Mahakama ya Juu ya Kenya imetengua matokeo ya
uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita nchini humo na kumpa ushindi
Rais wa sasa wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.
Mahakama ya Juu ya Kenya imetengua matokeo ya uchaguzi mkuu
uliofanyika mwezi uliopita nchini humo na kumpa ushindi Rais wa sasa wa
nchi hiyo, Uhuru Kenyatta huku kinara wa muungano wa upinzani wa NASA
Raila Odinga akiibuka wa pili.Jopo la majaji sita, na kwa uamuzi wa wengi, leo Ijumaa limesema iligundua kuwa Tume ya Uchaguzi haikuweza kuendesha zoezi la uchaguzi kulingana na Katiba na Sheria Uchaguzi.
"Baada ya kuzingatia ushahidi wote, tumeridhika kuwa uchaguzi haukufanyika kwa mujibu wa kanuni za Katiba na kanuni husika", amesema Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga.
Majaji wawili katika jopo hilo walipinga uamuzi wa kubatilisha uchaguzi. Uchaguzi mpya wa Rais wa Kenya utafanyika siku sitini zijazo.
Baada ya Mahakama ya Juu Zaidi kufutilia mbali ushindi wa Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8, Uhuru na chama amesisitiza kutoridhishwa na uamuzi huo. Akiongea kutoka Ikulu ya rais, Uhuru alipinga uamuzi huo japo atauheshimu huku akisisitiza kuwa yuko tayari kwa ajili ya marudio ya uchaguzi.
Wakati huo huo, wakizungumza nje ya Mahakama ya Juu zaidi baada ya
kushinda kesi hiyo, viongozi hao walisema, makamishna wa Tume Huru ya
Uchaguzi na Mipaka (IEBC) waliosababisha mchakato wa uchaguzi mbovu, ni
lazima kufunguliwa mashtaka.
Wakiongozwa na Raila Odinga, viongozi hao walisema, hawataruhusu makamishna hao kusimamia uchaguzi tena unaotarajiwa katika kipindi cha miezi miwili.
Shughuli katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi zilikwama kwa muda baada ya wafuasi wa NASA kuingia jijini kwa mbwembwe wakishereheka ushindi wao kwenye kesi dhidi ya ushindi wa Uhuru Kenyatta. Katika upande wa pili wafuasi wa Rais Kenyatta na chama cha Jubilee walionekana kutulia huku wakisema watajitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio ili kuhakikisha wanapata ushindi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.