ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 4, 2014

MWANZA YATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MCHUNGAJI DAUDI ISAYA ONYANGO ALIYEFARIKI KWA AJALI.

Wachungaji wa makanisa mbalimbali ya AICT Kanda ya Ziwa wakiwa katika ibada maalum ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mchungaji Daudi Isaya Onyango aliyefariki kwa ajali akiwa safarini mkoani Geita ambako alikwenda kwaajili ya kazi ya kusambaza vitabu vya neno la Mungu.
Mwili wa Mchungaji Daudi Isaya Onyango ukiingia katika kanisa la AICT Makongoro kwaajili ya ibada ya kuagwa na wakazi wa Mwanza kisha kusafirishwa kuelekea mkoani Mara kwaajili ya mazishi.
Mchungaji Daudi Isaya Onyango alizaliwa mnamo mwaka 1963 tarehe 3 mwezi march.
Mama Rose ambaye ni mjane wa marehemu (wa pili kutoka kushoto) akiwa na wanae kwenye ibada hiyo.
Waumini walio hudhuria ibada hiyo iliyofanyika leo asubuhi katika kanisa la AICT Makongoro Mwanza.
Wananchi na watu wa mataifa mbalimbali wako hapa.
Upande wa akinamama.
Ibada ikiendelea.
Historia ya marehemu Mchungaji Isaya Onyango ikisomwa.
Wachungaji wa makanisa mbalimbali, waumini na marafiki waliomjua wameshiriki ibada hii.
Askofu Mussa Magwesela wa Dayosisi ya Geita aliongoza ibada hiyo kwa kumfananisha marehemu Mchungaji Onyango na mwanariadha aliyesubiri kuvikwa taji la uzima mara baada ya kumaliza mbio.
Jiografia ya kanisa wakati wa ibada.
Sifa kuu ya kila mchungaji aliyepata nafasi kumzungumzia Mchungaji Daudi Isaya Onyango alimzungumzia kama rafiki. 
Mwakilishi wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Alliance Mission alimzungumzia Mchungaji Daudi Isaya Onyango kama mfano wa kuigwa kwa kupenda watoto na kuwasaidia kutatua matatizo yao kwa ukaribu akiwaonyesha upendo wa kweli.
Kwaya ya Vijana AIC Makongoro ikiimba wimbo maalum.
Ni wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Mchungaji Daudi Isaya Onyango.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza Jackson Songora akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mchungaji Daudi Isaya Onyango katika ibada iliyofanyika Kanisa la AICT Makongoro Mwanza. 
Kwaya ya Makongoro akinamama.
Familia ya Marehemu Mchungaji Onyango ilipata nafasi kutoa heshima za mwisho na hapa wanaonekana vijana wa marehemu  wakiwa na mjomba wao Allen Olimo (mwenye koti kulia).
Mjane wa marehemu akipata usaidizi kuuaga mwili wa marehemu mumewe.
Hali ilikuwa mbaya kwa mabinti wa marehemu.
Maaskofu na wachungaji wakiuaga mwili wa marehemu mchungaji  Daudi Isayo Onyango.
Askofu Mussa Magwesela wa Dayosisi ya Geita akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mchungaji Daudi Isaya Onyango katika ibada takatifu iliyofanyika katika kanisa la AICT Makongoro Mwanza.
Mbele ni Mchungaji toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye alilelewa na kanisa la AIC Tanzania akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mchungaji Daudi Isaya Onyango ambaye alimtaja marehemu kuwa alikuwa ni rafiki yake kipenzi katika ushauri. 
Ibada ya kuhitimisha ibada ilifanyika kanisani hapa kisha safari kuelekea kijiji cha Songoro kata ya Buruma, wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa mazishi ilifanyika. 
Safari kuelekea kijiji cha Songoro kata ya Buruma, wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa mazishi ilifanyika.
Meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya mkolani Mhe. Stansalaus Mabula (mwenye miwani kulia) akikumbushana mambo muhimu na marafiki zake mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa la AICT Makongoro kumalizika.

Friday, January 3, 2014

TAZAMA PICHA JINSI LIONEL MESSI ALIVYOPANDA MLIMA KILIMANJARO

Messi ni mmoja kati ya masuper star waliepanda mlima Kilimanjaro, mlima mrefu katika bara la Africa mlima unaopatikana katika ardhi ya Tanzania. Mlima kilamanjaro ni moja ya vivutio vinavyoliletea taifa letu sifa na utajiri. Kwanini tusijivunie Utanzania wetu kupitia rasilimali zetu Mungu ibariki Tanzania.
PICHA na Muhsin Mukongo.

Thursday, January 2, 2014

LIGI KUU ENGLAND MAN U CHALI.


Ligi kuu ya England inazidi kupamba moto, huku Arsenal wakiendelea kukalia kiti cha uongozi, baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Cardiff City.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, anasema:
"Tunajua tutacheza michezo 10 hapa nyumbani na tunataka kuifanya sehemu hii kuwa ngome yetu, bila kujali wengine wanafanya nini.
"Iwapo tunaweza kufanya hivyo, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi."
Arsenal, haiko salama sana katika nafasi yake ya kwanza ikiwa na pointi 45, kwani kwa karibu sana inanyemelewa na Manchester City yenye pointi 44, huku Chelsea ikiweka kibindoni pointi 43 ikiwa katika nafasi ya tatu. Liverpool imejisogeza juu kutoka nafasi ya tano sasa iko nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi 39, huku Everton ikipigwa kumbo na kusogezwa nafasi ya tano kwa kuwa na pointi 38. Wakati Tottenham ikipanda juu katika nafasi ya sita kwa kupata pointi 37, mabingwa watetezi Manchester United imesukumwa chini hadi nafasi ya saba kwa kukusanya pointi 34.
Wakati timu hizo zikipigana kufa kupona kunyakua ubingwa wa ligi kuu au kuwemo katika nne bora, timu nyingine zinapigana kuepuka kushuka daraja. Timu zilizo katika hatari zaidi mpaka sasa baada ya timu zote kucheza mechi 20, ni Sunderland iliyoko nafasi ya 20 kati ya timu 20 za ligi hiyo,ikiwa na pointi 14 tu. West Ham inashikilia nafasi ya 19 ikiwa na pointi 15 na Crystal Palace ni ya 18 ikipata pointi 17 na kuipisha Cardiff City katika nafasi ya 17 iliyokuwa inashikilia kabla ya mchezo wa Jumatano.

LOWASSA AUKARIBISHA MWAKA 2014 AKIWA KIJIJINI KWAKE NGARASHI,MONDULI.

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza katika tafrija aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.Pembeni yake ni mkewe mama Regina Lowassa.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye tafrija hiyo aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh. Goodluck Ole-Medeye wakati wa tafrija hiyo iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.

Wageni waalikwa mbalimbali

PART TWO: SKYLIGHT BAND YAPAGAWISHA MKESHA WA MWAKA MPYA NDANI YA PANTONI FB CHACHA JIJINI MWANZA

DSC_0527
Dr. Sebastian Ndege a.k.a JEMBE akizungumza na wakazi wa jiji la Mwanza waliojumuika na Skylight Band katika mkesha wa mwaka mpya ndani ya Pantoni FB CHACHA kwenye party la nguvu lililopewa jina la "THE ROCK CITY CRUISE PARTY" maalum kwa wakazi wa Mwanza na kwa mara ya kwanza kushuhudia steji mpya pamoja na vyombo vipya vya Bendi hiyo.
DSC_0606
Mmiliki wa Pantoni FB CHACHA Bw. Kitama akiwasalimia mashabiki wa Skylight Band jijini Mwanza.
DSC_0399
Huu ndio muonekano wa steji mpya ya Skylight Band iliyofungwa ndani ya Pantoni FB CHACHA.
DSC_0705
Mashabiki wa Skylight Band jijini Mwanza wakiburudika kwenye mkesha wa mwaka mpya ndani ya Pantoni FB CHAHA.
DSC_0432
Diva's wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao jijini Mwanza. Kulia ni Winnie pamoja na Mary Lucos.
DSC_0447
Digjna Mbepera na Winnie wakifanya yao jukwaani.
DSC_0458
Mary Lucos katika feelings kali.
DSC_0651
Kipaji kipya ndani ya Skylight Band Hashim Donode akitoa burudani kwa mara kwanza kwa mashabiki wa bendi hiyo jijini Mwanza ndani ya Pantoni FB Chacha kwenye mkesha wa mwaka mpya.
DSC_0716
Full mzuka kwa timu nzima ya Skylight Band.
DSC_0664
DSC_0799
DSC_0698
Mashabiki wakisebeneka kwa raha zao ndani ya Pantoni FB CHACHA.
DSC_0703
DSC_0727
DSC_0941
Blogger GSENGO wa jijini Mwanza Bw. Albert Sengo akisebeneka na Sam Mapenzi kwenye mkesha wa mwaka mpya.
DSC_1000
Mzuka unapokolea.
DSC_0753
Rappa wa Skylight Band Sony Masamba alizaliwa tarehe 1/1..... Uongozi wa Skylight Band ulimfanyia bonge la Surprise..
DSC_0754
DSC_0763
Pichani akipongezwa na Captain Chacha pamoja na Meneja wa kinywaji cha K-Vant Bw. James (mwenye t-shirt ya mistari) ambao ni mmoja wa wadhamini waliofanikisha bata hilo.
DSC_0765
Mpango mzima wa cake ulihusika pia.
DSC_0810
Baada ya cake birthday boy aliingia kwa steji na kutoa burudani.
DSC_0616
Pichani juu na chini ni Sehemu ya umati wa wakazi wa jijini la Mwanza wakipatia huduma za vinywaji na nyama choma kwenye fukwe za Club Jembe ya jijini Mwanza.
DSC_0623
DSC_0807
Umati wa wakazi wa jijini Mwanza ukiwa umefurika ndani ya Pantoni FB CHACHA huku Skylight Band ikitumbuiza.
DSC_0820
Steji ya kimataifa vyombo vipya kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Mwanza haijawahi kutokea.

DSC_0824
DSC_1010
Skelewu....Skelewu.....Skeleleeeeeeee...!!!
DSC_1014
Sam Mapenzi sambamba na Lubea wa Skylight Band kwa pamoja wakicheza SKELEWU.
DSC_0500
Sam Mapenzi akipagawisha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0551
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akifanya yake huku akipewa sapoti na Mary Lucos, Hashim Donode pamoja na Digna Mbepewa.
DSC_0869
Dance if you wanna dance.
DSC_0870
Sisters wakitumia vyao tartiiiib...
DSC_1002
Vunja kabati.
DSC_0516
Burudani ikiendelea kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya Pantoni FB CHACHA mkesha wa mwaka mpya.
DSC_0940
Blogger Zainul Mzige akiwa na Team Skylight pamoja Dr. Sebastian Ndege a.k.a JEMBE