI

6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

7. OFISI YA WAZIRI
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb., Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8. WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb., Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb., Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Ummy A. Mwalimu, b.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Saada Mkuya Salum,

PONGEZI KWA WANATAALUMA WALIOTEULIWA KUWA WABUNGE

Wazalendo wanzangu, 

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya M. Kikwete kwa kuwateua wanataaluma Mhe. Janet Mbene (M.Sc - Economics) na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (PhD - Geology), wazalendo hao ni wadau wetu muhimu katika Mtandao wa Wanaataluma Tanzania. 

Pia na tunamshukuru na Mhe. Rais kwa kumteua Mhe. James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi kuwa Mbunge, Mhe. Mbatia ni msomi mzuri sana, mwanaharakati na Mzalendo wa kweli kwa Taifa letu .

 Uteuzi wa wanataaluma hawa unadhihirisha ukweli kuwa Mhe. Rais ana nia njema ya kujenga umoja wa kitaifa na kutumia baadhi ya vipaji tulivyonavyo katika kuleta suluhisho za baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo kwa sasa. 

Pia inatukumbusha kuwa unapokuwa na taaluma fulani basi ni vizuri ukaitumia kwa faida ya jamii inayokuzunguka kwa ujumla na sio kwa faida yako binafsi. Janet, James na Sospeter wote wamekuwa wakishirikiana vizuri sana na jamii na kila wanachofanya wanaweka Uzalendo na Utaifa kwanza. 

Nawapongeza wote walioteuliwa na ni matumaini yangu kuwa watatumia vizuri nafasi hizo kwa kutumia taaluma zao na uzoefu wao katika njanja mbali mbali na kutoa mchango wa katika kuleta maendeleo ya kweli na ya haraka kwa watanzania. 

Kama Miaka 50 iliyopita nchi kama Singapore, Korea ya Kusini , Malaysia n.k zilikuwa na uchumi unaolingana na wetu au chini yetu , Je ni kwa nini leo hii wao wameendelea kwa kasi kubwa na sisi bado tunajikongaja ? Swali hili kila mtu anahitaji kujiuliza na kuona jinsi gani asasa tutabaidilika kifikra, mawazo na kimatendo ili kila mmoja wetu katika eneo lake achukue hatua zitakazochangia kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii yetu.

 Baadhi ya mambo ambayo kwa mtizamo wangu mimi yanahitaji kupewa kipaumbele ili yasaidie kutufikisha kwenye Tanzania tunayoitaka ni: 
1. Kuwa wazalendo wa kweli 
2. Kuwa na Maadili na kuzingatia miiko ya taaluma husika
 3. Kuzingatia misingi ya Uongozi/utawala bora 
4. Uwekezaji sahihi katika Elimu 
5. Matumizi sahihi ya rasilimali zetu 

Mungu awabariki wote, Mungu ibariki Tanzania. 
Nawatakia kila la heri, 

Phares Magesa, 
Rais- Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN),

MEDIA NIGHT GALA AT MWANZA HOTEL

Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya baraza la habari Tanzania (MCT)Jaji Robert Mihayo akionyesha kitabu kilichozinduliwa usiku wa jana, kiitwacho State of the media report 2011, mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani huku akishuhudiwa na mgeni rasmi mh.mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (L) na Rais wa UTPC Abubakar Karsan (R) katika hafla hiyo iliyofanyika Mwanza hotel ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya baraza la habari Tanzania (MCT)Jaji Robert Mihayo akimkabidhi nakala ya kwanza mgeni rasmi mh.mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo. 

Kisha neno la shukurani.. 

Ndipo Burudani ikafuata... 
Wanahabari wakipata flash kwenye mtoko huo.. 

Hapa ilikuwa mwanzo kabisa kabla hazija kolea mkichwa ili watu washushe matirio.. 

Blogger maarufu wa HOSANNAINC akigonga chiaz na mgeni rasmi. 

Yakafuata mambo yetu ya mboga saba kujisevia.. 

Drafti likiendelea kuchezeka kimya kimya...

Meza yetu na mapilipili mwaaaa... 

Meza zilichafuka balaaaaa... 

Meza iliyotishaaa "Muraaa...! Reta hapa.. bhana" 

Misosiso.. 

Wadau wakiendelea kujinafasi kwa nafasi bila tafash... 

Huyu hapa mshereheshaji wa sherehe hiyo iliyofana Mc Chonya. 

Ikafika zamu ya kuonyesha vipaji on the stage akapanda braza Alan Mlawa hakika aliutendea vyema wimbo wa Rangi ya chungwa akisaidiana na wanamuziki wa Jambo Stars band. 

Mpiga gitaa la bass akifanya mikuno. 

Dance lililofana usiku huo.. 

Ni maraha mwanzo mwisho.. 

Aaaah nami si nikageuka Samba Mapangala wafanya mchezo.. 'Dunia tunapita..eEEEee'

Wadau wa ukweli wakiongozwa na Alan Kisoi pale kati wakisutumukazzZZ.. 

Aaaaah Victaaaaaaa... 

Chungulia imo-MO. 

Kutoka kushoto ni Henry Mabumo, Albert G. Sengo na Jerome 'Kamanda' 

KonazzzZZZ.. 

Mwisho wa siku bendi nzima ikashikwa na waandishi wa habari... watu wewe.

Thursday, May 3, 2012

SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI MEI 3, 2012 MWANZA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo akihutubia waandishi wa habari waliohudhuria kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kitaifa ilikuwa jijini Mwanza. 

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Victoria Palace jijini Mwanza.

Wadau wa habari na maadhimisho ya siku yao. 

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Ernest Ndikilo amewaasa waandishi wa habari nchini kuzama vijijini na kuandika habari za maeneo hayo ili kuwakwamua wananchi wenye uhitaji kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameitendea haki tasnia yao. 

Mwanahabari mahiri Victor Maleko (mwenye kamera) naye hakukosa kusanyikoni. 

Mwenyekiti wa Mwanza Press Club (MPC) na mjumbe wa bodi ya UTPC Jimmy Luhende akitoa shukurani na yake machache ndani ya kusanyiko hilo la wandishi wa habari. 

Masuala mbalimbali yaliibuka na kujadiliwa ikiwa ni pamoja na suala la Muungano, Sheria kandamizi, Mchakato wa kuelekea kuundwa katiba mpya, Zoezi la Sensa linalokuja, Vyama vya siasa na Serikali pamoja na Kaziya uhuru wa vyombo vya habari kuhakikisha uwazi na utawala bora. 

MTC Executive Secretary Mr. Kajubi Mukajanga akitoa somo. 

Wito umetolewa kwa waandishi kutotumika kwa maslahi ya wachache wenye uroho, hali iliyoipeleka nchi kuwa na hali mbaya kama ilivyo sasa.

Je hadi leo, uhuru wa habari umewatendea haki kwa kiasi gani waandishi hawa? 

Mazungumzo kwa chati.... 

In deep... 

Mwanza imepokea wageni kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya Siku hii muhimu ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.