ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 26, 2013

WANAOIPENDEZESHA MWANZA.!!

Moja kati ya mzigo dukani kwa Bob White 'Mzee wa Pamba za Mabinti'
Mzigo mwingine kwa 'Bob White'
Mwingine tena....
Hapo vijjjeh!..?
Kwa - kwa.
Ni ndani ya Whitney Fashion kwa Fred.
Mapigo ya akina dada.
Nyingine.
Trouser.
Shoes.
T. shirts.
Tuhamie kwa Hamisi Fashion.
Hamisi Fashion (kulia) akimpa ushauri mteja wake.
Sendoz kali.
Koti swadaktar...

BAADA YA MASHABIKI WAKE WATANO KUFA KWENYE AJALI: RUSUMO FC YAFANYA TAMASHA LA KUMBUKUMBU

 Bango la Kumbukumbu
Makamu M-Kiti NDFA akikabidhi Rambirambi 200,000 kwa Mwenyekiti wa Klabu
Wanafunzi wakiimba wimbo maalum Kuwakumbuka marehemu hao.
Utulivu kwa Dua ya Kuwakumbuka
Kulia ni Shabiki wa Rusumo Fc (Emma), Suley Mohamed Mfadhili wa Rusumo Fc, Upupu na Brayan.
Kushoto Makam M-Kiti Chama cha soka wilaya Ngara (NDFA) Seif Upupu, Brayan na OCD
RUSUMO FC
RUSUMO VETERAN
OCD Abel Mtagwa (Kulia) Godfrey Byaran na Mwisho Kabisa Makam M-Kiti chama cha soka wilaya Seif UpupuMTAGWA NA BRAYAN
Wa pili kulia ni OCD Ngara na Viongozi wengine.
Tamasha limefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyakahanga, kijiji cha Rusumo Mpakani mwa Tanzania na Rwanda upande wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera

Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya(OCD) Abel Mtagwa, Mgeni wa Heshima Makamu mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya Ngara (NDFA) Seif Omary Upupu aliyeambatana na Mwakilishi wa Vilabu Godfrey Brayan

NDFA kilitoa rambirambi ya Sh Laki mbili (200,000) kwa klabu kisha kufanyika harambee ndogo kwa ajili ya kuwapa wafiwa na ilipatikana Sh laki mbili na Thelathini (230,000)

Tamasha hilo lilianza kwa maandamano kutoka kituo cha Forodha Rusumo hadi Uwanjani na kisha kumalizika kwa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Rusumo Fc na Rusumo Veterans ambapo Maveterani walifungwa magoli 4-1

Klabu ya Rusumo Fc ilipata mkasa wa kuondokewa na mashabiki wake watano Tar 14.10.2012 baada ya kupata ajali majira ya saa mbili usiku katika eneo maarufu kwa jina la Zerozero nje kidogo ya mji wa Ngara wakati wakitokea Kabanga kucheza mechi ya Nusu Fainali ya michuano ya kombe la Polisi jamii wakiwa na gari la jeshi la polisi ambalo liligonga jiwe na kupinduka katika eneo hilo ilipo njiapanda ya barabara ya kwenda Rwanda kupitia Rusumo na ile ya Burundi kupitia Kabanga ambapo watu watano walifariki dunia.

"TWENZETU LIDAZ" leo

"tukacheze Skelewu"

"na Kukere" 

KONYAGI YASHINDA UBORA WA BIDHAA, YAPAA KWENDA HISPANIA KUCHEKI KABUMBU

Mkurugenzi Mkuu wa TDL akiwa na Mabosi wa SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13)
PICHA NDOGO CHINI NI BAADHI YA WAFANYAKAZI TDL WALIO TEULIWA KWENDA KUTIZAMA KABUMBU UGHAIBUNI
Mweisiga 'Mzee wa jiji'
Chibehe 'Mzee wa Tanzania'
Bi Khadija 'Mkuu wa msafara'
Huyu ndiye Mrema 'Mzee wa Mwanza'

 
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd (KONYAGI) imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13), ni miongoni mwa Kampuni tanzu za Sabmiller ya Afrika Kusini.

Akiongea na waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, aliyepambana mpaka kupatikana kwa ushindi huo. amesema kuwa wanajivunia kuwa washindi miongoni mwa makampuni mengi yaliyo chini ya Sabmiller.

“Ushindi huu ni ishara kubwa ya mafanikio KONYAGI na sisi hatutarudi nyuma hii ni chachu katika kutufanya tuendelee kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa bei nafuu na kuzishinda kampuni zingine” alisema Mgwassa.

Amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa sana mana kila Kampuni miongoni mwetu inajitahidi kuzalisha bidhaa kwa kiwango cha hali ya juu na sisi kushinda ni ishara kuwa bidhaa zetu zinakubalika kila mahali hapa Africa hata nje ya Africa.

                                                            ZAWADI YA KWENDA

Licha ya kupewa tuzo ya ubora, pia TDL imepewa nafasi kwa Wafanyakazi wake watano kwenda kuangalia mpambano mkubwa la ligi kuu  ya Hispania (LA LIGA) kati ya Barcelona na Real Madrid.
Mgwassa aliwataja wafanyakazi wanaokwenda Hispania kuangalia mechi hiyo kuwa ni Joseph Chibehe, Khadja Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesige Mchuruza.

Thursday, October 24, 2013

SIKILIZA ALICHOSEMA ZITTO KABWE KUHUSU HATUA ZA KUNG'AMUA WATOROSHAJI FEDHA TZ

Haya ni mazungumzo aliyofanya leo asubuhi kupitia Clouds Fm ndani ya Kipindi cha Power Breakfast alipohojiwa naye Gelard Hando (Bofya Play kusikiliza)




Serikali Kikwazo

Wakati shinikizo la Dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na Utoroshaji wa fedha kutoka nchi za Kiafrika, serikali ya Tanzania inavuta miguu.


Moja ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata taarifa za makampuni makubwa ya kimataifa(MNCs) yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana taarifa (automatic exchange of tax information) .


Kufutia shinikizo la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa "secrecy jurisdictions" (tax havens) Zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa taarifa. Tanzania mpaka sasa haijaweka sahihi na serikali haijatoa taarifa yeyote kwa Umma.


Ghana, Afrika Kusini na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama Tanzania zimeweka saini mkataba huu tayari. Asilimia 44 ya fedha za kigeni nchini zinatokana na mauzo ya madini nje. Makampuni ya madini ndio yanaongoza kukwepa kodi. 

Tanzania inapoteza jumla ya dola za kimarekani kati ya milioni 500 na bilioni 1.25 kwa mwaka kutokana na Makampuni makubwa ya kimataifa kukwepa kodi. Hii ni sawa na kusema Tanzania inapoteza dola takribani milioni mbili kila siku kwa uporaji huu.


Naitaka serikali kutoa taarifa kwa nini haichuki hatua kuzuia mwanya huu wa mapato ya Umma. Serikali ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi. Huu sio wakati wa kuvuta miguu katika suala nyeti la umma. Badala ya kukimbilia kutoza kodi wanyonge, tuhakikishe makampuni makubwa yanayonyonya rasilimali zetu yanalipa kodi inayotakiwa. 


Zitto Kabwe, MB

Waziri Kivuli wa Fedha

24 Oktoba, 2013 

Geneva, Switzerland

HARUSI ZA NIGERIA ZAGEUKA KUWA SEHEMU YA UTALII WENGI WAMEKUWA WAKITINGA NCHINI HUMO KUSHUHUDIA

Harusi za Nigeria ni moja kati ya sherehe zinazofana sana barani Afrika kutokana na mpangilio wa muonekano sambamba na ubunifu katika mavazi.
Kila mmoja hujituma katika kufanikisha sherehe ya harusi ndiyo sababu huwa bombaa..
Kila kukicha vihusishi kama keki huwa ni vya style ya aina kwa aina.
Sare ni moja kati ya misingi inayozingatiwa.

Ni taswira ambazo huto choka kuziangalia.
Heshima katika sare na wenye sare.
Rangi hupendezesha mazingira kuwa na mwonekano wa mvuto zaidi.
Chekshia kuanzia style ya nguo ushonaji, maua walobeba hadi style za nywele.

Hapa je..
Safi.

Utaipenda.
Hizi ndizo sababu zinazofanya taifa la Nigeria kuwa na nyongeza nyingine katika utalii na sasa wageni wana miminika nchini humo kushuhudia yanayojiri zikiwemo tamaduni ambazo zimeenziwa kwa miaka dahari sasa.

Wednesday, October 23, 2013

SHULE ZENYE MAJINA YA WATU MASHUHURI NCHINI NYINGI ZIKO KATIKA HALI TETE

Ndugu Juma Makongoro akikabidhi Madawati 30 kwa Bw. Madaraka Nyerere ambaye ni moja kati ya wajumbe wa shule ya msingi Ikizu A. Picha na Maktaba ya G. Sengo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya msingi Ikizu A wakiimba katika mahafali ya shule hiyo kwa mwaka huu 2013.
Imekuwa suala la kawaida kwa shule nyingi nchini ambazo zina majina ya watu mbalimbali mashuhuri au zile ambazo walizosoma watu mashuhuri wa taifa hili kuwa katika hali mbaya kimazingira na kukumbwa na uhaba mkubwa wa vitendea  kazi.

Suala hili limeota mizizi na kila kukicha shule nyingi zimekuwa zikiibuliwa suala ambalo limezua maswali mengi moja ni kuu ni Either Mamlaka zinazohusika (Kamati za shule) zinajisahau kuwa viongozi wao wakubwa wametoka shule hizo na kuacha kuzikarabati au viongozi wenyewe kutokujenga mazoea ya kuzitembelea shule zao walizosoma kuona matatizo na changamoto wanazokabiliana nazo.

Katika hilo wadau mbalimbali nchini wakiwemo wafanyabiashara, wanasiasa na watumishi wa sekta mbalimbali hapa nchini wameombwa kuchangia fedha ili kufanikisha ukarabati wa majengo ya darasa yaliyoanguka,kuboresha nyumba za waalimu pamoja na changamoto ya kuweka umeme katika shule ya msingi Ikizu mkoani Mara.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Afisa wa Uvuvi Kanda ya Ziwa Juma Makongoro ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maafali ya darasa la saba kwa Shule ya Msingi Ikizu A iliyopo wilayani Bunda, kijiji cha Nyamswa mkoani Mara. (MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)

Moja kati ya watu mashuhuri waliosoma katika Shule hiyo ni pamoja na  Mwenyekiti wa Tume ya Katiba nchini  Jaji Joseph Sinde Warioba, Brigedia Lyakitimbu, Kanali Wema Chakoma, Watoto wote wa Chief Makongoro. 

HISTORIA Shule ya Ikizu A enzi za ukoloni na kipindi cha miaka ya 80 hadi mwishoni mwa miaka ya 90 inatajwa kuwa ni moja kati ya shule zilizokuwa zikiongoza katika utoaji elimu bora, hali ya mazingira safi kwa kuwa na bustani nzuri zenye maua na miti, maji ya bomba, vyumba vya madarasa vilivyopakwa rangi na vyenye sakafu ya saruji pamoja na mazingira bora yaliyokuwa yakivutia kila mwalimu kutaka kuhamia ili kufundisha shule hiyo lakini leo hali ni tete.

AIRTEL MONEY NA BENKI YA POSTA WAUNGANA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WATEJA WAO

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Betrice Singano Mallya akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja baina ya Airtel  na Benki ya Posta Tanzania kwa kutoa huduma za kifedha pamoja. Pembeni ni Kaimu Mtendaji Mkuu Jema Msuya na Meneja Mkuu Kitengo cha Mitandao ya Simu wa Benki ya Posta Tanzania, Mshama Mshama. Mwingine ni Meneja Operesheni Airtel Money, John Ndunguru.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Jema Msuya akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja baina ya Airtel  na Benki ya Posta Tanzania kwa kutoa huduma za kifedha pamoja pembeni ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Betrice Singano Mallya.  Pembeni ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Jema Msuya na Meneja Mkuu Kitengo cha Mitandao ya Simu wa Benki ya Posta Tanzania, Mshama Mshama. Mwingine ni Meneja Operesheni  Airtel Money, John Ndunguru.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Jema Msuya na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Betrice Singano Mallya wakibadilishana mkataba wa makubaliano kutoa huduma za kifedha pamoja baina ya Airtel Tanzania na Benki ya Posta Tanzania. Wanaoshuhudia pembeni ni  Meneja Mkuu Kitengo cha Mitandao ya Simu wa Benki ya Posta Tanzania, Mshama Mshama na Meneja Operesheni Airtel Money, John
Ndunguru.

Airtel Money na Banki ya Posta waungana kutoa huduma za kifedha kwa wateja wao

·        Muungano wao utasaidia kurahisisha huduma za kibenki kupitia Airtel Money
·        Airtel Money na Bank ya posta zapeleka huduma za kifedha maeneo ya pembezoni mwa Tanzania


Dar es Salaam, Tanzania, Octoba 22, 2013: Airtel Tanzania leo imeungana rasmi na Benki ya Posta ya Tanzania (TPB) kwa lengo la kufungua mipaka kwa wateja wa Airtel Money na Benki hiyo nchini kujipatia huduma za kifedha mahali popote na wakati wowote huku wakifaidi huduma ya –HAKATWI MTU HAPA inayomuwezesha mteja wa Airtel popote kutuma na kutoa pesa bila makato kupitia Airtel Money

Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “Airtel inalenga kutoa ufumbuzi wa kudumu wa changamoto zinazoikabili sekta ya fedha hasa kwa wananchi walioko maeneo ya pembezoni mwa nchi ambapo bado hawajafikiwa na huduma za benki.  Uhusiano huu na benki ya Posta utawawezesha wateja wa airtel na wateja wa Benki hii kupata huduma za kifedha kwa urahisi na usalama zaidi bila kubeba pesa kila wakati. 

Kwa kutumia Airtel Money wateja wenye Akaunti Benki ya Posta wanaweza kutuma na kutoa pesa kwenye akaunti zao, kuhamisha au kufanya malipo kwa wafanyabiashara wenzao wawapo mahali popote, wakati wowote ndani ya Tanzania.

“Kutokana na wigo mpana tulionao Airtel nchini, hii itakuwa ni suluhisho kwa wateja kupata uhakika wa huduma sawa na zile za ATM za benki kwa ukaribu zaidi wa hata km 150 kutokana wingi mawakala wetu zaidi ya 20,000 waliosambaa maeneo ya mjini na vijijini” aliongeza kusema Bw, Colaso

Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Bw, Jema Msuya alisema “Tunajisikia fahari sana kuunganisha nguvu na kampuni ya Airtel  kwa kuwa inaendeleza dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za kifedha za kisasa na za kiushindani zaidi kwa kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu na wateja wa Airtel kupitia Benki yetu

Bw, Msuya aliendelea kusema “kupitia umoja wetu kati ya Airtel Money na Banki ya posta sasa mteja wetu ataweza kupata taarifa za  akaunti yake ya Benki ya posta kama vile kujua salio la akaunti yake, kupata taarifa fupi, kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yake bila shida awapo mahali popote iwe nyumbani au ofisini kwake masaa 24 kila siku kwa kutumia simu yake ya Airtel”

Nae Meneja Mradi wa Airtel Money Bw, John Ndunguru alisema “ni rahisi sana mteja kutumia huduma hii ya Airtel Money na Benki ya Posta, piga tu *150*21# kisha fuata mtiririko wa maelezo, kwa urahisi wake moja kwa moja tunakuhakikishia utafurahia mihamala yako yote kwa usalama zaidi na kuokoa muda wako na gharama za kwenda benki kila wakati”

Huduma ya kifedha ya Airtel Money ni rahisi na salama kwa kuwa namba ya simu iliyounganishwa na  Airtel Money imewekewa namba ya siri Maalum kwaajili ya kuizuia kutotumiwa na mtu mwingine tofauti na mmiliki halali wa namba ya hiyo, huduma hii sasa inatoa urahisi sana kwa wateja wake kuweza kulipia bili mbalimbali  kama vile LUKU, Ada za Lesesni za Magari,  DSTV, Dawasco pamoja na kutuma, kutoa au kuhamisha pesa kwenye akaunti washirikia wa Airtel Money ikiwemo Benki ya Posta (TPB)

Huduma ya Airtel Money inapatikana kwa wateja wote wa Airtel wa malipo kabla na baada katika maduka yote ya Airtel yaliyosambaa nchi nzima

Airtel pia kupitia huduma hii ya Airtel money wiki iliyopita ilizindua huduma kabambe inayowawezesha wateja wa Airtel huduma ya malipo baada au  ya mwezi (post paid) kulipia ankara zao za kila mwezi kwa Airtel Money bila kutembelea maduka ya Airtel na kuokoa muda wa kwenda mapaka katika maduka ya Airtel au pesa zao kwenye nauli kwa kufanya malipo popote walipo sasa.