Bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huipata wakiwa wadogo sana na usipokua makini tabia hii itakufanya vibaya sana kisaikolojia.
Tabia ya kujichua sasa iko wazi kwa jinsia zote yaani wanawake na wanaume japokua imekua ikiathiri zaidi wanaume sababu ya maumbile yao.
Japo wengi hufanya kwa siri na kuficha ili wasijulikane na wengine. Vijana wengi wamekuwa wakiangalia video hizo wakiwa wamejificha wenyewe chumbani, na hasa nyakati za usiku.
Kuangalia video za ngono kuna madhara mbalimbali ya kiafya na kisaikolojia. Haya hapa ni baadhi ya madhara unayoweza kuyapata kama utaangalia sana video za ngono.
Kuishiwa hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume
Kuangalia sana video za ngono hukufanya ushindwe kusisimuliwa na mwanamke au mwanaume wa kawaida, video za ngono zina wanawake na wanaume wazuri sana ambao wako vile sababu ya kufanyiwa upasuaji mbalimbali wa kuongeza makalio na matiti, hata wanaume hufanyiwa upasuaji wa kuongeza uume hivyo mwanamke anayeangalia atatamani uume mkubwa kama ule au mwanaume anayeangalia atatamani mwanamke kama yule ambaye katika mazingira ya kawaida hayupo.
Sasa wanaume wanao angalia video za ngono hawawezi kusisimka au kuamsha uume hata mwanamke wa kawaida akipita uchi na hii huweza kuathiri sana mahusiano yao na kuonekana hawana nguvu za kiume kwani wao hutegemea video hizo kuamsha uume.
Kujichua au kupiga punyeto sana
Video za ngono zina wanawake na wanaume tofauti, kila video nzuri unayoangalia utaenda kujichua huku ukimuwaza wanaume au mwanamke husika. Hii itakufanya ujichue hata mara kumi kwa siku kama unaziangalia mara kwa mara. Kuishiwa nguvu za kiume, kusahau sana, kushindwa kumpa mwanamke mimba, kuchoka sana na kufika kileleni haraka wakati wa tendo la ndoa ni moja ya madhara makuu ya punyeto.
Kushindwa kudumu kwenye mahusiano
Kuangalia video za ngono hukufanya uwaze kujiridhisha mwenyewe tu na hata mwenza wako akitaka kulala na wewe unakua hutaki tena. Lakini hata kwa vijana ambao hawako kwenye mahusiano hujikuta wanakua waoga sana kuwafuata wanawake au wasione sababu ya kua kwenye mahusiano. Vile vile wanaume hushindwa kuwaridhisha wenza wao na wanawake kusingizia kuchoka kila siku.
Kuanza kufanya ngono ambazo sio za kawaida
Hivi karibuni idadi kubwa ya wanawake wamekua wakijihusisha sana na mapenzi ya kinyume na maumbile. Hii imesababishwa sana na kuangalia video za ngono na kuona ni kitu cha kawaida wakati kina madhara mengi. Wanawake waliozoea kuingiliwa nyuma hata wakiolewa huendelea kufanywa na wanaume wa nje hasa kama waume waliowaoa hawajawahi kujihusisha na tabia hiyo. Aina zingine za ngono ambazo zinababishwa na tabia ya kuangalia video hizi ni ushoga, usagaji, au mwanamke kulala na wanaume zaidi ya mmoja au mwanaume kulala na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
Inawezekana wewe unayesoma hapa tayari hii tabia inakuumiza sana kwa sasa na umeshindwa kuiacha, kuna mambo ya msingi unaweza kufanya ili uweze kuacha kuangalia video hizi..
Ondoa zana zote za kuangalia video hizi
Kama una tarakilishi (computer) au simu futa video zote, futa tovuti (website) zote za video ambazo unazitumia kuangalia. Kuna watu wamo kwenye makundi ya WhatsApp ya kutumiana video za ngono, ondoka kabisa huko kwani unajiharibu.
Anza kufanya mazoezi
Ni mazoezi pekee yanayoweza kumfanya mtu aweze kuachana na tabia zote ambazo sio za kawaida ambazo alikua anazifanya kipindi cha nyuma. Unapofanya mazoezi utatumia nguvu nyingi na mwili wako utachoka na kupata usingizi. Vilevile ufanyaji wa mazoezi hukuepusha na kukaa bila shughuli yoyote.
Jijengee tabia ya kukaa na marafiki zako muda mrefu au kufanya shughuli nyingine zitakazokuweka ‘busy’
Kama una tabia ya kuangalia video hizi basi, fanya mpango uwe unafanya mambo mengine muda ambao umekua ukiangalia hizi video, ikiwemo kusoma vitabu au kuongea na watu. Hii itakusaidia kusahau video hizo na kuacha kabisa.
Pata ushauri wa kitaalamu na matibabu
Unaweza kumuona mtaalamu wa ushauri wa kisaikolojia ili kukusaidia ushauri wa namna ya kufanya ili kuepukana na tabia hiyo. Kama umeshapata madhara kiafya, basi waone wataalamu wa afya hasa masuala ya uzazi ili wakushauri namna ya kulitibu tatizo lako.
Jenga mahusiano ya karibu na mpenzi wako
Hii itakusaidia kumuwaza yeye zaidi ya video za ngono na pia pale unapopata hamu ya kufanya mapenzi basi hutoogopa kumwambia ili mfanye. Kuwa karibu na mpenzi wako kutakujengea ujasiri na kuyakuza mahusiano yenu.