Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema watu
zaidi ya laki moja na elfu kumi wamepoteza makazi yao baada ya kutokea
mafuruko katika jimbo la Benue katikati mwa nchi hiyo.
Katika taarifa ya siku ya Ijumaa
kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Buhari amesema timu za uokoaji
zimefika katika eneo la maafa kusaidia familia za waathirika.
Hadi hivi sasa hakuna taarifa kamili kuhusu hasara iliyopatikana kufuatia mafuriko hayo.
Tokea mwanzoni mwa mwaka huu, Nigeria
imekumbwa na mvua kali za msimu ambazo zimesababisha hasara katika nchi
hiyo ya Afrika Magharibi.
Jimbo la Benue linategemea sana kilimo
na hukumbwa na mafuriko mara kwa mara kutokana na mvua kali na
kufunguliwa mabwawa ya nchi jirani ya Cameroon. Mwaka 2012 Nigeria
ilikumbwa na mafuruko mabaya katika majimbo 30 kati ya 36 ya nchi hiyo.
Mamia ya watu waliaga dunia na wengine milioni mbili kuachwa bila
makazi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.