Mwili wa Mchungaji Daudi Isaya Onyango ukiingia katika kanisa la AICT Makongoro kwaajili ya ibada ya kuagwa na wakazi wa Mwanza kisha kusafirishwa kuelekea mkoani Mara kwaajili ya mazishi. |
Mchungaji Daudi Isaya Onyango alizaliwa mnamo mwaka 1963 tarehe 3 mwezi march. |
Mama Rose ambaye ni mjane wa marehemu (wa pili kutoka kushoto) akiwa na wanae kwenye ibada hiyo. |
Waumini walio hudhuria ibada hiyo iliyofanyika leo asubuhi katika kanisa la AICT Makongoro Mwanza. |
Wananchi na watu wa mataifa mbalimbali wako hapa. |
Upande wa akinamama. |
Ibada ikiendelea. |
Historia ya marehemu Mchungaji Isaya Onyango ikisomwa. |
Wachungaji wa makanisa mbalimbali, waumini na marafiki waliomjua wameshiriki ibada hii. |
Askofu Mussa Magwesela wa Dayosisi ya Geita aliongoza ibada hiyo kwa kumfananisha marehemu Mchungaji Onyango na mwanariadha aliyesubiri kuvikwa taji la uzima mara baada ya kumaliza mbio. |
Jiografia ya kanisa wakati wa ibada. |
Sifa kuu ya kila mchungaji aliyepata nafasi kumzungumzia Mchungaji Daudi Isaya Onyango alimzungumzia kama rafiki. |
Kwaya ya Vijana AIC Makongoro ikiimba wimbo maalum. |
Ni wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Mchungaji Daudi Isaya Onyango. |
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza Jackson Songora akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mchungaji Daudi Isaya Onyango katika ibada iliyofanyika Kanisa la AICT Makongoro Mwanza. |
Kwaya ya Makongoro akinamama. |
Familia ya Marehemu Mchungaji Onyango ilipata nafasi kutoa heshima za mwisho na hapa wanaonekana vijana wa marehemu wakiwa na mjomba wao Allen Olimo (mwenye koti kulia). |
Mjane wa marehemu akipata usaidizi kuuaga mwili wa marehemu mumewe. |
Hali ilikuwa mbaya kwa mabinti wa marehemu. |
Maaskofu na wachungaji wakiuaga mwili wa marehemu mchungaji Daudi Isayo Onyango. |
Askofu Mussa Magwesela wa Dayosisi ya Geita akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mchungaji Daudi Isaya Onyango katika ibada takatifu iliyofanyika katika kanisa la AICT Makongoro Mwanza. |
Ibada ya kuhitimisha ibada ilifanyika kanisani hapa kisha safari kuelekea kijiji cha Songoro kata ya Buruma, wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa mazishi ilifanyika. |
Safari kuelekea kijiji cha Songoro kata ya Buruma, wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa mazishi ilifanyika. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.