ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 2, 2019

NEW ZEALAND YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI.


Marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastika yaanza kutumika nchini New Zealand.

Waziri wa mazingira wa nchi hio Eugenie Sage, ametoa ufafanuzi kuhusiana na sheria hiyo inayopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki inayotumika mara moja kupitia tovuti ya wizara hiyo. Sheria hio iliopitishwa mwaka jana imeanza kutumika Julai 1.

Sage alisema Marufuku hio ni hatua katika kuhakikisha bahari zinakuwa salama kwa afya na pia kusaidia kutunza mazingira.Aliongeza kwamba Marufuku hio itasaidia kupunguza plastiki katika mito, vijito, maji yanayotiririka, mifumo ya maji ya mvua na baharini hivyo basi athari kwa  ndege wa baharini, samaki, kobe na viumbe wengine wa baharini zitapungua.

Sheria hio imeweka adhabu ya tozo la hadi dola elfu 67 kwa atakayevunja sheria hiyo. Kwa mara ya kwanza sheria ya marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki ilianza kutumika nchini Bangladesh mnamo mwaka 2002.

Nchi ya Tanzania ilianza kutumia sheria ya marufuku ya matumizi ya plastiki mnamo mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Kila mwaka zaidi ya mifuko ya plastiki trioli 1 hutengenezwa duniani na karibu tani 8 za mifuko ya plastiki huishia baharini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.