Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepiga marufuku matangazo ya
biashara yanayowekwa mtumiaji anapopiga simu ili kutoa fursa kwa
watumiaji kupata mawasiliano bila usumbufu.
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema leo (Ijumaa) kuwa
mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa simu
wakilalamikia matangazo hayo yanayotolewa na kampuni za simu.
Amesema tayari TCRA imeshaziandikia barua kampuni zote za simu kusitisha
matangazo hayo na itakutana nazo kwa majadiliano ya kina Julai 6.
Amesema mamlaka haitambui utaratibu huo na inauchukulia kama kero kwa
watumiaji wa simu ambao hutegemea kutumia njia hiyo ya mawasiliano
kurahisisha mambo.
“Tuna imani mtu anapopiga simu ana shida ya haraka na anahitaji afanye
mawasiliano, unapomuwekea matangazo kwa dakika tatu au nne ni usumbufu,”
amesema.
Katika siku za karibuni imekuwa ni kawaida kwa mtu anayepiga simu
kusikiliza wimbo au matangazo ya biashara na baadaye kuambiwa namba
anayopiga haipatikani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.