Airtel Money na Banki ya Posta waungana kutoa huduma za kifedha kwa wateja wao
· Muungano wao utasaidia kurahisisha huduma za kibenki kupitia Airtel Money
· Airtel Money na Bank ya posta zapeleka huduma za kifedha maeneo ya pembezoni mwa Tanzania
Dar es Salaam, Tanzania, Octoba 22, 2013: Airtel Tanzania leo imeungana rasmi na Benki ya Posta ya Tanzania (TPB) kwa lengo la kufungua mipaka kwa wateja wa Airtel Money na Benki hiyo nchini kujipatia huduma za kifedha mahali popote na wakati wowote huku wakifaidi huduma ya –HAKATWI MTU HAPA inayomuwezesha mteja wa Airtel popote kutuma na kutoa pesa bila makato kupitia Airtel Money
Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “Airtel inalenga kutoa ufumbuzi wa kudumu wa changamoto zinazoikabili sekta ya fedha hasa kwa wananchi walioko maeneo ya pembezoni mwa nchi ambapo bado hawajafikiwa na huduma za benki. Uhusiano huu na benki ya Posta utawawezesha wateja wa airtel na wateja wa Benki hii kupata huduma za kifedha kwa urahisi na usalama zaidi bila kubeba pesa kila wakati.
Kwa kutumia Airtel Money wateja wenye Akaunti Benki ya Posta wanaweza kutuma na kutoa pesa kwenye akaunti zao, kuhamisha au kufanya malipo kwa wafanyabiashara wenzao wawapo mahali popote, wakati wowote ndani ya Tanzania.
“Kutokana na wigo mpana tulionao Airtel nchini, hii itakuwa ni suluhisho kwa wateja kupata uhakika wa huduma sawa na zile za ATM za benki kwa ukaribu zaidi wa hata km 150 kutokana wingi mawakala wetu zaidi ya 20,000 waliosambaa maeneo ya mjini na vijijini” aliongeza kusema Bw, Colaso
Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Bw, Jema Msuya alisema “Tunajisikia fahari sana kuunganisha nguvu na kampuni ya Airtel kwa kuwa inaendeleza dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za kifedha za kisasa na za kiushindani zaidi kwa kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu na wateja wa Airtel kupitia Benki yetu
Bw, Msuya aliendelea kusema “kupitia umoja wetu kati ya Airtel Money na Banki ya posta sasa mteja wetu ataweza kupata taarifa za akaunti yake ya Benki ya posta kama vile kujua salio la akaunti yake, kupata taarifa fupi, kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yake bila shida awapo mahali popote iwe nyumbani au ofisini kwake masaa 24 kila siku kwa kutumia simu yake ya Airtel”
Nae Meneja Mradi wa Airtel Money Bw, John Ndunguru alisema “ni rahisi sana mteja kutumia huduma hii ya Airtel Money na Benki ya Posta, piga tu *150*21# kisha fuata mtiririko wa maelezo, kwa urahisi wake moja kwa moja tunakuhakikishia utafurahia mihamala yako yote kwa usalama zaidi na kuokoa muda wako na gharama za kwenda benki kila wakati”
Huduma ya kifedha ya Airtel Money ni rahisi na salama kwa kuwa namba ya simu iliyounganishwa na Airtel Money imewekewa namba ya siri Maalum kwaajili ya kuizuia kutotumiwa na mtu mwingine tofauti na mmiliki halali wa namba ya hiyo, huduma hii sasa inatoa urahisi sana kwa wateja wake kuweza kulipia bili mbalimbali kama vile LUKU, Ada za Lesesni za Magari, DSTV, Dawasco pamoja na kutuma, kutoa au kuhamisha pesa kwenye akaunti washirikia wa Airtel Money ikiwemo Benki ya Posta (TPB)
Huduma ya Airtel Money inapatikana kwa wateja wote wa Airtel wa malipo kabla na baada katika maduka yote ya Airtel yaliyosambaa nchi nzima
Airtel pia kupitia huduma hii ya Airtel money wiki iliyopita ilizindua huduma kabambe inayowawezesha wateja wa Airtel huduma ya malipo baada au ya mwezi (post paid) kulipia ankara zao za kila mwezi kwa Airtel Money bila kutembelea maduka ya Airtel na kuokoa muda wa kwenda mapaka katika maduka ya Airtel au pesa zao kwenye nauli kwa kufanya malipo popote walipo sasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.