Barcelona imesema kuwa liverpool
iliitisha £183m kwa uhamisho wa nyota wake Phillipe Countinho katika
siku ya mwisho ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho siku ya Ijumaa.
''Liverpool ilikuwa inataka Yuro milioni 200 na kwa kweli hatungeweza kukubali hilo'', alisema mkurugenzi wa Barcelona Albert Soler.
Tunamshukuru mchezaji huyo kwa juhudi alizofanya , kwa sababu alijaribu sana na kutuonyesha kuwa alitaka kuichezea Barcelona.
Soler ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumamosi aliongezea: Hali ilimalizika ilivyomalizika na hakuna chengine tunachoweza kufanya.
Barcelona ilimtaka Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa PSG kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho cha £200m.
Liverpool imesema kuwa Coutinho hauzwi na kukataa maombi ya £72m, £90m na jingine la £114m kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho nchini Uhispania ambalo lilifungwa siku moja baada ya lile la Uingereza kufungwa.
Coutinho aliyefunga mabao 14 msimu uliopita na kuhudumia miezi sita akiwa na jeraha la kifundo cha mguu aliweka kandarasi mpya ya miaka katika uwanja wa Anfield mnamo mwezi Januari.
Licha ya klabu za Ligi ya Premia kutumia £1.4bn kipindi chote cha kuhama wachezaji- ambayo ni rekodi mpya - Alexis Sanchez, Virgil van Dijk, Riyad Mahrez, Thomas Lemar, Diego Costa na Ross Barkley bado hawakufanikiwa kuhama.
Siku ya mwisho ya kuhama wachezaji msimu uliopita ilikuwa £155m.
Chelsea walitumia £35m kumnunua Danny Drinkwater naye Mamadou Sakho akanunuliwa £26m na Crystal Palace kutoka Liverpool, taarifa za kuhama kwao zikitangazwa baada ya muda rasmi wa kuhama wachezaji.
Wawili hao ndio waliosaidia kuvunja rekodi ya mwaka jana.
Chelsea walinunua pia Davide Zappacosta, Spurs wakamchukua mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente kwa £15m, klabu hiyo ya Wales nayo ikajaza nafasi hiyo kwa kumchukua Wilfried Bony kwa £12m.