ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 5, 2019

LAZIMA UDATE MAKAMUZI YA MALKIA WA TAARAB TANZANIA


Umechelewa kuipata hii toka kwa Malkia wa Taarab nchini Tanzania 'KHADIJA OMAR KOPA'  lakini ipate sasa na iwe kama kumbukumbu, ya Tamasha kubwa la Burudani 'Wasafi Festival' lililofanyika CCM Kirumba Mwanza 2018.

TBL YASHIRIKIANA NA MUHAS KUFANIKISHA ELIMU YA LISHE KWA WAJAWAZITO NA UGONJWA WA SELI MUNDU (SICKLE CELL)

Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutingazi akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Rais wa Chama cha Madaktari Tanzaia,Dkt Elisha Osat, (kulia) akichangia mada wakati wa mafunzo hayo, (Kushoto) anayesikiliza ni Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutingazi. Wadau wanaoshiriki mafunzo wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wakufunzi Baadhi ya washiriki wa mafunzo katika picha ya pamoja. Katika mwendelezo wa kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali katika jamii, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeshirikiana na Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS), kufanikisha mafunzo ya siku 3 kwa wauguzi kutoka hospitali za Dar es Salaam kuhusiana na Afya ya Lishe kwa akina mama wajawazito na ugonjwa wa Seli mundu (Sickle Cell ).

 Akiongea wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha MUHAS, Meneja wa masuala Endelevu wa TBL ,Irene Mutingazi,alisema kuwa TBL imejitosa katika kusaidia katika sekta ya afya kama ambavyo imekuwa ikisaidia kukabiliana na huduma changamoto mbalimbali za kijamii kupitia sera yake ya kusaidia huduma za kijamii inayolenga kuwaleta Watu Pamoja Katika Ulimwengu Maridhawa. “Mafunzo haya kwa wauguzi kutoka hospitali za Dar es Salaam tuna imani yatasaidia kupunguza changamoto ya elimu ya lishe duni na ugonjwa wa Selimundo kwa kuwa wataifikisha kwa walengwa wanaowahudumia hususani akina mama wajawazito na wagonjwa wa Seli mundu”,alisema. 

 Aliongeza kuwa TBL kupitis sera yake ya kuifanya Dunia Maridhawa itasaidia kushirikiana na wadau mbalimbali kukabiliana na changamoto mbalimbali katika jamii hususani katika sekta ya elimu na afya. 

 Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzaia,Dkt Elisha Osat,alisema sekta ya afya inakabiliwa na changamoto mbalimbali na aliwashukuru wadau kama TBL ambao wamekuwa wakijitoa kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo. --

Thursday, July 4, 2019

KILA GAZETI LA MWANANCHI KUNA BODABODA.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications Limited, Frances Nanai akionyesha sehemu Kipande cha Gazeti la Mwanaspoti ambacho msomaji ukinunu unapaswa kujaza taarifa zako na unaweza kujishindia Bodaboda au Simu ya mkononi ama pesa taslimu mara baada ya uzinduzi wa Promosheni ya “Shinda Mchongo wa Mwanaspoti” uliyozinduliwa katika ofisi za Mwananchi Communications Limited. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications Limited, Francis Nanai na Mwakilishi wa Michezo ya kubahatisha Tanzania, Jihudi Ngolo wakikata utepe kuashilia uzinduzi wa Promosheni ya”Shinda Mchongo wa Mwanaspoti” ulifanyika katika ofisi za Mwananchi Communications Limited. Kulia ni Meneja masoko wa MCL, Sara Munema na  Mkuu wa kitengo cha uzalishaji wa habari Mwananchi Communications Limited, Frank Sanga

Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha uzalishaji wa habari Mwananchi Communications Limited, Frank Sanga, Mkurugenzi Mkuu wa MCL, Francis Nanai, Mwakilishi wa Michezo ya kubahatisha Tanzania, Jihudi Ngolo na Meneja masoko wa MCL,Sara Munema wakipiga mako) mara baada ya uzinduzi rasmi wa Promosheni ya  “Shinda Mchongo wa Mwanaspo” uliyozinduliwa katika ofisi za Mwananchi Communications Limited. 

JIMMY MANZAKA LIVE KATIKA CHEZA KIDANSI MWANZA.


Mwanamuziki Jimmy Manzaka raia wa Congo anayefanya shughuli zake nchini Tanzania mwishoni mwa wiki ameshiriki kwenye tamasha la burudani ya muziki wa bandi linalojulikana kama Cheza Kidansi na kufanya makubwa, kiasi cha kutajwa kwenye list ya wanamuziki waliofanya vyema usiku huo adhimu. Coco Shanel ni moja kati ya nyimbo zilizobamiza kwa stege na mkali huyo.

WAFANYABIASHARA WENGI MWANZA WANACHELEWA KUAMKA - NA HIZI NDIZO ATHARI ZAKE.


Katika safari yoyote ya mafanikio huwa ipo misingi na mambo ya lazima ambayo ni lazima uyajue ili kufanikiwa. Kwa kuyajua mambo hayo yatakupa dira na mwelekeo mzuri wa kufikia mafanikio makubwa.

Ni kweli unaweza ukawa una malengo mazuri uliyojiwekea, lakini bila kuyajua mambo hayo na kuyafanyia kazi itakuwa ni ngumu sana kufikia mafanikio yako. Watu wengi wenye mafanikio wanayajua mambo haya na kuyafanyia kazi mara kwa mara. Je, unajua ni mambo gani ambayo ni ya lazima sana katika safari yako ya mafanikio? 

JEH KUCHELEWA KUAMKA KUNA ATHARI GANI KATIKA MAENDELEO YA WAJASILIAMALI WENGI MWANZA?

WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA WARSHA YA WADAU KUJADILI FURSA ZA BOMBA LA MAFUTA -EACOP SHINYANGA

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga leo Julai 3,2019.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama amefungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga. 

Tuesday, July 2, 2019

KWAHERI DANIEL S. KASEKO 1940 2019



 Hatimaye mwili wa Baba yangu Mkubwa Daniel S. Kaseko umeagwa leo nyumbani hapa Nyakato Jijini Mwanza ambako alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na kisha kusafirishwa kuelekea katika kijiji cha Malampaka wilayani Maswa mkoani Simiyu kwaajili ya mazishi yatakayofanyika Jumatano ya tarehe 3 july 2019.

Sote watoto, wajukuu, vitukuu, vilembwe. familia nzima ndugu jamaa na marafiki tunafarijiwa na maandiko matakatifu kupitia - 2 Timotheo 4:7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda. AMEN

BY Albert.

HERI YA UHURU TAIFA LA CONGO



 Bana Congo tosimbana/ clips officiel avec Donat mwanza

NEW ZEALAND YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI.


Marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastika yaanza kutumika nchini New Zealand.

Waziri wa mazingira wa nchi hio Eugenie Sage, ametoa ufafanuzi kuhusiana na sheria hiyo inayopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki inayotumika mara moja kupitia tovuti ya wizara hiyo. Sheria hio iliopitishwa mwaka jana imeanza kutumika Julai 1.

Sage alisema Marufuku hio ni hatua katika kuhakikisha bahari zinakuwa salama kwa afya na pia kusaidia kutunza mazingira.Aliongeza kwamba Marufuku hio itasaidia kupunguza plastiki katika mito, vijito, maji yanayotiririka, mifumo ya maji ya mvua na baharini hivyo basi athari kwa  ndege wa baharini, samaki, kobe na viumbe wengine wa baharini zitapungua.

Sheria hio imeweka adhabu ya tozo la hadi dola elfu 67 kwa atakayevunja sheria hiyo. Kwa mara ya kwanza sheria ya marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki ilianza kutumika nchini Bangladesh mnamo mwaka 2002.

Nchi ya Tanzania ilianza kutumia sheria ya marufuku ya matumizi ya plastiki mnamo mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Kila mwaka zaidi ya mifuko ya plastiki trioli 1 hutengenezwa duniani na karibu tani 8 za mifuko ya plastiki huishia baharini.

CGF ANDENGENYE APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO NA MAOKOZI.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akipokea Sare za kuzimia moto (Fire suite), kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa. Vifaa hivyo vimepokelewa Makao mapema hii leo Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akipokea Mikanda maalum kwa ajili ya maokozi (Rescue Belt), kutoka Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa. Vifaa hivyo vimepokelewa mapema hii leo Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vifaa vya kuzimia moto na maokozi vilivyotolewa na Kampuni ya Wilna International Japan na kukabidhiwa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Lengo la kuboresha utendaji kazi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)



Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, CGF Thobias Andengenye, amepokea msaada wa vifaa vya kuzimia moto na maokozi vitakavyotumika kwa shughuli mbalimbali za Jeshi hilo.

Amepokea msaada huo mapema hii leo Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam, kutoka kwa Kampuni ya Wilna International Japan.

Hata hivyo, Andengenye ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo na kushirikiana na Jeshi hilo katika Kuokoa Maisha na Mali za Watanzania. 

Aidha, Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa, amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo wa vifaa vya kuzimia moto na maokozi ili kurahisisha utendaji kazi wa Jeshi hilo.

WAZIRI LUGOLA AONGOZA KIKAO CHA KUFUATILIA MALI ZA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA JIJINI DODOMA

 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Kangi Lugola akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa  Mamlaka  ya  Vitambulisho  vya  Taifa (NIDA), lengo la kikao hicho ni ukaguzi na utambuzi wa mali za mamlaka hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu  Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,  akizungumza wakati wa kikao na Uongozi  wa  Mamlaka  ya  Vitambulisho  vya  Taifa (NIDA), lengo la kikao hicho ni ukaguzi  na  utambuzi wa  mali  za  mamlaka hiyo.Kushoto ni waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola. Kikao hicho kimefanyika  leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akizungumza wakati wa kikao na Uongozi  wa  Mamlaka  ya  Vitambulisho  vya  Taifa (NIDA), lengo la kikao hicho ni ukaguzi na utambuzi wa mali za mamlaka hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Kangi Lugola (katikati), Katibu Mkuu wa wizara, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto)  na Naibu Katibu Mkuu ,Ramadhani Kailima (kulia) wakikagua orodha ya mali za Mamlaka  ya  Vitambulisho  vya  Taifa (NIDA),  wakati  wa  kikao  na uongozi wa mamlaka hiyo  lengo  ikiwa  ni ukaguzi  na utambuzi wa mali za mamlaka hiyo.Waliosimama ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Anold Kihaule na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha NIDA, Merckion Ndofi(kushoto). Kikao hicho kimefanyika  leo  jijini  Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mkurugenzi  wa  Sheria  wa  Wizara  ya  Mambo  ya  Ndani  ya Nchi, Merlin Kombaakizungumza wakati wa kikao na Uongozi   wa   Mamlaka   ya   Vitambulisho   vya   Taifa (NIDA),  lengo  la  kikao hicho  ni ukaguzi na utambuzi wa mali za mamlaka hiyo. Kikao  hicho  kimefanyika  leo  jijini DodomaPicha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi  Mkuu  wa  Mamlaka  ya  Vitambulisho  vya  Taifa(NIDA), Dk. Arnold  Kihaule akiwasilisha muhtasari wa mali za mamlaka hiyo mbele ya uongozi  wa  juu  wa  Wizara  ya Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, lengo la kikao hicho ni ukaguzi na utambuzi wa mali za mamlaka hiyo.Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi